Zipo
jitihada kadhaa zilizokwishafanywa na uongozi wa Mkoa wa Rukwa
ukiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Eng. Stella Manyanya katika kuhakikisha
eneo la maporomoko hayo linaimarishwa na kuwa kivutio kikubwa cha utalii
na chanzo cha mapato kwa halmashauri husika na taifa kwa ujumla.
Jitihada
hizo ni pamoja kuwahamasisha wananchi wa kijiji cha Kapozwa na wadau
wengine katika kutambua umuhimu wa maporomoko hayo ambapo mpaka hivi
sasa wananchi hao wameshashiriki kufyatua matofali kwa ajili ya kujenga
kituo cha utalii katika eneo hilo.
Jitihada
zingine ni zile za kupima viwanja na kuandaa michoro katika eneo hilo
ambapo ramani imeshaidhinishwa na tathmini ya kuwafidia wananchi maeneo
yao imeshafanyika.
Aidha
zimekuwepo jitihada za kutafuta fedha kutoka Serikalini na kwa wahisani
mbalimbali katika kusaidia kujenga na kuimarisha utalii katika
maporomoko hayo (Kalambo Falls). Wakala wa Misitu Taznania (TFS)
wamesaidia upatikanaji wa kiasi cha fedha (Tsh. Mil. 10) ambazo
zitasaidia kufungua baadhi ya mitaa katika eneo liliopimwa na shughuli
zingine zitakazohitajika katika eneo hilo.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya anawaomba wadau wote wa utalii
nchini ikiwemo Serikali, Mashirika binafsi, Wawekezaji na Wahisani
mbalimbali kuwa na jicho la pamoja katika kuona Maporomoko ya Mto
Kalambo (Kalambo Falls) yanachukuliwa umuhimu wa pekee wa kuendelezwa na
kutangazwa kwa nguvu kwani ni miongoni mwa kivutio kikubwa cha utalii
nchini na barani Afrika kwa ujumla.
Maporomoko
ya Mto Kalambo (Kalambo Falls) yenye urefu wa mita 235 yapo Mkoani
Rukwa katika Wilaya ya Kalambo na ni sehemu ya mpaka kati ya Nchi ya
Tanzania na Zambia. Nchi ya Zambia imekuwa ikitumia fursa ya mpaka huo
kuendeleza eneo lao la mpakani na kuitangaza Kalambo Falls jambo ambalo
likiachwa kwa muda mrefu bila Tanzania kuchukua hatua kama hiyo
itapelekea dunia kubaki na picha isiyo sahihi kuwa maporomoko hayo yapo
nchini Zambia wakati sehemu kubwa ipo Tanzania na hata muonekano mzuri
unapatikana kutokea Tanzania na maji ya mto huo yanatokea Tanzania.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akiangalia ramani ya viwanja
vilivyopimwa katika kijiji cha Kapozwa kwa ajili ya kuendeleza utalii
katika kijiji hicho cha mpakani na nchi ya Zambia yalipo maporomoko ya
mto Kalambo (Kalambo Falls). Mkuu huyo wa Mkoa alikabidhiwa ramani hiyo
na Kaimu Afisa Ardhi na Maliasili Wilaya ya Kalambo Ndugu Makwasa Biswalo.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya na Meneja wa Misitu Wilaya ya
Sumbwanga na Kalambo Ndugu Martin Hamis wakipanda mti wa kumbukumbu
katika eneo lililopimwa la kijiji cha kapozwa kwa ajili ya kuendeleza
utalii wa maporomoko ya mto Kalambo (Kalambo Falls).
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya na wapimaji wa ardhi kutoka chuo
cha Ardhi Morogoro waliokuwa wakishirikiana na wataalamu wa ardhi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo kupima ardhi ya kijiji cha Kapozwa kwa
ajili ya kuiendeleza kiutalii wakiangalia Maporomoko ya Moto Kalambo
(Kalambo Falls).
Sehemu ambayo ni nusu ya maporomoko ya mto Kalambo (Kalambo Falls).
Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies Pangisa akiangalia bonde la maporomoko ya mto Kalambo (Kalambo Falls).
Sehemu
ya jitihada za wananchi wa kijiji cha Kapozwa ambao wamefyatua matofali
kwa ajili kujenga kituo cha utalii kwa ajili ya maporomoko ya mto
Kalambo (Kalambo Falls).
Sehemu
ya mchoro kwa ajili ya kujenga kituo na geti la utalii katika
maporomoko ya mto Kalambo (Kalambo Falls). Jitihada hizi zimefanywa na
uongozi wa Mkoa wa Rukwa ukiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Eng. Stella
Manyanya.
Vijana
wa nchi jirani ya Zambia wakiwa wanapunga upepo kandokando ya
maporomoko ya mto Kalambo. Upande wa nyuma zinaonekana ngazi maalum
ambazo ni sehemu ya miundombinu iliyojengwa na Serikali ya Zambia
kuwavutia watalii katika eneo hilo. Serikali ya Tanzania ina changamoto
kubwa ya kuhakikisha eneo hilo muhimu la utalii linaendelezwa ili
kulijengea umiliki halali tofauti na ilivyo hivi sasa ambapo inaonekana
limetelekezwa kwa muda mrefu.
Sehemu ya bonde ambalo ni maangukio ya maji ya mto Kalambo yanapotengenezwa maporomoko (Kalambo Falls).
(Na Hamza Temba – Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)
No comments:
Post a Comment