Pages

KAPIPI TV

Friday, November 14, 2014

MBOWE ANENA KIGOMA

Na Magreth Magosso,Kigoma
.
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimewalaumu waliokuwa wakishika nyadhifa ya Katibu mkuu wa chama  hicho awali Zitto Kabwe na Amani Kabourou ambye kwa sasa ni mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM Mkoa wa Kigoma ,kwa kile walichodai hawana fadhila  ilihali wanafahamu chama kiliwapa mtaji wa kuishi maisha mazuri ya leo.

Mbali na hilo,chama hicho kimekanusha kuwaminyia nafasi ya kutaka kuwania nafasi ya mwenyekiti wa chama ,hali hiyo inachangiwa na ukosefu  wa ujasiri na  uaminifu,ambapo historia chadema imechangia vifo vya watu kadhaa hadi leo ilipofika.

Akizungumza hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika jana katika uwanja wa Mwanga Centa uliopo katika Manispaa ya Kigoma Ujiji Mkoa wa Kigoma ,Mwenyekiti wa Chadema Taifa Freman Mbowe alisema lengo wananchi wa Kigoma wakiunge mkono chama hicho, ili ifikapo 2015 chama kishike dola kwa mujibu wa aganao la UKAWA.

Alisema changamoto inayoikabili kigoma ni sintofahamu ya ukweli wa mambo juu ya chama hicho kilivyosulubiwa tangu kuanzishwa kwake mwaka 1992,ambapo muasisi wa awali  Costa Shinganya anaishi nchini  Malawi baada ya kufilisiwa mali na serikali iliyopo madarakani kwa kubaini kusaidia chama.

“ hawa wote walitia mchanga vitumbua vyao  wenyewe ,subira hawana wakumbuke awali niligharamia maisha ya Kabourou  na mkewe nauli ya kutoka ughaibuni  na kodi ya pango la nyumba ya kuishi nchini zamani hiyo”

“bwana mdogo nilimpa fedha za kujaza fomu ya uchaguzi hadi uchaguzi husika na gari nililompa kwenye chaguzi za mwaka 2005 analo hadi leo ,lakini ni mtovu wa madili ,kamati si chini ya tatu ziliundwa kwa jili yake leo ananunua vijana kujiunga na chama cha ACT” alisema Mwenyekiti huyo.

Akielezea utendaji kazi wa serikali Mbowe alisema,wananchi waondoa itikadi ya uchama na badala yake waelekeze nguvu kuchagua chama makini chenye tija ya kuwaondoa raia katika umaskini uliotopea na wasichague  viongozi wasiowajibika kwa  wahujumu wa maendeleo ya nchi.

Pia alisema sakata la IPTL ni mtandao mpana wa baadhi ya uongozi wa juu wa serikali ambapo kwa pamoja wameshiriki kuhujumu uchumi na rasilimali fedha za umma,ambapo ingesaidia kuwaondoa raia katika adha mbalimbali zinazowakabili.

“uongozi wa ccm umechoka kuongoza shida hawataki kutoka ,msifanye makosa 2015,najua  kigoma mkiamua mapinduzi mnaweza nyie ni chanzo cha mageuzi ya chama kimoja ,nipo radhi kushirikiana na  vyama vyote  hata ACT isipokuwa ccm” alibainisha Mbowe.

Kwa upande wa Kaimu katibu wa chadema Zanzibar Said Mwalimu aliwaonya waislamu wasipende kubebwa katika kujikwamua na umaskini ,badala yake wajitume kutafuta elimu na waweze kufikia mafanikio waliyonayo upande wa pili na kusihi wasikubali kubaguliwa kwa udini.

No comments: