Pages

KAPIPI TV

Monday, December 22, 2014

WAKAZI WA JIMBO LA KIGOMA KASKAZINI WAKOSA HAKI YA KUPIGAKURA!!!

Na Magreth Magosso,Kasulu

ZAIDI ya wakazi  47,000 waishio katika  Kijiji cha  Zashe na kijiji na Kata ya Kagunga vilivyopo  pembezoni mwa ukanda wa Ziwa Tanganyika Mkoa wa Kigoma wameshindwa kujitokeza kwa wingi  jana katika Marudio ya Uchaguzi wa  viongozi wa Serikali za mitaa.

Changamoto kubwa iliyochangia hali hiyo ni pamoja na kuenguliwa kwa Chama cha Alliance And Tranciparecy For Change Tanzania kutokana na pingamizi walilowekewa na wasimamizi husika wa vijiji hivyo vyenye vitongoji 11,huku uongozi wa chama wakidai walizuiwa tangu 13,Novemba,2014 kwa sababu zisizoeleweka .

Akizungumza na Mtandao huu Mwenyekiti wa Chama cha ACT Sendwe Ibrahimu alisema  kijiji cha Kagunga ina vitongoji  vitano kwa mujibu wa watu waliojiandikisha ,waliopiga kura na waliosusa kushiriki mchakato huo .

Mkware

 Mkware Wananchi waliojiandikisha walikuwa 435,waliokwenda kupiga kura 184 tu,na waliogoma kupiga kura 256,kitongoji cha Mlama waliojiandikisha kupiga kura 549,waliopiga kura 92 tu,na walioshindwa kwenda kupiga kura 557.kitongoji cha kagunga waliojiandikisha 760,waliopiga kura 210  na wasiopiga kura 550.

Makombe

Kitongoji cha Makombe waliojiandikisha 682  waliopiga kura 142   na wasiopiga kura 540 ,kitongoji nyamilambo 459 wananchi waliojiandikisha kupiga kura,waliopiga kura 300,wasiopiga kura 259na kitongoji cha Lusolo  wakazi 570 walijiandikisha na waliopiga kura 320 na wasiopiga kura 250 .

Kijiji cha Zashe

Kwa Upande wa kijiji cha Zashe kina vitongoji vitano ikiwa na jumla ya wakazi zaidi ya 18,000 ambapo katika kitongoji cha Kware wakazi waliojiandikisha walikuwa 464,waliopiga kura 194 na wasiopiga kura walikuwa 270.

Kitongoji cha Mwibole waliojiandikisha walikuwa 210,walioshiriki kupiga kura walikuwa 50 huku walioshindwa kufika katika vituo vya kupiga kura walikuwa 160,Wakatihuohuo katika kitongoji cha Misele waliojiandikisha 361,waliopiga kura 111 na wasiopiga kura 250.

Kitongoji cha Mibombo waliojiandikisha walikuwa wakazi 314 ,waliopiga kura 174 na wasiopiga kura 140 na Kitongoji cha Ngonya waliojiandikisha 367,waliopiga kura 480 na wasioshiriki kupiga kura 207.

Kasulu

Kwa upande wa Wilaya ya Kasulu ,uchaguzi ulirudiwa  katika halmashauri nzima ya wilaya hiyo inayomiliki mitaa 109 ,vitongoji 288 na vijiji 70 ,ambapo uchaguzi ulikuwa na changamoto mbalimbali hasa muda wa kupiga kura hauendani na uhalisia wa kigoma na ukiukwaji wa kanuni husika na kupelekea baadhi ya viongozi wa  ccm na Nccr-mageuzi kushikana mashati na lugha chafu,

Kwa mujibu wa taratibu mwisho wa kupiga kura kitaifa ni saa 10 za alasiri kwa kigoma ni shida kutokana na hali ya kijiografia hivyo kwa busara za vyama vilishoriki na uongozi husika waliongeza muda kulingana na muda walioanza shughuli hiyo.

Akifafanua hilo Katibu itikadi na uenezi Mkoa wa kigoma Kalembe Masudi alisema Matokeo ya awali hadi leo Chama cha ccm kinaongoza katika ngazi ya kitongoji,kijiji na mitaa kama ifuatavyo,kwa upande wa kasulu mjini ccm inaongoza kwa kunyakua mitaa 73,ACT yashika viti 4  na UKAWA viti 15, Huku mitaa 19 bado wanaendelea  kuhesabu kura katika mitaa husika.

Kwa upande wa Vitongoji  ccm imeshika viti 128 kati ya vitongoji 288  vya hapo, Huku  viti 27 vimeshikwa na vyama vya upinzani wakati vitongoji 133 bado wanaendelea kuhesabu kura  wakati huohuo kati ya vijiji 70 Chama cha ccm kinaongoza kwa viti 29 na upinzani  vikiwa na viti 15 na vijiji 26 wakiendelea kuhesabu kura zilizosalia kwenye maeneo husika.

No comments: