Pages

KAPIPI TV

Thursday, April 10, 2014

NHIF YAKUTANA NA WAKUU WA SHULE ZA SEKONDARI MIKOA YA SHINYANGA,SIMIYU NA TABORA.

Afisa Matekelezo na Uratibu NHIF mkoa wa Tabora Bw.Hema Daniel akizungumza katika mkutano wa Wakuu wa Shule za Sekondari kanda ya Magharibi ambapo aliwataka  wakuu hao kuwahamasisha wanafunzi kujiunga na mfuko wa afya ya Jamii.
Bw.Hema alipata fursa pia ya kujibu maswali ya wakuu hao wa Shule za Sekondari kuhusu changamoto za mfuko huo ambao umeboreshwa na kupanua wigo kwa kuhakikisha kila mwananchi anajiunga na kunufaika na mfuko huo wa afya ya Jamii

Baadhi ya wakuu wa shule za Sekondari  mikoa ya Tabora,Shinyanga na Simiyu wakimsikiliza kwa makini Afisa Matekelezo na Uratibu NHIF mkoa wa Tabora Bw.Hema wakati alipokuwa akizungumza na wakuu hao juu ya mfuko wa Afya ya Jamii.

CHAMA CHA AMCOS NGURUKA KUFANYIWA UPYA UKAGUZI WA HESABU

Na Magreth Magosso,Kigoma

CHAMA cha wakulima wa zao la tumbaku cha Hongera Amcos Kata ya Nguruka wilayani Uvinza Mkoa wa Kigoma, kimetakiwa kifanyiwe upya ukaguzi wa mahesabu,kutokana na sintofahamu ya mwenendo wa viongozi wake kutokuzingatia  misingi ya utawala bora,hali inayowakwaza wananchama wa chama hicho.

Kauli hiyo imekuja baada ya Naibu Waziri wa kilimo na chakula Godfrey Zambi kubainika kuwa kuna baadhi ya viongozi wanakitumia chama  hicho kwa maslai yao binafsi badala ya kuwakwamua wahusika ili waondokane na umaskini katika familia zao na jamii husika.

Aidha,Waziri huyo aliitaka Ofisi ya Mlajisi Mkuu wa mjini Dododoma,asikilize kero za wananchama wa chama hicho wakiwemo wanachama tisa ambao wamefukuzwa bila kanuni,taratibu na sheria kwa misingi ya kujenga utawala bora ili kujenga usawa na haki kwa kila mwanachama.

Naye Afisa Mlajisi makao Makuu  Moshi  Mkama amewatahadharisha viongozi wanaotumia vibaya madaraka katika ushirika  kuwa watachukuliwa sheria kali hasa  sheria mpya iliyoanza Januari ,2014 ambayo inabainisha kiongozi atakaye jihusisha na ubadhirifu na kukiuka misingi ya utawala bora sheria inamtaka afungwe miaka miwili jela  na faini  zaidi ya  milioni mbili iwapo atatiwa hatiani.
           
Kwa nyakati tofauti baadhi ya wanachama wa chama hicho Godfrey  Muhoza na Rose Rutaba  walisema viongozi wao wanatumia vibaya nyadhifa zao kwa wanachama wake,ambapo wakibaini mwanachama anayefuatilia nyendo na mwenendo wa mapato na matumizi ya chama anaonekana ni muhasi na hivyo humtoa kwenye chama.

Pia walidai hali ya viongozi kutokujali  utawala bora ni chachu ya wakulima wa zao hilo kuwa na maisha duni ili hali wachache wanaishi maisha bora kwa migongo ya wakulima ambao wao wanakuwa daraja la mafanikio ya wakubwa katika vyama vya ushirika,hali inayowakwaza baadhi ya wakulima wasijiunge na vyama hivyo baada ya kuona hujuma ndani yake.
Chama hicho ni miongoni mwa vyama vyenye utata wa kumaliza changamoto ya utawala bora na matumizi mazuri ya fedha na hiyo itakuwa ni tume ya pili kukagua chama hicho baada ya ile ya mkoa wa kigoma,ilishindwa kutatua hilo, na kwa mujibu wa Naibu waziri maafisa ushirika wa wilaya na mkoa hawatakuwa sehemu ya tume hiyo kwa lengo la kutenda haki kwa lengwa.

Tuesday, April 8, 2014

BENKI YA NBC YAZINDUA HUDUMA YA BIMA YA BURE YA MKOPO JIJINI DAR

photo1
photo2
Mkuu wa Idara ya Mikopo wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Andrew Lyimo, (kulia) akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa huduma ya Bima ya Bure ya Mkopo  jijini Dar es Salaam.  Kushoto ni Mkuu wa Idara ya Bima wa NBC, Bi. Kemibaro Omuteku.

MWENYEKITI WA BUNGE MAALUM LA KATIBA SAMWEL SITTA AKUTANA NA VIONGOZI WA DINI


PIX 1
Mhe. Mufti Sheikh Issa Shaaban Simba  akimkaribisha Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Mhe. Samuel Sitta leo jijini Dar es Salaam wakati alipomtembelea kumuelezea maendeleo ya vikao vya Bunge linaloendelea mjini Dodoma.
PIX 3
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Mhe. Samuel Sitta (kulia) akiongea na waandishi wa habari mara baada ya ziara yake katika Ofisi za Bakwata kuelezea maendeleo ya cikao vya Bunge Maalum la Katiba mjini Dodoma. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Bakwata Suleiman Lolila.(PICHA ZOTE NA BUNGE MAALUM LA KATIBA).

Na. Benedict Liwenga-Maelezo
MWENYEKITI wa Bunge maalum la Katiba Samweli Sitta amesema  katiba mpya ni kwa manufaa ya wanachi wote kwa ajili ya kuwaletea maendeleo katika nyanja mbalimbali.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam alipokutana na Mhe. Mufti Sheikh Issa Shaaban Simba   katika Ofisi za Bakwata zilizoko Kinondoni jijini Dar es Salaam ikiwa ni utaratibu aliojiwekea kwa ajili ya kuwashirikisha Viongozi wa madhehebu na dini ili nao wapate taarifa ya maendeleo ya bunge la katiba. 

Mhe. Sita amesema kuwa Viongozi wa dini ni watu muhimu sana kwakuwa wanabeba wafuasi wengi katika jamii na kuwepo kwao kunasaidia katika maendeleo ya nchi hususani kujenge Amani ya nchi yetu na kuwahamasisha wananchi kuwa wavumilivu,watulivu,waelewa na wenye kupenda Amani.

Namuomba Mhe. Mufti pamoja viongozi wengine wa dini waizidi kutuombea ili tuweze kufikia muafaka katika kupata katiba mpya na bora yenye kuleta mabadiliko katika nch yetu” Alisema Mhe. Sitta.

Mhe. Sita Ameongeza kuwa Watanzania wanataka katiba itakayoijenga Taasisi imara zitakazoweza kusimamia mambo muhimu na kuweza kuondokana na  uhalifu ikiwemo janga la madawa ya kulevya ambalo limekuwa likiisumbua sana nchii kwa msaada wa sheria mpya janga hili linawezekana kudhibitiwa.

Pia amewaomba wajumbe wa kamati kumi na mbili za bunge la katiba,wasome kwa makiini ibala ya sura ya 1 na ya 6 ambazo ni muhimu sana katika kuijenga nchi, ili waweze kutoka na mawazo mazuri na yakinifu  kwa manufaa ya nchi na watu wake na kuweza kukuza uchumi na kuleta maendeleo.

“Katiba itunge sheria ambazo ni imara zenye kufuata kanuni na taratibu dhabiti ili kuleta mabadiliko katika kuiongoza nchi na kuweza kuwasaidia wananchi wake” Alisema Mhe. Sitta.
Aidha, ameongeza kuwa Bunge hilo maalum linatarajia kuhailishwa mwezi wa nne tarehe 28 kwa ajili ya kupisha bunge la Bajeti,na kwa kuwa siku  70 hazitoshi kumaliza bunge hilo amemuomba Mheshimiwa Rais Kuwaongezea muda hivyo wanatarajia kurudi tena mwezi wa nane kuweza kuendelea na mijadala ya katiba mpya.

Monday, April 7, 2014

WAZIRI NYALANDU AZINDUA MAJENGO YA CHUO CHA MUSOMA UTALII TABORA

Waziri wa Maliasili na Utalii Bw.Lazaro Nyalandu akikata utepe kama ishara ya uzinduzi wa Majengo ya Chuo cha Musoma Utalii  Tabora wakati wa mahafali ya kumi ya Chuo hicho.
Waziri Nyalandu akiweka jiwe la msingi katika Chuo cha Musoma Utalii mkoani Tabora,Kulia ni Mkurugenzi wa Chuo hicho Bw.Shabani Mrutu.
Waziri Nyalandu akipatiwa maelezo ya malengo ya uanzishwaji wa Chuo cha Musoma Utalii Tabora kutoka kwa Mkurugenzi wa Chuo hicho Bw.Shabani Mrutu ofisi kwake.
Waziri wa maliasili na Utalii Bw.Lazaro Nyalandu akiwasalimia baadhi ya wahitimu wa kozi mbalimbali wakati wa mahafali ya kumi ya chuo cha Musoma Utalii Tabora.
Mkurugenzi wa Chuo cha Musoma Utalii Bw.Shaban Mrutu akisoma taarifa fupi ya Chuo kwa mgeni rasmi wakati wa mahafali ya kumi ya chuo hicho.
Waziri wa maliasili na Utalii Bw.Lazaro Nyalandu akizungumza katika mahafali ya kumi ya Chuo cha Musoma Utalii Tabora ambapo aliwataka wahitimu kuwa wavumilivu na kuongeza juhudi katika kutafuta elimu.
Mmoja wa wahitimu wa Chuo cha Musoma Utalii akimpa mkono mgeni rasmi Waziri Nyalandu wakati wa mahafali hayo ya kumi.
Waziri  wa maliasili ya Utalii Bw.Lazaro Nyalandu akiwa na mwenyeji wake Mkurugenzi wa Chuo cha Musoma Utalii Tabora Bw.Shaban Mrutu.








Jengo la Utawala Chuo cha Musoma Utalii Tabora ambalo ni miongoni mwa majengo yaliyozinduliwa na Waziri wa maliasili na Utalii Bw.Lazaro Nyalandu wakati wa mahafali ya kumi ya chuo hicho.

JAPAN YATOA MSAADA WA MAGARI KWA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI.

PIX 2
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima (kulia) na Balozi wa Japan nchini, Masaki Okada wakikata utepe ikiwa ishara ya makabidhiano ya magari matano yaliyotolewa na Serikali ya Japan kwa ajili ya kusaidia Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini. Magari hayo yamekabidhiwa katika viwanja vya Kituo cha Zimamoto Kanda ya Ilala, jijini Dar es Salaam. 
PIX 3
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima akiiwasha moja ya magari matano yaliyotolewa na Serikali ya Japan kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji. Magari hayo matano yalitolewa na Balozi wa Japan nchini, Masaki Okada wakati wa tafrija fupi ya makabidhiano ya magari hayo yaliyofanyika katika viwanja vya Kituo cha Zimamoto Kanda ya Ilala, jijini Dar es Salaam. 
PIX 4
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima akitoa hotuba fupi ya kuishukuru Serikali ya Japan kwa kuisadia wizara yake kupitia Jeshi la Zimamoto na Uokoaji magari matano kwa ajili ya kazi ya kuzima moto na uokoaji nchini. Kushoto ni Balozi wa Japan nchini, Masaki Okada ambaye alikabidhi magari hayo kwa niaba ya Serikali yake. Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Kamishna Jenerali Pius Makuru Nyambacha. makabidhiano ya magari hayo yaliyofanyika katika viwanja vya Kituo cha Zimamoto Kanda ya Ilala, jijini Dar es Salaam.
PIX 5
Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Kamishna Jenerali Pius Makuru Nyambacha akitoa hotuba fupi ya kumkaribisha mgeni rasmi ambaye ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima (katikati) ili aweze kuzungumza na baadaye kukabidhiwa magari matano ya kuzima motona uokoaji. Magari hayo yametolewa na Serikali ya Japan kupitia balozi wake nchini, Masaki Okada (kushoto) katika viwanja vya Kituo cha Zimamoto Kanda ya Ilala, jijini Dar es Salaam.
PIX 6
Sehemu ya magari matano yaliyokabidhiwa na Balozi wa Japan, Masaki Okada kwa niaba ya Serikali yake. Magari hayo matano yaliyotolewa kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji yalipokelewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima katika viwanja vya Kituo cha Zimamoto Kanda ya Ilala, jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).

KANISA LA T.A.G TABORA WASHEHEREKEA MIAKA 75

Maandamano ya maadhimisho ya miaka 75 ya Kanisa la TAG nchini ambayo yamefanyika mjini Tabora kuanzia uwanja wa Ally Hassan Mwinyi hadi kanisa la TAG jirani na hospitali ya mkoa wa Tabora Kitete.
Baadhi ya waumini walioshiriki maandamano hayo ya amani wakisheherekea maadhimisho hayo mjini Tabora.
Maandamano ya maadhimisho ya miaka 75 yalipewa ulinzi wa kutosha na Jeshi la Polisi ambapo usalama ulikuwa wa kuridhisha.



Friday, April 4, 2014

KANISA KATOLIKI JIMBO KUU TABORA LADAIWA KUTAKA KULIPULIWA!!!

Kanisa Katoliki Jimbo kuu la Tabora ambalo limedaiwa kutaka kulipuliwa majira ya saa nne asubuhi ya leo baada ya kubainika kuwa mtu mmoja ambaye alifika Kanisani hapo na kutaka kumrubuni mlinzi kwa kumpatia kiasi cha shilingi elfu ishirini ili aweze kutekeleza dhamira yake ambayo haikufanikiwa baada mlinzi kutoa taarifa kwa uongozi wa Kanisa hilo ambao walitoa taarifa kwa makachero wa Jeshi la Polisi Tabora na kufanikiwa kukamatwa kwa mtu huyo.


Thursday, April 3, 2014

WAVUVI KUVAMIA BUNGE LA RASIMU YA KATIBA-KIGOMA


Na Magreth Magosso,Kigoma
 
CHAMA  Cha  Wavuvi Mwalo wa Kibirizi  Manispaa ya Kigoma Ujiji,watishia kwenda mkoani  Dodoma kwenye Bunge Maalumu la Mchakato wa rasimu ya pili ya Katiba,kwa kile wanachodai kutaka kujua sintofahamu ya wizi wa mashine za mitumbwi sanjari na kutekwa kwa wavuvi katika Ziwa Tanganyika.
 
Akifafanua hilo Salum Shaban Kiongozi wa Wavuvi pia Miongoni mwa tume maalum iliyoundwa na Mkuu wa Mkoa Lt. Issa Machibya hivi karibuni iliyokwenda DRC-Congo kwa lengo la kurudi na mashine  18 zilizoibwa  eneo la mwalo wa katonga na kibirizi Machi,3,2014,kugonga mwamba, ndio chachu ya kufika bungeni ili kupeleka kilio chao.

Hali hiyo ya sintofahamu ya kuvamiwa kwa wavuvi na mali zao inatokana na  serikali ya DRC-Congo kukaidi Mkataba  wa Ujirani mwema waliowekeana mwaka jana kuwa ,`mali ya wizi dhidi ya kigoma naWilaya ya kaleme zirudishwe bila masharti magumu endapo mali zitathibitika zimetoka kati ya wilaya hizo’.
 
Shabani alisema, mkataba huo una maslai ya kulinda ujirani mwema sambamba na kuweka mkakati wa kubaini majambazi yanayozidi kuwateka wavuvi toka wilaya ya kigoma ambapo wengi wanaotuhumiwa na vitendo hivyo ni raia wa DRC-congo baada ya kubaini mashine zao zipo mikononi mwa serikali hiyo sanjari na kuwatia nguvuni wahalifu husika.
 
“Tumegundua wenzetu hawako vyema na mfumo wa sheria zaidi ya kutumia ubabe haiwezekani anawatarifu zana zipo lakini tulipofika anabadilika hali iliyotufanya tukae kule zaidi ya siku tano cha kushangaza hili suala hata WaziriMkuu anajua akadai muhusika wa wizara  hayupo nchini”
 
“kumbuka wilaya ya kigoma na Uvinza mapato yao makubwa ni masoko ya samaki ambayo yote ukanda wa ziwa Tanganyika,ulinzi duni ziwani  ,sheria haing`ati ,ajira zinapungua kwa vijana,hatari 2020 soko za samaki kutoweka” alibainisha Shabani.
 
Kwa upande wa Mwenyekiti wa wavuvi Ramadha Kanyongo na Kaimu wake Sendwe Ibrahim alisema zao la samaki ni uchumi wa kigoma mjini na uvinza ambapo kwa mwalo wa kibirizi  halmashauri ya kigoma ujiji inakusanya milioni11,kwa mwezi,katonga M. 8  ambapo kwa wilaya ya kigoma vijijini soko la muyobozi  m.5 na kagongo M.2, wilaya ya Uvinza soko la samaki Buhingu million 6.
 
Aliongeza kwa kusema serikali ikishindwa kudhibniti 2020 uchumi wa halmashauri hizo zipo mashakani kutokana na wadu wa uvuvi kushindwa kusonga mbele kwenye kazi hiyo kutokana na gharama kubwa ya mashine ya boti ambapo mashine moja si chini ya milioni 5 mpya ,iliyotumika milioni 3.5.
 
Akijibu hoja ya raia wa DRC-congo kujikita na wizi wa mashine kwa wavuvi wa kigoma,Balozi ndogo ya nchi hiyo Ricky Molema akiri  Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Lt.Machibya anahaja ya kusaidia wananchi wake sanjari na wavuvi kushuka kiuchumi na kupotea kwa ajira ya vijana.
 
Molema alibainisha kuwa,viongozi wa juu  wa  Nchi husika,wanawajibu wa kuwa na moyo wa dhati kuondoa changamoto ya wavuvi na mali zao ziwe salama, ili jamii husika zisibadili mwelekeo wa kuishi kwa leo na siku za usoni na kushauri kuwepo na doria ya pamoja ziwani ili kuthibiti uhalifu.
 
Hivyo kutokana na madhira hayo wanajipanga kwenda Bungeni ili wakaonane na waziri mwenye dhamana na Uvuvi na Mifugo sanjari na Wabunge wa Mkoa wa Kigoma ili wajue hatma ya hilo.

Aidha mtandao huu mebaini kuwa mwaka 2003 mwalo wa kibirizi ulikuwa na mitumbwi yenye mashine 160 ambapo kwa sasa imebaki mitumbwi 45,katonga walikuwa na vipe 200 na sasa 168 ,Mtandao  huu  naamini dhati ya viongozi itathubutu kuongeza ulinzi katika Ziwa Tanganyika kwa kuboresha uhitaji wake.
 

Tuesday, April 1, 2014

TABORA HALI SI SHWARI,MAJAMBAZI HUVAMIA KWA BUNDUKI KILA SIKU USIKU.

Salumu Abel Muhunda mkazi wa Kata ya Cheyo manispaa ya Tabora amejeruhiwa vibaya na kundi la Majambazi ambayo yalimvamia wakati akiuza dukani  huko eneo la Mwanga Shop ambapo majambazi hayo yalivamia yakiwa na bunduki na kufyatua risasi hewani huku yakimjeruhi kwa kumpiga mapanga na nyundo kichwani na baadae kumpora kiasi kikubwa cha fedha.
Muhunda  ambaye kwasasa amelazwa hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Tabora Kitete ni mmoja kati ya watu walioathirika na matukio ya unyang'anyi wa kutumia silaha unaofanywa na majambazi hayo ambayo hufanya unyama huo kila siku na kwasasa takribani miezi mitatu mfululizo eneo la manispaa ya Tabora waathirika wakubwa ni wafanyabishara ya maduka madogo ya mitaani pamoja na M-pesa.


MAHAFALI YA 18 CHUO CHA UTUMISHI WA UMMA TABORA NA SINGIDA



Mgeni Rasmi akikabidhi zawadi mbalimbali kwa wahitimu waliofanya vizuri katika vitengo vyao.
Maandamano kuelekea ukumbini yakiongozwa na mgeni rasmi Mh. Celina Kombani aliyevaa Joho jekundu.

Viongozi ngazi za juu Chuo cha Utumishi wa Umma nchini
Mtendaji mkuu Chuo cha Utumishi wa Umma TPSC nchini Bw.Said Nassor akizungumza mikakati endelevu ya Chuo hicho wakati wa mahafali hayo.

Saturday, March 29, 2014

SINGPRESS YAPATA KATIBU MTENDAJI MPYA


DSC07415
Mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari (Singpress) mkoa wa Singida, Seif Takaza akifungua mkutano mkuu wa kawaida wa klabu hiyo uliofanyika mjini Manyoni mwishoni mwa wiki.Kulia ni makamu mwenyekiti Damiano Mkumbo na kulia ni kaimu katibu mtendaji,Emmanuel Michael.(Picha na Nathaniel Limu).
DSC07419
Baadhi ya wanachama wa klabu ya waandishi wa habari (Singpress) mkoa wa Singida,wakifuatilia mkutano mkuu wa kawaida wa (mwaka 2013) klabu hiyo uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa kanisa Katoliki mjini Manyoni.

Na Nathaniel Limu, Manyoni
KLABU ya waandishi wa habari (Singpress) mkoa wa Singida imemchagua kwa kishindo Pascal Tantau (32),kuwa katibu wake mtendaji kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Abby Nkungu ambaye anadai kwa sasa afya yake ina mgogoro.

Pascal kijana aliyemaliza chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) alipata kura 15 za ndio,mbili zilimkataa na moja iliharibika.

Pascal atakuwa madarakani hadi mwishoni mwakwani (2015) uchaguzi mkuu utakapofanyika kwa mujibu wa katiba ya klabu hiyo.

Pascal aliwashukuru wanachama wenzake kwa kumwamini na kumkabidhi nafasi hiyo nyeti. Ameahidi kwamba atawatumikia kwa nguvu zake zote na kwa maarifa lengo kuu ikiwa ni  klabu hiyo iweze kupaa kimaendeleo katika kipindi chake cha uongozi.

“Niwaahidi pia kwamba katika uongozi wangu nitatumia mbinu shirikishi ili kila mwananchama aweze kutoa mchango wake mbalimbali kuendeleza klabu na kuboresha ustawi wa wananchama.Nitajitahidipia kuhakikisha klabu inakuwa na mahusiano mazuri na wadau wake mbalimbali”, alisema kwa kujiamini.

Abby Nkungu amelazimika kujiuzulu nafasi ya ukatibu mtendaji wa Singpress,kwa madai kwamba ameagizwa na daktari wake aishiye nchini Kenya, kuwa asifanye kazi yo yote ambayo atalazimika kutumia akili nyingi.

Ilielezwa mbele ya mkutano huo mkuu, kwamba Nkungu aliweza kuombwa na kamati tendaji kusaidia kuandaa maandalizi ya mkutano mkuu,alikataa kata kata.

Hata alipoitwa tena na kamati tendaji ili aweze kufafanua zaidi juu kutakiwa na daktari wake awe kwenye mapumziko yasiyo na bughudha yo yote…yaani ‘total rest’,wakati anaendelea na kazi kama kawaida zikiwemo za safari ndefu pia alitupilia mbali wito huo.

Kutokana na hali hiyo mkutano mkuu huo umeazimia Nkungu asigombee tena uongozi wowote katika klabu ya Singpress kwa muda wote wa maisha yake yaliyobaki.Pia amesimamishwa uanachama kwa kipindi cha miezi tisa.

Hii ni mara ya pili,Nkungu kusimamishwa uanachama wa klabu ya Singpress.

MWALIMU AMVUNJA MGUU DENTI KISA MAPENZI - KIGOMA


Na Magreth Magosso,Kigoma

Mwanafunzi wa Darasa la saba katika Shule ya Msingi Bangwe Kata ya Bangwe kwenye Manispaa ya kigoma Ujiji mkoani hapo  amepigwa na mwalimu wake katika maeneo mbalimbali ya mwili wake na kumvunja mguu wa kulia baada ya kumkatalia kumpa penzi.


Akizungumza na mwandishi wetu  jana wodi namba 5 katika hospitali ya Rufaa ya Maweni mwanafunzi huyo aliyetambuliwa kwa jina la Zubeda Athuman (14)  alisema chanzo cha mwalimu huyo kumchukia na hatimaye kufikia hatua ya kumpiga na kumvunja mguu  ni wivu wa kukataliwa kupewa penzi ,hali iliyomfanya mwalimu huyo kumpa  adhabu za hapa na pale kila aendapo shule.


Hali hiyo ilimfanya  mwanafunzi huyo kuwadokeza wazazi wake ambapo walimwambia avumilie,ndipo jumatano ya wiki hii mwalimu alimpa adhabu ya kuchimba shimo na alikataa kufanya hivyo baada ya kuona hana kosa la msingi la kumpa adhabu hiyo.


Mwalimu huyo alifikia hatua ya kumfuata nyumbani kwao  machi,22,2014 saa 12.30 jioni hali iliyowashtua wazazi na kumuhoji mtoto juu ya hilo ndipo binti alipokwenda shule Machi,24,2014  alimuliza mwalimu huyo sababu ya kumfuta kwao, hali hiyo ilimchefua mwalimu na kutoa maneno ya kashfa  na kumpiga  vibao vya uso na kusababisha maumivu mbalimbali ya mwili wake ikiwemo kuvunjika kwa mguu.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Maweni Macris Yakayeshi akiri mwanafunzi huyo kuvunjika mguu wa kulia sambamba na kuvimba uso na kupelekea mdomo kwenda upande na wiki ijayo anatarajia kumwekea `P.O.P’.


Dr.Yakayeshi alibainisha kuwa kutokana na tatizo alilonalo itamlazimu kukaa na mhogo si chini ya wiki sita ili mguu utengamae sambamba na kuitaka jamii ibadilike na matukio ya udhalilishaji wa kijijnsia huku akidai alifikishwa hapo kifua kikiwa wazi ili hali binti ni rika la balehe na kuomba sheria ichukue mkondo wake.


Mwenyekiti wa Mtaa wa Kamala katani humo Curthbert Kusongwa alisema, kwa maelezo aliyoyapata kutoka kwa walimu wa shule hiyo walidai binti alikataa adhabu aliyopewa na kumpiga kofi mwalimu na ndipo mwalimu akamwambia akamlete mzazi wake,wazazi walipofika alidai alimvamia mwalimu na kuanza kumpiga hali iliyolazimu jeshi la polisi kuingilia  hekaheka kiyo.


Akizungumzia tukio hilo Athumani Moshi ambaye ni baba wa Zubeda alisema  alishangaa kumuona mwanae amerudishwa shule huku akiwa amevimba uso na mdomo ndipo akadai kuitwa na mwalimu husika,alipofika shule na kuonana na mwalimu husika hakuwa muungwana kutokana na kauli chafu na kebehi.


Moshi alisema baada ya kauli hizo  ghafla mwalimu akamkata mtama mwanae na kuanguka chini ndipo wakapigana,huku akikiri awali alipata kuelezwa juu ya adha ya mwalimu huyo kwa binti yake hadi kufikia hatua ya kumfuata usiku siku za mapumziko sanjari na kumpa adhabu zisizostahili kwa kisa alikataa kuwa nae kimapenzi.


Kamanda wa Polisi mkoani hapa Zedekia Makunja alipoulizwa kama analifahamu hili akadai naam ila wataitwa machi,31,mwaka huu.


Kwa nyakati tofauti Mariamu Issa na Winyfrida Bwire walisema sheria ya mwanafunzi juu ya adhabu inajulikana ,walimu hawana budi kulea watoto kwa kuwafundisha adabu ,huku wakidai kuna namna kati ya mwanafunzi na mwalimu haiwezekani kukataa kwa adhabu amvunje mguu.

Thursday, March 27, 2014

SIRI YA CCM KUNG'ANG'ANIA SERIKALI MBILI KIKATIBA


katuni 83f0e
Katika maisha ya kawaida, binadamu ana msimamo wake na hata uamuzi asiopenda ubadilike.
Katika medani ya siasa nchini msimamo wa Chama Cha Mapinduzi ( CCM) kuhusu Muungano na muundo unafahamika. Ni muundo wa kutaka Serikali mbili ambao chama hicho unakipigania kwa udi na uvumba.(Hudugu Ng'amilo)

Hata hivyo, msimamo huo ni kinyume na mapendekezo au matakwa ya wengi kama ilivyoainishwa kwenye Rasimu ya Pili ya Katiba iliyoandaliwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

Tume hiyo iliyokuwa chini ya Jaji Joseph Warioba ilikusanya maoni ya wananchi na ilipendekeza muundo wa Muungano wa Serikali tatu.

Hivi karibuni akifungua Bunge Maalumu la Katiba, Rais Jakaya Kikwete akaunga mkono msimamo wa chama chake, jambo lililoibua mjadala unaoendelea hadi sasa.
Hoja ya Serikali mbili

Kwanini CCM wanataka Serikali mbili na siyo tatu au moja kama ilivyo maoni ya wananchi walio wengi kwa mujibu wa maelezo ya Tume ya Warioba? Makala haya yanachambua hoja hiyo.

Profesa Bakar Mohammed ni Mhadhiri Mwandamizi na Mkuu wa Idara ya Siasa na Utawala ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, anayesema msimamo wa CCM wa kudai Serikali mbili unatokana na hofu ya uhafidhina wa kuogopa mabadiliko.

Anasema viongozi wengi wa CCM wanasumbuliwa na hofu na woga wa mabadiliko na kwamba wanakuwa wagumu kuyakubali yanapotaka kutokea.

"Kama mtu unaangalia madaraka zaidi, lazima kunakuwa na woga, na hii ni hulka ya binadamu kuwa na woga wa kuacha kile ulichokizoea... Lakini ukiangalia masilahi ya nchi na kuacha yale yanayokusukuma kusingekuwa na wasiwasi huu unaoonekana sasa," anasema.

Anasema CCM inachofanya ni kuhakikisha haking'oki madarakani, huku viongozi wake wakiamini kuwa wana sifa za kuongoza na siyo wengineo.

Profesa Bakari anailinganisha hofu ya sasa ya CCM na ile waliyokuwa nayo viongozi wa chama hicho miaka ya 1990 zilipoanza vuguvugu za mabadiliko ya siasa za vyama vingi. Anasema CCM kiliendesha propaganda kuwa mfumo wa vyama vingi haukuwa na tija na ungeleta vita.0
inShare

Hofu hiyo anasema ndiyo inayokifanya chama hicho kikongwe kuhofia kung'olewa madarakani.
"Woga huo bado upo, wanaogopa pengine mfumo ukiwa wa Serikali tatu uwezekano wa wao kubaki madarakani utakuwa mdogo," anafafanua.

Anaongeza kusema kuwa hofu ya CCM siyo kwa ajili ya masilahi ya nchi, badala yake inaonekana chama kinaangalia masilahi yake.
Ingekuwa vyema anasema kwa CCM kueleza madhara yanayoweza kulikumba taifa ikiwa muundo wa Serikali tatu utapita.

"Wanatoa hoja kuwa mfumo wa Serikali tatu unaweza kusambaratisha nchi, lakini hakuna uhakika kama mfumo huu uliopo nchi hauwezi kusambaratika," anasema.
 
Hofu ya kuyumba na kuanguka
Mhadhiri mwingine wa chuo hicho, Dk. Benson Bana anasema siri ya CCM kung'ang'ania Serikali mbili inatokana na hofu ya kuyumba na kuanguka.

Anasema CCM kimekuwa madarakani na mfumo huo kwa miaka 50 na kwamba hofu yao ni kuwa ukiondoa Serikali mbili kinaweza kuyumba na kuachia madaraka.

Anasema misingi ya wanasiasa ni madaraka, na kwamba ukishayapata, huwezi kuyaachia kirahisi.
"Misingi ya wanasiasa ni madaraka... Kuyalinda, kuyahifadhi na kuyatumia madaraka yale kwa namna yoyote...Huwezi kuyaachia madaraka kirahisi. Utafanya ujanja, utatumia mbinu chafu ili tu kuhakikisha unabaki madarakani, na hiki ndicho wanachofanya CCM," anasema.

Dk. Bana anasema CCM kingeeleweka na kingekuwa na mwonekano mzuri zaidi endapo wangepigania kuwapo kwa Serikali moja.

"Wangekuwa wanataka muungano imara, endelevu na uliokomaa wangeelekeza katika Serikali moja...Lakini hawataki kwa sababu wanajua moja inaweza ikawanyima uongozi," anasema.Dk. Bana anasema ni vyema wananchi wakaelimishwa huu muungano una faida gani na wanafunzi shuleni katika elimu ya uraia waelezwe faida zake.

"Ingekuwa wazi tungejua nani anafaidika na nini, mikopo misaada, nani anachangia nini...Je zile sababu za waasisi za kuungana bado zipo sasa miaka 50 ya Muungano, ule woga kuwa Zanzibar itamezwa bado upo leo?" Anahoji.

Anaongeza kuwa ni vyema kwa watawala kutazama mazingira ya sasa ya siasa zetu kwa kile anachoeleza kuwa hata Katiba ikipita ikakubali kuwapo wa Serikali mbili, bado wananchi watahoji mantiki ya muundo huo.

Msomi mwingine wa siasa, Dk. Alexander Makuliko anasema hofu ya CCM ni kuwa ndio iliyouasisi Muungano wa Serikali mbili, hivyo isingependa hali hiyo ibadilike.

Anaendelea kusema kuwa CCM imezoea mfumo huu na kuwa ikiukosa itaathirika, kwakuwa ni sera yake na imekuwa ikiitekeleza, lakini msimamo wa wananchi ndiyo kitu cha msingi kuzingatiwa. Hoja zijengwe na zisikilizwe, ubabe hautakiwi, busara inahitajika zaidi.

Anasema pamoja na suala la Serikali mbili kuwa ni pimajoto ya uhai wa CCM, hata hivyo hoja zinazotolewa katika kutetea msimamo wao ni nzuri tu na zinazoeleweka vyema.

"Sioni kama wanang'ang'ania, lakini ukweli ni kuwa kila chama kina sera yake, na CCM kimeweka sera yake katika suala la Muungano wao wanasema ni Serikali mbili, na siyo tatu...kwamba tatu zitaongeza gharama na mengineyo, ni sababu za msingi kabisa," anasema.

Anaongeza kuwa hoja zinazotolewa na chama tawala ni kubwa na siyo za kupuuzwa, lakini vilevile kero zinazotajwa kuhusu mfumo wa Muungano uliopo nazo zipo na zinaweza kutatuliwa katika mfumo uliopo.

"Unajua hivi vyama kila kimoja kinataka kuvutia kwake, hata bila rasimu ya Warioba...Ninashauri walete hoja, kisha watu wazipime hizo hoja, kwanini serikali mbili, na wale wa tatu tayari wameleta hoja na ushahidi, watu waachwe wapime," anasema na kuongeza:

''Jambo la msingi kuzingatiwa ni kuwa mawazo ya wananchi wengi yataonekana wakati wa kura za maoni. Angalizo ni kuhakikisha kuwa kura hiyo isije ikachakachuliwa.''
CHANZO MWANANCHI

Wednesday, March 26, 2014

MITAMBO YA TELEVISHENI KWA MFUMO WA ANALOJIA KUZIMWA TABORA NA SINGIDA MARCHI 31 2014

Naibu mkurugenzi wa Idara ya Utangazaji Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA Bw.Frederick Ntobi akizungumza na waandishi wa habari Tabora kuhusu kuzima mitambo ya Analojia mikoa ya Tabora na Singida ifikapo tarehe 31 marchi mwaka 2014.
Meneja wa kanda ya kati TCRA Bi.Maria Sasabo akizungumzia ubora wa matangazo ya kupitia mfumo wa Dijitali nafaida zake.
Moja kati ya Antena za King'amuzi cha Startimes ambacho waandishi wa habari walielekezwa matumizi yake sahihi na namna kinavyoweza kukupatia picha zenye ung'avu.