Pages

KAPIPI TV

Sunday, August 31, 2014

CHAMA CHA MPIRA WA MIGUU KIGOMA CHAWATEGA WANASIASA

WITO umetolewa kwa wanasiasa,watumie fursa walizonazo katika jamii ili kuendeleza tasnia ya michezo Nchini.

Akielezea hilo jana Kigoma Ujiji Katibu wa Chama cha Mpira Kigoma (KRF) Issa  Bukuku alisema  wanasiasa wananafasi kubwa ya kuleta maendeleo katika jamii  kutokanan na kuwa na makundi ya watu wenye uwezo wa aina mbalimbali ambapo wakitumiwa vyema ni tija kwa raia husika.
 
Ofisi za serikali ya mkoa wa hapa na halmashauri  zinadai idara husika  hazina bajeti ya kuendesha michezo ili hali serikali kuu inadhihirisha  kuwa  kuna fungu la  fedha zinatengwa katika wizara husika za utamaduni na michezo zipo katika halmashauri na manispaa lakini uhalisia wa mambo ni utata.
 
Hali hiyo imefika KRF ya hapa kufunga ofisi zake zaidi ya miezi mitatu kufuatia hali ngumu ya uchumi kwa watendaji hatimaye ofisi kufungwa kwa masaa yote na kufunguliwa pale inapotokea kuna ajenda ya mchakato wa mashindano ya ligi daraja la kwanza ya Vodacom ama Kopa cokacola .
 
 “unashangaa kuona  KRF ya kigoma kubip nyakati za kipute ,mikoa yote utata itafanya kazi kwa wakati maalum si tija ya kujiwekeza ili ziwe na uwezo wa kujiendesha kwa  leo na kesho  tunatafuta mkate wa kila siku , katiba ya vyama vya mpira haina taratibu za kutoa fedha kwa watendaji tumeshindwa kuajiri  mhudumu wa kuwepo katika ofisi ” alibainisha Bukuku.
 
Alisema  mwaka 2010 waliomba watengewe eneo kwa ajili ya shule maalum ya Vipaji  lakini  hadi leo hakuna  majibu kutoka kwa viongozi wa mkoa na kusisitiza soka la hapa ni la msimu si ajira yenye kuwekeza na kuajiri kutokana na  mfumo  mbovu uliopo na kuomba wanasiasa wawajibike katika hili ili wakidhi hitaji la wapiga kura.

Pamoja na kufanya harambee 2010  kupata fedha za kuendesha ofisi ili kusaidia kambi ya vijana katika moja ya mashindano makubwa ya Vodacom  mwitikio kutoka kwa wadau katika hilo walifika  watano tu,hali iliyowavunja nguvu na moyo kwa viongozi  na vijana husika  na kusihin wanasiasa waingilie kati kuokoa jahazi husika.

Kwa upande wa Katibu Mkoa Chama cha Chadema mkoani hapa Shaban Madede alipohojiwa na gazeti hili juu ya kuhamasisha wadau wawekeze katika michezo akiri kupitia mikutano ya hadhara ya chama hicho atalisemea hilo na kuwasihi viongozi wasifunge ofisi bali  waweke utaratibu wa ratiba itakayobainisha siku za uwajibikaji wao.

Huku katibu  mwenezi wa Chama cha ACT   wilayani hapa Anzuruni Kibera adai viongozi wa KRF  wanajingiza kwenye vyama vya siasa hali inayochangia ugumu wa vyama kuwekeza nguvu,akili na mali kwa walengwa na kushauri ikiwa wanahitaji hilo wakubali mawazo ya wanasiasa .

Mwandishi wetu alimtafuta Meya wa manispaa ya Ujiji kwa njia ya simu ya mkononi  Bakari Beji  kupata ufafanuzi juu ya bajeti ya fedha  kwa idara husika,alidai lipo na alipoulizwa  mchanganuo wa utendaji kazi wa fedha hizo hakuwa tayari kujibu.

No comments: