Meneja wa Uwanja wa ndege wa Mpanda, Mkoa wa Katavi Seneti Lyatuu
akiwaonesha timu ya ukaguzi wa miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais,
Tume ya Mipango upanuzi wa uwanja wa ndege wa Mpanda. Nyuma yake
(mwenye suti nyeusi) ni Mhandisi Caroline Mntambo kutoka Mamlaka ya
Viwanja vya Ndenge Tanzania, Makao Makuu, Dar es Salaam.
Meneja wa Uwanja wa Ndege wa Mpanda Bw. Seneti Lyatuu akifafanua
jambo wakati timu ya ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya
Rais, Tume ya Mipango walipotembelea kiwanja hicho. Timu ya ukaguzi ikitazama barabara ya kutua na kurukia ndege katika uwanja wa ndege wa Mpanda Barabara ya kutua na kurukia ndege katika uwanja wa ndege wa Mpanda, mkoani Katavi Mhandisi
Caroline Mntambo (mwenye suti nyeusi) akifafanua jambo kwa timu ya
wakaguzi kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango. Uwanja wa ndege wa
Mpanda umekarabatiwa na kupanuliwa hivyo , kuwa katika hali nzuri kwa
matumizi ya ndege zote za binafsi na biashara
PICHA NA JOYCE MKINGA
………………………………………………………………….
Na Mwandishi wetu, Mpanda
Serikali imekamilisha ukarabati na
upanuzi wa uwanja wa ndege wa Mpanda, mkoa wa Katavi na hivyo kuufanya
uwe wa kiwango kizuri tayari kwa kutumika kwa ndege za binafsi na
biashara.
Meneja wa Uwanja wa Ndege wa
Mpanda, Bw Seneti Lyatuu alisema uwanja huo umeboreshwa na hivyo,
unaweza kutumika kutua na kuruka ndege za kiwango cha kati na hata zile
ndege kubwa zinaweza kutua kwa dharura.
Aliiambia timu ya ukaguzi wa
miradi ya maendeleo kutoa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango iliyotembelea
uwanja huo mwishoni mwa wiki kuwa uwanja huo umeongeza idadi ya wasafiri
mara dufu kutokana na ukarabati na upanuzi uliofanyika.
Meneja wa Uwanja huo alisema idadi ya abiria imeongezeka kutoka abiria 285 mwaka 2009 hadi 2,390 mwaka 2013/14.
Bw. Lyatuu alisema kuwa uwanja huo
umekarabatiwa na barabara ya kuruka na kutua ndege imerefushwa kwa
kiwango cha lami kutoka urefu wa mita 1,500 na upana wa mita 30 hadi
kufikia urefu wa mita 1,820 na upana wa mita 30.
Alisema maeneo mengine yaliyokarabatiwa ni pamoja na kujenga uzio na mifereji ya kupitishia maji ya mvua.
“Kwa sasa kiwanja kipo vizuri na
ndege za aina zote zinaweza kutua hapa uwanjani hivyo, tunawakaribishwa
wadau wote kuutumia uwanja huu” alisema Bw Lyatuu.
Eng. Caroline Mntambo kutoka
Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Makao Makuu Dar es Salaam alisema kuwa
tayari wamealika mashirika ya ndege yanayofanya biashara hapa nchini
kuanzisha safari katika uwanja huo. Mashirika hayo ni pamoja na ATC,
Precision Air, Fast jet nk.
Eng Mntambo alisema kwa sasa shirika la ndege la Auric Air tayari limeanzisha safari za kwenda Mpanda ambapo linasafirisha abiria kutoka Dar- Mpanda – Mwanza mara tatu kwa wiki.
Alisema ndege zingine zinazotua uwanjani hapo kwa sasa ni pamoja na za UNHCR, ndege za kukodi na ndege za serikali.
No comments:
Post a Comment