Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya
Posta Tanzania (TPB), Moses Manyata (wa kwanza kushoto)akizungumza
katika mkutano na waandishi wa habari kuhusiana na hatua ya benki hiyo
kuisaidia timu ya waandishi wa habari za michezo nchini Taswa SC. Benki
hiyo ilikabidhi hundi ya Sh milioni 2 na pia itasaidia jezi kwa timu ya
mpira wa miguu na netiboli. Kwa kwanza kushoto ni Afisa Mawasiliano wa
TPB, Chichi Banda na wa kwanza kulia ni Taswa SC, Majuto Omary.
Kaimu
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Moses Manyata (wa
kwanza kushoto)akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari
kuhusiana na hatua ya benki hiyo kuisaidia timu ya waandishi wa habari
za michezo nchini Taswa SC. Benki hiyo ilikabidhi hundi ya Sh milioni 2
na pia itasaidia jezi kwa timu ya mpira wa miguu na netiboli
……………………………………………………………………………….
Benki
ya Posta Tanzania (TPB) imeidhamini klabu ya waandishi wa habari za
michezo nchini (Taswa SC), kufuatia juhudi zake za kuhamasisha na
kuendeleza michezo nchini.
Benki hiyo imeisaidia klabu hiyo fedha taslims
sh. Milioni 2 na inatarajia kuwapa jezi seti moja moja kwa timu ya
mpira wa miguu na mpira wa pete (netiboli) ikiwa ni kuthamini mchango
wao Taswa SC katika sekta ya michezo nchini.
Kaimu
Afisa Mteandaji Mkuu wa TPB, Moses Manyatta alisema kuwa wanafuraha
kubwa kusikia kuwa waandishi wa habari za michezo wameamua kufanyakazi
kwa vitendo kwa kuanzisha timu ya mpira wa miguu ambayo kwa sasa ina
miaka zaidi ya 20 na timu ya mpira wa pete (netiboli) ambayo ina mwaka
mmoja na nusu.
“Tumefarijika
kutokana na ukweli kuwa mbali ya kuandika, mmeamua kufanya michezo kwa
vitendo na kuwa mfano wa kuigwa, TPB ipo bega kwa bega nanyi na
tutaendelea kushirikiana katika sekta mbali mbali tofauti na michezo,”
alisema Manyatta.
Alisema
kuwa TPB ni benki halisi ya Kitanzania yenye kutoa huduma bora kwa
wateja wake na kwa sasa imeingia katika sekta ya michezo ambapo kwa sasa
inashirikiana na timu kongwe nchini, Yanga na Simba katika zoezi la
kuandikisha upya wanachama na mashabiki wa timu hizo.
Mwenyekiti
wa Taswa SC, Majuto Omary aliipongeza TPB kwa kutoa msaada huo na
kuahidi kuwa wadau wakubwa wa benki hiyo katika shughuli zake
mbalimabli.
Majuto
alisema kuwa wameomba udhamini kwa makampuni mengi kutokana na ukweli
kuwa timu yao inachangamoto nyingi pamoja na kuwa na mafanikio makubwa.
“Tunawapa
pongezi kubwa sana TPB, mmeonyesha kuwa ni benki halisi ya Kitanzania
yenye kutoa huduma bora hapa nchini, Taswa SC ipo bega kwa bega nanyi
katika kuendeleza gurudumu la maendeleo la nchi hii,” alisema Majuto.
Majuto
pia aliwaomba wanachama wa timu ya Taswa SC kuwa mstari wambele katika
shughuli za TPB kwani wameonyesha kuwajali katika shughuli za kila siku.
No comments:
Post a Comment