Pages

KAPIPI TV

Sunday, September 28, 2014

BODABODA WATEMBELEA WAGONJWA HOSPITALINI NA KUTOA MISAADA -TABORA

Baadhi ya wanachama wa chama cha Waendesha Bodaboda mkoa wa Tabora ambao walitembelea hospitali ya rufaa ya mkoa wa Tabora Kitete kuona wagonjwa na kufanya usafi wa mazingira ambapo tukio hilo lilikwenda sambamba na kutoa misaada kwa wagonjwa ikiwemo Sabuni,vyandarua na vinywaji kama Juisi katika Wadi ya kulaza watoto kinamama wajawazito.
Mwenyekiti wa Chama cha Waendesha Bodaboda Bw.Waziri Kipusi(mwenye shati ya draft)akikabidhi msaada wa vyandarua kwa mmoja kati ya wakunga katika Wadi ya kinamama wajawazito.
Mwenyekiti wa waendesha Bodaboda Waziri Kipusi alikabidhi vyandarua kwa kinamama waliojifungua watoto ambao hawajatimiza muda wa kuzaliwa(NJITI)
Katibu wa Waendesha Bodaboda Kassim Kiduli akikabidhi msaada wa sabuni kwa akinamama waliojifungua huku akitoa nasaha fupi zilizowafanya kinamama hawa kuangua kicheko kwa furaha.
Waziri Kipusi akimpatia juisi mmoja kati ya watoto wagonjwa

Mmoja kati ya Waendesha Bodaboda Bi.Zay Mchemba akihojiwa na waandishi wa habari wa habari namna ambavyo anashiriki katika kazi hiyo ya Bodaboda.





No comments: