Mshindi
wa taji la Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Mtemvu huenda akavuliwa taji
hilo kama serikali kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo na Baraza lake la Sanaa la Taifa ambalo ndio watoaji vibali vya
mashindano hayo na kusimamia dhima na maudhui ya shindano hilo pamoja
na kusimamia maadili yake itaingilia kati moja kwa moja suala hilo kwa
kuunda tume maalum ya kulichunguza na kutafuta ukweli halisi wa umri wa
mrembo huyo na kutoa mapendekezo ya ama Sitti avuliwe taji hilo na
kuvikwa Mshindi wa pili, Lillian Kamazima (pichani kulia) ama
vinginevyo. Kushoto ni Jihhan Dimachk aliyeshika nafasi ya tatu.
Shindano la Miss Tanzania 2014
lilifanyika katika ukumbi wa Mlimani City,jijini Dar es Salaam Oktoba
11, na Sitti Mtemvu kuvikwa taji hilo na kuanza utata wa umri wake
halisi licha ya kuanika hadharani cheti chake cha kuzaliwa ambacho wadau
wa sanaa ya urembo kukitilia shaka na kushindwa kuoanisha na pasi yake
ya kusafiria na leseni ya udereva iliyotolewa nchini Marekani. http://mrokim.blogspot.com/2014/10/taji-la-miss-tanzania-2014-kuundiwa-tume.html
No comments:
Post a Comment