Wafanyabiashara wa mabasi ya kusafirisha abiria aina ya Hiace
katika manispaa ya kigoma ujiji wilaya ya kigoma Mkoa wa Kigoma ,wapo hatarini
kufutiwa leseni kutokana na kukataa
uwepo wa mfumo wa soko huria na kutaka kuipangia sheria serikali.
Uamuzi huo
unakuja siku chache tu baada ya uongozi wa serikali ya wilaya ,kwa kushirikiana
na manispaa husika kutoa onyo kwa wafanyabiashara wasiokubali kufuata
sheria,kanuni na taratibu wa uwepo wa aina zingine za usafirishaji wa abiria.
Wafanyabiashara
hao waliamua kufanya majarabio la mgomo
zaidi ya mara mbili baada ya
kugundua uwepo wa vibajaji na michomoko inachangia pato finyu ambapo katika
ulipaji wa mapato katika mamlaka husika
hawalingani .
Hayo
yalibainika kigoma ujiji juzi katika
taarifa ya utekelezwaji wa miradi mbalimbali ya jamii katika ziara ya kamati ya
siasa ya mkoa ,iliyokuwa ikiongozwa na mwenyekiti wa ccm kigoma Dkt. Aman
Kabourou .
Alisema
mgomo wa mara kwa mara kwa wafanyabiashara hao dhidi ya magari aina ya michomoko
na Bajaji imekuwa kero isiyo na mashiko kwa wakazi na serikali husika na
kuwataka waongeze ubunifu wa huduma kwa walaji.
“tume maalum
zimeundwa katika kila aina ya usafiri na
idara husika ili kila mmoja akae na watu wake wajadili adha na mkakati wa uwajibikaji na akaetengua kanuni na
taratibu kukiona” alisema Maneno.
Kwa upande
wa Mwenyekiti ccm Dkt.Kabourou alisema adha ya migomo ya mabasi inadhulumu haki za wadau wengine wa usafiri na kudumaza
maendeleo ya jamii kwa kuzuia ajira binafsi kwa vijana.
Alisema anaunga hoja ya kufungiwa leseni kwa wale
watakaobanika ni chanzo cha kudumaza sera ya biashara ya ushindani ambapo kwa
wakazi wa vijijini wanatumia gari za michomoko katika shughuli za
biashara na kusihi wasiwe juu ya sheria.
Aliongeza kwa
kusema wenye mabasi ya abiria waongeze wigo wa kupeleka huduma katika maeneo
yaliyo pembezoni mwa kigoma ujiji na kuwataka waachane na kasumba ya kuwaweka
abiria kwa muda mrefu kituoni hali
inayochangia wakimbiwe na abiria.
Kwa upande wa Katibu wa Itikadi na uenezi ccm
Kalembe Masudi alisema changamoto ipo katika ulipaji wa kodi,sheria ya ukomo wa
abiria na vituo ambapo kwa upande wa michomoko na bajaji zinapakia abiria
mahali popote ilihali hiace ikifanya hivyo hulipishwa faini.
Ashauri
kupitia kamati teule washirikiane kuondoa tofauti na kila mmoja aridhie uwepo wa mwenzake na
kutambua serikali imeridhia mfumo wa biashara
na kusihi wawe wabunifu na
kukidhi hitaji la abiria.