Pages

KAPIPI TV

Wednesday, July 23, 2014

BABAREVO AMTWANGA SHEMEJI YAKE MSIBANI-KIGOMA

MSANII  wa Muziki wa kizazi  kipya ( Bongo fleva) Clayton Revocatus (Baba Revo) anadaiwa kumshushia kichapo shemeji yake Pili Abdallah kwa madai ya kutaka shemeji mtu arudishe mali za marehemu mdogo wake Patrick Revocatus ambaye,amefariki mwishoni mwa wiki iliyopita mwaka huu.
 
Akizungumza na mwandishi wa KAPIPIJhabari.COM kigoma Ujiji juzi Pili alisema,chanzo cha kupigwa na msanii huyo ni kutokana na  msanii huyo kudai cheni aina ya silva  yenye thamani y ash.100.000 ambayo aliuziwa na mdogo na Mbunge wa Kigoma Kaskazi   Bashir  Kabwe aliyokuwa akiivaa marehemu enzi ya uhai wake.
 
“marehemu alikuwa hana mali zaidi ya sh.10,000 tu ilikuwa  katika pochi yake,ambayo nilitumia kumpeleka hospitali ya rufaa maweni,shemeji na nduguze walimtenga  marehemu wakati anaugua, haja zote anamalizia kitandani  na nilimsitiri ” alisema Pili.
 
Marehemu alivunjika mguu ambao  hakuupatia tiba kwa wakati na Julai ,18,2014 alizidiwa ,kwa kushirikiana na rafiki zake wakampeleka hospitali hiyo na usiku wa siku hiyo alifariki pasipo msanii huyo kuonyesha  hisia za huzuni  na  baada ya mazishi alimtaka shemeji yake arudishe vitu vya marehemu.
 
Mama mzazi wa mpenzi wa marehemu Janeth John  alisema  hakumuoa bali waliishi kwa kuibana yapata miezi sita sanjari na kufahamu mahusiano yao ambayo alimuonya mwanae kwa muda mrefu achane na familia hiyo.
 
Alisema ameingia gharama ya kulipa cheni hiyo ambayo binti yake anadai hakuchukua  sanjari na sh.10,000 iliyokuwa kwenye waleti ya marehemu kwa lengo la kuondoa shari na  msanii huyo.
 
Kwa upande wa msanii huyo Baba Revo alipohojiwa na gazeti hili akiri kuvurugu kwenye msiba wa nduguye na kusisitiza marehemu hakuwa na mali zaidi ya wallet na cheni ambayo shemeji mtu alipaswa awape wahusika.
 
Alisema  marehemu alitakiwa apasuliwe mguu lakini shemeji yake alimtorosha hospitalini marehemu na kudai ana haki  kuelimisha na kuadibisha  jamii husika na kuonya  wanawake waache ukatili hasa wa kunyanyasa wanaume .
 
Kamanda wa Polisi mkoani humo,Frasser Kashai alipoulizwa juu ya hilo alisema hajui na kuvilaumu baadhi ya vituo vidogo  vya Polisi vinachangia kuzorotesha baadhi ya matukio kufika kwa wakati katika vituo vikubwa na kudai kulifuatilia suala hilo .
 
Msanii huyo ni mkazi wa mtaa wa Kitabwe kata ya mwanga kusini wilaya ya kigoma mkoani hapa,ameshangaa shemeji huyo kufungulia jalada la kesi la mashambulizi kituo cha kati ambapo yeye alimfungulia kituo cha msufini wakati huohuo Kamanda Kashai anasema ni ruksa ilimradi pawe karibu na eneo analoishi mlalamikaji.

No comments: