Pages

KAPIPI TV

Thursday, April 10, 2014

CHAMA CHA AMCOS NGURUKA KUFANYIWA UPYA UKAGUZI WA HESABU

Na Magreth Magosso,Kigoma

CHAMA cha wakulima wa zao la tumbaku cha Hongera Amcos Kata ya Nguruka wilayani Uvinza Mkoa wa Kigoma, kimetakiwa kifanyiwe upya ukaguzi wa mahesabu,kutokana na sintofahamu ya mwenendo wa viongozi wake kutokuzingatia  misingi ya utawala bora,hali inayowakwaza wananchama wa chama hicho.

Kauli hiyo imekuja baada ya Naibu Waziri wa kilimo na chakula Godfrey Zambi kubainika kuwa kuna baadhi ya viongozi wanakitumia chama  hicho kwa maslai yao binafsi badala ya kuwakwamua wahusika ili waondokane na umaskini katika familia zao na jamii husika.

Aidha,Waziri huyo aliitaka Ofisi ya Mlajisi Mkuu wa mjini Dododoma,asikilize kero za wananchama wa chama hicho wakiwemo wanachama tisa ambao wamefukuzwa bila kanuni,taratibu na sheria kwa misingi ya kujenga utawala bora ili kujenga usawa na haki kwa kila mwanachama.

Naye Afisa Mlajisi makao Makuu  Moshi  Mkama amewatahadharisha viongozi wanaotumia vibaya madaraka katika ushirika  kuwa watachukuliwa sheria kali hasa  sheria mpya iliyoanza Januari ,2014 ambayo inabainisha kiongozi atakaye jihusisha na ubadhirifu na kukiuka misingi ya utawala bora sheria inamtaka afungwe miaka miwili jela  na faini  zaidi ya  milioni mbili iwapo atatiwa hatiani.
           
Kwa nyakati tofauti baadhi ya wanachama wa chama hicho Godfrey  Muhoza na Rose Rutaba  walisema viongozi wao wanatumia vibaya nyadhifa zao kwa wanachama wake,ambapo wakibaini mwanachama anayefuatilia nyendo na mwenendo wa mapato na matumizi ya chama anaonekana ni muhasi na hivyo humtoa kwenye chama.

Pia walidai hali ya viongozi kutokujali  utawala bora ni chachu ya wakulima wa zao hilo kuwa na maisha duni ili hali wachache wanaishi maisha bora kwa migongo ya wakulima ambao wao wanakuwa daraja la mafanikio ya wakubwa katika vyama vya ushirika,hali inayowakwaza baadhi ya wakulima wasijiunge na vyama hivyo baada ya kuona hujuma ndani yake.
Chama hicho ni miongoni mwa vyama vyenye utata wa kumaliza changamoto ya utawala bora na matumizi mazuri ya fedha na hiyo itakuwa ni tume ya pili kukagua chama hicho baada ya ile ya mkoa wa kigoma,ilishindwa kutatua hilo, na kwa mujibu wa Naibu waziri maafisa ushirika wa wilaya na mkoa hawatakuwa sehemu ya tume hiyo kwa lengo la kutenda haki kwa lengwa.

No comments: