Pages

KAPIPI TV

Thursday, July 24, 2014

"AJIRA YA VIJANA KWA USAFIRI WA BAISKELI TABORA NI MOJA KATI YA AJIRA TULIZOZITEGEMEA"

Usafiri baiskeli mkoani Tabora wazidi kuimarisha ajira kwa vijana hatua ambayo sasa imefanya kuwepo kwa ongezeko la vijana wengi mjini kuliko ilivyokuwa hapo awali,kwa hivi sasa imeshuhudiwa baadhi ya vijana wa vijiji jirani na Tabora mjini wamekuwa wakijidamka mapema asubuhi kuja mjini kufanya kazi ya kusafirisha abiria kwa usafiri huo wa baiskeli na kujipatia fedha kwa ajili ya kujikimu kimaisha wakati huu wa majira ya kiangazi ambapo vijijini hakuna shughuli za kilimo.Hata hivyo licha ya vijana hao kupata fursa ya kujiajiri wenyewe lakini wamekuwa katika mazingira hatarishi kutokana na ukweli kwamba wengi wao hawajui sheria za usalama barabarani na hivyo kujikuta wanavunja sheria na kusababisha ajali zinazochangia vifo visivyo vya lazima au kubaki na ulemavu wa kudumu.Jambo hili linahitaji kuchukuliwa hatua ya kuwadhibiti vijana hao bila kuathiri mwenendo mzima wa ajira zao kwakuwa wengi wao kutokana na ajira hizo wanategemewa na familia zao.Ajira za vijana kwa kutumia usafiri wa baiskeli katika mtazamo wa harakaharaka ni dhahiri kwamba ni ajira tulizozitegemea kwa kile kinachoonekana katika fikra za haraka kwa vijana waliowengi ni kujipatia fedha za chapchap kupitia mpango huo usio rasmi.Aidha kwa upande mwingine ni kweli kwamba kwasasa mkoa wa Tabora hakuna viwanda au kazi nyingine zaidi ya kupata vibarua kwenye majengo ya watu binafsi ambayo malipo yake ni kati ya shilingi 3000 na 5000 kwa kutwa nzima.Ukiachilia mbali ajira kwenye makampuni ya ulinzi imekuwa na usumbufu kwa vijana kutokana na kutolipwa mishahara kwa wakati jambo ambalo linawafanya vijana wengi kuona ni bora zaidi aendeshe baiskeli kuanzia majira ya saa 12 asubuhi hadi saa tatu usiku ambapo hujipatia wastani wa kiasi cha shilingi elfu kumi.Hii inawafanya idadi kubwa vijana kuingia kwenye ajira hii bila kikwazo kwani kwa wanaoishi mjini huweza kumudu kulipa kodi ya pango ya shilingi elfu kumi kwa mwezi lakini hata kuendesha maisha yake na familia ya watu wanne yaani Mke,watoto wawili na yeye mwenyewe.Kuendesha baiskeli hakuhitaji leseni wala kikwazo chochote kinachowabana kisheria zaidi ya kujaza upepo kwenye tairi za baiskeli na kuanza kunyonga pedeli kulingana na uzito wa mteja aliobebwa kwenye usafiri huo.Ni kazi nyepesi kama waionavyo vijana wenyewe.Lakini kwa wachunguzi wa mambo wanasema kuwa hata wimbi la vibaka katika maeneo mbalimbali Tabora mjini limepungua kwa kiasi kikubwa kwakuwa kijana anayejihusisha na ajira hiyo ya usafiri wa baiskeli anapomaliza muda wake hiyo saa tatu usiku huwa amechoka sana hata hawezi kwenda kukaa  vijiweni na kujihusisha na vitendo viovu. 

Wednesday, July 23, 2014

BABAREVO AMTWANGA SHEMEJI YAKE MSIBANI-KIGOMA

MSANII  wa Muziki wa kizazi  kipya ( Bongo fleva) Clayton Revocatus (Baba Revo) anadaiwa kumshushia kichapo shemeji yake Pili Abdallah kwa madai ya kutaka shemeji mtu arudishe mali za marehemu mdogo wake Patrick Revocatus ambaye,amefariki mwishoni mwa wiki iliyopita mwaka huu.
 
Akizungumza na mwandishi wa KAPIPIJhabari.COM kigoma Ujiji juzi Pili alisema,chanzo cha kupigwa na msanii huyo ni kutokana na  msanii huyo kudai cheni aina ya silva  yenye thamani y ash.100.000 ambayo aliuziwa na mdogo na Mbunge wa Kigoma Kaskazi   Bashir  Kabwe aliyokuwa akiivaa marehemu enzi ya uhai wake.
 
“marehemu alikuwa hana mali zaidi ya sh.10,000 tu ilikuwa  katika pochi yake,ambayo nilitumia kumpeleka hospitali ya rufaa maweni,shemeji na nduguze walimtenga  marehemu wakati anaugua, haja zote anamalizia kitandani  na nilimsitiri ” alisema Pili.
 
Marehemu alivunjika mguu ambao  hakuupatia tiba kwa wakati na Julai ,18,2014 alizidiwa ,kwa kushirikiana na rafiki zake wakampeleka hospitali hiyo na usiku wa siku hiyo alifariki pasipo msanii huyo kuonyesha  hisia za huzuni  na  baada ya mazishi alimtaka shemeji yake arudishe vitu vya marehemu.
 
Mama mzazi wa mpenzi wa marehemu Janeth John  alisema  hakumuoa bali waliishi kwa kuibana yapata miezi sita sanjari na kufahamu mahusiano yao ambayo alimuonya mwanae kwa muda mrefu achane na familia hiyo.
 
Alisema ameingia gharama ya kulipa cheni hiyo ambayo binti yake anadai hakuchukua  sanjari na sh.10,000 iliyokuwa kwenye waleti ya marehemu kwa lengo la kuondoa shari na  msanii huyo.
 
Kwa upande wa msanii huyo Baba Revo alipohojiwa na gazeti hili akiri kuvurugu kwenye msiba wa nduguye na kusisitiza marehemu hakuwa na mali zaidi ya wallet na cheni ambayo shemeji mtu alipaswa awape wahusika.
 
Alisema  marehemu alitakiwa apasuliwe mguu lakini shemeji yake alimtorosha hospitalini marehemu na kudai ana haki  kuelimisha na kuadibisha  jamii husika na kuonya  wanawake waache ukatili hasa wa kunyanyasa wanaume .
 
Kamanda wa Polisi mkoani humo,Frasser Kashai alipoulizwa juu ya hilo alisema hajui na kuvilaumu baadhi ya vituo vidogo  vya Polisi vinachangia kuzorotesha baadhi ya matukio kufika kwa wakati katika vituo vikubwa na kudai kulifuatilia suala hilo .
 
Msanii huyo ni mkazi wa mtaa wa Kitabwe kata ya mwanga kusini wilaya ya kigoma mkoani hapa,ameshangaa shemeji huyo kufungulia jalada la kesi la mashambulizi kituo cha kati ambapo yeye alimfungulia kituo cha msufini wakati huohuo Kamanda Kashai anasema ni ruksa ilimradi pawe karibu na eneo analoishi mlalamikaji.

ACT YAITOLEA MACHO UKAWA - KIGOMA



Na Magreth Magosso,Kigoma

Mwenyekiti  wa  chama cha  ACT Taifa  Lucas  Limbu  aomba  umoja wa Katiba ya watanzania UKAWA wakaze buti kuishinikiza serikali ya ccm , ikubali mabadiliko ya mfumo wa serikali tatu kwa mujibu wa mapendekezo ya umma kupitia Rasimu mpya ya katiba.
 
Akitoa kauli hiyo kigoma ujiji ,Limbu alidai serikali inakaidi kupokea maboresho ya katiba ya awali ya mwaka 1977 kupitia mchakato wa maboresho ya rasimu mpya ambapo Jaji mstaafu Sinde Warioba aliikabdihi rasmi kwa wajumbe husika ili kuboresha rasimu hiyo ambayo ni mwiba kwa viongozi wachache  waliozoea  mfumo nyonyaji ambao unazalisha  mabwenyenye wanaotumika kulinda maslai ya wachache.
 
“ccm imeacha kuenzi na kutumia  falsafa ya hayati Mwalimu Nyerere sanjari na misingi ya katiba ambapo misingi ni fursa kwa kila mtanzania kunufaika na rasilimali zilizopo kwa lengo la kuondoa matabaka katika jamii ili kuepusha vurugu zinazolinyemelea taifa kwa ujumla” alibainisha Limbu
 
Alisema Ukawa wasikubali kununuliwa na chama tawala ili kudhoofisha mawazo ya wengi dhidi ya mfumo bora wa serikali ,ambao utaondoa mfumo dume  unaochangia  vyama vya upinzani kushindwa kushika hatamu ya mabadiliko kwa jamii husika.
 
Alishauri serikali itumie mfumo pendekezwa  juu ya awamu za utawala dhidi ya urais uwe wa mlinganio sawa  wa muungano kulingana na kipindi  husika ,kwa dhati ya kujenga umoja na mshikamano wa taifa,ambapo alitaka ngazi ya urais ufuatwe  yaani Bara na visiwani kwa kuzingatia usawa na haki ya utawala wa nchi.
 
Pia alisema  kitendo cha Jaji mkuu wa serikali kumtusi Mbunge wa kigoma kaskazini hakistahili kuvumiliwa na kumtaka rais  Jakaya Kikwete achukue hatua za kumwajibisha jaji huyo,ambaye ameonesha utovu wa nidhamu kwa wananchi na dunia kwa ujumla.

Naye  mwenyekiti Baraza la wazee chama hicho wa hapa Jafari Kasisiko alisema jamii ifunguke kubaini vyama sahihi vyenye lengo na nia ya kutetea maslai ya wengi na waondokane na tabia ya kukumbatia vyama vyenye kuwaangamiza pasipo wenyewe kubaini

POLISI APONGEZWA BAADA YA KUKATAA RUSHWA YA WATUMIAJI WA DAWA ZA KULEVYA-TABORA

Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP Suzan Kaganda akimpongeza na kumpa zawadi ya pesa Mkaguzi wa Polisi Harun Kasubi baada ya kufanikiwa kuwakamata watu wapatao kumi na wawili waliokuwa wamejifungia ndani ya Guest house inayofahamika kwa jina la KENIOS wakiwa wanajidunga dawa za kulevya ambapo watu hao walitaka kumpa rushwa ya shilingi 90,000/=ili waachiwe huru.
Baadhi ya dawa za kulevya na vifaa vya matumizi ya dawa hizo zilizokamatwa zikiwa zinatumiwa na watu hao kumi na wawili waliokamatwa KENIOS GUEST HOUSE huko eneo la kata ya Isevya manispaa ya Tabora.
Kamanda wa Polisi ACP Suzan Kaganda ameuambia mtandao huu kuwa waliokamatwa katika operesheni ya kuwasaka watumiaji,wauzaji na wasambazaji wa dawa za kulevya mkoani Tabora ni Hamisi Athuman Mbao(39) ,Issa Abdallah(22),Ally Bakar(34),Densi Petro(34)Mrisho Shaban(22)Ramadhan Mbade(40)Haji Muki(40),Said Kasumari(24),Shaban Haruna(25)David Male(43)Ramadhan Hamis na Paschal Robert.

Kamanda Suzy amesema watu hao baada ya kukamatwa walitaka kutoa rushwa ya shilingi elfu tisini kwa kiongozi wa timu ya makachero wanaofuatilia dawa za kulevya mkoani Tabora ambaye ni mkaguzi wa Polisi Harun Kasubi ambapo alikataa na kuwafikisha kituo kikubwa cha Polisi Tabora.

 

TOFAUTI ZA DINI ZISIWAGAWE WATANZANIA , MWINYI.

Futari - 1
Futari - 3
Rais Mstaafu wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi akiwasili katika viwanja vya Karimjee kuhudhuria Futari iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki (wa pili kutoka kushoto) kwa watoto yatima kutoka vituo mbalimbali vya kulelea watoto hao vya jiji la Dar es salaam. Wengine wanaoonekana kutoka kulia ni Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es salaam, Kamishna Suleiman Kova na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Alhadi Mussa Salum.
Futari - 7
Baadhi ya akina mama na watoto waliohudhuria Futari hiyo wakipata Chakula.
Futari -4
Baadhi  watoto yatima kutoka vituo mbalimbali vya kulelea watoto hao vya jiji la Dar es salaam wakijumuika pamoja katika Futari iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki.
Futari -5
Rais mstaafu wa Awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa Futari iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam kwa watoto yatima kutoka vituo mbalimbali vya kulelea watoto hao vya jiji la Dar es salaam akijumuika pamoja  na watoto hao na wageni mbalimbali walioalikwa katika Futari hiyo.
Futari- 6
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Alhadi Mussa Salum (wa kwanza kushoto) na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahmani Kinana wakijumuika  katika Futari hiyo.
Futari -9
Futari -11
Rais wa Tanzania wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa Futari iliyoandaliwa na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam  akisisitiza umuhimu wa kulinda na kutunza amani iliyopo kwa kuendelea kudumisha upendo na ukarimu ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa maagizo yaliyomo katika vitabu vitakatifu.
Futari -12
Mkuu wa mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya (kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Songea Dkt. Christine Ishengoma(kulia) wakiungana na viongozi wengine  kushiriki  Futari iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam kwa watoto yatima kutoka katika vituo mbalimbali katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam.
Futari-2
Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es salaam, Kamishna Suleiman Kova (katikati) akifafanua jambo kwa viongozi wa mkoa wa Dar es salaam  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Bw. Saidi Meck Sadiki (wa pili kutoka kulia), Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bw. Raymond Mushi(kulia) na  Mkuu wa wilaya ya Temeke Bi. Sophia Mjema (kushoto) wakati wa Futari iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa huo katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
Na. Aron Msigwa –MAELEZO.
 Dar es salaam.
 
Rais mstaafu wa awamu ya pili , Ali Hassan Mwinyi ,amewataka watanzania kuwa makini kwa kutoruhusu tofauti za dini zilizopo hapa nchini kuwa chanzo cha mgawanyiko miongoni mwao.
 
Kauli hiyo ameitoa jana usiku jijini Dar es salaam wakati wa Futari iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Saidi Meck Sadiki  kwa watoto wanaoishi katika vituo vya kulelea watoto yatima, wananchi na viongozi mbalimbali iliyofanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam.
 
Mzee Ali Hassan Mwinyi ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa Futari hiyo amesema kuwa kila Mtanzania bila kujadili itikadi na dini aliyonayo ana wajibu wa kulinda na kutunza amani iliyopo kwa kuendelea kudumisha upendo na ukarimu kwa wenzake ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa maagizo yaliyomo katika vitabu vitakatifu.
 
“Nawasihi Watanzania wenzangu tuendelee kupendana, tuwe wamoja katika kushirikiana, kamwe tusiruhusu wala kukubali mgawanyiko wa dini wala itikadi zetu” Amesisitiza.
 
Amewashukuru viongozi wa mkoa wa Dar es salaam wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Saidi Meck Sadiki kwa uamuzi walioufanya wa kuandaa Futari iliyowaunganisha watoto yatima, wananchi na viongozi mbalimbali  bila kujadili itikadi na dini zao ikiwa ni ishara ya kuonyesha upendo na ukarimu walio nao.
 
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Saidi Meck Sadiki akizungumza wakati wa Futari hiyo aliyowaandalia wageni hao amesema kuwa serikali ya mkoa   inaendelea kutekeleza  mipango mbalimbali ya maendeleo ikiwemo  ukarabati  na ujenzi wa miundombinu iliyoharibiwa vibaya wakati wa msimu wa  mvua jijini Dar es salaam.
 
Bw. Sadiki ameziagiza Halimashauri za Wilaya za Temeke, Ilala na Kinondoni  na Wakala wa Barabara (TANROAD) mkoa wa Dar es salaam kuhakikisha kuwa wanarejesha hali ya kupitika kwa barabara iliyokuwepo mwanzo ili kuwaondolea kero ya usafiri wananchi.
 
Amezitaka mamlaka hizo kutumia fedha za ndani na zile zilizotolewa na Serikali Kuu kukamilisha ukarabati wa miundombinu  hiyo yakiwemo madaraja yaliyosombwa na maji kwa muda muafaka ili kuruhusu magari kuweza kufika katika maeneo hayo.
 
Katika hatua nyingine Bw. Meck Sadiki ametoa wito kwa wakazi wa jiji la Dar es salaam kushiriki kikamilifu katika suala la usafi na uhifadhi wa mazingira kwa kujenga utaratibu wa kusafisha mazingira ya jiji ili kulinda heshima ya jiji huku akisisitiza kuwa dini zote zinamtaka mwanadamu awe mwadilifu na mwenye kuzingatia usafi.
 
Amezitaka mamlaka zinazosimamia utekelezaji wa sheria za kuhifadhi mazingira jijini Dar es salaam kufanya kazi kwa kuzingatia weledi ili kuhakikisha maeneo yote ya jiji yanaendelea kuwa katika hali ya usafi.
Naye Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhadi Mussa Salum akuzungumza wakati wa Futari hiyo ameeleza kuwa viongozi wa dini na serikali kote nchini wanalo jukumu kubwa la kuwaongoza wananchi kutenda mema na kuendelea kuvumilia.

"MWANDISHI WA HABARI WA REDIO YA MHESHIMIWA RAGE MBARONI KWA KUJIFANYA USALAMA WA TAIFA,UONGOZI WA V.O.T WAMKANA

Kijana mwandishi wa habari  akiwa mbaroni baada ya kukamatwa na makachero wa Jeshi la Polisi Tabora mjini akijifanya ni Afisa usalama wa Taifa,Mwandishi huyu ambaye anafahamika kwa jina la Mussa Mbeko(24)aliwahi kufanya kazi katika kituo cha Redio Voice of Tabora kinachomilikiwa na Mheshimiwa mbunge wa Jimbo la Tabora mjini Bw.Ismail Rage ambapo hata hivyo Uongozi wa VOT umesema kuwa tayari ulikwisha mfukuza kijana huyo kwa makosa mbalimbali ya Utapeli hasa kujifanya usalama wa taifa.  
Kitambulisho alichokuwa akikitumia Mussa kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu

Uongozi wa Jeshi la Polisi wilaya ya Tabora ulimfikisha  Mwandishi huyo mbele ya Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP  Suzan Kaganda
Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP Suzan Kaganda akiwaonesha waandishi wa habari kitambulisho kilichokuwa kikitumiwa na Mussa Mbeko akijifanya ni Afisa Usalama wa Taifa.


TRA YAFUTURISHA BAADHI YA WANANCHI TABORA

Baadhi ya waalikwa akiwemo Meneja wa kanda wa Bima ya Afya mkoa wa Tabora Bw.Emmanuel Adina wakishiriki hafla ya Futari iliyoandaliwa na Mamlaka ya mapato Tanzania TRA katika hotel ya ORION Tabora mjini.
Baadhi ya viongozi wa Serikali na vyama vya siasa akiwemo Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake UWT mkoa wa Tabora Bi.Mwanne Mchemba walishiriki katika hafla hiyo ya Futari
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Tabora mjini Bw.Moshi Abraham maarufu Nkokota naye alikuwa ni mmoja kati ya wageni waalikwa
Baadhi ya walipa kodi ambao ni wamiliki wa makampuni ya mabasi Tabora kushoto ni  Bw.Medd Nassor Hamdani,mmiliki wa mabasi ya NBS na Bw.Humud Nassor ambaye ni mmiliki wa mabasi ya SUPER SONIC nao walikuwa ni miongoni mwa wageni waalikwa 

Baadhi ya walipa kodi wafanyabishara wa Tabora
Baadhi ya watumishi wa TRA Tabora nao walishiriki hafla hiyo ya Futari
Mkurugenzi wa Fedha  wa TRA Tanzania Bw.Salehe Mshoro akizungumza katika hafla hiyo ya Futari ambapo alizungumzia mafanikio makubwa ya ukusanyaji wa kodi ya mapato nchini huku akitumia fursa hiyo kuwashukuru wafanyabishara kwa ushirikiano wanaoitapatia TRA
Katibu wa ccm mkoa wa Tabora Bw.Idd Ali Ame akizungumza katika hafla hiyo ya Futari
Mmoja kati ya viongozi wa dini ya kiislam Tabora mjini Sheikh Issa Bilali akisoma dua maalum wakati wa hafla hiyo.
Mjumbe wa NEC Bw.John Mchele akipeana mkono na Mkurugenzi wa fedha wa TRA nchini Bw.Mshoro,pembeni ni Meya wa halmashauri ya manispaa ya Tabora Bw.Ghulam Dewij











BENKI YA EXIM TANZANIA YAANDAA FUTARI KWA WATEJA WAKE WA MKOANI TANGA


PIX 1
Baadhi ya wateja wa Benki ya Exim Tanzania na wafanyakazi wakifuatilia yaliyokuwa yakizungumzwa wakati wa futari iliyoandaliwa na benki hiyo mkoani Tanga kwa ajili ya wateja wake. Picha na mpiga picha wetu.
PIX 2
Meya wa Jiji la Tanga, Mhe. Omary Uledi, ambaye pia ni mgeni rasmi (wapili kulia)  akizungumza wakati wa futari iliyoandaliwa na Benki ya Exim Tanzania kwa wateja wake wa mkoani Tanga hivi karibuni. Wa pili kushoto ni Meneja wa Benki ya Exim Tawi la Tanga, Deogratius Makwaia, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Suleiman Lighuchu (watatu kushoto)na Katibu wa Bakwata wa Mkoa, Bw. Mohamed Riami (wa kwanza kulia). Picha na mpiga picha wetu.
PIX 3
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Suleiman Lighuchu akizungumza wakati wa futari iliyoandaliwa na Benki ya Exim Tanzania kwa wateja wake wa mkoani Tanga hivi karibuni. Wa pili kushoto ni Meneja wa Benki ya Exim Tawi la Tanga, Deogratius Makwaia, Mgeni Rasmi Meya wa Jiji la Tanga, Mhe. Omary Uledi (Wa pili kulia)na Katibu wa Bakwata wa Mkoa, Bw. Mohamed Riami (wa kwanza kulia). Picha na mpiga picha wetu.
PIX 4
Baadhi ya wateja wa Benki ya Exim Tanzania na wafanyakazi wakichukua vyakula mbali mbali vilivyoandaliwa malum kwa ajili ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo mkoani Tanga kwa ajili ya wateja wake. Picha na mpiga picha wetu.

MEYA WA ILALA JERRY SILAA AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA BARABARA YA UKONGA KUELEKEA MAZIZINI MPAKA MOSHI BAR


Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya
Ilala Jerry Silaa Jana amefanya ziara fundi ya ukaguzi wa ujenzi wa barabara ya ukonga Moshibar
kilometa 3 kiwango cha changalawe awamu yakwanza. Ikiwa ni utekelezaji wa miradi ya
dharura kulingana na uharibifu wa miundo mbinuulitokea baada ya Mvua kubwa. Mradi huo
ambao unaghalimu kiasi cha shilingi millioni 90.Pesa za Ujenzi huohizo zinatoka Halmashauri ya Manispaa ya Ilala.Pia Barabara hiyo itawekwa Lami kwa awamu ya pili ndani ya mwaka huu kwa kilomita tatu.Picha Zote Na Dj Sek Blog

Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa wa Kwanza kushoto akiwa na Mhandisi wa Barabara(mwenye shati Jeusi) pamoja na Diwani wa ukonga Elizabeth Mbano(katikati) na wa kwanza Kulia ni Mhandisi wa Manispaa Bwana Muhinda Kassimu wakitazama maendeleo ya ujenzi wa kipande cha barabara kutoka ukonga-mazizini mpaka moshi bar.
Mhandisi wa Manispaa Bwana Muhinda Kassimu Akielezea namna ambavyo awamu ya kwanza ya ukarabati wa barabara hiyo utakavyo kuwa  kwa kiwango cha changarawe na itafuata awamu ya pili ambayo ni Lami.
Diwani wa ukonga Elizabeth Mbano akiongea na vyombo vya habari kushukuru Manispaa kwa kuikumbuka barabara hiyo kwani imekuwa ikileta sana shida ya usafiri kwa wakazi wa eneo hilo hasa kipindi cha mvua.
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa Akielezea namna Barabara hiyo itakavyotengenezwa na pia akasisitiza kwamba Pesa za Ujenzi wa Barabara Hiyo zimetoka ndani ya manispaa na si Vinginevyo.
Greda likirekebisha Barabara ya Ukonga-mazizini kulekea moshi bar
Mwonekano wa Bara barabara hiyo
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akimwelezea mkazi wa mazizini namna mradi wa barabara hiyo ulivyo.
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akimuelezea kwa kumuonyesha mkazi wa mazizini gharama za mradi huo na pia pesa za mradi huo kutoka ndani ya Halmashauri na si vinginevyo.
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akiwa amempa nafasi mkazi wa Mazizini kupitia majalada yenye maelezo na mikataba ya ujenzi wa barabara hiyo
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akiongea na wakazi wa mazizini waliotaka kujua mradi utachukua mda gani na utaisha lini.