Pages

KAPIPI TV

Thursday, July 24, 2014

SITOWACHEKEA WACHAFUZI WA MAZINGIRA - MH.MAHENGE


_DSC0298
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira Mh. Dkt. Injinia Binilith Satano Mahenge akipata maelezo kutoka kwa Afisa Mazingira wa Wilaya ya Ilala bw. Abdon Mapunda (wa pili kushoto) alipotembelea bwawa la maji taka la Vingunguti jijini Dar es Salaam.
_DSC0304
Maji machafu yanayotoka katika viwanda mbalimbali vilivyopo Vingunguti jijini Dar es Salaam ambayo hutiririsha maji yake katika mto wa msimbazi, maji ambayo yanahatarisha afya ya binadamu.
_DSC0342
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira Mh. Dkt. Injinia Binilith Satano Mahenge (wa katikati) akizungumza na Menejimenti ya kiwanda cha kuzalisha mafuta ya kupikia (Murza Oil Mills Limited) kilichopo vingunguti jijini Dar es Salaam, wakati wa ziara yake ya kukagua mazingira katika kiwanda hicho na kuwataka watumie mfumo sahihi wa maji taka ili kulinda mazimgira na kuepuka athari mbalimbali kwa wananchi.
_DSC0380
Meneja wa kiwanda cha Murza Oil Mills Limited Bw. Dinesh Kana (wa tatu kushoto) akitoa maelezo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira Mh. Dkt. Injinia Binilith Satano Mahenge (wa nne kushoto) kuhusu mfumo wa maji taka ambao wanautumia katika kiwanda hicho.
_DSC0394
sehemu ya dampo la Pugu Kinyamwezi lilopo jijini Dar es Salaam
_DSC0398
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira Mh. Dkt. Injinia Binilith Satano Mahenge akipata maelezo kutoka kwa Bw. Richard Matari ambaye ni msimamizi wa dampo la Kinyamwezi lililopo Pugu jijini Dar es Salaam, baada ya waziri kuwasili katika dampo hilo na kutaka kujua utendaji wa kazi zao katika kulinda Mazingira.
………………………………………………………………………….

Na Rashda Swedi- VPO
Viwanda vitakavyokiuka masharti na kanuni za kulinda mazingira havina budi kufungiwa mpaka vitakapofuata taratibu na  sheria za utunzaji wa Mazingira.

Hayo yamesemwa hivi karibuni jijini Dar es Salaam  na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Mzingira Mh. Dkt. Injinia Binilith Mahenge alipofanya ziara fupi ya kutembelea kiwanda cha kuzalisha mafuta  (Murza Oil Mills Limited) kilichopo Vingunguti.  

hata hivyo Mheshimiwa Mahenge alisema hayo baada ya kutoridhishwa na mfumo wa maji taka ya kiwanda hicho na kuwaambia waboreshe zaidi mfumo  wa maji taka kwa lengo la kulinda mazingira kwa sababu  wasipofanya hivyo Serikali itachukua hatua ya kukifunga  kiwanda hicho.

wakati huo huo, mwanasheria wa NEMC Bw.Manchale Heche amesema kuwa, kutokana na ziara waliyoifanya pamoja na Mh. Waziri wamegundua mengi na hawatafumbia macho suala la viwanda vinavyotumia magogo,kuni na wale wasiokuwa na mfumo mzuri wa majitaka endapo hawatafuata masharti waliyokubaliana nayo viwanda hivyo vitafungiwa.

Aidha, Waziri alitembelea pia bwawa la maji taka lililopo Vingunguti jijini Dar es Salaam na kugundua kuwa kuna uharibifu mkubwa wa Mazigira, kutokana na maji machafu yanayotoka katika viwanda mbalimbali karibu na eneo hilo kutiririsha maji yao kwenye mabwawa hayo.Kutokana na hilo amewataka  Manispaa kushirikiana na NEMC kuvijua viwanda vinavyopitisha maji machafu moja kwa moja bila kufuata utaratibu uliowekwa.

“Ni wajibu wa kila mtu kulinda mazingira na sio wajibu wa Ofisi ya makamu wa Rais tu kwani Mazingira ni yetu sote na ni muhimu kuyalinda” Mh. Mahenge alisema.Alisisitiza kuwa, huo hautakuwa mwisho wa ukaguzi wa viwanda utaratibu wa kukagua viwanda utaendelea kuangalia Mazingira rafiki kwa wananchi.

No comments: