Jamaa huyu ambaye alijiandikisha jina lake kuwa ni Mohammed Athuman huku jina lake kamili ni Ladislaus Joseph ambaye ni mkazi wa Igosha kijiji cha Kabila manispaa ya Tabora,aliondoka nyumbani kwake na kuelekea kijiji kingine kata ya Ikomwa na kufika katika moja ya msikiti wa Kijiji cha Ikomwa ambapo aliingia ndani na kuanza kufanya Ibada ya Sunna majira ya Sala ya Adhuhuri na mara baada ya kukamilisha Swala hiyo alichukua upanga mkali aliokuja nao msikitini hapo na kuanza kujichinja Shingo yake pasipo huruma na baadae kudondoka chini ndani ya msikiti huo ambao baadhi ya waumini walioshuhudia tukio hilo walitimua mbio kuhofia maisha yao. |
No comments:
Post a Comment