Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Rais Goodluck Jonathan wakati
muda mfupi kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za
Bara la Afrika uliofanyika jijini Washington DC chini ya uenyekiti wa
Rais Barack Obama wa Marekani Agosti 6, 2014
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akijadiliana jambo na Rais Barak Obama wa
Marekani kwenye ukumbi wa Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la
Afrika uliofanyika jijini Washington DC chini ya uenyekiti wa Rais Obama
wa Marekani Agosti 6, 2014
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa
kimataifa Mhe Bernard Membe na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe.
Librerata Mulamula kwenye Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la
Afrika uliofanyika jijini Washington DC chini ya uenyekiti wa Rais
Barack Obama wa Marekani Agosti 6, 2014
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akifurahia jambo na Rais Barak Obama wa Marekani
kwenye ukumbi wa Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika
uliofanyika jijini Washington DC chini ya uenyekiti wa Rais Obama wa
Marekani Agosti 6, 2014
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akijadiliana jambo na Rais Barak Obama wa
Marekani kwenye ukumbi wa Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la
Afrika uliofanyika jijini Washington DC chini ya uenyekiti wa Rais Obama
wa Marekani Agosti 6, 2014
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akijadiliana jambo na Rais Barak Obama wa
Marekani kwenye ukumbi wa Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la
Afrika uliofanyika jijini Washington DC chini ya uenyekiti wa Rais Obama
wa Marekani Agosti 6, 2014
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mwenyekiti
wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU), Mhe. Dkt. Nkosazana Dlamini-Zum
wakimsikiliza Rais Barak Obama wa Marekani wakati akiongoza Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika uliofanyika jijini Washington DC Agosti 6, 2014
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na viongozi wengine wa Afrika wakipata
picha ya kumbukumbu na mwenyeji wao Rais Barak Obama wa Marekani wakati
wa Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika uliofanyika
jijini Washington DC chini ya uenyekiti wa Rais Obama wa Marekani
Agosti 6, 2014
Viongozi wa Afrika
wakisalimiana kwa furaha baada ya kupata picha ya pamoja wakati wa
Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika uliofanyika jijini
Washington DC chini ya uenyekiti wa Rais Obama wa Marekani Agosti 6,
2014
……………………………………………………………………………….
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa moja ya sababu
kubwa zinazokwamisha maendeleo makubwa zaidi na ya haraka zaidi ya
Afrika ni uzalishaji mdogo na matumizi ya chini mno ya umeme.
Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa hali hiyo inaeleza jinsi
ongezeko la uzalishaji na matumizi ya umeme linavyoweza kuharakisha
maendeleo ya Afrika na kuleta manufaa ya dhahiri kwa kila familia na kwa
kila Mwafrika.
Rais Kikwete ameyasema hayo jana, Jumatano, Agosti 6, 2014,
wakati alipozungumza kwenye Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara
la Afrika uliofanyika chini ya uenyekiti wa Rais Barack Obama, ambaye ni
mwenyeji wa Mkutano huo.
Rais Kikwete amewaambia wakuu wa nchi hizo kwenye Ukumbi wa
Mikutano wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani kuwa ni dhahiri kuwa bila
ongezeko kubwa la uzalishaji na matumizi ya umeme Bara la Afrika
halitatoka kwenye uduni.
Rais amesema kuwa kwa mujibu wa Ripoti ya Kanda ya Shirika la
Umoja wa Mataifa Mazingira (UNEP) “Efficient Lighting in Sub Saharan
African Countries” matumizi ya umeme katika Bara zima la Afrika ni
asilimia 31 tu na hivyo kulifanya Bara la Afrika kutumia asilimia tatu
tu ya umeme wote duniani.
Rais Kikwete amesema kuwa ili kuelewa udogo wa matumizi ya umeme
ya Bara la Afrika ni kuangalia matumizi ya nishani hiyo kwa kila mkazi
wa Bara hilo na yule wa Marekani. Amesema kuwa wakati kila raia wa
Marekani anatumia kilowati 13, 246 katika Afrika wastani ni kilowati
440.
Ameongeza Rais Kikwete: “Ukiondoa Afrika Kusini, matumizi ya
umeme kwa kila raia wa Afrika yanateremka na kufikia kilowati 160 tu.”
Amefafanua Rais Kikwete: “Uzalishaji wa jumla wa umeme wa Bara
la Afrika ni gigawati 63 ambazo ni sawa na umeme unaozalishwa na nchi
moja tu ya Ulaya – Hispania. Ukiondoa Afrika Kusini, nchi zinazobakia wa
Afrika zina uwezo wa kuzalisha gigawati 28 tu, kiasi ambacho
kinazalishwa na nchi moja tu ya Marekani Kusini ya Argentina.”
Rais Kikwete ambaye alikuwa anafafanua jinsi utoaji huduma ulio
dhahiri unavyoweza kunufaisha wananchi na kujenga mazingira ya taasisi
zisizokuwa za kiserikali kushamiri, ametaja mambo mengine ya msingi
ambayo ni lazima yawepo ili wananchi waweze kunufaika ikiwemo elimu,
ushamiri wa sekta binafsi, sera sahihi za kiuchumi, uwekezaji katika
ujenzi wa miundombinu na uboreshaji wa kilimo.
Pia Rais Kikwete ametaja mambo mengine muhimu yanayoweza
kusaidia kuboresha maisha ya wananchi kuwa ni uendelezaji na matumizi ya
teknolojia ya habari na mawasiliano pamoja na kulea na kukuza
demokrasia, utawala bora na utawala wa sheria.
Rais Kikwete ambaye yuko katika ziara ya kikazi ya siku tisa
katika Marekani, anaondoka mjini Washington, D.C., leo kwenda Houston
ambako atafungua na kushiriki katika mkutano wa uwekezaji katika uchumi
wa Tanzania.
Mwisho!
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
07 Agosti, 2014
No comments:
Post a Comment