Pages

KAPIPI TV

Friday, July 25, 2014

RAIS KIKWETE AMUAPISHA JAJI KIONGOZI WA MAHAKAMA KUU YA TANZANIA


PIX01
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete akimuapisha Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Shaban Ally Lila leo jijini Dar es Salaam.Picha zote na Frank Shija- MAELEZO
PIX02
Jaji Kiongozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jaji Shaban Ally Lila (kulia) akitia saini hati ya Kiapo mbele ya Rais Jakaya Kikwete wakati wa hafla ya kuapishwa kwake leo jijini Dar es Salaam. Katikati mwenye miwani Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akishuhudia tukio hilo.
PIX03
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini hati ya Kiapo cha Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Shaban Ally Lila wakati wa hafla ya kuapishwa kwa jaji huyo leo jijini Dar es Salaam.
PIX04
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi hati ya Kiapo Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu Tanzania Mhe. Shaban Ally Lila wakati wa hafla ya kuapishwa kwa jaji huyo leo jijini Dar es Salaam.
PIX05
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue(kushoto) akimpongeza Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu Tanzania Mhe. Shaban Ally Lila mara baada ya kuapishwa rasmi kushika wadhifa huo katika hafla iliyofanyika Ikulu leo jijini Dar es Salaam.
PIX06
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu Tanzania Mhe. Shaban Ally Lila akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Majaji wa Mahaka Kuu Tanzania mara baada ya kuapishwa rasmi kushika wadhifa huo katika hafla iliyofanyika Ikulu leo jijini Dar es Salaam.Kushoto kwake ni Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman

MAADHIMISHO YA SIKU YA KUMBUKUMBU YA MASHUJAA 25 JULAI, 2014

SERIKALI YAPOKEA MABEHEWA 25 YENYE THAMANI YA SH.BILIONI 4.3 KUTOKA INDIA

Waziri wa Uchukuzi Dk.Harrison Mwakyembe (katikati), akifurahia jambo wakati wa kupokea mabehewa hayo. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TRL, Mhandisi Kipalo Kisamfu na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk.Shaaban Mwinjaka.
Mkurugenzi Mkuu wa TRL, Mhandisi Kipalo Kisamfu (mwenye tai kushoto),akimuelekeza jambo Waziri Mwakyembe.
Waziri Mwakyembe akizungumza na waandishi wa habari wakati akipokea mabehewa hayo.
Wafanyakazi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (PTA) na wa TRL wakishusha toka katika meli moja ya mabehewa hayo.
Baadhi ya wanahabari waliokuwepo kwenye hafla hiyo.
Wafanyakazi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (PTA) na wa TRL wakishusha toka katika meli moja ya mabehewa hayo.
Waziri Mwakyembe akiangalia moja ya mabehewa hayo.
Baadhi ya mabehewa hayo yakiwa yamepangwa katika njia yake bandarini baada ya kushushwa kutoka katika meli.
Fundi wa Shirika la Reli Tanzania , Ephrahim Joel akikaza nati ya moja ya mabehewa hayo.
Fundi wa Shirika la Reli Tanzania , Francis Mpangala naye akikaza nati katika moja ya mabehewa hayo. (Imeandaliwa na mtandao wa habari za jamii.com.
………………………………………………………………
Na Dotto Mwaibale
 
SERIKALI imepokea mabehewa 25 mapya ya kubebea kokoto yenye thamani ya sh.bilioni 4.316 kwa ajili ya Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) kutoka Kampuni ya M/S Hindusthan Engineering and Industriles Limited ya India.
 
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya kupokea mabehewa hayo Dar es Salaam jana, Waziri wa Uchukuzi Dk.Harrison Mwakyembe alisema mabehewa hayo ni sehemu ya mpango kabambe wa Serikali wa kufufua Kampuni ya Reli Tanzania chini ya mapngo wa Tekeleza kwa Matokeo Makubwa sasa (BRN).
 
Alisema mpango wa BRN kwa Kampuni ya Reli Tanzania umelenga kuiwezesha kampuni hiyo kiutendaji ili iweze kusafirisha tani milioni 3.0 ifikapo mwaka 2016 kutoka tani 200,000 zilizosafirishwa mwaka 2012 kupitia Reli ya kati.
 
“Katika harakati za kufikia malengo haya makubwa, Serikali kupitia bajeti zake za mwaka 2012/2013 na 2014, ilitenga fedha kwa ajili ya kugharamia miradi mbalimbali iliyolenga kuboresha vitendea kazi vya Kampuni ya Reli Tanzania” alisema Mwakyembe.
 
Alitaja miradi iliyopangwa ni pamoja na kujenga upya vichwa vya Treni 8, kununua vinchwa vya treni vipya 13, mabehewa mapya 274 ya kubebea mizigo na mabehewa ya breki.
 
Mwakyembe alitaja mradi mwingine ni kununua mashine ya kushindilia kokoto, kununua mabehewa 22 mapya ya abiria na kununua mabehewa 25 mapya ya kubebea kokoto ambayo yamepokelewa jana.
 
Katika hatua hiyo Mwakyembe ametumia fursa ?hiyo kuipongeza TRL kwa kupokea mabehewa hayo kwa wakati na kuishukuru Kampuni ya Hindusthan Engineering and Industries Limited ya India kwa utengenezaji wa mabehewa hayo kwa muda uliopangwa.
 
Alisema lengo ni kuiwezesha TRL kufikia malengo ya kusafirisha mizigo tani 3.0 na kutembeza treni za abiria tano kwa wiki ifikapo mwaka 2016.

WANANCHI NA JWTZ WASHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA MASHUJAA TABORA

Baadhi ya askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania wakifyatua risasi hewani kama ishara ya kumbukumbu ya Mashujaa katika maadhimisho yaliyofanyika Tabora mjini kwenye Mnara wa kumbukumbu ya uamuzi wa Busara.
Baadhi ya makamanda wa JWTZ wakitoa heshima wakati wa maadhimisho ya Mashujaa Tabora mjini.

Mkuu wa wilaya ya Sikonge Bi.Hanifa Selengu akiweka Ngao na mkuki kama ishara ya Serikali kukumbuka mchango wa mashujaa waliopambana katika vita mbalimbali.
Baadhi ya makamanda wa JWTZ,Polisi na Magereza walihudhuria katika maadhimisho hayo.

Mkuu wa wilaya ya Sikonge Bi.Hanifa Selengu akihutubia katika maadhimisho hayo kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Tabora.
Baadhi ya wananchi wakiwemo wafanyabiashara ambao walilazimika wafunge shughuli zao kushiriki maadhimisho ya Mashujaa.





WAHANGA WA VITA WANENA-KIGOMA

Mkuu wa wilaya ya Kigoma Bw.Ramadhani Maneno  akiweka Ngao na mkuki kama ishara ya kuwakumbuka Mashujaa katika maadhimisho mkoani Kigoma
Mkuu wa wilaya ya Kigoma Bw.Ramadhani Maneno akiingia katika eneo lililotayarishwa kwa ajili ya Maadhimisho ya kumbukumbu ya Mashujaa mkoani Kigoma.
Baadhi ya makamanda wa JWTZ na wananchi wakiwa tayari katika maadhimisho ya kumbukumbu mkoani Kigoma
Gwaride rasmi katika maadhimisho ya Mashujaa.
 Na Magreth Magosso,Kigoma

WAHANGA waliopigana vita mbalimbali hapa nchini waishio Mkoa wa Kigoma,wamewataka vijana wazingatie nidhamu,uaminifu na kujiepusha kudharau matabaka ya jamii yaliyopo ,kwa lengo la kulinda taifa kwa maslai ya kizazi cha leo na siku zijazo.
 
Wakizungumza kwa nyakati tofauti  wahanga hao,kigoma ujiji  jana katika  kuenzi  siku ya kurudi nchini hapa kwa mashujaa waliopigana vita  mbalimbali ikiwemo ya  Uganda,msumbiji,Botswana ,vita vya kijadi na nyinginezo walisema walifanikisha hayo kwa kuzingatia nidhamu ,uaminifu kwa kujitolea  kupigania haki za wananchi husika.
 
Inspekta Mstaafu Jeshi la magereza Juliana Stephana na  Kamishna mstaafu Lt.Joseph Nyamkuzwa walisema  wananchi kwa ujumla hawana budi kumcha mungu ili kudumisha  upendo, ambao ni chachu ya kuthubutu kulinda maliasili na kutoa taarifa   za uvunjifu wa amani  iliyopo.
 
Na Lt. kanali mstaafu Raphael  Kakwila alisihi wazazi watoe elimu njema kwa vijana wao,ili waishi kwa nidhamu bora yenye ushawishi wa kuwajengea uwezo wa kizalendo ambao ni tija ya kuzuia uhalifu kwa maslai ya jamii lengwa.
 
Kwa upande wa mgeni rasmiambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya hapa, Ramadhan Maneno kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huoLt.mstaafu Issa Machibya alisema,siku hiyo ni chachu kwa jamii kutambua thamini  ya amani iliyopo.
 
“majirani zetu hawapendi kuona taifa linarithi amani tuliyoachiwa wahanga hawa walitoa damu na jasho kupigania haki za msingi na taifa sasa vijana ni wakati wenu kulinda nchi kwa kujiepusha na matukio ya uvunjifu wa utulivu,amani kwa kuwabainisha wahalifu” alianisha Maneno.
 
Alisema walitumia  zana  duni za kivita  lakini kutokana na uzalendo walionao walijitoa kwa dhati   kupigania maslai ya taifa ili kuipa nchi  heshima .huku awaasa wananchi watoe taarifa kwa vyombo vya usalama ili kudhibiti majanga ya uhalifu.
 
Aidha Shekhe Mkuu  Bakwata wa hapa Hassan Iddi  alisema wanasiasa,wananchi na viongozi wa dini wanajukumu la kuelimisha waumini wao juu ya faida ya amani na athari zake,kwa lengo la kuboresha ustawi wa umaa.
 
Akizungumzia utata Rasimu mpya ya katiba Shekhe Iddi alionya wanasiasa waache utashi wa maslai  binafsi na badala yake wanzingatie  misingi bora  ya wahanga waliothubutu  kufa ili kutetea umaa husika.

Thursday, July 24, 2014

SERIKALI YASAINI MIKATABA MIWILI YA UJENZI WA BARABARA ZA JUU KWA JUU


1 (4)Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile (kushoto) na Balozi wa Japan nchini Masaki Okada (kulia) wakibadilishana hati ya makubaliano ya mikataba miwili ya ujenzi wa barabara za juu kwa juu katika makutano ya TAZARA na usambazaji umeme jijini Dar es salaam leo zenye thamani ya zaidi ya bilioni 128.
2 (4)Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile (kushoto) na Balozi wa Japan nchini Masaki Okada (kulia) wakisaini hati ya makubaliano ya mikataba miwili ya ujenzi wa barabara za juu kwa juu katika makutano ya TAZARA na usambazaji umeme jijini Dar es salaam leo zenye thamani ya zaidi ya bilioni 128.
3 (4)Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile (kushoto) akionyesha michoro ya itakavyonekana barabara za juu kwa juu katika makutano ya TAZARA jijini Dar es salaam leo wakati wa kusaini hati ya makubaliano ya miradi miwili zenye thamani ya zaidi ya bilioni 128 na Balozi wa Japan nchini Masaki Okada (kulia).
Picha na Eleuteri Mangi- MAELEZO -Dar

UZINDUZI WA MRADI WA SAEMAUL UDONG KIJIJI CHA CHEJU UNGUJA


IMG_7086Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK.ALi Mohamed Shein akipata maelezo kutoka Naibu katibu Mkuu Wizara ya Kilimo na Maliasili Nd,Juma Ali Juma wakati alipotembelea kituo cha kukausha Embe Dodo katika Kijiji cha Cheju kibonde maji leo  kilichojengwa na Shirika la misaada la Koika nchini Korea kupitia    Mradi wa  SAEMAUL UDONG   .[Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]
IMG_7100Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK.ALi Mohamed Shein na Balozi wa Korea Bw.IL Chung (katikati) wakiangalia embe zilizokaushwa zikiwa katika Mpango maalum wa kuhifadhiwa  wakati alipotembelea kituo cha kukausha Embe Dodo katika Kijiji cha Cheju kibonde maji leo kilichojengwa na Shirika la misaada la Koika nchini Korea kupitia Mradi wa  SAEMAUL UDONG   .[Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]  
IMG_7107
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK.ALi Mohamed Shein na Balozi wa Korea Nchini Tanzania Bw.IL Chung (katikati) wakiangalia embe zilizokaushwa zikiwa katika Mpango maalum wa kuhifadhiwa  wakati alipotembelea kituo cha kukausha Embe Dodo katika Kijiji cha Cheju kibonde maji leo  kilichojengwa na Shirika la misaada la Koika nchini Korea kupitia Mradi wa SAEMAUL UDONG   .[Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]  
IMG_7141 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK.ALi Mohamed Shein(katikati) na Balozi wa Korea Nchini Tanzania Bw.IL Chung wakipata maelezo kutoka Naibu katibu Mkuu Wizara ya Kilimo na Maliasili Nd,Juma Ali Juma (kulia) wakati alipotembelea mitambo katika kituo cha kukausha Embe Dodo katika Kijiji cha Cheju kibonde maji leo kilichojengwa na Shirika la misaada la Koika nchini Korea kupitia  Mradi  SAEMAUL UDONG   .[Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]  
IMG_7152Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK.ALi Mohamed Shein akibadilishana mawazo na  na Balozi wa Korea Nchini Tanzania Bw.IL Chung mara baada ya kutembelea  kituo cha kukausha Embe Dodo katika Kijiji cha Cheju kibonde maji leo kilichojengwa na Shirika la misaada la Koika nchini Korea kupitia  Mradi  SAEMAUL UDONG   .[Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]

MBUNGE PETER MSIGWA AKABIDHI MSAADA

SAM_6953
chuo cha Kitanzani Islamic center kilichoko mjini Iringa. (Picha zote na Denis Mlowe)
SAM_6980
Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa akikabidhi msaada wa Sukari, kwa Kaimu Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Abubakari Chalamila kwa ajili ya kituo cha Kitanzani Islamic


Na Denis Mlowe,Iringa
MBUNGE wa Iringa Mjini(Chadema) Mchungaji Peter Msigwa amekikabidhi chuo cha Kitanzani Islamic Center msaada wa Sukari,Unga wa Ngano, tende na mafuta ya kupikia ikiwa ni utaratibu wake wa kila mwaka kukisaidia chuo hicho.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo jana kwa Shekhe Mkuu wa Mkoa Iringa Abubakar Chalamila, Mchungaji Msigwa alisema kuwa lengo la kugawa kipindi hiki ni kuwaunga mkono Waislamu katika mfungo wa Ramadhani na kuwakumbuka wale wote wanaoishi katika mazingira magumu.

Mchungaji Msigwa alisema ni jukumu la wadau kuweza kuwasaidia wale wote bila kujali itikadi za vyama kwa kuwa binadamu wote ni wamoja kwa sasa.

Mchungaji Msigwa alikabidhi tambi katoni zaidi ya katoni 50, katoni 40 za mafuta ya kupikia, kilo 250 za unga wa ngano na sukari kilo 750 vyote vikiwa na jumla ya thamani zaidi ya shilingi milioni 1.5.

Alisema ataendelea kutoa msaada kwa vituo vingine vya watoto yatima na wasiojiweza katika kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhan.

Akishukuru kwa msaada huo Kwa niaba ya chuo cha Kitanzani Islamic Center chenye jumla ya wanafunzi 120 ambao wanachukua mafunzo ya dini ya kiislamu Kaimu Shekhe Mkuu wa Mkoa Iringa, Abubakar Chalamila alisema ni jambo la kujivunia kuwa na mbunge asiyechagua itikadi za dini na mbunge ni akichaguliwa anakuwa wa watu wote bila kubagua watu wake.

“Namshukuru sana Msigwa kwa kuweza kutoa msaada huu na utafikishwa kwa wale wote waliolengwa kupewa na hasa wale wasiojiweza ndio watafaidika na msaada huu wa mbunge wa iringa mjini.” Alisema |Chalamila

Chalamila aliwataka wadau wengine kuwakumbuka watu wasiojiweza na wanaoishi katika mazingira magumu mara kwa mara kwa kuwa ni thawabu kubwa kuweza kuwasaidia.

"KILA MTU ANA HAKI YA KUGOMBEA UBUNGE,KAMA ULIWAJIBIKA VIZURI KWA WANANCHI WATAKUCHAGUA TENA"-MH.MUNDE

Na Mwandishi wetu.
"Hakuna mtu mwenye haki miliki ya Ubunge,kwani hiyo ni dhamana tu tuliyopewa na wananchi,lakini kwanini ifikie hatua ya watu kuhitilafiana na kugombana pasipo sababu za msingi"hii ni kauli ya Mbunge wa vitimaalumu  mkoa wa Tabora Mheshimiwa Munde Tambwe wakati akizungumza na mtandao huu.

Wakati huu kabla  ya kuelekea kwenye mchakato wa kura za maoni  kwa Chama cha Mapinduzi kumekuwa na hali ya kupigana vikumbo kwa baadhi ya makada wa Chama hicho hatua ambayo imebadili kabisa ukurasa wa maisha ya kawaida ya kibinadamu na kujenga sura mpya ya siasa za chuki kwa mtu mmoja kumchafua mwingine au kikundi cha watu fulani kumchafua mtu mmoja jambo ambalo linadhihirisha watu wamesahau kabisa majukumu yao na kugeuza kuwa ni ajenda muhimu ya katika maisha.

Jambo hili limemsukuma Mbunge wa vitimaalum Mheshimiwa Munde Tambwe na kuona kuwa watu wanakoelekea siko ambako CCM inataka kutekeleza malengo yake katika kuwahudumia wananchi ambao kimsingi ndio wamekiweka madarakani chama hicho.

"Ninavyofikiri mimi kwa muda huu sisi kama wanaccm ni vema tushirikiane,tujenge mshikamano katika kutekeleza Ilani ya Chama chetu badala ya kukaa tunajengeana chuki zisizo na msingi,yaani huyu kamsema yule na yule kamsema huyu,hii haitusaidii kabisa itatufanya tushindwe kujibu maswali ya msingi ya wananchi watakapo tuuliza nini tumefanya tangu tuwe madarakani"alisema Mheshimiwa Munde

"Ubunge si haki miliki ya mtu,kwani yeyote anahaki ya kugombea muda ukifika lakini kwasasa tunatakiwa kuwasaidia wananchi,wewe kama umewajibika ipasavyo kwa wananchi, wenyewe watakuchagua hata kama ni vipindi vitatu,lakini kama umepewa dhamana ya kuwa mbunge halafu unashindwa kutekeleza majukumu yako huna sababu ya kugombana na watu,wananchi wenyewe wataamua na wewe utavuna ulichopanda"msisitizo wa ziada wenye lengo la kujenga.

Kwa kauli hii ni vema pia watu waliopewa dhamana au ridhaa na wananchi ya kushika wadhifa walionao wapate fursa ya kujipima,je,wanayo nafasi tena ya kujitosa wakati wa kura za maoni utakapowadia?au ndio kuanzisha chuki na vurugu kwa kila mtu mwenye uwezo wa kifedha unayemuona amevaa sare ya Chama na kutoa misaada kwa watu  unamhisi anataka kuchukua nafasi yako?

"Hakuna mtu anakatazwa kushirikiana na wengine katika kufanya kazi za chama ni vema tukafuata taratibu na kanuni za chama chetu na muda ukifika refarii atapuliza kipenga kila mmoja wetu ataona kama anauwezo wa kuomba nafasi anayoitaka kuliko kuanza kujipitisha huku na kule na kujinadi,binafsi sitofanya hivyo isipokuwa nawaombeni makada wenzangu tushirikiane kutekeleza Ilani ya chama chetu ili wenzetu wa vyama vya upinzani wakose la kuhoji"alisema Mheshimiwa Munde

"Chama cha Mapinduzi kina utaratibu mzuri sana katika kuwapata viongozi wa kada mbalimbali wakiwemo wabunge ni dhahiri kwamba mtu akifuata taratibu na kanuni za chama chetu atakuwa na haki ya kuwania nafasi anayoitaka na si kweli kwamba kutumia fedha kwa maana ya kuwahonga wapigakura inaweza ikawa sababu ya kuchaguliwa hilo si kweli"alisema huku akitahadharisha wanachama hasa makada ni vema wakashirikiana katika kutekeleza majukumu ya chama katika kutimiza ahadi zilizotolewa na viongozi wakati wa kuomba ridhaa kwa wananchi uchaguzi wa mwaka 2010.

"KWA PAMOJA TUSHIRIKIANE KUUJENGA MKOA WETU,VIONGOZI TUWASAIDIE  WATU WAONDOKANE NA UMASIKINI WA KIPATO,CCM DAIMA"      
  

MAENDELEO BANK YAANZISHA HUDUMA ZA BIMA

0D6A0674
0D6A0704
Wafanyakazi wa Maendeleo Bank na wa UAP wakiwa katika picha ya Pamoja.
maendeleo
Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Bank Ibrahim Mwangala (kulia) akipeana mkono na Nick Itunga Mkurugenzi mtendaji wa UAP Insurance Nick Itunga baada ya kuzindua huduma ya bima kupitia Maendeleo Bank
………………………………………………………………………… Maendeleo Bank imezindua huduma ya bima ikiwa ni lengo la kuwapatia wateja huduma zote muhimu ndani ya dari moja. Pia inachangia juhudi za serikali kuboresha na kufikisha elimu na huduma za bima kwa wananchi wengi ambao hawajafikiwa. Maendeleo Bank Insurance Agency imeanzishwa ili kuunga mkono mkakati wa Serikali wa huduma za kifedha jumuishi ambazo zitahamasisha wananchi wengi watumie na wafikiwe na huduma za kifedha ikiwa ni pamoja na bima.

Katika huduma za bima, Maendeleo Bank Insurance Agency imejipanga kutoa huduma zote za bima isipokuwa za maisha. Huduma zifuatazo zinapatikana Maendeleo Bank Insurance Agency: Bima za binafsi na za biashara zikiwemo bima za moto na wizi, bima za magari ya aina zote pamoja na mitambo, bima za nyumba na vitu vya majumbani, bima za wafanyakazi, bima za maofisini, bima za biashara, bima za wakandalasi, bima za vitu vinavyosafirishwa na bima za afya.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ‘’Maendeleo Insurance Agency ‘’ Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Bank Ndugu Ibrahim Mwangalaba alisema ‘’Kwa kuungana na kampuni ya kimataifa ya Bima yaani, UAP Insurance ni faida kubwa kwa wateja wa Maendeleo Bank Insurance Agency kwani UAP Insurance inauwezo mkubwa wa kubeba bima zote zitakazopelekwa kwao na iwapo itatokea tatizo linalohitaji kugharimia madhara ya kilichowekewa bima, basi mteja wetu hatasumbuka kwani Maendeleo Bank Insurance Agency itafuatilia mambo yote kwa muda mfupi iwezekanavyo ili mteja asisumbuke.

 Mwangalaba aliongeza ‘’ Bima binafsi au za biashara ni muhimu mno katika kulinda kipato na mali za wateja wetu, uanzishwaji wa huduma za bima ni kuishi kwa vitendo katika kauli mbiu yetu ya pamoja nawe katika maendeleo, kwani tunapenda kuona maendeleo ya wateja wetu yakienda mbele si kurudi nyuma kwa matukio yanayoweza kuzuilika kwa kuwa na bima’’

SITOWACHEKEA WACHAFUZI WA MAZINGIRA - MH.MAHENGE


_DSC0298
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira Mh. Dkt. Injinia Binilith Satano Mahenge akipata maelezo kutoka kwa Afisa Mazingira wa Wilaya ya Ilala bw. Abdon Mapunda (wa pili kushoto) alipotembelea bwawa la maji taka la Vingunguti jijini Dar es Salaam.
_DSC0304
Maji machafu yanayotoka katika viwanda mbalimbali vilivyopo Vingunguti jijini Dar es Salaam ambayo hutiririsha maji yake katika mto wa msimbazi, maji ambayo yanahatarisha afya ya binadamu.
_DSC0342
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira Mh. Dkt. Injinia Binilith Satano Mahenge (wa katikati) akizungumza na Menejimenti ya kiwanda cha kuzalisha mafuta ya kupikia (Murza Oil Mills Limited) kilichopo vingunguti jijini Dar es Salaam, wakati wa ziara yake ya kukagua mazingira katika kiwanda hicho na kuwataka watumie mfumo sahihi wa maji taka ili kulinda mazimgira na kuepuka athari mbalimbali kwa wananchi.
_DSC0380
Meneja wa kiwanda cha Murza Oil Mills Limited Bw. Dinesh Kana (wa tatu kushoto) akitoa maelezo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira Mh. Dkt. Injinia Binilith Satano Mahenge (wa nne kushoto) kuhusu mfumo wa maji taka ambao wanautumia katika kiwanda hicho.
_DSC0394
sehemu ya dampo la Pugu Kinyamwezi lilopo jijini Dar es Salaam
_DSC0398
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira Mh. Dkt. Injinia Binilith Satano Mahenge akipata maelezo kutoka kwa Bw. Richard Matari ambaye ni msimamizi wa dampo la Kinyamwezi lililopo Pugu jijini Dar es Salaam, baada ya waziri kuwasili katika dampo hilo na kutaka kujua utendaji wa kazi zao katika kulinda Mazingira.
………………………………………………………………………….

Na Rashda Swedi- VPO
Viwanda vitakavyokiuka masharti na kanuni za kulinda mazingira havina budi kufungiwa mpaka vitakapofuata taratibu na  sheria za utunzaji wa Mazingira.

Hayo yamesemwa hivi karibuni jijini Dar es Salaam  na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Mzingira Mh. Dkt. Injinia Binilith Mahenge alipofanya ziara fupi ya kutembelea kiwanda cha kuzalisha mafuta  (Murza Oil Mills Limited) kilichopo Vingunguti.  

hata hivyo Mheshimiwa Mahenge alisema hayo baada ya kutoridhishwa na mfumo wa maji taka ya kiwanda hicho na kuwaambia waboreshe zaidi mfumo  wa maji taka kwa lengo la kulinda mazingira kwa sababu  wasipofanya hivyo Serikali itachukua hatua ya kukifunga  kiwanda hicho.

wakati huo huo, mwanasheria wa NEMC Bw.Manchale Heche amesema kuwa, kutokana na ziara waliyoifanya pamoja na Mh. Waziri wamegundua mengi na hawatafumbia macho suala la viwanda vinavyotumia magogo,kuni na wale wasiokuwa na mfumo mzuri wa majitaka endapo hawatafuata masharti waliyokubaliana nayo viwanda hivyo vitafungiwa.

Aidha, Waziri alitembelea pia bwawa la maji taka lililopo Vingunguti jijini Dar es Salaam na kugundua kuwa kuna uharibifu mkubwa wa Mazigira, kutokana na maji machafu yanayotoka katika viwanda mbalimbali karibu na eneo hilo kutiririsha maji yao kwenye mabwawa hayo.Kutokana na hilo amewataka  Manispaa kushirikiana na NEMC kuvijua viwanda vinavyopitisha maji machafu moja kwa moja bila kufuata utaratibu uliowekwa.

“Ni wajibu wa kila mtu kulinda mazingira na sio wajibu wa Ofisi ya makamu wa Rais tu kwani Mazingira ni yetu sote na ni muhimu kuyalinda” Mh. Mahenge alisema.Alisisitiza kuwa, huo hautakuwa mwisho wa ukaguzi wa viwanda utaratibu wa kukagua viwanda utaendelea kuangalia Mazingira rafiki kwa wananchi.