Pages

KAPIPI TV

Wednesday, July 23, 2014

ACT YAITOLEA MACHO UKAWA - KIGOMA



Na Magreth Magosso,Kigoma

Mwenyekiti  wa  chama cha  ACT Taifa  Lucas  Limbu  aomba  umoja wa Katiba ya watanzania UKAWA wakaze buti kuishinikiza serikali ya ccm , ikubali mabadiliko ya mfumo wa serikali tatu kwa mujibu wa mapendekezo ya umma kupitia Rasimu mpya ya katiba.
 
Akitoa kauli hiyo kigoma ujiji ,Limbu alidai serikali inakaidi kupokea maboresho ya katiba ya awali ya mwaka 1977 kupitia mchakato wa maboresho ya rasimu mpya ambapo Jaji mstaafu Sinde Warioba aliikabdihi rasmi kwa wajumbe husika ili kuboresha rasimu hiyo ambayo ni mwiba kwa viongozi wachache  waliozoea  mfumo nyonyaji ambao unazalisha  mabwenyenye wanaotumika kulinda maslai ya wachache.
 
“ccm imeacha kuenzi na kutumia  falsafa ya hayati Mwalimu Nyerere sanjari na misingi ya katiba ambapo misingi ni fursa kwa kila mtanzania kunufaika na rasilimali zilizopo kwa lengo la kuondoa matabaka katika jamii ili kuepusha vurugu zinazolinyemelea taifa kwa ujumla” alibainisha Limbu
 
Alisema Ukawa wasikubali kununuliwa na chama tawala ili kudhoofisha mawazo ya wengi dhidi ya mfumo bora wa serikali ,ambao utaondoa mfumo dume  unaochangia  vyama vya upinzani kushindwa kushika hatamu ya mabadiliko kwa jamii husika.
 
Alishauri serikali itumie mfumo pendekezwa  juu ya awamu za utawala dhidi ya urais uwe wa mlinganio sawa  wa muungano kulingana na kipindi  husika ,kwa dhati ya kujenga umoja na mshikamano wa taifa,ambapo alitaka ngazi ya urais ufuatwe  yaani Bara na visiwani kwa kuzingatia usawa na haki ya utawala wa nchi.
 
Pia alisema  kitendo cha Jaji mkuu wa serikali kumtusi Mbunge wa kigoma kaskazini hakistahili kuvumiliwa na kumtaka rais  Jakaya Kikwete achukue hatua za kumwajibisha jaji huyo,ambaye ameonesha utovu wa nidhamu kwa wananchi na dunia kwa ujumla.

Naye  mwenyekiti Baraza la wazee chama hicho wa hapa Jafari Kasisiko alisema jamii ifunguke kubaini vyama sahihi vyenye lengo na nia ya kutetea maslai ya wengi na waondokane na tabia ya kukumbatia vyama vyenye kuwaangamiza pasipo wenyewe kubaini

No comments: