Pages

KAPIPI TV

Monday, September 29, 2014

WAMILIKI WA DALADALA KUITUNISHIA MISULI SERIKALI KIGOMA

Na Magreth Magosso,Kigoma

Wafanyabiashara  wa mabasi ya kusafirisha abiria aina ya Hiace katika manispaa ya kigoma ujiji wilaya ya kigoma Mkoa wa Kigoma ,wapo hatarini kufutiwa leseni kutokana na  kukataa uwepo wa mfumo wa soko  huria  na kutaka kuipangia sheria serikali.

Uamuzi huo unakuja siku chache tu baada ya uongozi wa serikali ya wilaya ,kwa kushirikiana na manispaa husika kutoa onyo kwa wafanyabiashara wasiokubali kufuata sheria,kanuni na taratibu wa uwepo wa aina zingine za usafirishaji wa abiria.

Wafanyabiashara hao waliamua kufanya majarabio la mgomo  zaidi ya mara mbili baada  ya kugundua uwepo wa vibajaji na michomoko inachangia pato finyu ambapo katika ulipaji wa mapato  katika mamlaka husika hawalingani .
 
Hayo yalibainika kigoma ujiji juzi  katika taarifa ya utekelezwaji wa miradi mbalimbali ya jamii katika ziara ya kamati ya siasa ya mkoa ,iliyokuwa ikiongozwa na mwenyekiti wa ccm kigoma Dkt. Aman Kabourou  .
 
Alisema mgomo wa mara kwa mara kwa wafanyabiashara hao dhidi ya magari aina ya michomoko na Bajaji imekuwa kero isiyo na mashiko kwa wakazi na serikali husika na kuwataka waongeze ubunifu wa huduma kwa walaji.

“tume maalum  zimeundwa katika kila aina ya usafiri na idara husika ili kila mmoja akae na watu wake wajadili adha na mkakati  wa uwajibikaji na akaetengua kanuni na taratibu kukiona” alisema Maneno.
 
Kwa upande wa Mwenyekiti  ccm Dkt.Kabourou  alisema adha ya migomo ya mabasi  inadhulumu  haki za wadau wengine wa usafiri na kudumaza maendeleo ya jamii kwa kuzuia ajira binafsi kwa vijana.
 
Alisema  anaunga hoja ya kufungiwa leseni kwa wale watakaobanika ni chanzo cha kudumaza sera ya biashara ya ushindani  ambapo kwa  wakazi wa vijijini wanatumia gari za michomoko katika shughuli za biashara na kusihi wasiwe juu ya sheria.
 
Aliongeza kwa kusema wenye mabasi ya abiria waongeze wigo wa kupeleka huduma katika maeneo yaliyo pembezoni mwa kigoma ujiji na kuwataka waachane na kasumba ya kuwaweka abiria kwa  muda mrefu kituoni hali inayochangia  wakimbiwe na abiria.

 Kwa upande wa Katibu wa Itikadi na uenezi ccm Kalembe Masudi alisema changamoto ipo katika ulipaji wa kodi,sheria ya ukomo wa abiria na vituo ambapo kwa upande wa michomoko na bajaji zinapakia abiria mahali popote ilihali hiace ikifanya hivyo hulipishwa faini.
 
Ashauri kupitia kamati teule washirikiane kuondoa tofauti  na kila mmoja aridhie uwepo wa mwenzake na kutambua serikali imeridhia mfumo wa biashara  na kusihi wawe  wabunifu na kukidhi hitaji  la abiria.

No comments: