Pages

KAPIPI TV

Friday, November 14, 2014

MBOWE ANENA KIGOMA

Na Magreth Magosso,Kigoma
.
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimewalaumu waliokuwa wakishika nyadhifa ya Katibu mkuu wa chama  hicho awali Zitto Kabwe na Amani Kabourou ambye kwa sasa ni mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM Mkoa wa Kigoma ,kwa kile walichodai hawana fadhila  ilihali wanafahamu chama kiliwapa mtaji wa kuishi maisha mazuri ya leo.

Mbali na hilo,chama hicho kimekanusha kuwaminyia nafasi ya kutaka kuwania nafasi ya mwenyekiti wa chama ,hali hiyo inachangiwa na ukosefu  wa ujasiri na  uaminifu,ambapo historia chadema imechangia vifo vya watu kadhaa hadi leo ilipofika.

Akizungumza hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika jana katika uwanja wa Mwanga Centa uliopo katika Manispaa ya Kigoma Ujiji Mkoa wa Kigoma ,Mwenyekiti wa Chadema Taifa Freman Mbowe alisema lengo wananchi wa Kigoma wakiunge mkono chama hicho, ili ifikapo 2015 chama kishike dola kwa mujibu wa aganao la UKAWA.

Alisema changamoto inayoikabili kigoma ni sintofahamu ya ukweli wa mambo juu ya chama hicho kilivyosulubiwa tangu kuanzishwa kwake mwaka 1992,ambapo muasisi wa awali  Costa Shinganya anaishi nchini  Malawi baada ya kufilisiwa mali na serikali iliyopo madarakani kwa kubaini kusaidia chama.

“ hawa wote walitia mchanga vitumbua vyao  wenyewe ,subira hawana wakumbuke awali niligharamia maisha ya Kabourou  na mkewe nauli ya kutoka ughaibuni  na kodi ya pango la nyumba ya kuishi nchini zamani hiyo”

“bwana mdogo nilimpa fedha za kujaza fomu ya uchaguzi hadi uchaguzi husika na gari nililompa kwenye chaguzi za mwaka 2005 analo hadi leo ,lakini ni mtovu wa madili ,kamati si chini ya tatu ziliundwa kwa jili yake leo ananunua vijana kujiunga na chama cha ACT” alisema Mwenyekiti huyo.

Akielezea utendaji kazi wa serikali Mbowe alisema,wananchi waondoa itikadi ya uchama na badala yake waelekeze nguvu kuchagua chama makini chenye tija ya kuwaondoa raia katika umaskini uliotopea na wasichague  viongozi wasiowajibika kwa  wahujumu wa maendeleo ya nchi.

Pia alisema sakata la IPTL ni mtandao mpana wa baadhi ya uongozi wa juu wa serikali ambapo kwa pamoja wameshiriki kuhujumu uchumi na rasilimali fedha za umma,ambapo ingesaidia kuwaondoa raia katika adha mbalimbali zinazowakabili.

“uongozi wa ccm umechoka kuongoza shida hawataki kutoka ,msifanye makosa 2015,najua  kigoma mkiamua mapinduzi mnaweza nyie ni chanzo cha mageuzi ya chama kimoja ,nipo radhi kushirikiana na  vyama vyote  hata ACT isipokuwa ccm” alibainisha Mbowe.

Kwa upande wa Kaimu katibu wa chadema Zanzibar Said Mwalimu aliwaonya waislamu wasipende kubebwa katika kujikwamua na umaskini ,badala yake wajitume kutafuta elimu na waweze kufikia mafanikio waliyonayo upande wa pili na kusihi wasikubali kubaguliwa kwa udini.

Thursday, November 13, 2014

RAIS KIKWETE APATA NAFUU NA KUTOKA HOSPITALINI

1 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete  akisindikizwa na Daktari Bingwa Edward Schaeffer kutoka Hospitali ya Johns Hopkins alipokuwa amelazwa baada ya kufanyiwa upasuaji mwishoni mwa wiki iliyopita.Kulia nia Mke wa Rais Mama Salma Kikwete. 2 4 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Daktari Edward Schaeffer muda mfupi baada ya kuruhusiwa kutoka katika hospitali ya Johns Hopkins huko Baltimore, Maryland nchini Marekani ambapo alifanyiwa upasuaji mwishoni mwa wiki iliyopita.(picha na Freddy Maro)

Tuesday, November 11, 2014

"JAMAA AINGIA MSIKITINI NA KUJICHINJA SHINGO,ANUSURIKA KIFO,ALAZWA HOSPITALI"-TABORA

Jamaa huyu ambaye alijiandikisha jina lake kuwa ni Mohammed Athuman huku jina lake kamili ni Ladislaus Joseph ambaye ni mkazi wa Igosha kijiji cha Kabila manispaa ya Tabora,aliondoka nyumbani kwake na kuelekea kijiji kingine kata ya Ikomwa na kufika katika moja ya msikiti wa Kijiji cha Ikomwa ambapo aliingia ndani na kuanza kufanya Ibada ya Sunna majira ya Sala ya Adhuhuri na mara baada ya kukamilisha Swala hiyo alichukua upanga mkali aliokuja nao msikitini hapo na kuanza kujichinja Shingo yake pasipo huruma na baadae kudondoka chini ndani ya msikiti huo ambao baadhi ya waumini walioshuhudia tukio hilo walitimua mbio kuhofia maisha yao.  
Baadhi ya maafisa wa Jeshi la Polisi mkoani Tabora baada ya kupata taarifa ya tukio hilo walikwenda kumchukua na kumkuta bado akiwa hai lakini hali yake haikuwa nzuri na hivyo kumkimbiza hospitali ya mkoa wa Tabora Kitete kwa ajili ya kupatiwa matibabu ambapo tayari sehemu ya Koromeo ilikuwa nje ikiwa imejeruhiwa vibaya.
Hata hivyo mtu huyo ambaye alikuwa hana uwezo wa kusema chochote alipotakiwa kueleza nini sababu ya yeye kujidhuru aliomba kalamu na karatasi na kuandika ujumbe huo wa kutaka msaada wa haraka wa matibabu huku akiwa amelazwa hospitali ya mkoa wa Tabora Kitete.



“WANANCHI WA MUHEZA WAHAMASIKA KUJIUNGA NA MFUKO WA AFYA YA JAMII, ZAIDI YA KAYA 65 ZENYE WANACHAMA 390 WAHAMASIKA NA KUJIUNGA PAPO HAPO”

NHIF MUHEZA Mkuu wa wilaya ya Muheza,Subira Mgalu akisisitiza jambo wakati uzinduzi wa kuhamasisha wananchi kujiunga na mfuko wa afya ya Jamii(CHF) kwenye kata ya Potwe wilayani Muheza uliofanyika leo ambapo zaidi ya kaya 65 zenye wanachama 390 walihamasiska na kujiunga
paoo hapo. 2 3MAAFISA wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF) wahamasika kwenye zoezi hilo na kuamua kuwalipia wanafunzi wa shule za msingi wapatao 80 kwenye Kata ya Potwe wilayani Muheza wanaoishi kwenye mazingira magumu wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha wananchi kujiunga na mfuko wa afya ya Jamii (CHF) wilayani humo ambapo zoezi hilo linaendelea kwa muda wa siku kumi. 4Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) wilayani Muheza George Mhada kushoto akipokea fedha kutoka kwa Diwani wa
Kata ya Potwe katikati Rashid Mdachi  anayeshuhudia ni Mkuu wa wilaya ya Muheza,Subira Mgalu wakati wa uzinduzi wa uhamasishaji wa wananchi kujiunga na mfuko wa afya ya Jamii(CHF) wilayani humo ambapo zaidi ya kaya 65 zenye
wanachama 390 zilifanikiwa kujiunga. 5Msanii wa Maigizo mkoani Tanga Dr.Nyau na swahiba wake wakifanya yao kwenye uzinduzi wa wa Kampeni ya Kuhamasisha wananchi kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) leo uliofanyika kata ya Potwe wilayani Muheza ambapo zaidi ya kaya 65 zenye wanachama 390
zilifanikiwa kujiunga. 7Afisa wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF)kutoka Makao Makuu Isaya Shekifu wa pili kulia akifuatilia uandikishwaji wa wanachama
wapya wa mfuko wa afya ya Jamii(CHF) leo wakati wa uzinduzi wake uliofanyika Kata ya Potwe wilayani Muheza wa kwanza kulia ni Afisa Tabibu wa Zahanati ya Potwe kulikofanyika uzinduzi huo,Dr.Swalehe Mudhihiri ambapo
zaidi ya kaya 65 zenye wanachama 390 zilifanikiwa kujiunga.
8 Mkuu wa wilaya ya Muheza, Subira Mgalu na wafanyakazi wa mfuko wa Bima ya Afya mkoani Tanga,viongozi wa Kata ya Potwe na wanafunzi wa shule ya msingi kwenye Kata hiyo leo ambapo zaidi ya kaya 65 zenye wanachama 390 zilifanikiwa kujiunga. 9 Wananchi kutoka sehemu mbalimbali kwenye Kata ya Potwe
wilayani Muheza wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Muheza ambaye hayupo pichani wakati wa uzinduzi wa uhamasishaji wa wananchi kujiunga na mfuko wa afya ya jamii(CHF) leo ambapo zaidi ya kaya 65 zenye wanachama 390 walihamasika na kujiunga papo hapo.

PROFESA JOHN NKOMA AWAFUNDA MABLOGGER JINSI YA KUANDIKA KWA USAWA HABARI ZA UCHAGUZI

1Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini Tanzania TCRA Profesa John Nkoma akizungumza katika mkutano na Mablogger wakati alipofungua mkutano huo uliojadili jinsi ya kuripoti kwa usawa habari za uchaguzi wa serikali za mitaa, Ubunge na Rais kuanzia mwaka huu mpaka mwakani, Mkutano huo umefanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam ambapo pia viongozi wa Muda wa kuratibu uanzishwaji wa  Chama cha Mablogger wamechaguliwa ambao ni Joachim Mushi, Aron Msigwa mwakilishi kutoka serikalini, Shamimu Mwasha Blog za Biashara, Francis Godwin mablogger wa mikoani, Othman Maulid mwakilishi kutoka Zanzibar, Khadija Khalili, William Malecela na Henry Mdimu ambao wataongoza kwa muda wakati wa mchakato huo mkutano huo umesimamiwa na Mamlaka ya Mawasiliano TCRA.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE)DSC_5572Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Assah Mwambene akifunga rasmi mkutano huo uliofanyika Mlimani City jijini Dar es salaam.10Baadhi ya Malogger wakiwa katika mkutano huo. 9Kutoka kushoto ni Josephat Lukaza wa Lukaza Blog, Shamimu Mwasha wa 8020Fashion na Geofrey Wapamoja Blog wakiwa katika mkutano huo 8Baadhi ya maofisa kutoka TCRA wakiwa katika mkutano huo.  6John Bukuku Mkurugenzi wa Fullshangweblog.com akiwa katika mkutano huo. 5Baadhi maofisa wa TCRAwakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa katika mkutano huo. 4Baadhi maofisa wa TCRAwakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa katika mkutano huo. 3Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini Tanzania TCRA Profesa John Nkoma katikati Mkurugenzi wa Utangazaji TCRA Habbi Gunze ma Aron Msigwa Ofisa Mwandamizi kutoka Idara ya Habari Maelezo wakiwa katika mkutano huo. 2Andrew Kisaka Ofisa Mwanamizi wa Utangazaji TCRA akitoa mada katikamkutano huo.

Friday, November 7, 2014

WANANCHI TABORA WAMUUNGA MKONO MH.MBOWE KWA KUMUAHIDI KUPIGIA KURA YA HAPANA KATIBA PENDEKEZWA

Baadhi ya wananchi wakisalimiana na Mwenyekiti wa Chadema Bw.Freeman Mbowe wakati wa ziara yake Tabora mjini ambapo alizindua Operesheni DELETE CCM ambayo itashirikisha mikoa ya Tabora,Kigoma,Katavi,Morogoro kwa awamu ya kwanza.
Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema akitua katika viwanja vya Town School mjini Tabora kwa ajili ya mkutano wa Operesheni DELETE CCM.

Umati mkubwa wa wananchi wa Tabora mjini ulihudhuria katika mkutano huo
Baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani wa mkoa wa Tabora walipata fursa ya kusalimia wananchi katika mkutano huo
Wananchi walimtaka Bw.Freeman Mbowe achangishe fedha kwa ajili ya kuimarisha utekelezaji wa Operesheni DELETE CCM.
Baadhi ya wananchi wakisukuma gari la Bw.Mbowe kwa maandamano yaliyoziba barabara kadhaa kwa muda mfupi baada ya kumalizika kwa mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Town School Tabora mjini.








SERIKALI ZA VIJIJI, KATA ZAAGIZWA KUDHIBITI VITENDO VYA UTORO SHULENI

Na Allan Ntana, Tabora

UONGOZI wa serikali za vijiji na kata kwa kushirikiana na watendaji wameagizwa kuunda kamati za ufuatiliaji wa wazazi na walezi wanaowazuia watoto wao kwenda shule kwa kuweka utaratibu maalumu utakasaidia kuwabana ili kudhibiti vitendo vya utoro vinavyozidi kukithiri katika shule nyingi wilayani Sikonge mkoani Tabora.

Agizo hilo limetolewa na diwani wa kata ya Kipanga Mashaka Msalangi aliyekuwa mgeni rasmi katika kampeni maalumu ya kutokomeza vitendo vya utumikishwaji watoto wadogo katika kilimo na mifugo suala ambalo limechangia kwa kiasi kikubwa utoro wa wanafunzi walio wengi.

Alisema vitendo vya utoro kwa wanafunzi mashuleni vinazidi kuongezeka jambo ambalo ni hatari sana kwa ustawi wa kizazi kijacho kwa kuwa watoto walio wengi watashindwa kupata elimu ya darasani kwa sababu ya wazazi wao ambao wanaendekeza vitendo vya kuwatumikisha katika mashamba ya tumbaku na kuchunga mifugo tu.

Msalangi alibainisha kuwa agizo hilo kwa viongozi wote wa serikali za vijiji na kata kwa kushirikiana na watendaji wa vijiji na kata hizo limetolewa kwa wakati muafaka, wanapaswa kuandaa mpango kamili utakaosaidia kudhibiti vitendo vya utoro kwa wanafunzi wote wa shule
za msingi na sekondari ili kumaliza tatizo hilo.

‘Hili sio ombi bali ni agizo kwa viongozi wote wa serikali  za vijiji na watendaji wa vijiji na kata hasa katika kata yangu ya Kipanga, ni lazima tuwe na mpango mkakati utakaosaidia kudhibiti utoro kwa watoto wetu kwani wengi wao huacha shule na kwenda kutumikishwa katika kilimo
cha tumbaku na kuchunga mifugo kwa ujira kidogo’ alieleza.

Msalangi aliunga mkono jitihada zinazofanywa na mradi wa PROSPER katika kuhakikisha utumikishwaji watoto katika kata hiyo, vijiji vyake vyote na wilaya ya Sikonge kwa ujumla unakomeshwa kabisa huku akibainisha kuwa jitihada hizo zinazofanywa na mradi huo kwa
kushirikiana na taasisi za TAWLAE na TDFT zinapaswa kuungwa mkono na wadau wote wa maendeleo.
 

Alipongeza mikakati kadha wa kadha inayofanywa na taasisi hizo ikiwemo uanzishwaji wa miradi ya ujasiriamali inayolenga kuwawezesha akina mama na vijana kiuchumi ili kuondokana na umaskini unaochochea utumikishwaji watoto katika kazi hatarishi hususani katika vijiji vya Imalampaka, Ukondamoyo na vinginevyo.

Mkurugenzi wa Sera wa mradi wa PROSPER Bi.Mary Kibogoya alisema ili kumaliza tatizo la utoro mashuleni tunapaswa kutokomeza vitendo vyote vya utumikishwaji watoto katika kilimo cha tumbaku na kuweka sheria ndogo ndogo za kudhibiti utumikishwaji watoto sambamba na kuhakikisha watoto wote wenye umri wa kwenda shule wanapelekwa.

Aidha alisema serikali za vijiji kwa kushirikiana na halmashauri ya wilaya wanapaswa kuhakikisha jamii nzima kuanzia ngazi ya vitongoji, vijiji na kata inashirikishwa katika mikakati yote ya kutokomeza vitendo vya utumikishwaji watoto ambapo alishauri kamati zilizoundwa na mradi huo zifanye kazi ipasavyo bila kuoneana haya.

Awali akisoma taarifa ya utekelezaji majukumu ya mradi, Mratibu wa mradi huo wilayani Sikonge Jesca Michael Kibiki alisema mpaka sasa watoto wapatao 4590 wenye umri kati ya miaka 14-17 wameondolewa kwenye utumikishwaji katika mashamba ya tumbaku sambamba na kuunda kamati 10 za kupinga utumikishwaji, kujengea uwezo wahamasishaji jamii 20, kupunguza umaskini na kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia shuleni.

Thursday, November 6, 2014

RAIS KIKWETE AAPISHA MAKATIBU WAKUU, MABALOZI NA MAKATIBU TAWALA WAPYA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

KIKWETE AAPISHA WAKUU WA MIKOA WAPYARais Jakaya Mrisho Kikwete akumuapisha Dkt
Yohana Budeba kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 6, 2014PICHA NA IKULU

3Rais Jakaya Mrisho Kikwete  akumpa vitendea kazi Dkt
Yohana Budeba kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 6, 2014
4Rais Jakaya Mrisho Kikwete akumuapisha
Injinia Mbogo Futakamba  kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maji ikulu jijini
Dar es salaam leo Novemba 6, 2014 5Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpa vitendea kazi
Injinia Mbogo Futakamba  kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maji ikulu jijini
Dar es salaam leo Novemba 6, 2014 7 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akumuapisha na kumpa vitendea kazi Dkt
Donan Mmbando  kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii
Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 6, 2014 8 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpa vitendea kazi Dkt
Donan Mmbando  kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii
Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 6, 2014 10Rais Jakaya Mrisho Kikwete akumuapisha
Mhe Jack Mugendi Zoka kuwa Balozi wa Tanzania nchini Canada Ikulu
jijini Dar es salaam leo Novemba 6, 2014 11Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpa vitendea kazi
Mhe Jack Mugendi Zoka kuwa Balozi wa Tanzania nchini Canada Ikulu
jijini Dar es salaam leo Novemba 6, 2014 12Rais Jakaya Mrisho Kikwete akumuapisha
Mhe Charles Pallangyo kuwa Katibu Tawala wa mkoa wa Geita  Ikulu
jijini Dar es salaam leo Novemba 6, 2014 13Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpa vitendea kazi
Mhe Charles Pallangyo kuwa Katibu Tawala wa mkoa wa Geita  Ikulu
jijini Dar es salaam leo Novemba 6, 2014 15 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akumuapisha
Bw, Adoh Stephen Mapunda kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Ikulu
jijini Dar es salaam leo Novemba 6, 2014 16 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpa vitendea kazi
Bw, Adoh Stephen Mapunda kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Ikulu
jijini Dar es salaam leo Novemba 6, 2014 18Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni
Sefue wakiwa katika picha ya pamoja na Makatibu wakuu na Makatibu
Tawala wa Mikoa wapya baada ya kuwaapisha Ikulu jijini Dar es salaam
leo. 19Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Balozi mpya wa Tanzania Nchini
Canada Mhe. Jack Mugendi Zoka , pamoja na mabalozi wengine kutoka
kushoto Balozi Mbelwa Kairuki (Mkurugenzi wa Idara ya Asia na
Austrlia). Balozi Simba yahya (Mkurugenzi dara ya Mashariki ya Kati na
Balozi Celestine Mushi, Mkurugenzi wa Idara ya Uhusiano wa Kimataifa. 20 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimuapisha Dkt Ibrahim Hamisi Msangi
kuwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi leo Ikulu jijini Dar es salaam 21Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimuapisha Mhe Halima Omary Denengo
kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara leo Ikulu jijini Dar es salaam
22  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimuapisha Mhe John Vianney Mongella

kuwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi leo Ikulu jijini Dar es salaam
23Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimuapisha Mhe Samwel William
Shellukindo kuwa Balozi na Msaidi wa Rais Masuala ya Diplomasia leo
Ikulu jijini Dar es salaam