Pages

KAPIPI TV

Friday, October 24, 2014

UKARABATI NA UPANUZI WA UWANJA WA NDEGE WA MPANDA WAKAMILIKA


??????????????????????????????? Meneja wa Uwanja wa ndege wa Mpanda,  Mkoa wa Katavi Seneti Lyatuu akiwaonesha timu ya ukaguzi wa miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango upanuzi wa uwanja wa ndege wa Mpanda. Nyuma yake (mwenye suti nyeusi) ni Mhandisi Caroline Mntambo kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndenge Tanzania, Makao Makuu, Dar es Salaam. ??????????????????????????????? Meneja wa Uwanja wa Ndege wa Mpanda  Bw.  Seneti Lyatuu akifafanua jambo wakati timu ya ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango walipotembelea kiwanja hicho. ??????????????????????????????? Timu ya ukaguzi ikitazama barabara ya kutua na kurukia ndege katika uwanja wa ndege wa Mpanda ??????????????????????????????? Barabara ya kutua na kurukia ndege katika uwanja wa ndege wa Mpanda, mkoani Katavi ???????????????????????????????Mhandisi Caroline Mntambo (mwenye suti nyeusi) akifafanua jambo kwa timu ya wakaguzi kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango. Uwanja wa ndege wa Mpanda umekarabatiwa na kupanuliwa hivyo , kuwa  katika hali nzuri kwa matumizi ya ndege zote za binafsi na biashara
PICHA NA JOYCE MKINGA
………………………………………………………………….
Na Mwandishi wetu, Mpanda
Serikali imekamilisha ukarabati na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Mpanda, mkoa wa Katavi na hivyo kuufanya uwe wa kiwango kizuri tayari kwa kutumika kwa ndege za binafsi na biashara.

Meneja wa Uwanja wa Ndege wa Mpanda, Bw Seneti Lyatuu alisema uwanja huo umeboreshwa na hivyo, unaweza kutumika kutua na kuruka ndege za kiwango cha kati na hata zile ndege kubwa zinaweza kutua kwa dharura.

Aliiambia timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango iliyotembelea uwanja huo mwishoni mwa wiki kuwa uwanja huo umeongeza idadi ya wasafiri mara dufu kutokana na ukarabati na upanuzi uliofanyika.

Meneja wa Uwanja huo alisema idadi ya abiria imeongezeka kutoka abiria 285 mwaka 2009 hadi 2,390 mwaka 2013/14.

Bw. Lyatuu alisema kuwa uwanja huo umekarabatiwa na barabara ya kuruka na kutua ndege imerefushwa kwa kiwango cha lami kutoka urefu wa mita 1,500 na upana wa mita 30 hadi kufikia urefu wa mita 1,820 na upana wa mita 30.

Alisema maeneo mengine yaliyokarabatiwa ni pamoja na kujenga uzio na mifereji ya kupitishia maji ya mvua.

“Kwa sasa kiwanja kipo vizuri na ndege za aina zote zinaweza kutua hapa uwanjani hivyo, tunawakaribishwa wadau wote kuutumia uwanja huu” alisema Bw Lyatuu.

Eng. Caroline Mntambo kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Makao Makuu Dar es Salaam alisema kuwa tayari wamealika mashirika ya ndege yanayofanya biashara hapa nchini kuanzisha safari katika uwanja huo. Mashirika hayo ni pamoja na ATC, Precision Air, Fast jet   nk.

Eng Mntambo alisema kwa sasa shirika la ndege la Auric Air tayari limeanzisha safari za kwenda Mpanda ambapo linasafirisha abiria kutoka Dar- Mpanda – Mwanza mara tatu kwa wiki.

Alisema ndege zingine zinazotua uwanjani hapo kwa sasa ni pamoja na za UNHCR, ndege za kukodi na ndege za serikali.

IDADI YA WAJASILIAMALI YAONGEZEKA TABORA

Baadhi ya wakazi wa Tabora mjini wakionekana katika hali ya utafutaji wa riziki.
Na Mwandishi wetu Tabora mjini.
Kumekuwa na dalili za waziwazi kuwa idadi ya wajasiliamali imeendelea kuongezeka Tabora mjini hali inayotokana na kuongezeka kwa watu wanaofanya shughuli mbalimbali za kutafuta riziki zao ikiringanishwa na miaka mitatu iliyopita.

Ushahidi wa kuongezeka kwa makundi ya wajasiliamali ni pale inapodhihirika kuwa watu wengi wanaonekana kufanya shughuli zao binafsi za kuwaongezea kipato huku ikibainika kuwa kumekuwepo mzunguuko wa pesa kila kona na kuwafanya watu kuwa katika hekaheka za mara kwa mara za utafutaji.

Biashara ndogondogo zinaendelea kushamili,huku ikionesha kuwa idadi kubwa ya wanawake wamekuwa wakijishughulisha kuliko idadi ya wanaume.

Ongezeko na huduma za taasisi za kifedha kama mabenki ambazo zimeonesha hali ya kutoa mikopo kwa wajasiliamali na kuwafanya waongeze juhudi katika kujitafutia riziki zao.

Serikali ya mkoa wa Tabora imeacha milango wazi kwa wajasiliamali kuendesha shughuli zao bila kubughudhiwa na mtu yeyote.  


TAJI LA MISS TANZANIA 2014 KUUNDIWA TUME!!!

 Mshindi wa taji la Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Mtemvu huenda akavuliwa taji hilo kama serikali kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na Baraza lake la Sanaa la Taifa ambalo ndio watoaji vibali vya mashindano hayo na kusimamia dhima na maudhui ya shindano hilo pamoja na kusimamia maadili yake itaingilia kati moja kwa moja suala hilo kwa kuunda tume maalum ya kulichunguza na kutafuta ukweli halisi wa umri wa mrembo huyo na kutoa mapendekezo ya ama Sitti avuliwe taji hilo na kuvikwa Mshindi wa pili, Lillian Kamazima (pichani kulia) ama vinginevyo. Kushoto ni Jihhan Dimachk aliyeshika nafasi ya tatu.
 
Shindano la Miss Tanzania 2014 lilifanyika katika ukumbi wa Mlimani City,jijini Dar es Salaam Oktoba 11,  na Sitti Mtemvu kuvikwa taji hilo na kuanza utata wa umri wake halisi licha ya kuanika hadharani cheti chake cha kuzaliwa ambacho wadau wa sanaa ya urembo kukitilia shaka na kushindwa kuoanisha na pasi yake ya kusafiria na leseni ya udereva iliyotolewa nchini Marekani. http://mrokim.blogspot.com/2014/10/taji-la-miss-tanzania-2014-kuundiwa-tume.html

KAMATI YA BUNGE YA ARDHI, MALIASILI NA MAZINGIRA YATEMBELEA ENEO LA TANGANYIKA PAKERS AMBAKO NHC INATEKELEZA MRADI WA NYUMBA WA KAWE CITY

SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFAKaimu Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Bw. Felix Maagi akiiongoza Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira wakati ilipotembelea eneo la mradi wa nyumba ambao unatarajiwa kuanza katika uwanja wa kulenga shabaha wa jeshi la wananchi Kunduchi, baada ya makubaliano kati ya jeshi la wananchi na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC). Kamati hiyo ikiongozwa na mwenyekiti wake na jimbo la Kahama Mbunge Mh. James Lembeli na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. Profesa Anna Tibaijuka ilitembelea eneo hilo ili kujiridhisha na kujionea hali halisi na kupata maelezo ya kina kabla ya kuanza kutekelezwa kwa mradi huo. Kulia ni Mjube wa Kamati hiyo Mh. Hamud Jumaa na Mbunge wa jimbo la Kibaha Vijijini, kulia ni James Lembeli Mbunge wa Kahama na Mwenyekiti wa kamati hiyo.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM) 2Isaack Peter Mkurugenzi wa Ubunifu Shirika la Nyumba la Taifa NHC akielekeza jambo wakati alipokuwa akionyesha eneo hilo kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. Profesa Anna Tibaijuka na wajumbe wa kamati hiyo wakati alipotembelea eneo hilo huku Kunduchi. 3Mjumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi, Mazingira na Maliasili Mh. Hery Shekifu akifafania jambo huku Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. Profesa Anna Tibaijuka na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Mh. James Lembeli wakimsikililiza 4Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Mh. James Lembeli akizungumza jambo wakati kamati hiyo ilipotembelea eneo la kulenga shabaha la jeshi Kunduchi, kulia ni Mama Zakhia Megji Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa Shirika la Nyumba NHC na kushoto ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. Profesa Anna Tibaijuka 5Baadhi ya watendaji na maofisa wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC wakiwa katika picha ya pamoja kwenye uwanja wa Kulenga Shabaha wa jeshi Kunduchi ambao kwa sasa matumizi yake yanabadilisha na kuwa mradi wa nyumba za Shirika la Nyumba la NHC. 7Baadhi ya wajumbe wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi , Maliasili na Mazingira wakishuka kwenye gari mara baada ya kuwasili katika eneo la Tanganyika Pakers ambapo mradi wa Kawe City unatarajiwa kuazishwa na shirika hilo la NHC. 8Huu ndiyo uwanja wa Kulenga Shabaha wa jeshi Kunduchi mahali ambapo sasa panaanzishwa mradi wa nyumba za NHC. 9Waziri wa Ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi Mh. Profesa Anna Tibaijuka akishuka kwenye gari mara baada ya kuwasili katika eneo la Tanganyika Pakers Kawe jijini Dar es salaam. 10Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira na mbunge wa Kahama Mh. James Lembeli akishuka kwenye gari katika eneo la Tanganyika Pakers mahali ambapo patatekelezwa mradi wa Kawe City unaofanywa na Shirika la Nyumba la Taifa NHC. 12Waziri wa Ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi Mh. Profesa Anna Tibaijuka akizungumza na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Mh. James Lembeli katikati ni mjumbe wa kamati hiyo na Mbunge wa jimbo la Lushoto Mh. Hery Shekifu 13Isaack Peter Mkurugenzi wa Ubunifu Shirika la Nyumba la Taifa NHC akendelea kutoa maelezo kwa kamati hiyo wakati ilipotembelea katika eneo la Tanganyika Pakers Kawe. 14Wajumbe wa kamati hiyo wakipata maelezo kabla ya kuanza ziara yao leo katika makao makuu ya shirika la Nyumba la Taifa NHC Upanga jijini Dar es salaam. 15Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Mh. James Lembeli akizungumza wakati kamati hiyo ilipokuwa ikipata maelezo ya awali kabla ya kutembelea maeneo yatakapotekelezwa miradi hiyo mikubwa ya makazi , Kushoto ni Waziri wa Ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi Mh. Profesa Anna Tibaijuka na kutoka kulia ni Mh. Mary Mwanjelwa mjumbe wa kamati hiyo na mbunge wa viti maalum Mbeya mjini na Mh. Abdulkarim Shah Makamu mwenyekiti wa kamati hiyo na na Mbunge wa Mafia. 17Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Nyumba la NHC Mh. Zakhia Megji, Bw. Felix Maagi Kaimu Mkurugenzi wa NHC na Mbunge wa jimbo la Ubungo na mjumbe wa kamati hiyo Mh. John Mnyika ambaye naonekana akitoa mchango wake wakati wa wajumbe hao walipokuwa wakipata taarifa ya awali..

Thursday, October 23, 2014

PRESIDENT KIKWETE OPENS TANZANIA-CHINA BUSINESS FORUM IN BEIJING


D92A6612President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete pose for a group photograph with Tanzania and Chinese delegates who attended the Tanzania and China Business and Investment Forum that was held at Diaoyutai State Guest House in Beijing this morning. President Kikwete who officiated at the opening of the forum, is in working visit in China at the invitation of the Chinese President Xi Jinping.(photo by Freddy Maro)

WAZIRI UMMY MWALIMU ATAKA HALMASHAURI YA KINONDONI KUSIMAMIA SHERIA ZA MAZINGIRA

WAZIRI UMMY MWALIMUMkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Mhandisi Mussa Natty(kushoto) akizungumza na Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Ummy Mwalimu wakati wa ziara ya kujifunza masuala ya usimamizi wa taka zinazozalishwa katika halmashauri hiyo.
2Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Mhandisi Mussa Natty (kushoto) akizungumza na Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Ummy Mwalimu wakati wa ziara ya kujifunza masuala ya usimamizi wa taka zinazozalishwa katika halmashauri hiyo.Kulia ni wataalamu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais na watendaji wa halmashauri hiyo.
3Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Ummy Mwalimu, akizungumza na watendaji wa kata za manispaa ya Kinondoni(hawapo pichani) wakati wa ziara hiyo.Kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Mhandisi Mussa Natty.
4Badhi ya watendaji wa kata mbalimbali za manispaa ya Kinondoni wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Ummy Mwalimu, wakati alipotembelea kujifunza masuala ya usimamizi wa taka zinazozalishwa katika halmashauri hiyo.
5Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Ummy Mwalimu (katikati) akiongozwa na Mwenyekiti wa soko la Tandale, Sultan Kiumbo kuingia kwenye ofisi ya soko hilo, wakati alitembelea kujifunza changamoto za mazingira zinazolikabili soko hilo.
6Mwenyekiti wa soko la Tandale, Sultan Kiumbo, akmueleza jambo Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Ummy Mwalimu, wakati alipotembelea soko hilo kujifunza changamoto za mazingira.
7 Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Ummy Mwalimu, akisalimiana na mama lishe katika soko la Tandale jijini Dar es Salaam, wakati alipotembelea soko hilo kujifunza changamoto za mazingira.
8Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Ummy Mwalimu, akizugumza na muuza mbogamboga kujua jinis anavyoshughulikia taka anazozalisha kwenye soko la Tandale jijini Dar es Salaam, wakati alipotembelea soko hilo kujifunza changamoto za mazingira.
9Mwenyekiti wa soko la Tandale, Sultan Kiumbo, akimuonesha Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Ummy Mwalimu, mabaki ya matunda yalitupwa, wakati alipotembelea soko hilo kujifunza changamoto za mazingira.
Picha zote na Hussein Makame-MAELEZO

MKE WA RAIS MAMA SALMA KIKWETE NA MATUKIO YA PICHA KATIKA ZIARA YA RAIS DR. JAKAYA KIKWETE NCHINI CHINA

1Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea ua kutoka kwa mfanyakazi wa Hoteli ya Diaoyutai iliyoko Beijing mara baada ya kuwasili hotelini hapo. Mama Salma ameambatana na mumewe Rais Dkt. Jakaya Kikwete ambaye amewasili nchini China tarehe 21.10.2014 kwa ziara ya kiserikali. 2Rais Dkt. Jakaya Kikwete akiwapungia wafanyakazi wa Hoteli ya Diaoyutai ya mjini Beijing mara baada ya kuwasili nchini China kwa ziara ya kikazi tarehe 21.10.2014. 3Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa pamoja na Bwana Yang Hua, Mmoja wa viongozi wakuu wa China National Offshore Oil Corporation (CNOOC), wakisikiliza kwa makini maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Mwenyekiti wa Shirika hilo Bwana Wang Yilin kwa Rais Dkt. Jakaya Kikwete alipotembelea makao makuu ya Shirika hilo yaliyoko Beijing nchini China tarehe 22.10.2014. Shirika hilo hujishughulisha na utafiti wa mafuta na gesi baharini, uchimbaji na uuzaji wa maliasili hizo. 4Rais Dkt. Jakaya Kikwete na Mwenyekiti wa China National Offshore Oil Corporation Bwana Wang Yilin wakizindua rasmi mtambo mpya wa utafutaji wa mafuta na gesi baharini, Uzinduzi huo ulifanyika kwenye Makao Makuu ya Shirika hilo huko Beijing tarehe 22.10.2014. 5Rais Dkt. Jakaya Kikwete akiongoza ujumbe wa Tanzania unaozuru nchini China wakiangalia vifaa mbalimbali vinavyotumiwa na Shirika la  CNOOC la China katika kazi ya utafutaji wa mafuta na gesi baharini wakati walipotembelea Makao Makuu ya Shirika hilo huko Beijing tarehe 22.10.2014. 6Rais Dkt. Jakaya Kikwete akishirikiana na Mkewe Mama Salma Kikwete na Professa Li Songshan (kushoto kwa Rais Kikwete), Mwanzilishi wa Kijiji cha Sanaa cha Afrika kuondoa kitambaa ikiwa ni ishara ya kufungua rasmi kijiji hicho kilichopo katika wilaya ya Songzhuang nchini China tarehe 22.10.2014. 7 8 Rais Dkt. Jakaya Kikwete akiangalia baadhi ya ngoma za asili ya Afrika zilizokuwa zikipingwa na vijana wa kichina mara baada ya ufunguzi rasmi wa kituo cha sanaa za Afrika huko Songzhuang tarehe 22.10.2014. 9Rais Dkt. Jakaya Kikwete akiandika kumbukumbu yake katika kitambaa maalum mara baada ya kuzindua rasmi Kijiji cha sanaa za Afrika. Mke wa Rais Mama Salma Kikwete anaonekana wa kwanza kushoto akifuatiwa na Professa Li Singshan. Kulia kwa Rais Kikwete ni Dkt. Han Rong, Mke wa Professa Li na Mwanzilishi mwenza wa Kijiji hicho na wa kwanza kushoto ni Bwana Joseph Kahama. 10Rais Dkt. Jakaya Kikwete akiandika kumbukumbu yake katika kitambaa maalum mara baada ya kuzindua rasmi Kijiji cha sanaa za Afrika. Mke wa Rais Mama Salma Kikwete anaonekana wa kwanza kushoto akifuatiwa na Professa Li Singshan. Kulia kwa Rais Kikwete ni Dkt. Han Rong, Mke wa Professa Li na Mwanzilishi mwenza wa Kijiji hicho na wa kwanza kushoto ni Bwana Joseph Kahama. 11Waanzilishi wa Kijiji cha Sanaa za Afrika Professa Li Songshan na Mke wake Dkt. Han Rong wakimkabidhi zawadi ya picha Rais Dkt. Jakaya Kikwete na Mke wake mara baada ya ufunguzi rasmi wa kijiji hicho tarehe 22.10.2014.
PICHA NA JOHN  LUKUWI.

ADHA YA MAJI YAENDELEA KUWATESA WAKAZI WA KIJIJI CHA SONGAMBELE HALMASHAURI YA NSIMBO WILAYANI MLELE


MAAMUZI MADIWAN
Madiwani na watalaam wa Halmashauri ya Nsimbo wakijadili mstakabali wa maendeleo ya Halmashauri yao Nsimbo,pamoja na kujadili masuala ya elimu, Afya, Miundo mbinu ya barabara,utawala,na maengineyo lakini suala la maji lilichukua nafasi ya kipekee katika kikao hicho cha baraza la madiwani kilichomalizika mwishoni mwa wiki iiliyo
(Picha zote Kibada Kibada -Nsimbo Mlele Katavi).
???????????????????????????????
Mama akisukuma maji kwenye kisima kifupi kilichopo hapo huku akina mama wengine na watoto wakisubiri zamu yao ifike ili waweze kuchota maji  ambayo yanatoka kidogokidogo kwenye kisima hicho hapo madumu yanaonekana hayana maji,  dumu  moja kujaa inawachukua zaidi ya saa, hivyo kuwafanya watumie muda mwingi kutafuta   maji badala ya kufanya shughuli nyingine za maendeleo.
……………………………………………….
 
Na Kibada Kibada –Nsimbo Mlele
Wakazi wa Songambele Halmashauri ya Nsimbo Wilayani Mlele wanakabiliwa na Changamoto ya uhaba wa maji kufuatia visima vifupi vilivyopo kutokuwa maji ya kutosha.
 
Hali  hiyo ya uhaba wa maji kwa baadhi ya Vijiji vya Kata ya Nsimbo na maeneo mengine ya Halmashauri hiyo  inayowafanya akina mama na watoto kuamka  kila siku alfajiri  majira saa kumi usiku kwenda kutafuta maji kwa au  kusubiria  maji  kwenye visim vifupi vilivyopo ambavyo navyo havitoi maji ya kutosha hivyo kutumia muda mrefu kutafuta na kukosa muda wa kufanya shughuli nyingine za maendeleo.
 
Akizungumzia  hali ilivyotete  kuhusu upatikanaji wa maji katika Kijiji  cha Songambele  na Kata ya Nsimbo kwa ujumla Afisa Mtendaji wa Kata ya Nsimbo Wilbroad Milala anasema kwa kweli hapo maji ni shida kubwa kwa wakazi wa hapo.
 
Milala anasema hata visima vilivyopo havitoi maji ya kutosha wakati mwingine kama msimu huu wa kiangazi maji hukata hata miezi miwili bila kutoa maji hali inayofanya wakazi hao hasa akina mama na watoto kufuata maji kwenye mbuga umbali wa takribani kilometa tatu hadi nne maji amabyo siyo safi wala salama.
 
Kufuatia kuwepo kwa changamoto hiyo ya Maji wawakilishi wa wananchi ambao ni madiwani kupitia kwenye vikao vya baraza la madiwani suala la maji lilionekana kuchukua nafasi ya kipekee kuzungumzia ikiwa ni pamoja na kutafuta mbinu za kulipatia ufumbuzi.
 
Akiongea katika kikao cha Baraza la madiwani kwa nyakati tofauti Mjini Nsimbo Diwani wa Kata ya NsimboMichael Kasanga, Diwani wa Kata ya Mtapenda Eliezer Fyula,walieleza kuwa lazima hatua zichukuliwe kwa haraka ili kulipatia ufumbuzi suala la upatikanaji wa maji kwa wakazi wa Halamshauri hiyo hasa maeneo yale yenye visima vifupi vichimbwe visima virefu.
 
Wakaeleza kuwa pia visima vinapoharibika taarifa iwe inatolewa mapema kwenye Idara ya Maji ili kuona namna ya kuweza kulipatia ufumbuzi pale panapo wezeakana kama kununua vifaa vya ukarabati wa pump.
 
Awali Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu na Maji  Raphael Kalinga akiwasilisha taarifa ya Kamati yake alieleza mikakati inayochukuliwa na halmashauri ili kukabiliana na changamoto ya uhaba wa maji ikiwa ni pamoja na kutenga fedha kupitia bajeti zake na fedha kutoka kwenye mifuko ya maji ili kusaidia upatikanaji wa maji ikiwa pia na kuomba ufadhili kutoka kwa wahisani mbalimbali kusaidia suala la maji.
 
Aidha aliwashauri madiwani kuwahamasisha wananchi kuanzisha kamati za mifuko ya maji ili fedha inayopatikana iwe inasaidia katika matengenezo madogo madogo pindi pump za visima vya maji vinapo haribika fedha hizo zitasaidia ukarabati mdogo mdogo.
 
Katika hatua nyingine Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Nsimbo limemwagiza Kaimu Mhandisi wa Mji katika Halmashauri  Enock Msengi kuhakikisha anapoondoka awe anakaimisha ofisi kwa mwenzake anayekuwa ofisini kuliko kuacha amefunga ofisi na pia mali za ofisi inatakiwa awe anacha ofisi ikiwa wazi na awe anaandika barua ya kukabidhi ofisi kuliko kijiondokea kama anavyofanya kwa kuwa ofisi siyo mali yake bali ni mali ya Serikalai.

Wednesday, October 22, 2014

SIKONGE YATOA MSAADA WA VIFAA VYA MIL.12 KWA WANAFUNZI WASIOJIWEZA

NHIF NA MPANGO WA KUPELEKA MADAKTARI BINGWA MIKOANI

MAOFISA WA UN WAHAMASISHA WANAFUNZI WA JANGWANI KUTEKELEZA AJENDA ZA UMOJA WA MATAIFA

MAOFISA WA UNAfisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa Bi. Usia Nkhoma Ledama, akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Jangwani akiwa ameambatana na maafisa wenzake wa mashirika ya Umoja wa Mataifa ikiwa ni shamrashamra ya maadhimisho ya miaka 69 toka Umoja wa Mataifa unazishwe. Kushoto kwa Bi Ledama ni Albert Okal (ILO).

Shamrashamra za maadhimisho ya miaka 69 toka Umoja wa Mataifa uanzishwe zimeanza nchini, na leo jumatano maofisa waandamizi wa UN walitembelea shule ya sekondari ya Jangwani na kuwahabarisha wanafunzi hao juu ya shughuli za Umoja wa Mataifa hapa nchini.

Mjadala kati ya maofisa hao Phillemon Mutashubirwa, Programme Manager wa UN Habitat, Usia Nkhoma Ledama, Afisa habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa(UNIC), Albert Okal (ILO),Greta Sayungi (UNICEF), ulijikita katika masuala ya HIV/AIDS, EBOLA, Usafi na umuhimu wakuosha mikono ili kujikinga na maradhi, elimu ya ujasiriamali, ajira kwa vijana, kazi za kujitolea, malengo ya Milenia na malengo ya Umoja wa Mataifa kwa ujumla wake.

Ijumaa wiki hii Umoja wa Mataifa utaadhimisha mkiaka 69 toka uanzishwe na kilele cha maadhimisho hayo yatafanyika katika viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam.
DSC_0106
Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa Bi. Usia Nkhoma Ledama akifafanua jambo wakati akizungumza na wanafunzi wa shule yasekondari Jangwani jijini Dar. Kutoka kushoto ni Phillemon Mutashubirwa (UN Habitat), Greta Sayungi (UNICEF) pamoja na Dr Bwijo Bijo (UNDP)
DSC_0094Pichani juu na chini ni Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Jangwani wakiwasiliza maafisa wa Umoja wa Mataifa waliowatembelea shuleni hapo.
DSC_0083