MAAMBUKIZI ya virusi vya Ukimwi (VVU), kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto yamepungua kwa asilimia 90. Imeelezwa.
Hayo yalisemwa na Meneja wa shirika la EGPAF Mkoa wa Tabora,
Dk. Alphaxard Lwitakubi, mara baada ya Rais Jakaya Kikwete kukagua
banda la shirika hilo katika maonyesho ya wiki ya vijana iliyoambatana
na kilele cha kuzimwa kwa Mwenge wa Uhuru.
Lwitakubi, alisema lengo la EGPAF ni kufikia asilimia 98 ifikapo mwishoni mwa mwaka 2015.
Alisema
hatua hiyo itafikiwa endapo wanaume wataambatana na wake zao kwenda
kwenye vituo vya afya kama inavyotakiwa, kwani hadi sasa zimefikiwa
asilimia 48 kwa mwaka 2014 kutoka asilimia 5 mwaka 2010.
Dk.
Lwitakubi, alisema Shirika la EGPAF limekuwa likijihusisha na kazi za
kuzuia na kutokomeza maambukizi ya virusi vya Ukimwi (VVU), kutoka kwa
mama kwenda kwa mtoto.
Alisema EGPAF inafanya kazi zake katika mikoa ya Tabora, Kilimanjaro, Arusha, Lindi, Shinyanga, Geita na Simiyu.
Aliongeza kuwa EGPAF pia imekuwa ikijihusisha na wagonjwa wa majumbani katika mikoa ya Pwani, Zanzibar na Mwanza huku likitoa huduma za uchunguzi wa
saratani ya shingo ya kizazi mikoa ya Tabora, Kilimanjaro,
Shinyanga, Arusha, Simiyu, Lindi na Geita.
Kwa
upande wake, Mratibu wa Mawasiliano na Utetezi wa EGPAF, Mercy Nyanda,
alisema katika huduma zao kumekuwa na mafanikio, kwani kwa sasa
wajawazito wengi wanajifungulia vituoni tofauti hapo mwanzo.
Nyanda, alisema uelewa kwa jamii umeongezeka zaidi kuhusu hali halisi ya maamukizi ya VVU na jamii hiyo kuendelea kubadilika.
No comments:
Post a Comment