Wafanyakazi wa Maendeleo Bank na wa UAP wakiwa katika picha ya Pamoja.
Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo
Bank Ibrahim Mwangala (kulia) akipeana mkono na Nick Itunga Mkurugenzi
mtendaji wa UAP Insurance Nick Itunga baada ya kuzindua huduma ya bima
kupitia Maendeleo Bank
…………………………………………………………………………
Maendeleo Bank imezindua huduma ya bima ikiwa ni lengo la
kuwapatia wateja huduma zote muhimu ndani ya dari moja. Pia inachangia
juhudi za serikali kuboresha na kufikisha elimu na huduma za bima kwa
wananchi wengi ambao hawajafikiwa. Maendeleo Bank Insurance Agency
imeanzishwa ili kuunga mkono mkakati wa Serikali wa huduma za kifedha
jumuishi ambazo zitahamasisha wananchi wengi watumie na wafikiwe na
huduma za kifedha ikiwa ni pamoja na bima.
Katika huduma za bima, Maendeleo
Bank Insurance Agency imejipanga kutoa huduma zote za bima isipokuwa za
maisha. Huduma zifuatazo zinapatikana Maendeleo Bank Insurance Agency:
Bima za binafsi na za biashara zikiwemo bima za moto na wizi, bima za
magari ya aina zote pamoja na mitambo, bima za nyumba na vitu vya
majumbani, bima za wafanyakazi, bima za maofisini, bima za biashara,
bima za wakandalasi, bima za vitu vinavyosafirishwa na bima za afya.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa
‘’Maendeleo Insurance Agency ‘’ Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Bank
Ndugu Ibrahim Mwangalaba alisema ‘’Kwa kuungana na kampuni ya kimataifa
ya Bima yaani, UAP Insurance ni faida kubwa kwa wateja wa Maendeleo Bank
Insurance Agency kwani UAP Insurance inauwezo mkubwa wa kubeba bima
zote zitakazopelekwa kwao na iwapo itatokea tatizo linalohitaji
kugharimia madhara ya kilichowekewa bima, basi mteja wetu hatasumbuka
kwani Maendeleo Bank Insurance Agency itafuatilia mambo yote kwa muda
mfupi iwezekanavyo ili mteja asisumbuke.
Mwangalaba aliongeza ‘’ Bima
binafsi au za biashara ni muhimu mno katika kulinda kipato na mali za
wateja wetu, uanzishwaji wa huduma za bima ni kuishi kwa vitendo katika
kauli mbiu yetu ya pamoja nawe katika maendeleo, kwani tunapenda kuona
maendeleo ya wateja wetu yakienda mbele si kurudi nyuma kwa matukio
yanayoweza kuzuilika kwa kuwa na bima’’
No comments:
Post a Comment