Pages

KAPIPI TV

Thursday, April 3, 2014

WAVUVI KUVAMIA BUNGE LA RASIMU YA KATIBA-KIGOMA


Na Magreth Magosso,Kigoma
 
CHAMA  Cha  Wavuvi Mwalo wa Kibirizi  Manispaa ya Kigoma Ujiji,watishia kwenda mkoani  Dodoma kwenye Bunge Maalumu la Mchakato wa rasimu ya pili ya Katiba,kwa kile wanachodai kutaka kujua sintofahamu ya wizi wa mashine za mitumbwi sanjari na kutekwa kwa wavuvi katika Ziwa Tanganyika.
 
Akifafanua hilo Salum Shaban Kiongozi wa Wavuvi pia Miongoni mwa tume maalum iliyoundwa na Mkuu wa Mkoa Lt. Issa Machibya hivi karibuni iliyokwenda DRC-Congo kwa lengo la kurudi na mashine  18 zilizoibwa  eneo la mwalo wa katonga na kibirizi Machi,3,2014,kugonga mwamba, ndio chachu ya kufika bungeni ili kupeleka kilio chao.

Hali hiyo ya sintofahamu ya kuvamiwa kwa wavuvi na mali zao inatokana na  serikali ya DRC-Congo kukaidi Mkataba  wa Ujirani mwema waliowekeana mwaka jana kuwa ,`mali ya wizi dhidi ya kigoma naWilaya ya kaleme zirudishwe bila masharti magumu endapo mali zitathibitika zimetoka kati ya wilaya hizo’.
 
Shabani alisema, mkataba huo una maslai ya kulinda ujirani mwema sambamba na kuweka mkakati wa kubaini majambazi yanayozidi kuwateka wavuvi toka wilaya ya kigoma ambapo wengi wanaotuhumiwa na vitendo hivyo ni raia wa DRC-congo baada ya kubaini mashine zao zipo mikononi mwa serikali hiyo sanjari na kuwatia nguvuni wahalifu husika.
 
“Tumegundua wenzetu hawako vyema na mfumo wa sheria zaidi ya kutumia ubabe haiwezekani anawatarifu zana zipo lakini tulipofika anabadilika hali iliyotufanya tukae kule zaidi ya siku tano cha kushangaza hili suala hata WaziriMkuu anajua akadai muhusika wa wizara  hayupo nchini”
 
“kumbuka wilaya ya kigoma na Uvinza mapato yao makubwa ni masoko ya samaki ambayo yote ukanda wa ziwa Tanganyika,ulinzi duni ziwani  ,sheria haing`ati ,ajira zinapungua kwa vijana,hatari 2020 soko za samaki kutoweka” alibainisha Shabani.
 
Kwa upande wa Mwenyekiti wa wavuvi Ramadha Kanyongo na Kaimu wake Sendwe Ibrahim alisema zao la samaki ni uchumi wa kigoma mjini na uvinza ambapo kwa mwalo wa kibirizi  halmashauri ya kigoma ujiji inakusanya milioni11,kwa mwezi,katonga M. 8  ambapo kwa wilaya ya kigoma vijijini soko la muyobozi  m.5 na kagongo M.2, wilaya ya Uvinza soko la samaki Buhingu million 6.
 
Aliongeza kwa kusema serikali ikishindwa kudhibniti 2020 uchumi wa halmashauri hizo zipo mashakani kutokana na wadu wa uvuvi kushindwa kusonga mbele kwenye kazi hiyo kutokana na gharama kubwa ya mashine ya boti ambapo mashine moja si chini ya milioni 5 mpya ,iliyotumika milioni 3.5.
 
Akijibu hoja ya raia wa DRC-congo kujikita na wizi wa mashine kwa wavuvi wa kigoma,Balozi ndogo ya nchi hiyo Ricky Molema akiri  Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Lt.Machibya anahaja ya kusaidia wananchi wake sanjari na wavuvi kushuka kiuchumi na kupotea kwa ajira ya vijana.
 
Molema alibainisha kuwa,viongozi wa juu  wa  Nchi husika,wanawajibu wa kuwa na moyo wa dhati kuondoa changamoto ya wavuvi na mali zao ziwe salama, ili jamii husika zisibadili mwelekeo wa kuishi kwa leo na siku za usoni na kushauri kuwepo na doria ya pamoja ziwani ili kuthibiti uhalifu.
 
Hivyo kutokana na madhira hayo wanajipanga kwenda Bungeni ili wakaonane na waziri mwenye dhamana na Uvuvi na Mifugo sanjari na Wabunge wa Mkoa wa Kigoma ili wajue hatma ya hilo.

Aidha mtandao huu mebaini kuwa mwaka 2003 mwalo wa kibirizi ulikuwa na mitumbwi yenye mashine 160 ambapo kwa sasa imebaki mitumbwi 45,katonga walikuwa na vipe 200 na sasa 168 ,Mtandao  huu  naamini dhati ya viongozi itathubutu kuongeza ulinzi katika Ziwa Tanganyika kwa kuboresha uhitaji wake.
 

No comments: