WITO umetolewa kwa wanasiasa,watumie fursa walizonazo katika
jamii ili kuendeleza tasnia ya michezo Nchini.
Akielezea hilo jana Kigoma Ujiji Katibu wa Chama cha Mpira
Kigoma (KRF) Issa Bukuku alisema wanasiasa wananafasi kubwa ya kuleta maendeleo
katika jamii kutokanan na kuwa na
makundi ya watu wenye uwezo wa aina mbalimbali ambapo wakitumiwa vyema ni tija
kwa raia husika.
Ofisi za serikali ya mkoa wa hapa na halmashauri zinadai idara husika hazina bajeti ya kuendesha michezo ili hali
serikali kuu inadhihirisha kuwa kuna fungu la fedha zinatengwa katika wizara husika za utamaduni
na michezo zipo katika halmashauri na manispaa lakini uhalisia wa mambo ni
utata.
Hali hiyo imefika KRF ya hapa kufunga ofisi zake zaidi ya
miezi mitatu kufuatia hali ngumu ya uchumi kwa watendaji hatimaye ofisi
kufungwa kwa masaa yote na kufunguliwa pale inapotokea kuna ajenda ya mchakato
wa mashindano ya ligi daraja la kwanza ya Vodacom ama Kopa cokacola .
“unashangaa kuona KRF ya kigoma kubip nyakati za kipute ,mikoa
yote utata itafanya kazi kwa wakati maalum si tija ya kujiwekeza ili ziwe na uwezo
wa kujiendesha kwa leo na kesho tunatafuta mkate wa kila siku , katiba ya vyama
vya mpira haina taratibu za kutoa fedha kwa watendaji tumeshindwa kuajiri mhudumu wa kuwepo katika ofisi ” alibainisha
Bukuku.
Alisema mwaka 2010 waliomba
watengewe eneo kwa ajili ya shule maalum ya Vipaji lakini hadi leo hakuna majibu kutoka kwa viongozi wa mkoa na
kusisitiza soka la hapa ni la msimu si ajira yenye kuwekeza na kuajiri kutokana
na mfumo mbovu uliopo na kuomba wanasiasa wawajibike
katika hili ili wakidhi hitaji la wapiga kura.
Pamoja na kufanya harambee 2010 kupata fedha za kuendesha ofisi ili kusaidia
kambi ya vijana katika moja ya mashindano makubwa ya Vodacom mwitikio kutoka kwa wadau katika hilo walifika
watano tu,hali iliyowavunja nguvu na
moyo kwa viongozi na vijana husika na kusihin wanasiasa waingilie kati kuokoa
jahazi husika.
Kwa upande wa Katibu Mkoa Chama cha Chadema mkoani hapa Shaban Madede alipohojiwa na gazeti hili juu
ya kuhamasisha wadau wawekeze katika michezo akiri kupitia mikutano ya hadhara
ya chama hicho atalisemea hilo na kuwasihi viongozi wasifunge ofisi bali waweke utaratibu wa ratiba itakayobainisha
siku za uwajibikaji wao.
Huku katibu mwenezi wa Chama cha ACT wilayani
hapa Anzuruni Kibera adai viongozi wa
KRF wanajingiza kwenye vyama vya siasa
hali inayochangia ugumu wa vyama kuwekeza nguvu,akili na mali kwa walengwa na kushauri
ikiwa wanahitaji hilo wakubali mawazo ya wanasiasa .
Mwandishi wetu alimtafuta Meya wa manispaa ya Ujiji kwa njia ya simu ya mkononi Bakari Beji kupata ufafanuzi juu ya bajeti ya fedha kwa idara husika,alidai lipo na alipoulizwa mchanganuo wa utendaji kazi wa fedha hizo
hakuwa tayari kujibu.