Pages

KAPIPI TV

Tuesday, November 11, 2014

PROFESA JOHN NKOMA AWAFUNDA MABLOGGER JINSI YA KUANDIKA KWA USAWA HABARI ZA UCHAGUZI

1Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini Tanzania TCRA Profesa John Nkoma akizungumza katika mkutano na Mablogger wakati alipofungua mkutano huo uliojadili jinsi ya kuripoti kwa usawa habari za uchaguzi wa serikali za mitaa, Ubunge na Rais kuanzia mwaka huu mpaka mwakani, Mkutano huo umefanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam ambapo pia viongozi wa Muda wa kuratibu uanzishwaji wa  Chama cha Mablogger wamechaguliwa ambao ni Joachim Mushi, Aron Msigwa mwakilishi kutoka serikalini, Shamimu Mwasha Blog za Biashara, Francis Godwin mablogger wa mikoani, Othman Maulid mwakilishi kutoka Zanzibar, Khadija Khalili, William Malecela na Henry Mdimu ambao wataongoza kwa muda wakati wa mchakato huo mkutano huo umesimamiwa na Mamlaka ya Mawasiliano TCRA.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE)DSC_5572Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Assah Mwambene akifunga rasmi mkutano huo uliofanyika Mlimani City jijini Dar es salaam.10Baadhi ya Malogger wakiwa katika mkutano huo. 9Kutoka kushoto ni Josephat Lukaza wa Lukaza Blog, Shamimu Mwasha wa 8020Fashion na Geofrey Wapamoja Blog wakiwa katika mkutano huo 8Baadhi ya maofisa kutoka TCRA wakiwa katika mkutano huo.  6John Bukuku Mkurugenzi wa Fullshangweblog.com akiwa katika mkutano huo. 5Baadhi maofisa wa TCRAwakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa katika mkutano huo. 4Baadhi maofisa wa TCRAwakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa katika mkutano huo. 3Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini Tanzania TCRA Profesa John Nkoma katikati Mkurugenzi wa Utangazaji TCRA Habbi Gunze ma Aron Msigwa Ofisa Mwandamizi kutoka Idara ya Habari Maelezo wakiwa katika mkutano huo. 2Andrew Kisaka Ofisa Mwanamizi wa Utangazaji TCRA akitoa mada katikamkutano huo.

No comments: