Pages

KAPIPI TV

Saturday, August 30, 2014

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA MH. JANETH MBENE ATEMBELEA BANDA LA NSSF MAONYESHO YA WAJASIRIAMALI KANDA YA KATI

Meneja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa
Kigoma, Josephat Komba akimuelezea Mgeni Rasmi, Naibu Waziri wa Viwanda na
Biashara, Janeth Mbene huduma mbalimbali zitolewazo na NSSF kwenye banda lao
wakati wa maonesho ya wajasiriamali Kanda ya Kati.
 Banda la NSSF linavyooneka kwenye maonesho ya Wajasiriamali
wa Kanda ya Kati yanayofanyika 
 Maofisa wa NSSF walioshiriki Kwenye Maonesho ya
wajasiriamali kanda ya Kati wakiwa na Meneja wa Mkoa wa Kigoma, Josephat Komba
wakimsubiri Mgeni Rasmi kuja kutembelea banda la NSSF.
Daktari wa NSSF akimpima Shinikizo la Damu Afisa Uhusiano
Mwandamizi wa NSSF ,Theopista Muheta wakati wa maonesho ya wajasiriamali anda
ya kati.
Mmoja ya Washiriki wa Maonesho ya Wajasiliamali Kanda ya kati akipima uzito tayari kupewa Ushauri juu ya uwiano wa uzito wake na urefu (BMI) na Daktari wa NSSF.
 Wakazi wa Mkoa wa Kigoma wakipata maelekezo ya Mafao
yatolewayo na NSSF kwa wanachama wa Hiari na wasio wa Hiari.
 
 
Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limeshiriki
kwenye maonesho ya wajasiriamali Kanda ya Kati yanayofanyika Mkoani Kigoma
kwenye viwanja vya Community Centre kuanzia Tarehe 27/08/2014 mpaka tarehe
02/09/2014.
 
Katika Maonesho hayo NSSF imekuwa ikitoa Elimu ya Uanachama
wa HIARI kwa Wajasiriamali wanaoshiriki kwenye maonesho hayo na kuandikisha
wanachama kwa HIARI. Pia NSSF inatoa Elimu kwa wajasiliamali jinsi ya kukopa
NSSF kupitia SACCOS.
 
Mgeni Rasmi, Naibu waziri wa Viwanda na Biashara, Janeth
Mbene aliwapongeza NSSF kwa kushiriki kwenye maonesho hayo na pia kwa juhudi
zao za kutoa elimu kwenye maonesho mengi .
Mgeni Rasmi aliusifia mpango wa Wakulima Scheme kwa kuweza
kuwafikiria wakulima na kuwapa mafao ya hifadhi ya jamii.

No comments: