Baadhi ya wakazi wa Tabora mjini wakionekana katika hali ya utafutaji wa riziki. |
Kumekuwa na dalili za waziwazi kuwa idadi ya wajasiliamali imeendelea kuongezeka Tabora mjini hali inayotokana na kuongezeka kwa watu wanaofanya shughuli mbalimbali za kutafuta riziki zao ikiringanishwa na miaka mitatu iliyopita.
Ushahidi wa kuongezeka kwa makundi ya wajasiliamali ni pale inapodhihirika kuwa watu wengi wanaonekana kufanya shughuli zao binafsi za kuwaongezea kipato huku ikibainika kuwa kumekuwepo mzunguuko wa pesa kila kona na kuwafanya watu kuwa katika hekaheka za mara kwa mara za utafutaji.
Biashara ndogondogo zinaendelea kushamili,huku ikionesha kuwa idadi kubwa ya wanawake wamekuwa wakijishughulisha kuliko idadi ya wanaume.
Ongezeko na huduma za taasisi za kifedha kama mabenki ambazo zimeonesha hali ya kutoa mikopo kwa wajasiliamali na kuwafanya waongeze juhudi katika kujitafutia riziki zao.
Serikali ya mkoa wa Tabora imeacha milango wazi kwa wajasiliamali kuendesha shughuli zao bila kubughudhiwa na mtu yeyote.
No comments:
Post a Comment