Na Allan Ntana, Tabora
UONGOZI wa serikali za vijiji na kata kwa kushirikiana na watendaji wameagizwa kuunda kamati za ufuatiliaji wa wazazi na walezi wanaowazuia watoto wao kwenda shule kwa kuweka utaratibu maalumu utakasaidia kuwabana ili kudhibiti vitendo vya utoro vinavyozidi kukithiri katika shule nyingi wilayani Sikonge mkoani Tabora.
Agizo hilo limetolewa na diwani wa kata ya Kipanga Mashaka Msalangi aliyekuwa mgeni rasmi katika kampeni maalumu ya kutokomeza vitendo vya utumikishwaji watoto wadogo katika kilimo na mifugo suala ambalo limechangia kwa kiasi kikubwa utoro wa wanafunzi walio wengi.
Alisema vitendo vya utoro kwa wanafunzi mashuleni vinazidi kuongezeka jambo ambalo ni hatari sana kwa ustawi wa kizazi kijacho kwa kuwa watoto walio wengi watashindwa kupata elimu ya darasani kwa sababu ya wazazi wao ambao wanaendekeza vitendo vya kuwatumikisha katika mashamba ya tumbaku na kuchunga mifugo tu.
Msalangi alibainisha kuwa agizo hilo kwa viongozi wote wa serikali za vijiji na kata kwa kushirikiana na watendaji wa vijiji na kata hizo limetolewa kwa wakati muafaka, wanapaswa kuandaa mpango kamili utakaosaidia kudhibiti vitendo vya utoro kwa wanafunzi wote wa shule
za msingi na sekondari ili kumaliza tatizo hilo.
‘Hili sio ombi bali ni agizo kwa viongozi wote wa serikali za vijiji na watendaji wa vijiji na kata hasa katika kata yangu ya Kipanga, ni lazima tuwe na mpango mkakati utakaosaidia kudhibiti utoro kwa watoto wetu kwani wengi wao huacha shule na kwenda kutumikishwa katika kilimo
cha tumbaku na kuchunga mifugo kwa ujira kidogo’ alieleza.
Msalangi aliunga mkono jitihada zinazofanywa na mradi wa PROSPER katika kuhakikisha utumikishwaji watoto katika kata hiyo, vijiji vyake vyote na wilaya ya Sikonge kwa ujumla unakomeshwa kabisa huku akibainisha kuwa jitihada hizo zinazofanywa na mradi huo kwa
kushirikiana na taasisi za TAWLAE na TDFT zinapaswa kuungwa mkono na wadau wote wa maendeleo.
Alipongeza mikakati kadha wa kadha inayofanywa na taasisi hizo ikiwemo uanzishwaji wa miradi ya ujasiriamali inayolenga kuwawezesha akina mama na vijana kiuchumi ili kuondokana na umaskini unaochochea utumikishwaji watoto katika kazi hatarishi hususani katika vijiji vya Imalampaka, Ukondamoyo na vinginevyo.
Mkurugenzi wa Sera wa mradi wa PROSPER Bi.Mary Kibogoya alisema ili kumaliza tatizo la utoro mashuleni tunapaswa kutokomeza vitendo vyote vya utumikishwaji watoto katika kilimo cha tumbaku na kuweka sheria ndogo ndogo za kudhibiti utumikishwaji watoto sambamba na kuhakikisha watoto wote wenye umri wa kwenda shule wanapelekwa.
Aidha alisema serikali za vijiji kwa kushirikiana na halmashauri ya wilaya wanapaswa kuhakikisha jamii nzima kuanzia ngazi ya vitongoji, vijiji na kata inashirikishwa katika mikakati yote ya kutokomeza vitendo vya utumikishwaji watoto ambapo alishauri kamati zilizoundwa na mradi huo zifanye kazi ipasavyo bila kuoneana haya.
Awali akisoma taarifa ya utekelezaji majukumu ya mradi, Mratibu wa mradi huo wilayani Sikonge Jesca Michael Kibiki alisema mpaka sasa watoto wapatao 4590 wenye umri kati ya miaka 14-17 wameondolewa kwenye utumikishwaji katika mashamba ya tumbaku sambamba na kuunda kamati 10 za kupinga utumikishwaji, kujengea uwezo wahamasishaji jamii 20, kupunguza umaskini na kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia shuleni.

No comments:
Post a Comment