chuo cha Kitanzani Islamic center kilichoko mjini Iringa. (Picha zote na Denis Mlowe)
Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji
Peter Msigwa akikabidhi msaada wa Sukari, kwa Kaimu Shekhe Mkuu wa Mkoa
wa Iringa, Abubakari Chalamila kwa ajili ya kituo cha Kitanzani Islamic
Na Denis Mlowe,Iringa
MBUNGE wa Iringa Mjini(Chadema)
Mchungaji Peter Msigwa amekikabidhi chuo cha Kitanzani Islamic Center
msaada wa Sukari,Unga wa Ngano, tende na mafuta ya kupikia ikiwa ni
utaratibu wake wa kila mwaka kukisaidia chuo hicho.
Akizungumza wakati wa kukabidhi
msaada huo jana kwa Shekhe Mkuu wa Mkoa Iringa Abubakar Chalamila,
Mchungaji Msigwa alisema kuwa lengo la kugawa kipindi hiki ni kuwaunga
mkono Waislamu katika mfungo wa Ramadhani na kuwakumbuka wale wote
wanaoishi katika mazingira magumu.
Mchungaji Msigwa alisema ni jukumu
la wadau kuweza kuwasaidia wale wote bila kujali itikadi za vyama kwa
kuwa binadamu wote ni wamoja kwa sasa.
Mchungaji Msigwa alikabidhi tambi
katoni zaidi ya katoni 50, katoni 40 za mafuta ya kupikia, kilo 250 za
unga wa ngano na sukari kilo 750 vyote vikiwa na jumla ya thamani zaidi
ya shilingi milioni 1.5.
Alisema ataendelea kutoa msaada kwa vituo vingine vya watoto yatima na wasiojiweza katika kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhan.
Akishukuru kwa msaada huo Kwa
niaba ya chuo cha Kitanzani Islamic Center chenye jumla ya wanafunzi 120
ambao wanachukua mafunzo ya dini ya kiislamu Kaimu Shekhe Mkuu wa Mkoa
Iringa, Abubakar Chalamila alisema ni jambo la kujivunia kuwa na mbunge
asiyechagua itikadi za dini na mbunge ni akichaguliwa anakuwa wa watu
wote bila kubagua watu wake.
“Namshukuru sana Msigwa kwa kuweza
kutoa msaada huu na utafikishwa kwa wale wote waliolengwa kupewa na
hasa wale wasiojiweza ndio watafaidika na msaada huu wa mbunge wa iringa
mjini.” Alisema |Chalamila
Chalamila aliwataka wadau wengine
kuwakumbuka watu wasiojiweza na wanaoishi katika mazingira magumu mara
kwa mara kwa kuwa ni thawabu kubwa kuweza kuwasaidia.
No comments:
Post a Comment