Pages

KAPIPI TV

Tuesday, April 15, 2014

BABU NA MJUKUU WAKE WAFANIKIWA KUINGIA HATUA YA TATU KATIKA SHINDANO LA TANZANIA MOVIE TALENTS

Mmoja wa washiriki wa shindano la Tanzania Movie Talents akihojiwa na Msanii Joti mara baada ya kufanikiwa kuingia hatua ya tatu hapo kesho huku mjukuu wake pia akifanikiwa kuingia hatua hiyo pia.
Washiriki wa Shindano la kusaka vipaji vya Uigizaji Tanzania lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents wakiwa kwenye mazoezi wakati walipokabidhiwa muswada (script) kwaajili ya kuifanyia mazoezi na kwenda kuonyesha uwezo wao kwa majaji.
Msanii wa Vichekesho Joti akihojiana na Mmoja wa washiriki wa shindano la Tanzania Movie Talents mara baada ya kutoka kwa majaji, shindano limeingia hatua ya pili leo kwa kuchagua washiriki 30 ambao watatafutwa washiriki 15 bora hapo kesho.
Mshiriki namba 00554 akihojiwa na msanii Joti mara baada ya kufanikiwa kuingia hatua ya tatu hapo kesho ambapo watapatikana washindi kumi na tano bora na hatimaye kupata washindi watatu bora wa kanda ya kati ambapo kila mmoja atajinyakulia kitita cha shilingi laki tano za kitanzania
 
Baadhi ya washiriki wa shindano la Tanzania Movie Talents wakibadilishana mawazo mara baada ya kupatikana kwa washiriki 30 ambao wataendelea na mashindano hapo kesho kwaajili ya kupata washiriki 15 bora.
 Mmoja wa washiriki wa shindano la Tanzania Movie Talents akiwa amenyongonyea mara baada ya safari yake katika mashindano kuishia leo kutokana na kukosa nafasi ya kuingia katika hatua ya tatu hapo kesho.Picha na Josephat Lukaza wa Proin Promotions – Dodoma
Washiriki wa Shindano la Tanzania Movie Talents ambao ni babu na mjukuu wake kiuhalisia wakipongezana mara baada ya kufanikiwa kuingia hatua ya tatu ya kutafuta washiriki 15 bora na hatimaye kupatikana washindi watatu bora wa kanda ya kati ambapo kila mmoja ataondoka na kitita cha shilingi laki tano za kitanzania.
……………………………………………………………………………..
 
Na Josephat Lukaza wa Proin Promotions Limited – Dodoma

Leo Shindano la Tanzania Movie Talents limeingia ya hatua ya pili ya mchujo ambapo washiriki 30 wameweza kupatikana kwaajili ya kuendelea na shindano hilo hapo kesho ambapo washiriki 15 ndio watachukuliwa kwaajili ya kuendelea na mashindano hayo na hatimaye kupatika washindi watatu bora ambao watawakilisha kanda ya Kati na kwa kila mshindi mmoja kuibuka na kitita cha shilingi laki tano (500,000/=).

Mpaka sasa washiriki 30 wameshapatikana kwa kanda ya Kati na hatimaye kesho washindi watatu watapatikana na kuiwakilisha kanda ya Kati katika fainali kubwa itakayofanyika Mkoani Dar Es Salaam na hatimaye mshindi katika fainali hiyo kujinyakulia kitita cha Shilingi Milioni 50 za kitanzania (50,000,000/=)

Katika Washindi 30 waliopatikana leo, washiriki wawili wameweza kuonyesha vipaji vyao huku washiriki hao wakiwa ni ndugu kabisa, washiriki hao ni babu na mjukuu wake wa kike ambao wameweza kufanikiwa kuingia hatua ya tatu kesho ambapo washindi wa Kanda ya Kati watapatikana.

Shindano la Tanzania Movie Talents linatarajiwa kumalizika kesho Kanda ya Kati Mkoani Dodoma na hatimaye kuhamia Kanda ya Juu Kusini ambapo usaili utafanyika Mkoani Mbeya na usaili wa Kanda ya Juu Kusini utaanza tarehe 19 April 2014 saa 1 asubuhi na wakazi wa Kanda ya Juu Kusini wanaombwa kujitokeza kwa wingi ili kuweza kuonyesha vipaji vyao na kuweza kuitumia fursa hii, Vilevile fomu za usaili zitapatikana Siku hiyohiyo ya usaili na fomu hizo hazina gharama yoyote ile.

BALOZI SEFUE AONESHA HATI YA MUUNGANO

MAELFU YA ABIRIA WAKWAMA UBUNGO


mabasi_28773.jpg
Dar es Salaam.

 Uharibifu wa barabara uliotokana na mvua zinazoendelea kunyesha, umeendelea kuwatesa wakazi wa Dar es Salaam na mikoa mbalimbali nchini hasa baada ya mabasi ya mikoani kuzuiwa kufanya safari zake jana.

Amri ya kuzuia mabasi hayo ilitolewa jana ikiagiza mabasi yote yasiondoke katika Kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo hadi itakapotangazwa vinginevyo, kutokana na uharibifu wa Barabara za Kilwa, Morogoro na Bagamoyo ambako madaraja yamevunjika.

Dereva wa Basi la Adventure liendalo Kigoma, Joseph Luciano alisema walitangaziwa na Sumatra na trafiki kuwa wasubiri mpaka hapo watakapojulishwa kuondoka.

"Hatuwezi kuondoka mpaka Serikali itakapotangaza ili kuepuka faini ambayo wenzetu, wale wanaopakia nje, wametozwa," aliongeza huku ikielezwa kuwa baadhi ya mabasi yalitozwa faini kwa kukiuka amri hiyo.

Abiria anayesafiri kwenda Kibondo, Kigoma, Lydia Lutakinikwa alisema: "Nilikuja kuchukua mzigo wa duka langu tangu Ijumaa na nimekuwa nikilala gesti. Nimeishiwa hela hivyo nalazimika kuendelea kuwapo kwenye hili basi kwa kuwa sina tena pesa ya kwenda kulipia malazi."

Kondakta wa Basi la Taqwa liendalo Nairobi, Yahaya Maulid alisema wameruhusu kubadilishwa tiketi za abiria wao, kama walivyoelekezwa na mamlaka husika ili kutoa nafasi kwao kujipanga upya.

Mkuu wa Usalama Barabarani Ubungo, Inspekta wa Polisi, Yusuf Kamutta alisema zaidi ya mabasi 400 yameathiriwa na uamuzi huo... "Tumezuia mawakala wasitoe tiketi mpya kwa sababu abiria wa leo (jana) ndiyo wanaotarajiwa kusafiri kesho, hivyo wanaweza kuuza tiketi za kuanzia keshokutwa."

Msururu wa magari Pwani
Kutokana na kuharibika kwa baadhi ya madaraja katika Mkoa wa Pwani, magari yaliyokuwa yakisafiri kutoka maeneo mbalimbali yalikwama katika maeneo tofauti. Baadhi yalikwama Visiga na mengine Mlandizi jirani na Kituo cha Polisi katika misururu mirefu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Ulrich Matei aliwataka wamiliki wa magari makubwa ya mizigo wanaotumia barabara hiyo kusitisha safari zao kwa kipindi hiki hadi hapo hali itakapotengamaa.

Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Pwani na uongozi wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) ililazimika kuweka kambi kwa siku nzima eneo la Mlandizi jirani na daraja la Ruvu kusimamia shughuli ya ukarabati wa daraja dogo lililokuwa na hitilafu.

Meneja wa Tanroads Mkoa wa Pwani, Tumaini Sarakikya alisema hadi jana mchana magari yalikuwa yameanza kupita upande mmoja, lakini baadaye jioni yangeanza kupita bila wasiwasi

Waliokufa Dar wafikia 13
Mafuriko yaliyotokana na mvua hizo yamesababisha vifo vya watu 13 mkoani Dar es Salaam hadi jana, huku Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) pekee ikipokea maiti tisa.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick alisema maiti mbili zilipatikana Wilaya ya Temeke na nyingine moja ilikutwa eneo la Jangwani, Ilala na miili hiyo imehifadhiwa MNH na Hospitali ya Temeke.
Alisema jitihada zinaendelea kubaini iwapo kuna miili zaidi katika mito na mabonde ambayo yalikumbwa na mafuriko hayo na ameomba mwananchi kutoa ushirikiano.

Ofisa Uhusiano wa MNH, Aminiel Aligaesha alisema hadi jana hospitali hiyo ilikuwa imepokea maiti tisa zote zikiwa za wanaume na kati ya hizo, mbili zimetambuliwa na ndugu zao.

Kwa upande mwingine, Kamanda wa Upelelezi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Mark Njela alisema maiti moja ya mwanamume ilikutwa jana kwenye Mto wa Mabibo nyuma ya Kampuni ya Ami.
Imeandikwa na Sanjito Msafiri (Pwani), Pamela Chilongola, Ibrahim Yamola, Joseph Zablon (Dar).

Monday, April 14, 2014

ZANA ZA WAVUVI ZILIZOIBWA NA KUPELEKWA CONGO ZAREJESHWA KIGOMA

Na Magreth Magosso,Kigoma

IMEFAHAMIKA kuwa,baadhi ya mitumbwi inayoibwa katika Ziwa Tanganyika mkoani hapa imekuwa ikitumika kwenye kazi za doria katika mto Lukoga mashariki ya nchi ya Congo-DRC.

Kauli hiyo imekuja baada ya baadhi ya mashine 2,mitumbwi 2 sanjari na karabai kumi za wavuvi  kurudishwa kwa wahanga wa uvuvi kigoma ,kufuatia kamati ya wajumbe maalum kufuatilia mchakato wa kuzipata zana 18 ambazo ziliibwa machi,3,2014 sambamba na kutekwa kwa mvuvi moja katika ziwa hilo.

Ally Mziya ni mmoja wa waliozipata zana hizo alisema  wahalifu wanaoiba zana za uvuvi wanamahusiano ya karibu na baadhi ya askari jeshi wa wilaya ya Kalemi ,hali inayochangia kusuasua kwa zana 16 kurudishwa kigoma,kutokana na sheria ya nchi hiyo ,huku akiomba serikali  zote mbili zishirikiane kwa dhati ili kuondoa changamoto hiyo.
 
Akijibu hilo Ubalozi mdogo wa DRC-Congo Ricky Molema alisema kamati yao ya ulinzi wilaya ya kalemi imebaini kundi hilo la uhalifu  wa ziwani na wapo katika mchakato wa kuwabana waachane na kasumba hiyo, ili kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizo,huku akidai si kweli wanatumia zana za wizi za kigoma katika kufanikisha doria zao.
 
Akikabidhi zana hizo kwa baadhi ya wavuvi Mkuu wa wilayani kigoma Ramadhan Maneno alidai jumatatu atakuwa na mkutano na wadau wa uvuvi ili kutambua raia wanaoishi kinyume na sheria ili warudishwe kwao kwa lengo la kupunguza mtandao wa kihalifu unaoathiri uchumi wa wilaya ya kigoma na Uvinza.

Naye mgeni rasmi katika makabidhiano hayo,Mkuu wa MKoa huu Lt.Mstaafu  Issa Machibya alisema wavuvi wawe sehemu ya polisi jamii ili kubaini viashiria vya uhalifu dhidi yao,hali itakayokomesha unafiki miongoni mwao na kuwataka wakuu wa wilaya ya Uvinza na Kigoma wabaini wahamiaji haramu ili kuwadhibiti na waishi kwa taratibu na sheria za idara ya uhamiaji kwa lengo la kukomesha uhalifu mkoani hapo.

Ofisa upelelezi wa Mkoa  Dismas Kisusi na Mwenyekiti wa wavuvi  Ramadhan Kanyongo kwa nyakati tofauti walisema vitendo vya uhalifu ziwani vilianza kushamiri katika ukanda wa mwambao wa ziwa Tanganyika kuanzia mwaka 2011 hadi 2014 hali inayochangiwa na hali halisi ya mipaka ya mkoa huo ,

Sanjari na  bajeti finyu ya ulinzi katika ziwa hilo,lakini leo(jana) Lt.Machibya amedai dolia zipo za kudumu kwa siku 365 na kusisitiza wahalifu watakiona na kukiri zana zilizorudishwa ni chache kulingana na zilizochukuliwa.

SAMSUNG YAZINDUA SIMU MPYA GALAXY S5 IKILENGA MAMBO MUHIMU YA WATEJA WAKE


heart rate
Meneja wa Simu za mkononi wa Samsung Tanzania , Bw. Silvester Manyara, akiwaonyesha waandishi wa habari jinsi simu mpya inavyopima mapigo yake ya moyo. Pembeni yake ni Bw. Kishor Kumar, Meneja wa kitengo cha simu na mambo ya teknohama wa Samsung Tanzania.
samsung team
Team ya Samsung Tanznia Bw. Silvester Manyara, Bw. Jang na Bw. Kishor Kumar kwenye picha ya pamoja wakionyesha Simu mpya ya Galaxy S% iliyozinduliwa rasmi hapa Dar es Salaam.
waandishi wa hbr pamoja na wananchi
Waandishi wa habari pamoja na wateja wakishuhudia uzinduzi wa simu mpya ya Samsung Galaxy S5.

“Teknolojia ya kisasa duniani, camera iliyobora zaidi sokoni, na unmatched support for fitness na kusaidia kufanya maisha ya kila siku ya wateja wa Samsung kuwa na maana zaidi”

Kampuni inayoongoza kwa kutengeneza vifaa vya umeme ya Samsung imeungana na nchi nyingine duniani kuzindua simu ya mkononi mpya ya Galaxy inayojulikana kama Galaxy S5 ; simu ya kisasa na bora zaidi ya mkononi ilitengenezwa kwa matakwa ya mtumiaji

Simu mpya ya Galaxy S5,nyepesi, inayofanya kazi kwa haraka na imezinduliwa rasmi siku ya leo tarehe 11/4/2014 kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Dar es salaam. Simu mpya ya Galaxy S5 inamrahisishia vitu vingi mtumiaji na kumpa ujuzi kupitia features maalum anavyoweza kutumia katika shughuli zake za kila siku

Akiongea na waandishi wa habari Meneja wa kitengo cha simu na teknohama wa vifaa kampuni ya Samsung Tanzania Bwn.Kishor Kumar alikua na haya ya kusema “Kupitia Galaxy S5,Samsung imevuka matarajio yetu kwa kutuletea bidhaa inayolenga zaidi matakwa ya wateja wake.” Bw. Kishor Kumar aliendelea kwa kusema “ Wateja wanataka bidhaa na simu ambazo zitawarahisishia kwa njia moja au nyingine maisha yao ya kila siku. Simu ya Galaxy S5 imetengenezwa na ubunifu wa kipekee wa hali ya juu ikiwa na vigezo vyote zinazotegemewa na watu”

Bw.Kishor alienda mbali zaidi kwa kuongeza kua simu ya  Galaxy S5 imeboreshwa maradufu; rahisi kwenye utumiaji na imuongezwa  ubora wa kamerayake pamoja na vipimo vya kulinda usalama wa simu (security feature).

Galaxy S5 ina umbile jembamba la kuvutia, kioo kikubwa cha simu, fremu ya metalic, chaguo kubwa la rangi za kisasa, finishing choices ambazo zinaonyesha muundo mpya wa simu duniani. Simu hii inajumuisha kamera ya kisasa,muunganiko wa kasi wa mtandao, vifaa vya kuangalia ubora wa hali yako and vifaa vilivyoboreshwa vya ulinzi (protection and security feature) ambavyo vinakufanya uwe na mawasiliano in style.

Sunday, April 13, 2014

MAKAMU WA RAIS AFANYA ZIARA YA KUKAGUA ATHALI ZA MAFURIKO DAR NA MAENDELEO YA UJENZI WA DARAJA LA MPIJI.

01
2Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na baadhi ya viongozi kuelekea eneo la tukio kukagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Mpiji lililokatika kutokana na Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini. Picha na OMR 03Nguzo za umeme zikiwa zimeinama baada ya kuzidiwa nguvu na maji hayo yaliyobomoa daraja. Picha na OMR
04Malori yakimwaga vifusi vya Mawe kwenye daraja hilo. Picha na OMR 05Malori yakimwaga vifusi vya Mawe kwenye daraja hilo. Picha na OMR 06Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa maelekezo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Eng. Mussa Ibrahim Iombe, wakati alipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Mpiji lililokatika kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini.Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mecky Sadick.  Picha na OMR 07.Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuhitimisha ziara yake hiyo, katika eneo la Daraja la Mpiji, linalounganisha Bagamoyo na Dar es Salaam, leo Aprili 13, 2014. Picha na OMR 08 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiondoka eneo la tukio Daraja la Mpiji baada ya kumaliza ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja hilo lililokatika kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini. Picha na OMR 09Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiondoka eneo la tukio Daraja la Mpiji baada ya kumaliza ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja hilo lililokatika kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini. Picha na OMR

CAG LUDOVIK UTOUH AONYA BAHASHA KIGOMA!!!

Na Magreth Magosso,Kigoma

MKAGUZI  wa mahesabu wa kitaifa(CAG) Ludovik  Utouh amewataka Viongozi wa halmashauri za wilaya Mkoa wa Kigoma waache  kuwashawishi kwa bahasha za fedha watendaji wake, pindi wafanyapo ukaguzi wa mahesabu katika maeneo yao.

Akifafanua hilo kwenye mkutano na viongozi wa serikali za hapa, Utouh alisema  amepewa malalamiko toka kwa vijana wake kuwa,wanashawishiwa kwa takrima na bahasha ili kubatilisha uhalisia wa matumizi ya fedha za serikali katika miradi husika kwa lengo la kukwepa kupata hati chafu .

Aliwasihi wakurugenzi wachane na kasumba ya kuogopa wakaguzi wa mahesabu kwani wakaguzi ni chachu ya kuboresha mfumo wa utendaji kazi  wa mazoea na wafanye kazi kwa kufuata kanuni,taratibu za kifedha ili kuubadilisha maisha ya wananchi kupitia miradi husika.

“ imarisheni vitengo vya ukaguzi wa ndani na kamati za ukaguzi kwa lengo la kuunga mkono juhudi za serikali katika kubadilisha mfumo wa kimazoea na badala yake viongozi muwe wabunifu na wazalendo wananchi wanalaumu serikali lakini ukweli watendaji ni shida”alisema Utouh

Kwa upande wa naibu Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kasulu Bernad Balishinga alisema,halmashauri zinachangamoto za kufanya kazi kwa mazoea kutokana na wakuu wa idara na watumishi kufanya kazi kwa muda mrefu katika kituo kimoja hali inayochangia kuacha kufuata sheria,kanuni na taratibu za kazi.

Naye Mkuu wa wilaya ya Uvinza Hadija Nyembo akiri ubadhirifu wa fedha za miradi  za wananchi waishio katika kata na vijiji zinatafunwa na watendaji wa kata wakishirikiana na wenyeviti wa vijiji hali inayochangiwa na kutokuwa na watendaji maalum ili wakipotoka iwe rahisi kushtakiwa.

Aidha Mkuu wa wilaya Venance Mwamoto alimuomba mkaguzi huyo kuwa uwekwe utaratibu wa mkataba wa kuwashirikisha wananchi katika mchakato wa miradi ili waondokane na hulka ya miradi kuachiwa wachache na hatimaye miradi ya umma kujengwa chini ya kiwango .

Mkaguzi huyo alizitaka halmashauri ziwe na maboresho ya mfumo wa matumizi ya fedha IFMS-Epicor,lengo kuweka utunzaji sahihi na kumbukumbu juu ya matumizi ya fedha na kushauri watoe mafunzo kwa wahazina na wahazini ili wawe na viwango vya utunzaji fedha kwa kiwango cha kimataifa(IPSAS).

Saturday, April 12, 2014

"KIONGOZI WA KISIASA KUTOWANIA NAFASI YA UONGOZI KWENYE VYAMA VYA MSINGI NI KUMNYIMA HAKI YA KIMSINGI"-WAKASUVI

Viongozi ngazi ya juu ya Chama kikuu cha Ushirika wa Wakulima wa Tumbaku kanda ya Magharibi Wetcu wakiwa katika mkutano wa 21 wa mwaka 2014.
Wajumbe wa mkutano wa 21 wa mwaka 2014 wa WETCU ambapo kwa sehemu kubwa wajumbe hao waliangazia suala la changamoto mbalimbali zinazowakabili wakulima na namna wanavyoshindwa kupiga hatua licha ya kuwa wanapata malipo ya mauzo ya tumbaku kwa mfumo wa Dola za kimarekani.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tabora  Bw. Hassan  Wakasuvi ambaye pia ni mjumbe wa mkutano huo alisisita suala la kuangalia upya kanuni za uundwaji wa  vyama vya ushirika ambapo zinamnyima haki mkulima ambaye atahitaji kuwa kiongozi wa chama cha  ushirika wakati akiwa ni kiongozi wa chama chochote cha kisiasa.



KATIBU MKUU WA CCM,AENDELEA NA ZIARA YAKE MKOANI KIGOMA.

Katibu Mkuu wa CCM;Ndugu Kinana na Wananchi wakishiriki ujenzi wa Ghala la kuhifadhi mazao na mashine ya kusaga nafaka katika kijiji cha cha Kidahwe,Kigoma Vijijini.Ghala hilo  linalenga kusaidia katika kuhifadhi mazao ya wakulima na kijiji hicho baada ya kuvuna ili kusubiri soko na bei nzuri ya mazao kwa mfumo wa stakabadhi ghalani.Usimikaji wa mashine katika ghala hilo utawasaidia  pia wakulima kuchakata mazao yao (hasa mahindi na muhugo) na kuuza unga badala ya mahindi.Gharama za mradi huo ni shiliingi milioni 104,800,000/=.
Katibu wa NEC-CCM wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akishiriki ujenzi wa Ghala la kuhifadhi mazao na mashine ya kusaga nafaka katika kijiji cha cha Kidahwe,Kigoma Vijijini.Ghala hilo  linalenga kusaidia katika kuhifadhi mazao ya wakulima na kijiji hicho baada ya kuvuna ili kusubiri soko na bei nzuri ya mazao kwa mfumo wa stakabadhi ghalani.Usimikaji wa mashine katika ghala hilo utawasaidia  pia wakulima kuchakata mazao yao (hasa mahindi na muhugo) na kuuza unga badala ya mahindi.Gharama za mradi huo ni shiliingi milioni 104,800,000/=.
Katibu wa NEC-CCM wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (kulia) akifafanua jambo kwa Wananchi (hawapo pichani) walipokwenda kukagua kushiriki na kukagua ujenzi wa Ghala la kuhifadhi mazao na mashine ya kusaga nafaka katika kijiji cha cha Kidahwe,Kigoma Vijijini.
Baadhi ya Wazee wa kijiji cha Nkungwe wakifuatilia yaliyokuwa yanazungumwa na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana katika kijiji cha Nkungwe,kuhusiana na tatizo la ufumbuzi wa mradi wa maji.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na Wananchi wa kijiji cha Nkungwe kuhusiana na mradi wa maji unaojengwa,ambao kwa sasa umesimama kutokana na ukosefu wa fedha.
Ujenzi wa tanki hilo la maji kama lionekanavyo pichani.
Katibu Mkuu Ndugu Kinana akipata maelezo mafupi kuhusiana na ujenzi wa tanki la maji katika kijiji cha Nkungwe,Kigoma vijijini.
Ndugu Kinana (wa tatu kulia),akishiriki kufukia mabomba ya mradi wa maji katika kijiji cha Nkungwe,Kigima vijijini.Mradi huo ukikamilika unatarajiwa kusaidia vijiji zaidi ya 30.
Ndugu Kinana akiwasalimia wananchi mbalimbali (hawapo Pichani),wakati alipokuwa akiwasili katika kijiji cha Nkungwe kukagua mradi wa maji ambao umeshindwa kukamilika kutokana na ukosefu wa fedha. Kinana amewaahidi wananachi kulitafutia ufumbuzi suala hilo ili mradi huo ukamilike na kuanza kutoa huduma kwa wananchi.
Mjumbe wa NEC,Balozi Ally Karume akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana mara baada ya kukagua mradi mkubwa wa maji katika kijiji cha Nkungwe,Kigoma vijijini.Mradi huo umeshindwa kukamilika kutokana na ukosefu wa fedha,lakini pia Kinana amewahidi wananchi kulitafutia ufumbuzi wa haraka tatizo hilo na hatimaye mradi huo kukamilika na kuwasiadia wananchi mbalimbali wa maeneo hayo.
Katibu wa NEC-CCM wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (katikati) akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kata ya Mahembe, Jimbo la Kigoma Kaskazini.
Baadhi ya Wanakijiji cha Mahembe wakiwa kwenye mkutano huo wa hadhara
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akisoma orodha ya vijiji vitakavyopatiwa umeme na maji katika wilaya ya Kigoma Vijijini. Kikiwemo Kijiji cha Mahembe ambacho tayari kimepata umeme.
Mkutano wa hadhara ukiendelea kwenye kijiji cha Mahembe,Kigoma vijiji ambapo wananchi wengi walijitokeza kusikiliza yaliyokuwa yakisemwa kwenye mkutano huo.
Vijana wa bodaboda wakiwa kwenye msafara wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana katika kijiji cha Mwandiga,Kigoma Vijijini 
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipokelewa na wanachama mbalimbali wa CCM,alipokuwa akiwasili kwenye ofisi ya makao makuu ya wilaya ya Kigoma Vijijini,katika kata kijiji cha Mwandiga,Kigoma Vijijini .
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizunguma na baadhi ya Mabalozi mbalimbali wa CCM (hawapo pichani),kwenye kikao chao cha ndani,kilichofanyika katika ofisi ya makao makuu ya wilaya ya Kigoma Vijijini,katika kata kijiji cha Mwandiga,Kigoma Vijijini .

Baadhi ya Mabalozi mbalimbali wa CCM,wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Nduguu Kinana alipozungumza nao kwenye kikao chao cha ndani,kilichofanyika katika ofisi ya makao makuu ya wilaya ya Kigoma Vijijini,katika kata kijiji cha Mwandiga,Kigoma Vijijini .
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwa emeongozana na Viongozi wengine wa CCM,Mkoa na Wilaya katika kukagua mradi wa  wajasiliamali wa Kilimo,ndani ya kijiji cha Kidahwe Kigoma Vijijini mkoani Kigoma.