Pages

KAPIPI TV

Monday, December 22, 2014

WATOTO WALIVYOPATA AJIRA WAKATI WA KAMPENI ZA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA TABORA MJINI.

Baadhi ya watoto walionaswa na kamera ya mtaani ya mtandao huu katika moja ya mitaa iliyokuwa ikifanya kampeni za uchaguzi serikali za mitaa Tabora mjini.
HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA!!
Pamoja na Serikali kuridhia mikataba mbalimbali ya nchi za Afrika na Kimataifa pia zinazoainisha ulinzi  wa haki za mtoto,lakini imeshangaza kuwa watoto bado wanaendelea kutumika vibaya ikiwa ni pamoja na kazi za udharirishaji kama kukata viuno mbele ya hadhara kwa kupata ujira kati ya shilingi 500/= hadi elfu 3000/=.

Kamera ya mtaani ya KAPIPIJhabari.COM ilitembelea kuangalia mchakato wa kampeni za uchaguzi wa Serikali za mitaa ulivyokuwa ukiendeshwa na vyama mbalimbali vya kisiasa na kubaini mapungufu kadhaa ikiwemo kubwa zaidi la kuwatumikisha watoto hawa katika kampeni hizo jambo linalopingana na Mikataba ya kimataifa inayolinda na kutetea haki za watoto ulimwenguni.

Jambo hili ingawa lilichukuliwa kama ni suala la kawaida lakini wataalam wa masuala ya watoto wamekuwa wakiyapigia kelele hasa shughuli kama hizi ambazo zinamdharirisha mtoto huku akidanganywa kwa malipo hayo kiduchu.

Hata hivyo mtandao huu ulifuatilia kutaka kujua namna walivyokusanywa watoto hao na kupatiwa ajira hiyo ya muda....,Je,kuna mtu alikuwa nyuma yao au wagombea ndio walikuwa wakiwasaka watoto hao waje wakate viuno mbele ya hadhara na kuwa kivutio kikubwa cha kusikiliza kampeni hizo za kuwapata viongozi wa mitaa?

Maelezo yaliyotolewa na watu mbalimbali wakiwemo watoto wenyewe,
WATU WAZIMA:-"Hawa watoto tunawaona tu karibu kila mkutano wa kampeni  za CCM kwenye mitaa yetu,ila ninachojua mimi hawa wanalipwa wakimaliza kufanya hiyo shoo yao"
                                "Unajua kuwa mimi ni mhusika lakini tumelazimika kuwatumia hawa watoto kwa sababu wasanii wengine wakubwa wanataka pesa nyingi sasa hizo sisi hatuna kwahiyo tunaona ni bora tuwatumie hawa watoto na wao wapate pesa ya sabuni kidogo"alisema mmoja kati ya wanachama waliokuwa wakifanya maandalizi ya kampeni katika mtaa mmoja kata ya Mbugani hapa manispaa ya Tabora.

 WATOTO WENYEWE:-"Sisi anatuitaga huyo baba ndio tunakuja kucheza shoo halafu wanatupatia shilingi 2000 tunagawana wakati tukimaliza tu"
                                         "Mimi nikipata hela nampelekea mama ananiwekea,nikifikisha nyingi ntanunua nguo"

BAADHI YA WASANII:-"Mimi kundi langu tunapiga shoo kama kawaida lakini hawa jamaa wametuzingua eti wanataka tufanye shoo  kwa shilingi elfu 10,000/= sisi tuliwaambia shilingi elfu 70,000/=ndio maana unaona wanawatumia hao watoto kwa pesa ndogo,hawaoni hata dhambi kwa Mungu"

Pamoja na watoto hao kufanyishwa kazi hiyo ya udharirishaji  mwanzo wa kampeni hadi siku ya mwisho wa kampeni hakuna hatua zozote zilizochukuliwa dhidi ya utumikishwaji watoto hao ambao wanaandaliwa kuwa ni taifa la kesho,huku uchunguzi ukibainisha kuwa kati ya watoto hao hakukuwepo mtoto hata mmoja wa mgombea bali waliotumika walikuwa ni watoto wa watu hohehahe.


No comments: