Pages

KAPIPI TV

Friday, July 25, 2014

WAHANGA WA VITA WANENA-KIGOMA

Mkuu wa wilaya ya Kigoma Bw.Ramadhani Maneno  akiweka Ngao na mkuki kama ishara ya kuwakumbuka Mashujaa katika maadhimisho mkoani Kigoma
Mkuu wa wilaya ya Kigoma Bw.Ramadhani Maneno akiingia katika eneo lililotayarishwa kwa ajili ya Maadhimisho ya kumbukumbu ya Mashujaa mkoani Kigoma.
Baadhi ya makamanda wa JWTZ na wananchi wakiwa tayari katika maadhimisho ya kumbukumbu mkoani Kigoma
Gwaride rasmi katika maadhimisho ya Mashujaa.
 Na Magreth Magosso,Kigoma

WAHANGA waliopigana vita mbalimbali hapa nchini waishio Mkoa wa Kigoma,wamewataka vijana wazingatie nidhamu,uaminifu na kujiepusha kudharau matabaka ya jamii yaliyopo ,kwa lengo la kulinda taifa kwa maslai ya kizazi cha leo na siku zijazo.
 
Wakizungumza kwa nyakati tofauti  wahanga hao,kigoma ujiji  jana katika  kuenzi  siku ya kurudi nchini hapa kwa mashujaa waliopigana vita  mbalimbali ikiwemo ya  Uganda,msumbiji,Botswana ,vita vya kijadi na nyinginezo walisema walifanikisha hayo kwa kuzingatia nidhamu ,uaminifu kwa kujitolea  kupigania haki za wananchi husika.
 
Inspekta Mstaafu Jeshi la magereza Juliana Stephana na  Kamishna mstaafu Lt.Joseph Nyamkuzwa walisema  wananchi kwa ujumla hawana budi kumcha mungu ili kudumisha  upendo, ambao ni chachu ya kuthubutu kulinda maliasili na kutoa taarifa   za uvunjifu wa amani  iliyopo.
 
Na Lt. kanali mstaafu Raphael  Kakwila alisihi wazazi watoe elimu njema kwa vijana wao,ili waishi kwa nidhamu bora yenye ushawishi wa kuwajengea uwezo wa kizalendo ambao ni tija ya kuzuia uhalifu kwa maslai ya jamii lengwa.
 
Kwa upande wa mgeni rasmiambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya hapa, Ramadhan Maneno kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huoLt.mstaafu Issa Machibya alisema,siku hiyo ni chachu kwa jamii kutambua thamini  ya amani iliyopo.
 
“majirani zetu hawapendi kuona taifa linarithi amani tuliyoachiwa wahanga hawa walitoa damu na jasho kupigania haki za msingi na taifa sasa vijana ni wakati wenu kulinda nchi kwa kujiepusha na matukio ya uvunjifu wa utulivu,amani kwa kuwabainisha wahalifu” alianisha Maneno.
 
Alisema walitumia  zana  duni za kivita  lakini kutokana na uzalendo walionao walijitoa kwa dhati   kupigania maslai ya taifa ili kuipa nchi  heshima .huku awaasa wananchi watoe taarifa kwa vyombo vya usalama ili kudhibiti majanga ya uhalifu.
 
Aidha Shekhe Mkuu  Bakwata wa hapa Hassan Iddi  alisema wanasiasa,wananchi na viongozi wa dini wanajukumu la kuelimisha waumini wao juu ya faida ya amani na athari zake,kwa lengo la kuboresha ustawi wa umaa.
 
Akizungumzia utata Rasimu mpya ya katiba Shekhe Iddi alionya wanasiasa waache utashi wa maslai  binafsi na badala yake wanzingatie  misingi bora  ya wahanga waliothubutu  kufa ili kutetea umaa husika.

No comments: