Pages

KAPIPI TV

Saturday, August 30, 2014

DAKTARI BINGWA WA MAGONJWA YA SARATANI YA MATITI KUTOKA INDIA ATOA SEMINA YA UGONJWA HUO KWA MADAKTARI WA TANZANIA

Daktari bingwa wa ugonjwa wa saratani ya matiti kutoka nchini India, Profesa Anthony Pais, akitoa mafunzo kuhusu ugonjwa huo kwa madaktari wa kitanzania na wadau mbaliombakli wa sekta ya afya. Semina hiyo ilifanyika Dar es Salaam jana, Hoteli ya Protea Courtyard Seaview.
Profesa Anthony Pais, akiwa na madaktari wa kitanzania. Kutoka kushoto ni Executive Chairman Tanzania Creative Industries Network (TACIN), Anic Kashasha na Dk.Paul Mareale.
Profesa Anthony Pais (kushoto), akielezea jambo kuhusu ugonjwa huo.
Mkurugenzi Mtendaji  wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) ,
Dk.Malina  Njelekela(kulia), akizungumza na wadau mbalimbali katika semina hiyo.

Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea, James Rugemalira akizungumza na waandishi wa habari. Kulia ni mke wake ambaye ni  Mkurugenzi wa Kampuni ya Mabibo Beer wines and Spirits Limited, Benedicta Rugemalira na Profesa Anthony Pais.
Profesa Pais (katikati), akiwa na wenyeji wake. Kutoka kulia ni Dk.Paul Mareale, James Rugemalira, Dk.Malina Njelekela na Benedicta Rugemalira.
Profesa Pais akizungumza na waandishi wa habari.
Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea, James Rugemalira (kushoto), akipeana mkono na daktari bingwa wa ugonjwa wa saratani ya matiti kutoka India, Profesa Anthony Pais (kulia), baada ya kutoa mafunzo kwa madaktari wa Tanzania na wadau wa sekta ya afya kuhusu ugonjwa huo, Dar es Salaam jana. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd, Benedicta Rugemalira, waliodhamini mafunzo hayo ya siku moja.
Profesa Pais (mwenye suti katikati), akiwa katika picha ya pamoja na wenyeji wake.
Profesa Pais (mwenye suti katikati), akiwa katika picha ya pamoja na wenyeji wake.
Mkurugenzi Mtendaji  wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) ,
Dk.Malina  Njelekela(kulia), akiteta jambo na viongozi wengine kwenye semina hiyo.
Profesa Pais akifurahia jambo na Executive Chairman Tanzania Creative Industries Network (TACIN), Anic Kashasha.
Wadau wakiwa kwenye semina hiyo. Kulia ni Mmoja wa Wakurugenzi wa Kampuni iliyokuwa ikifua umeme ya VIP, Joe Mgaya.
Wanahabari wakiwa kwenye semina hiyo.
Continue reading →

No comments: