Pages

KAPIPI TV

Monday, December 22, 2014

BREAKING NEWS: JOHNSON LUKAZA NA MWESIGWA LUKAZA WASHINDA KESI DHIDI YA EPA

Johnson Lukaza
Mwesigwa Lukaza
JOHNSON  LUKAZA WA KESI YA EPA ASHINDA KESI

Na Happiness Katabazi (UB)
HATIMAYE Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, imemwachilia huru Mwenyekiti  wa Makampuni ya Proin, Johnson Lukaza na mdomo wake Mwesiga Lukaza waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya wizi wa Sh.Bilioni Sita Katika Akaunti ya Madeni ya Nje ya Benki Kuu(EPA), baada ya kumuona Hana hatia Katika Kesi iliyokuwa ikimkabili.

Hukumu hiyo Imetolewa Jaji wa Mahakama Kuu Edson Mkasimongwa aliyekuwa alisaidia na Hakimu Mkazi Pamela Mazengo.

Lukaza ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza la Chuo Kikuu cha Bagamoyo (UB) alikuwa akitetewa na Wakili maarufu nchini Alex Mgongolwa aliyekuwa akisaidiwana na Wakili Alex Mshumbusi.

Akisoma hukumu hiyo Jaji Mkasimogwa alisema Kesi hiyo ya Mwaka 2008 , Mahakama imesikiliza ushahidi wa pande zote mbili Na kupitia vielelezo mbalimbali, Mahakama yake Imefikia uamuzi wa kuwaachiria huru washitakiwa wote Wawili kwasababu upande wa jamhuri umeshindwa kuleta ushahidi thabiti ambao ungeishawishi Mahakama hiyo iwakute na hatia washitakiwa Hao.

ZIZOU ENTERTAINMENT YATOA MSAADA WA VIFAA VYA MICHEZO KWA TIMU ZA VETERANI WATUMISHI NA CHIPUKIZI TABORA

Mwenyekiti wa timu ya Veterani Watumishi mkoa wa Tabora Laurent Paul akipokea msaada wa vifaa vya michezo kutoka kwa mwakilishi wa kampuni ya Zizou Entertainment ya jijini Dar-es-salaam,Shabani Moshi wakati wa makabidhiano ya vifaa hivyo kwenye viwanja vya Chipukizi Tabora mjini.
Kocha wa timu ya Chipukizi Didas Kunde akipokea jezi kwa ajili ya Timu ya Chipukizi zilizotolewa na Zizou Entertainment.
Timu ya  Veterani Watumishi ya mjini Tabora



WAKAZI WA JIMBO LA KIGOMA KASKAZINI WAKOSA HAKI YA KUPIGAKURA!!!

Na Magreth Magosso,Kasulu

ZAIDI ya wakazi  47,000 waishio katika  Kijiji cha  Zashe na kijiji na Kata ya Kagunga vilivyopo  pembezoni mwa ukanda wa Ziwa Tanganyika Mkoa wa Kigoma wameshindwa kujitokeza kwa wingi  jana katika Marudio ya Uchaguzi wa  viongozi wa Serikali za mitaa.

Changamoto kubwa iliyochangia hali hiyo ni pamoja na kuenguliwa kwa Chama cha Alliance And Tranciparecy For Change Tanzania kutokana na pingamizi walilowekewa na wasimamizi husika wa vijiji hivyo vyenye vitongoji 11,huku uongozi wa chama wakidai walizuiwa tangu 13,Novemba,2014 kwa sababu zisizoeleweka .

Akizungumza na Mtandao huu Mwenyekiti wa Chama cha ACT Sendwe Ibrahimu alisema  kijiji cha Kagunga ina vitongoji  vitano kwa mujibu wa watu waliojiandikisha ,waliopiga kura na waliosusa kushiriki mchakato huo .

Mkware

 Mkware Wananchi waliojiandikisha walikuwa 435,waliokwenda kupiga kura 184 tu,na waliogoma kupiga kura 256,kitongoji cha Mlama waliojiandikisha kupiga kura 549,waliopiga kura 92 tu,na walioshindwa kwenda kupiga kura 557.kitongoji cha kagunga waliojiandikisha 760,waliopiga kura 210  na wasiopiga kura 550.

Makombe

Kitongoji cha Makombe waliojiandikisha 682  waliopiga kura 142   na wasiopiga kura 540 ,kitongoji nyamilambo 459 wananchi waliojiandikisha kupiga kura,waliopiga kura 300,wasiopiga kura 259na kitongoji cha Lusolo  wakazi 570 walijiandikisha na waliopiga kura 320 na wasiopiga kura 250 .

Kijiji cha Zashe

Kwa Upande wa kijiji cha Zashe kina vitongoji vitano ikiwa na jumla ya wakazi zaidi ya 18,000 ambapo katika kitongoji cha Kware wakazi waliojiandikisha walikuwa 464,waliopiga kura 194 na wasiopiga kura walikuwa 270.

Kitongoji cha Mwibole waliojiandikisha walikuwa 210,walioshiriki kupiga kura walikuwa 50 huku walioshindwa kufika katika vituo vya kupiga kura walikuwa 160,Wakatihuohuo katika kitongoji cha Misele waliojiandikisha 361,waliopiga kura 111 na wasiopiga kura 250.

Kitongoji cha Mibombo waliojiandikisha walikuwa wakazi 314 ,waliopiga kura 174 na wasiopiga kura 140 na Kitongoji cha Ngonya waliojiandikisha 367,waliopiga kura 480 na wasioshiriki kupiga kura 207.

Kasulu

Kwa upande wa Wilaya ya Kasulu ,uchaguzi ulirudiwa  katika halmashauri nzima ya wilaya hiyo inayomiliki mitaa 109 ,vitongoji 288 na vijiji 70 ,ambapo uchaguzi ulikuwa na changamoto mbalimbali hasa muda wa kupiga kura hauendani na uhalisia wa kigoma na ukiukwaji wa kanuni husika na kupelekea baadhi ya viongozi wa  ccm na Nccr-mageuzi kushikana mashati na lugha chafu,

Kwa mujibu wa taratibu mwisho wa kupiga kura kitaifa ni saa 10 za alasiri kwa kigoma ni shida kutokana na hali ya kijiografia hivyo kwa busara za vyama vilishoriki na uongozi husika waliongeza muda kulingana na muda walioanza shughuli hiyo.

Akifafanua hilo Katibu itikadi na uenezi Mkoa wa kigoma Kalembe Masudi alisema Matokeo ya awali hadi leo Chama cha ccm kinaongoza katika ngazi ya kitongoji,kijiji na mitaa kama ifuatavyo,kwa upande wa kasulu mjini ccm inaongoza kwa kunyakua mitaa 73,ACT yashika viti 4  na UKAWA viti 15, Huku mitaa 19 bado wanaendelea  kuhesabu kura katika mitaa husika.

Kwa upande wa Vitongoji  ccm imeshika viti 128 kati ya vitongoji 288  vya hapo, Huku  viti 27 vimeshikwa na vyama vya upinzani wakati vitongoji 133 bado wanaendelea kuhesabu kura  wakati huohuo kati ya vijiji 70 Chama cha ccm kinaongoza kwa viti 29 na upinzani  vikiwa na viti 15 na vijiji 26 wakiendelea kuhesabu kura zilizosalia kwenye maeneo husika.

PROIN PROMOTIONS LTD WISH YOU MERRY XMASS AND HAPPY NEWS YEAR

JUMUIYA YA WANAFUNZI WA TANZANIA WUHAN (WUTASA) YAWAKARIBISHA WANAFUNZI WAPYA


Jumuiya ya Wanafunzi wa Tanzania Wuhan (WUTASA) iliandaa sherehe ya kuwakaribisha wanafuzi wapya Watanzania Wuhan, China. (Mdau Abdul Saiboko alikuwa ni mmoja wa wanafunzi hao ambaye ndiye aliyetumuvuzishia matukio haya yanayoonyesha jinsi sherehe ilivyofana Wuhan nchini China kama wanavyoonekana baadhi ya wanafunzi wapya waliohudhuria sherehe hiyo wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa sherehe hiyo.(PICHA NA MDAU ABDUL SAIBOKO-WUHAN-CHINA)
Mdau Abdul Saiboko wa kwanza kutoka kushoto na aadhi ya wadau wa China University of Geosciences (DIDA). wengine ni Yazidi, Masanja na Baraka.

Baadhi ya wadau wakiwa kwenye picha ya pamoja na mwenyekiti wa WUTASA Bwana Thomas Mtaki (wa tatu kutoka kushoto).
Katibu wa WUTASA bwana Mkoko akijaziwa mapochopocho.
Baadhi ya wadau waliohudhuria.
Mambo yakawa mduara kwa kwenda mbele kama inayoonyesha katika picha Mdau Abdul Saiboko akiikunja nyonga vilivyo wakati akicheza. Mambo ya mduara.​

UNESCO YAFADHILI MAENDELEO YA SAYANSI AFRIKA

IMG_7359
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili kwenye mahafali ya pili ya Taasisi ya Afrika ya Nelson Mandela ya Sayansi na Teknolojia yaliyofanyika jijini Arusha mwishoni mwa wiki.(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog)

Na Mwandishi Wetu, Arusha
SHIRIKA la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) limesema linafanyakazi na nchi 20 za Afrika kutengeneza mifumo ya kitaifa ya sayansi, teknolojia kusaidia mataifa hayo kufikia malengo yao ya maendeleo.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Getachew Engida wakati alipopata nafasi ya kutoa kauli ya shirika lake kwenye mahafali ya Pili ya Taasisi ya Afrika ya Nelson Mandela, Sayansi na Teknolojia iliyopo Tengeru mjini Arusha.

Alisema shirika lake limejikita zaidi kuhakikisha kwamba inatoa elimu itakayowezesha mabadiliko ya sayansi na hivyo kuwezesha wanaume kwa wake kufanyakazi kama wajasirimali.

“Elimu hiyo ni pamoja na mafunzo ya ukusanyaji takwimu, uimarishaji wa viashiria na ubunifu wa vifaa vya ufuatiliaji na kuimarisha utenegenezaji wa sera kwa kuangalia matukio yaliyothibitishwa,” alisema Naibu Mkurugenzi huyo.
IMG_7369
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO), Getachew Engida mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Taasisi hiyo kushiriki mahafali hayo.

Akizungumza mbele ya wahitimu wa Taasisi hiyo na Rais Jakaya Kikwete alisema kwamba sayansi na teknolojia vina nafasi ya pekee katika jamii na hivyo shirika kama UNESCO inachofanya ni kusaidia kuwapo kwa elimu hiyo.

Alisema sayansi na teknolojia ni msingi wa maendeleo kwani kupitia kuboreka kwa vitu hivyo viwili serikali nyingi zitaweza kukabiliana na umaskini uliokithiri na kupeleka watu wake katika maendeleo na ustawi.

Kiongozi huyo wa Unesco pia alimshukuru Rais Jakaya Kikwete kwa kuwezesha kuwepo kwa Taasisi hiyo ambayo ilibuniwa katika mkutano wa aliyekuwa Rais wa Benki ya Dunia, James Wolfensohn, na Rais Nelson Mandela wa Afrika Kusini mwaka 2001.
Ubunifu huo ulifanyiwa kazi na viongozi wa nchi za Afrika Januari 2005 katika mkutano wao wa Abuja ambapo walikubaliana kuanzisha vyuo vinne vya sayansi na teknolojia kwa jina la Nelson Mandela.
IMG_7570
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa (kushoto) pamoja na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO), Getachew Engida wakipitia ratiba ya mahafali ya pili ya Taasisi ya Afrika ya Nelson Mandela ya Sayansi na Teknolojia yaliyofanyika mwishoni mwa wiki Tengeru, mjini Arusha.

Alisema sayansi inashikilia majibu ya maswali ya maendeleo ya Bara la Afrika katika kukabili umaskini na kuwa na maendeleo endelevu katika sekta zote na jamii.

Naye Rais Kikwete akihutubia mkusanyiko huo aliwapongeza viongozi wa Taasisi hiyo kwa kuendeleza umaalumu wake.

“Taasisi hii ni sehemu ya mtandao wa vyuo vya Nelson Mandela vya Sayansi na Teknolojia katika Bara la Afrika. Chuo hiki cha Arusha ni mahsusi kwa ajili ya kanda ya Afrika Mashariki. Ndiyo maana Hati Idhini (University Charter) niliyokipa Chuo hiki inaeleza bayana kuwa Chuo hiki kinapaswa kuwa chenye hadhi maalum (special status). Hadhi hii yapaswa pia ionekane katika ubora wa elimu inayotolewa hapa. “ alisema Rais Kikwete.

Alisema ubora wake ni matokeo ya ubora wa wahadhiri wake, programu zake na miundombinu yake.
IMG_7509
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO), Getachew Engida akitoa kauli ya shirika lake kwenye mahafali ya Pili ya Taasisi ya Afrika ya Nelson Mandela ya Sayansi na Teknolojia iliyopo Tengeru mjini Arusha. Kulia ni Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Nelson Mandela na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Mohamed Gharib Bilal na baadhi ya viongozi wa juu wa chuo hicho.
IMG_7496
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues wakifurahi jambo wakati Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO), Getachew Engida (hayupo pichani) alipokuwa akisoma hotuba yake kwenye mahafali ya pili ya Taasisi ya Afrika ya Nelson Mandela ya Sayansi na Teknolojia mwishoni mwa wiki Tengeru jijini Arusha.
IMG_7542
Pichani juu na chini ni baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Afrika ya Nelson Madela, Sayansi na Teknolojia wakitoa burudani kwenye mahafali ya pili ya taasisi hiyo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki Tengeru jijini Arusha.
IMG_7527
IMG_7483
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (kushoto), Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO), Getachew Engida (katikati) pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues wakishuhudia burudani iliyokuwa ikitolewa na wafanyakazi wa taasisi hiyo.
IMG_7487
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO), Getachew Engida (katikati) akiteta jambo na Rais Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa mahafali ya pili ya Taasisi ya Afrika ya Nelson Mandela, Sayansi na Teknolojia yaliyofanyika mwishoni mwa wiki Tengeru, jijini Arusha. Kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa UNESCO Tanzania, Zulmira Rodrigues.
IMG_7492
Rais Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika tete-a-tete na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO), Getachew Engida (kaitkati). Kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa shirika la UNESCO Tanzania, Zulmira Rodrigues.
IMG_7619
Pichani juu na chini ni Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Nelson Mandela, Sayansi na Teknolojia na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Gharib Bilal akiwatunuku wahitimu mbalimbali wa shahada za juu za uzamili na uzamivu katika sayansi, teknolojia na tafiti za kisayansi wakati wa mahafali ya pili ya taasisi hiyo yaliyofanyika mwishoni mwa juma, Tengeru jijini Arusha.
IMG_7626
IMG_7353
Baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki waliohudhuria mahafali hayo.
DSC_0641
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na baadhi ya maprofesa wa taasisi hiyo.
DSC_0653
Pichani juu na chini Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na baadhi ya wahitimu.
DSC_0668
DSC_0703
Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na kamati ya maandali ya mahafali hayo.

WATANZANIA WASHAURIWA KUITUMIA NEEMA YA GESI KUPELEKA HIFADHI YA JAMII KWA KILA MTU

DSC_0013
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,na Mwenyekiti wa mkutano mkubwa wa kimataifa wa hifadhi ya jamii ulioandaliwa na serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Fedha, Mh. Aggrey Mwanri, akiendesha shughuli za mkutano huo uliomalizika hivi karibuni katika kituo cha kimataifa cha mikutano cha Arusha (AICC).(Picha na Zainul Mzige wa modewjiblog).

Na Mwandishi wetu, Arusha
MTAALAMU mmoja wa masuala ya uchumi anayefanyakazi na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Dar es salaam, Rogers Dhliwayo, ameishauri serikali kutumia neema ya gesi kutoa hifadhi ya kutosha kwa wananchi wake.

Dhliwayo alisema hayo wakati akijibu hoja ya Naibu waziri Afya na Ustawi wa jamii, Dk Kebwe S. Kebwe namna ya kufikia lengo la hifadhi ya jamii kwa wote kwa kasi kuliko ilivyo sasa ambapo inafikiriwa ifikapo mwaka 2025 ndio tutakuwa tumefikia asilimia 75 ya hifadhi ya jamii.

Dk. Kebwe alisema hayo wakati wa kujadili mada ya uchokozi iliyotolewa na Dhliwayo mtaalamu wa uchumi ambaye alishawahi kufanyakazi nchini Zimbabwe na Msumbiji.
Alisema kwamba mataifa mengi yametumia raslimali zao kufanya mambo makubwa kwa wananchi wao na Tanzania inaweza kufanya hivyo.
DSC_0005
Ofisa anayeshughulikia sera za hifadhi, UNICEF Tanzania, Bi. Usha Mishra akitoa mrejesho walichojifunza washiriki siku ya kwanza na kutoa mwongozo wa mambo mapya wanayotakiwa kujifunza katika mkutano uliomalizika hivi karibuni jijini Arusha.

Alisema ipo nchi ambayo ilitumia utajiri wake wa almasi kutengeneza miundombinu ya barabara na si vibaya kwa Tanzania kutumia utajiri wake wa gesi kuhakikisha kila mtanzania anapata hifadhi ya jamii.

Alisema kama taifa linaweza kuamua asilimia Fulani kutoka katika sekta ya gesi kuingia katika kuwezesha hifadhi ya jamii ambayo itahakikisha uwapo wa huduma sawa kwa wote.
Alisema uchumi wa Tanzania kutoka mwaka 2000 hadi sasa umekuwa ukikua kwa kasi ingawa kasi hiyo haionekani kwa wananchi ambapo wengi wamejikuta wakiwa katika umaskini wa kukithiri.

Alisema kutokana na tatizo hilo la umaskini wa kukithiri kutoondoka kwa hali hiyo kunasababisha na sekta husika kutotoa ajira za kutosha ambazo zingewezesha watu kuneemeka na uchumi unaokua kwa kasi.
DSC_0079
Mtaalamu wa masuala ya uchumi anayefanyakazi na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Dar es salaam, Rogers Dhliwayo akitoa mada chokonozi wakati wa mkutano mkubwa wa kimataifa wa hifadhi ya jamii ulioandaliwa na serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Fedha ambao umemalizika hivi karibuni jijini Arusha.

Alisema aidha kaya nyingi zimekuwa na idadi kubwa ya watu ikiakisi umaskini unaoambatana na kaya zenye watu wengi na uzazi wa mapema unaowakuta wasichana.

Alisema pamoja na mpango mzuri wa serikali kupitia TASAF kupunguza umaskini wa kukithiri ukishirikiana na mashirika ya Umoja wa Mataifa, ipo haja kwa serikali kuhakikisha kwamba kunakuwa na uratibu unawezesha mipango ya kupunguza umaskini inafanikiwa.

Alisema iwapo TASAF inashughulikia elimu na afya ni dhahiri itahitaji kuwapo kwa shule na walimu na katika afya hospitali na wauguzi na madaktari na dawa.” Ni lazima kuwepo na uratibu ili kufanikisha yote yaliyolengwa” alisema Dhliwayo.

Alisema Tanzania inaweza kujifunza kutoka mataifa ya Rwanda na Eritrea ambayo yamefanikiwa hifadhi ya jamii eneo la afya kufikia zaidi ya asilimia 90 huku wakitumia mifumo thabiti ya afya ya jamii kwa kaya.
DSC_0093
Kuki Tarimo kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii akitoa mada chonokonozi wakati wa mkutano huo.
Aidha amesema kwamba mataifa hayo yamefanikiwa katika malengo ya millennia na kupunguza idadi ya vifo vya wanawake katika uzazi.

Katika mkutano huo ambao uliitishwa na serikali ili kupata misingi ya utengenezaji wa sera na sheria ili kuwezesha watanzania wote kuwa na haki katika kei ya taifa kw akuwezeshwa kuondokana na umaskini wa kukithiri ulihudhuriwa na watalaamu 150 kutoka nchi mbalimbali duniani.

Pia ulifunguliwa na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Iddi ambaye alisema Tanzania kwa sasa inapojianda kuwa na uchumi wa kipato cha kati ipo haja ya kuimarisha sekta za hifadhi ya jamii.
DSC_0101
Mkurugenzi mshiriki anayeshughulikia masuala ya program kutoka makao makuu ya UNICEF, Bi. Alexander Yuster akichangia hoja wakati wa mkutano huo uliomalizika hivi karibuni.
DSC_0109
Meneja Mwendeshaji wa Shirika la Under The Same Sun, Gamariel Mboya akiuliza swali kuhusiana na serikali imejipangaje katika kuhakikisha watu wenye ulemavu wa ngozi wanapataje mafuta ya kuzuia mionzi ya jua inayopelekea ugonjwa kansa ya ngozi.
DSC_0135
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Kebwe Kebwe, akijibu swali kuhusiana na serikali imefanya nini kwa walemavu wa ngozi katika kuhakikisha mafuta kuzuia mionzi ya jua kwa watu hao yanapatikana kiurahisi ili kupunguza athari za kansa kwa walemavu hao. Kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima.
DSC_0159
Mwakilishi wa wazee waliostaafu akiuliza swali kwa Wizara ya afya na ustawi wa jamii kuhusiana na uboreshwaji wa huduma za afya kwa wazee ambapo imekuwa changamoto kubwa kwao.
DSC_0025
Ujumbe wa Makatibu wakuu kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ukishiriki wa mkutano huo.
DSC_0115
Mtaalamu wa mawasiliano wa Shirika la UNICEF Tanzania, Jacqueline Namfua akifurahi jambo wakati wa mkutano huo.
DSC_0029
Pichani juu na chini ni baadhi ya wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa, watengeneza sera, watafiti na waendeshaji wa mifuko ya hifadhi kutoka mataifa ya Kenya, Uganda, Bangladesh, Mozambique, Lesotho, Malawi, Afrika Kusini, Ghana, Ethiopia, Zambia, Sudan Kusini na wenyeji Tanzania uliomalizika hivi karibuni jijini Arusha.
DSC_0107 DSC_0128 DSC_0067
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, akifuatilia kwa umakini maoni mbalimbali yaliyokuwa yakiwasishwa kwenye mkutano.

WATOTO WALIVYOPATA AJIRA WAKATI WA KAMPENI ZA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA TABORA MJINI.

Baadhi ya watoto walionaswa na kamera ya mtaani ya mtandao huu katika moja ya mitaa iliyokuwa ikifanya kampeni za uchaguzi serikali za mitaa Tabora mjini.
HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA!!
Pamoja na Serikali kuridhia mikataba mbalimbali ya nchi za Afrika na Kimataifa pia zinazoainisha ulinzi  wa haki za mtoto,lakini imeshangaza kuwa watoto bado wanaendelea kutumika vibaya ikiwa ni pamoja na kazi za udharirishaji kama kukata viuno mbele ya hadhara kwa kupata ujira kati ya shilingi 500/= hadi elfu 3000/=.

Kamera ya mtaani ya KAPIPIJhabari.COM ilitembelea kuangalia mchakato wa kampeni za uchaguzi wa Serikali za mitaa ulivyokuwa ukiendeshwa na vyama mbalimbali vya kisiasa na kubaini mapungufu kadhaa ikiwemo kubwa zaidi la kuwatumikisha watoto hawa katika kampeni hizo jambo linalopingana na Mikataba ya kimataifa inayolinda na kutetea haki za watoto ulimwenguni.

Jambo hili ingawa lilichukuliwa kama ni suala la kawaida lakini wataalam wa masuala ya watoto wamekuwa wakiyapigia kelele hasa shughuli kama hizi ambazo zinamdharirisha mtoto huku akidanganywa kwa malipo hayo kiduchu.

Hata hivyo mtandao huu ulifuatilia kutaka kujua namna walivyokusanywa watoto hao na kupatiwa ajira hiyo ya muda....,Je,kuna mtu alikuwa nyuma yao au wagombea ndio walikuwa wakiwasaka watoto hao waje wakate viuno mbele ya hadhara na kuwa kivutio kikubwa cha kusikiliza kampeni hizo za kuwapata viongozi wa mitaa?

Maelezo yaliyotolewa na watu mbalimbali wakiwemo watoto wenyewe,
WATU WAZIMA:-"Hawa watoto tunawaona tu karibu kila mkutano wa kampeni  za CCM kwenye mitaa yetu,ila ninachojua mimi hawa wanalipwa wakimaliza kufanya hiyo shoo yao"
                                "Unajua kuwa mimi ni mhusika lakini tumelazimika kuwatumia hawa watoto kwa sababu wasanii wengine wakubwa wanataka pesa nyingi sasa hizo sisi hatuna kwahiyo tunaona ni bora tuwatumie hawa watoto na wao wapate pesa ya sabuni kidogo"alisema mmoja kati ya wanachama waliokuwa wakifanya maandalizi ya kampeni katika mtaa mmoja kata ya Mbugani hapa manispaa ya Tabora.

 WATOTO WENYEWE:-"Sisi anatuitaga huyo baba ndio tunakuja kucheza shoo halafu wanatupatia shilingi 2000 tunagawana wakati tukimaliza tu"
                                         "Mimi nikipata hela nampelekea mama ananiwekea,nikifikisha nyingi ntanunua nguo"

BAADHI YA WASANII:-"Mimi kundi langu tunapiga shoo kama kawaida lakini hawa jamaa wametuzingua eti wanataka tufanye shoo  kwa shilingi elfu 10,000/= sisi tuliwaambia shilingi elfu 70,000/=ndio maana unaona wanawatumia hao watoto kwa pesa ndogo,hawaoni hata dhambi kwa Mungu"

Pamoja na watoto hao kufanyishwa kazi hiyo ya udharirishaji  mwanzo wa kampeni hadi siku ya mwisho wa kampeni hakuna hatua zozote zilizochukuliwa dhidi ya utumikishwaji watoto hao ambao wanaandaliwa kuwa ni taifa la kesho,huku uchunguzi ukibainisha kuwa kati ya watoto hao hakukuwepo mtoto hata mmoja wa mgombea bali waliotumika walikuwa ni watoto wa watu hohehahe.


Sunday, December 21, 2014

TIGO YATOA MSAADA HOSPITALI YA WILAYA YA URAMBO

Mkurugenzi wa kampuni ya Simu za mkononi ya Tigo kanda ya Ziwa Bw.Ally Maswanya akikabidhi msaada wa vifaa vya hospitali  kwa  Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya wilaya ya Urambo Dr.Heri  Kagya  vifaa hivyo ni pamoja na  magodoro 35,Shuka 35 na Blanketi 35 ikiwa ni sehemu ya Kampuni ya Tigo kurejesha  fadhila kwa wananchi ambao ni watumiaji wa mtandao huo.
Mkurugenzi wa Tigo kanda ya ziwa Bw.Ally Maswanya akizungumza kabla ya kukabidhi msaada huo wa vifaa vya hospitali ambapo aliahidi Kampuni ya Tigo itatoa msaada wa vyandarua zaidi ya mia mbili ili viweze kusaidia katika Wadi mbalimbali husasni ya akina mama wajawazito.
Meneja wa Tigo mkoa wa Tabora Bw.Brite Kisanga akizungumza dhamira ya kampuni ya Tigo kutoa msaada huo kwa hospitali ya wilaya ya Urambo.
Mkurugenzi wa kampuni ya Tigo Bw.Ally Maswanya akikabidhi msaada wa mashuka 35 kwa Mganga Mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya Urambo.(Picha na KAPIPIJhabari.COM)