Na Magreth Magosso,Kigoma
MKUU wa Mkoa
wa kigoma Kanali mstaafu Issa Machibya ,awaasa
wananchi wache kula nyama za mwituni,
kwa lengo la kudhibiti ugonjwa wa Ebola mkoani hapa.
Akizungumzia
hilo jana kwenye uzinduzi wa mkakati wa kutokomeza vifo kwa watoto wenye virusi
vya ukimwi ,ikiwa na dhima ya kuhamasisha jamii ibadilike na vitendo vya
unyanyapaa kwa waathirika hasa wajawazito sanjari
na matumizi sahihi ya dawa aina ya ARVs .
Machibya
alisema kigoma ipo hatarini kuwa na wagonjwa wa Ebola kutokana na na
mwingiliano wa karibu kwa wakazi wa DRC-Congo ambao wanahistoria ya maradhi
hayo ambapo kwa sasa wanakabiliwa na janga hilo.
“najua kuna
watu wanauza nyama za pori huko mitaani,lakini kwa sasa acheni kula nyama
hovyohovyo,sokwe ,nyani,ngedele,popo hawa wanaasili ya vimelea vya ugonjwa
huo,kule congo ni kawaida hata jamii ya swala pori msile tutalipuka” alibainisha Machibya.
Pia amewapa
wananchi jukumu la kuweka ulinzi kwa watu wenye ulemavu wa ngozi huku akidai wasiige tabia hasi za mauwaji hao yanayofanywa
na mikoa ya simiyu,shinyanga na tabora .
Alisema
changamoto ya umaskini inachangiwa na jamii husika ,kushindwa kutumia elimu ya
uraia na sayansi ili kutambua fursa zilizopo hapa na nje ili kuongeza kipato cha kila mtu na taifa kwa
ujumla.
Kwa upande
wa Meneja wa ICAP Itrosi Sanga na Mganga Mkuu Leonard Subi wa hapa kwa nyakati tofauti walisema sekta ya afya inakabiliwa na uhaba wa vifaa
vya DBS ambavyo hubainisha mtoto
aliyezaliwa na mama mwenye virusi vya ukimwi kama ameambukizwa.
Walisema kwa
mkoa wa kigoma wanapeleka sampo ya damu ya mtoto husika katika hospitali ya
Bugando kupata majibu ya mtoto ,hali inayochangia ucheleweshaji wa majibu kwa
mlengwa.
Baadhi ya
wahanga Dafroza Bernad,Gati Matiku na Shida Seleman walipongeza asasi ya Icap
kwa kuwawezesha katika maisha yao na kuongeza kuwa,shida ipo upande wa serikali
hasa wahudumu wa afya kutowapa haki sahihi za mahitaji ya afya zao.
Akijibia
hilo Mratibu wa Afya ya Uzazi na mtoto
Martha Ndalituke alisema lengo ni kutokomeza mabukizi ya vvu kwa mama kwenda kwa mtoto kutoka 15%
hadi 5% na wahudumu wakikiuka madili
,wahanga wapeleka adha kwake ili walengwa wawajibishwe .
No comments:
Post a Comment