Pages

KAPIPI TV

Thursday, August 7, 2014

JK:TUNAKWAMISHWA NA UZALISHAJI NA MATUMIZI MADOGO MNO YA UMEME


o1
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Rais Goodluck Jonathan wakati muda mfupi kabla ya kuanza kwa  Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika uliofanyika jijini Washington DC chini ya uenyekiti wa Rais Barack Obama wa Marekani  Agosti 6, 2014
o3
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akijadiliana jambo na Rais Barak Obama wa Marekani kwenye ukumbi wa Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika uliofanyika jijini Washington DC chini ya uenyekiti wa Rais Obama wa Marekani  Agosti  6, 2014
o2
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa kimataifa Mhe Bernard Membe na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Librerata Mulamula kwenye Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika uliofanyika jijini Washington DC chini ya uenyekiti wa Rais Barack Obama wa Marekani  Agosti  6, 2014
o4
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifurahia jambo na Rais Barak Obama wa Marekani kwenye ukumbi wa Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika uliofanyika jijini Washington DC chini ya uenyekiti wa Rais Obama wa Marekani  Agosti  6, 2014
o5
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akijadiliana jambo na Rais Barak Obama wa Marekani kwenye ukumbi wa Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika uliofanyika jijini Washington DC chini ya uenyekiti wa Rais Obama wa Marekani  Agosti  6, 2014
o6 o7
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akijadiliana jambo na Rais Barak Obama wa Marekani kwenye ukumbi wa Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika uliofanyika jijini Washington DC chini ya uenyekiti wa Rais Obama wa Marekani  Agosti  6, 2014
o8
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mwenyekiti wa Kamisheni  ya Umoja wa Afrika (AU), Mhe. Dkt. Nkosazana Dlamini-Zum wakimsikiliza Rais Barak Obama wa Marekani wakati akiongoza  Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika uliofanyika jijini Washington DC Agosti 6, 2014
oo1
Rais Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na viongozi wengine wa Afrika wakipata picha ya kumbukumbu na mwenyeji wao Rais Barak Obama wa Marekani wakati wa Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika uliofanyika jijini Washington DC chini ya uenyekiti wa Rais Obama wa Marekani  Agosti  6, 2014
oo3
Viongozi wa Afrika wakisalimiana kwa furaha baada ya kupata picha ya pamoja wakati wa Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika uliofanyika jijini Washington DC chini ya uenyekiti wa Rais Obama wa Marekani  Agosti  6, 2014
……………………………………………………………………………….
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa moja ya sababu kubwa zinazokwamisha maendeleo makubwa zaidi na ya haraka zaidi ya Afrika ni uzalishaji mdogo na matumizi ya chini mno ya umeme.
 
Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa hali hiyo inaeleza jinsi ongezeko la uzalishaji na matumizi ya umeme linavyoweza kuharakisha maendeleo ya Afrika na kuleta manufaa ya dhahiri kwa kila familia na kwa kila Mwafrika.
 
Rais Kikwete ameyasema hayo jana, Jumatano, Agosti 6, 2014, wakati alipozungumza kwenye Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika uliofanyika chini ya uenyekiti wa Rais Barack Obama, ambaye ni mwenyeji wa Mkutano huo. Rais Kikwete amewaambia wakuu wa nchi hizo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani kuwa ni dhahiri kuwa bila ongezeko kubwa la uzalishaji na matumizi ya umeme Bara la Afrika halitatoka kwenye uduni. Rais amesema kuwa kwa mujibu wa Ripoti ya Kanda ya Shirika la Umoja wa Mataifa Mazingira (UNEP) “Efficient Lighting in Sub Saharan African Countries” matumizi ya umeme katika Bara zima la Afrika ni asilimia 31 tu na hivyo kulifanya Bara la Afrika kutumia asilimia tatu tu ya umeme wote duniani. Rais Kikwete amesema kuwa ili kuelewa udogo wa matumizi ya umeme ya Bara la Afrika ni kuangalia matumizi ya nishani hiyo kwa kila mkazi wa Bara hilo na yule wa Marekani. Amesema kuwa wakati kila raia wa Marekani anatumia kilowati 13, 246 katika Afrika wastani ni kilowati 440. Ameongeza Rais Kikwete: “Ukiondoa Afrika Kusini, matumizi ya umeme kwa kila raia wa Afrika yanateremka na kufikia kilowati 160 tu.”
 
Amefafanua Rais Kikwete: “Uzalishaji wa jumla wa umeme wa Bara la Afrika ni gigawati 63 ambazo ni sawa na umeme unaozalishwa na nchi moja tu ya Ulaya – Hispania. Ukiondoa Afrika Kusini, nchi zinazobakia wa Afrika zina uwezo wa kuzalisha gigawati 28 tu, kiasi ambacho kinazalishwa na nchi moja tu ya Marekani Kusini ya Argentina.”
 
Rais Kikwete ambaye alikuwa anafafanua jinsi utoaji huduma ulio dhahiri unavyoweza kunufaisha wananchi na kujenga mazingira ya taasisi zisizokuwa za kiserikali kushamiri, ametaja mambo mengine ya msingi ambayo ni lazima yawepo ili wananchi waweze kunufaika ikiwemo elimu, ushamiri wa sekta binafsi, sera sahihi za kiuchumi, uwekezaji katika ujenzi wa miundombinu na uboreshaji wa kilimo.
 
Pia Rais Kikwete ametaja mambo mengine muhimu yanayoweza kusaidia kuboresha maisha ya wananchi kuwa ni uendelezaji na matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano pamoja na kulea na kukuza demokrasia, utawala bora na utawala wa sheria.
 
Rais Kikwete ambaye yuko katika ziara ya kikazi ya siku tisa katika Marekani, anaondoka mjini Washington, D.C., leo kwenda Houston ambako atafungua na kushiriki katika mkutano wa uwekezaji katika uchumi wa Tanzania. Mwisho! Imetolewa na; Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu – Dar es Salaam. 07 Agosti, 2014

KONGAMANO LA KUHIMIZA UWEKEZAJI TANZANIA LAFANYIKA NCHINI MAREKANI

1
6
Rais Jakaya Kikwete ambaye alikuwa Mzungumzaji Mkuu katika Kongamano la kuvutia wawekezaji nchini lililofanyika jana Washington DC, Marekani. Wengine pichani kutoka kulia ni Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo, Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu na Balozi wa Marekani nchini Tanzania Mhe. Mark Childress.
2
Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula akiongea katika Kongamano la kuvutia Uwekezaji nchini lililofanyika Washington DC, Marekani.
3
Kaimu Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania Bi. Devota Mdachi akifafanua kwa kina fursa za uwekezaji katika sekta ya utalii wakati alipokuwa akiongea katika Kongamano la kuvutia Uwekezaji nchini lililofanyika Washington DC, Marekani.
4
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini Bi. Julieth Kairuki akisisitiza jambo wakati alipokuwa akiongea katika Kongamano la kuvutia Uwekezaji nchini lililofanyika Washington DC, Marekani.
5
Meza Kuu ya Wazungumzaji katika Kongamano la kuvutia wawekezaji nchini lililofanyika Washington DC, Marekani. Kutoka Kushoto ni Mwezeshaji Bw. Kamran Khan; Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu; Waziri wa Uchukuzi Mhe. Harrison Mwakyembe; Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii nchini Bi. Devota Mdachi na Uwekezaji nchini lililofanyika

Wednesday, August 6, 2014

MKE, MUME WAKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA-ARUSHA

IMG_20140804_104207
Gari aina ya Toyota Corolla lenye namba za usajili T.589 AZS likiwa limebeba magunia ya madawa ya kulevya aina ya bhangi mara baada ya kukamatwa eneo la Sanawari jijini Arusha na askari wa kitengo cha kuzuia Madawa ya Kulevya mkoani hapa. (Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha)
…………………………………………………………………
Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha
Jeshi la Polisi Mkoani Arusha limewakamata  watu watano wakiwa na magunia saba ya madawa ya kulevya aina ya bhangi wakiwemo mke na mume. Awali askari wa Kitengo cha Kuzuia Madawa ya Kulevya Mkoani hapa wakiwa doria walipata taarifa toka kwa raia wema iliyoeleza kuwepo kwa watu wanaosafirisha madawa hayo.
Mara baada ya kupata taarifa hiyo askari hao waliweka mtego maeneo ya Sanawari ambapo muda wa saa 3:30 usiku walifanikiwa kuwakamata watuhumiwa wawili ambao ni Hussein Rashid (35) mkazi wa Sakina, dereva pamoja na mwenzake Sebastian Wilbert (37) Fundi magari, mkazi wa Ilboru wakiwa wanasafirisha magunia matano ya madawa ya kulevya aina ya bhangi yenye uzito wa kilogramu 171 kuelekea nchi jirani ya Kenya kwa kutumia gari aina ya Toyota Corolla lenye namba za usajili T. 589 AZS.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Liberatus Sabas alisema kwamba, mara baada ya watuhumiwa hao kuhojiwa walikiri kosa hilo na kumtaja mwanamke aitwaye Flora John (38) Mkazi wa Ekenywa- Ngaramtoni kuwa ndio aliyewauzia.
Kamanda Sabas aliendelea kwa kusema kwamba, askari hao walianza kumfutilia mwanamke huyo ambapo jana Jumanne tarehe 05.08.2014 walikwenda nyumbani  kwake na kumkuta mtuhumiwa ambaye ni muuzaji akiwa na mume wake aitwaye John Meleji (45) Mkazi wa Ekenywa na mara baada ya kufanya upekuzi walikuta gunia moja la madawa ya kulevya aina bhangi ndani ya nyumba hiyo.
Mbali na kuwakamata watuhumiwa hao ambao ni mke na mume pia askari hao walimkamata jirani yao aitwaye Loseriani Metelami (21) Mkulima mkazi wa Ekenywa baada ya yeye pia kukutwa na gunia moja la madawa ya kulevya aina ya bhangi hivyo kufanya jumla ya magunia yaliyokamatwa kuwa saba.
Watuhumiwa hao watano wanatarajiwa kufikishwa mahakamani hivi karibuni mara baada ya upelelezi kukamilika.

WANANCHI WAMIMINIKA BANDA LA NHIF NANENANE LINDI


???????????
 Ofisa Matekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Ambrose Manyanda akitoa huduma ya elimu inayohusu Mfuko kwa mdau aliyetembelea banda la Mfuko kwenye maonesho ya Nane Nane Mkoa wa Lindi.
???????????Meneja wa NHIF Mkoa wa Lindi Fortunata Raymond akiwakaribisha akina mama kwenye moja ya mabanda ya Mfuko kwa ajili ya kupata huduma ya upimaji wa Saratani huduma inayotolewa na Mfuko kwenye maonesho hayo.
???????????Wananchi wakisubiri kupata huduma ya upimaji afya bure katika banda la NHIF ambalo huduma za upimaji zinatolewa bure.
???????????Burudani ya ngoma na maigizo ikiendelea katika banda kla NHIF kwa lengo la kuelimisha.
???????????Sehemu ya ushauri wa namna ya kujikinga na maradhi yasiyoambukiza ikiendelea na huduma zake.
???????????Huduma zikiendelea bandani hapo.
???????????
Kaya ya Said Mnyou ikiwa katika picha ya pamoja baada ya kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF), wananchi wanajiunga moja kwa moja kwenye maonesho hayo.
???????????
Kikundi cha sanaa kikiendelea na uhamasishaji wa wananchi kujiunga na CHF na kunufaika na huduma zinazotolewa kwenye maonesho hayo.

BENKI YA POSTA YADHAMINI KLABU YA WAANDISHI, TASWA SC

1
2
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Moses Manyata (wa kwanza kushoto)akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kuhusiana na hatua ya benki hiyo kuisaidia timu ya waandishi wa habari za michezo nchini Taswa SC. Benki hiyo ilikabidhi hundi ya Sh milioni 2 na pia itasaidia jezi kwa timu ya mpira wa miguu na netiboli. Kwa kwanza kushoto ni Afisa Mawasiliano wa TPB, Chichi Banda na wa kwanza  kulia ni  Taswa SC, Majuto Omary.
3 
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Moses Manyata (wa kwanza kushoto)akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kuhusiana na hatua ya benki hiyo kuisaidia timu ya waandishi wa habari za michezo nchini Taswa SC. Benki hiyo ilikabidhi hundi ya Sh milioni 2 na pia itasaidia jezi kwa timu ya mpira wa miguu na netiboli
……………………………………………………………………………….
 
Benki ya Posta Tanzania (TPB) imeidhamini klabu ya waandishi wa habari za michezo nchini (Taswa SC), kufuatia juhudi zake za kuhamasisha na kuendeleza michezo nchini.
 
Benki hiyo imeisaidia klabu hiyo fedha taslims sh. Milioni 2 na inatarajia kuwapa jezi seti moja moja kwa timu ya mpira wa miguu na mpira wa pete (netiboli) ikiwa ni kuthamini mchango wao Taswa SC katika sekta ya michezo nchini.
 
Kaimu Afisa Mteandaji Mkuu wa TPB, Moses Manyatta alisema kuwa wanafuraha kubwa kusikia kuwa waandishi wa habari za michezo wameamua kufanyakazi kwa vitendo kwa kuanzisha timu ya mpira wa miguu ambayo kwa sasa ina miaka zaidi ya 20 na timu ya mpira wa pete (netiboli) ambayo ina mwaka mmoja na nusu.
 
“Tumefarijika kutokana na ukweli kuwa mbali ya kuandika, mmeamua kufanya michezo kwa vitendo na kuwa mfano wa kuigwa, TPB ipo bega kwa bega nanyi na tutaendelea kushirikiana katika sekta mbali mbali tofauti na michezo,” alisema Manyatta.
 
Alisema kuwa TPB ni benki halisi ya Kitanzania yenye kutoa huduma bora kwa wateja wake na kwa sasa imeingia katika sekta ya michezo ambapo kwa sasa inashirikiana na timu kongwe nchini, Yanga na Simba katika zoezi la kuandikisha upya wanachama na mashabiki wa timu hizo.
 
Mwenyekiti wa Taswa SC, Majuto Omary aliipongeza TPB kwa kutoa msaada huo na kuahidi kuwa wadau wakubwa wa benki hiyo katika shughuli zake mbalimabli.
 
Majuto alisema kuwa wameomba udhamini kwa makampuni mengi kutokana na ukweli kuwa timu yao inachangamoto nyingi pamoja na kuwa na mafanikio makubwa.
 
“Tunawapa pongezi kubwa sana TPB, mmeonyesha kuwa ni benki halisi ya Kitanzania yenye kutoa huduma bora hapa nchini, Taswa SC ipo bega kwa bega nanyi katika kuendeleza gurudumu la maendeleo la nchi hii,” alisema Majuto.
 
Majuto pia aliwaomba wanachama wa timu ya Taswa SC kuwa mstari wambele katika shughuli za TPB kwani wameonyesha kuwajali katika shughuli za kila siku.

JUHUDI ZA UONGOZI WA MKOA WA RUKWA KUENDELEZA UTALII WA MAPOROMOKO YA KALAMBO (KALAMBO FALLS) ZAENDELEA

 
Zipo jitihada kadhaa zilizokwishafanywa na uongozi wa Mkoa wa Rukwa ukiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Eng. Stella Manyanya katika kuhakikisha eneo la maporomoko hayo linaimarishwa na kuwa kivutio kikubwa cha utalii na chanzo cha mapato kwa halmashauri husika na taifa kwa ujumla. 
 
Jitihada hizo ni pamoja kuwahamasisha wananchi wa kijiji cha Kapozwa na wadau wengine katika kutambua umuhimu wa maporomoko hayo ambapo mpaka hivi sasa wananchi hao wameshashiriki kufyatua matofali kwa ajili ya kujenga kituo cha utalii katika eneo hilo.
 
 Jitihada zingine ni zile za kupima viwanja na kuandaa michoro katika eneo hilo ambapo ramani imeshaidhinishwa na tathmini ya kuwafidia wananchi maeneo yao imeshafanyika.
Aidha zimekuwepo jitihada za kutafuta fedha kutoka Serikalini na kwa wahisani mbalimbali katika kusaidia kujenga na kuimarisha utalii katika maporomoko hayo (Kalambo Falls). Wakala wa Misitu Taznania (TFS) wamesaidia upatikanaji wa kiasi cha fedha (Tsh. Mil. 10) ambazo zitasaidia kufungua baadhi ya mitaa katika eneo liliopimwa na shughuli zingine zitakazohitajika katika eneo hilo. 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya anawaomba wadau wote wa utalii nchini ikiwemo Serikali, Mashirika binafsi, Wawekezaji na Wahisani mbalimbali kuwa na jicho la pamoja katika kuona Maporomoko ya Mto Kalambo (Kalambo Falls) yanachukuliwa umuhimu wa pekee wa kuendelezwa na kutangazwa kwa nguvu kwani ni miongoni mwa kivutio kikubwa cha utalii nchini na barani Afrika kwa ujumla.
Maporomoko ya Mto Kalambo (Kalambo Falls) yenye urefu wa mita 235 yapo Mkoani Rukwa katika Wilaya ya Kalambo na ni sehemu ya mpaka kati ya Nchi ya Tanzania na Zambia. Nchi ya Zambia imekuwa ikitumia fursa ya mpaka huo kuendeleza eneo lao la mpakani na kuitangaza Kalambo Falls jambo ambalo likiachwa kwa muda mrefu bila Tanzania kuchukua hatua kama hiyo itapelekea dunia kubaki na picha isiyo sahihi kuwa maporomoko hayo yapo nchini Zambia wakati sehemu kubwa ipo Tanzania na hata muonekano mzuri unapatikana kutokea Tanzania na maji ya mto huo yanatokea Tanzania. 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akiangalia ramani ya viwanja vilivyopimwa katika kijiji cha Kapozwa kwa ajili ya kuendeleza utalii katika kijiji hicho cha mpakani na nchi ya Zambia yalipo maporomoko ya mto Kalambo (Kalambo Falls). Mkuu huyo wa Mkoa alikabidhiwa ramani hiyo na Kaimu Afisa Ardhi na Maliasili Wilaya ya Kalambo Ndugu Makwasa Biswalo.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya na Meneja wa Misitu Wilaya ya Sumbwanga na Kalambo Ndugu Martin Hamis wakipanda mti wa kumbukumbu katika eneo lililopimwa la kijiji cha kapozwa kwa ajili ya kuendeleza utalii wa maporomoko ya mto Kalambo (Kalambo Falls).
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya na wapimaji wa ardhi kutoka chuo cha Ardhi Morogoro waliokuwa wakishirikiana na wataalamu wa ardhi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo kupima ardhi ya kijiji cha Kapozwa kwa ajili ya kuiendeleza kiutalii wakiangalia Maporomoko ya Moto Kalambo (Kalambo Falls).
Sehemu ambayo ni nusu ya maporomoko ya mto Kalambo (Kalambo Falls). 
Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies Pangisa akiangalia bonde la maporomoko ya mto Kalambo (Kalambo Falls).
Sehemu ya jitihada za wananchi wa kijiji cha Kapozwa ambao wamefyatua matofali kwa ajili kujenga kituo cha utalii kwa ajili ya maporomoko ya mto Kalambo (Kalambo Falls).
Sehemu ya mchoro kwa ajili ya kujenga kituo na geti la utalii katika maporomoko ya mto Kalambo (Kalambo Falls). Jitihada hizi zimefanywa na uongozi wa Mkoa wa Rukwa ukiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Eng. Stella Manyanya.
Vijana wa nchi jirani ya Zambia wakiwa wanapunga upepo kandokando ya maporomoko ya mto Kalambo. Upande wa nyuma zinaonekana ngazi maalum ambazo ni sehemu ya miundombinu iliyojengwa na Serikali ya Zambia kuwavutia watalii katika eneo hilo. Serikali ya Tanzania ina changamoto kubwa ya kuhakikisha eneo hilo muhimu la utalii linaendelezwa ili kulijengea umiliki halali tofauti na ilivyo hivi sasa ambapo inaonekana limetelekezwa kwa muda mrefu.
Sehemu ya bonde ambalo ni maangukio ya maji ya mto Kalambo yanapotengenezwa maporomoko (Kalambo Falls).
(Na Hamza Temba – Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)

LAPF YATOA MIKOPO YA ELIMU KWA WANACHAMA WAKE

 Afisa matekelezo wa LAPF  Bi Christina Mbaga akitoa maelezo juu ya Mkopo wa Elimu unaotolewa kwa wanachama wa LAPF. Mkopo huu umekuwa kivutio kikubwa kwa wanachama na wasio wanachama. 
 Afisa Mifumo ya Computer Bi. hilda Kato akifafanua jambo kwa wanachama waliotembelea bandani hapo. 
Maafisa wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF walioshiriki katika maonyesho ya Nane Nane Nzuguni Mjini Dodoma wakiwa katika picha ya pamoja

MfukowaPensheniwa LAPF  umeanza kutoa Mikopo ya Elimu ya Juu kwa wanachama wake kwalengo la kuwasaidia wanachama wanaotaka kujiendeleza kielimu kwa kuwalipia ada ya masomo. LAPF inajua kuna baadhi ya wanachama walitamani kujiendeleza kielimu lakini kwa namna moja au nyingine wameshindwa kutokana na gharama za masomo hayo hivyo LAPF itawawezesha kutimiza malengo yao.  LAPF ndio Mfuko Pekee wa Pensheni nchini unaotoa mkopo wa Elimu kwa wanachama wake. 
LAPF, MCHANGO ULE ULE MAFAO ZAIDI.

Tuesday, August 5, 2014

KAMPUNI YA VINYWAJI BARIDI YA SBC YAZINDUA MIRINDA MPYA AINA YA GREEN APPLE

Kinywaji cha mirinda Green Apple kikiwa katika chupa.
Maofisa wa Kampuni hiyo Godlisten Mende (kulia), na Omari Madaya wakionesha kinywaji hicho kwa waandishi wa habari.
Meneja Mauzo wa SBC, Godlisten Mende (kulia), akionesha kinywaji hicho kwa waandishi wa habari. Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
Meneja Mauzo wa Kanda, Omar Madaya (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari wakati wa hafla ya kuzindua kinywaji hicho iliyofanyika Dar es Salaam jana.
Meneja Mauzo wa SBC, Godlisten Mende (kulia), akizungumza katika mkutano huo.
Wanahabari wakionja kinywaji hicho.
Mwanahabari huyu kama anasema “jamani mirinda hii ni tamu”.

Wanahabari wakichangamkia kinywaji hicho.
Wanahabari wakichukua taarifa kutoka kwa maofisa wa SBC.
Mmoja wa maofisa wa SBC (kushoto), akiwaelekeza jambo wenzake.