Katibu
Mkuu wa CCM;Ndugu Kinana na Wananchi wakishiriki ujenzi wa Ghala la
kuhifadhi mazao na mashine ya kusaga nafaka katika kijiji cha cha
Kidahwe,Kigoma Vijijini.Ghala hilo linalenga kusaidia katika kuhifadhi
mazao ya wakulima na kijiji hicho baada ya kuvuna ili kusubiri soko na
bei nzuri ya mazao kwa mfumo wa stakabadhi ghalani.Usimikaji wa mashine
katika ghala hilo utawasaidia pia wakulima kuchakata mazao yao (hasa
mahindi na muhugo) na kuuza unga badala ya mahindi.Gharama za mradi huo
ni shiliingi milioni 104,800,000/=.
Katibu
wa NEC-CCM wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akishiriki ujenzi wa Ghala
la kuhifadhi mazao na mashine ya kusaga nafaka katika kijiji cha cha
Kidahwe,Kigoma Vijijini.Ghala hilo linalenga kusaidia katika kuhifadhi
mazao ya wakulima na kijiji hicho baada ya kuvuna ili kusubiri soko na
bei nzuri ya mazao kwa mfumo wa stakabadhi ghalani.Usimikaji wa mashine
katika ghala hilo utawasaidia pia wakulima kuchakata mazao yao (hasa
mahindi na muhugo) na kuuza unga badala ya mahindi.Gharama za mradi huo
ni shiliingi milioni 104,800,000/=.
Katibu
wa NEC-CCM wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (kulia) akifafanua jambo
kwa Wananchi (hawapo pichani) walipokwenda kukagua kushiriki na kukagua
ujenzi wa Ghala la kuhifadhi mazao na mashine ya kusaga nafaka katika
kijiji cha cha Kidahwe,Kigoma Vijijini.
Baadhi
ya Wazee wa kijiji cha Nkungwe wakifuatilia yaliyokuwa yanazungumwa na
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana katika kijiji cha Nkungwe,kuhusiana na
tatizo la ufumbuzi wa mradi wa maji.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na Wananchi wa kijiji cha Nkungwe
kuhusiana na mradi wa maji unaojengwa,ambao kwa sasa umesimama kutokana
na ukosefu wa fedha.
Ujenzi wa tanki hilo la maji kama lionekanavyo pichani.
Katibu Mkuu Ndugu Kinana akipata maelezo mafupi kuhusiana na ujenzi wa tanki la maji katika kijiji cha Nkungwe,Kigoma vijijini.
Ndugu
Kinana (wa tatu kulia),akishiriki kufukia mabomba ya mradi wa maji
katika kijiji cha Nkungwe,Kigima vijijini.Mradi huo ukikamilika
unatarajiwa kusaidia vijiji zaidi ya 30.
Ndugu
Kinana akiwasalimia wananchi mbalimbali (hawapo Pichani),wakati
alipokuwa akiwasili katika kijiji cha Nkungwe kukagua mradi wa maji
ambao umeshindwa kukamilika kutokana na ukosefu wa fedha. Kinana
amewaahidi wananachi kulitafutia ufumbuzi suala hilo ili mradi huo
ukamilike na kuanza kutoa huduma kwa wananchi.
Mjumbe
wa NEC,Balozi Ally Karume akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu
Kinana mara baada ya kukagua mradi mkubwa wa maji katika kijiji cha
Nkungwe,Kigoma vijijini.Mradi huo umeshindwa kukamilika kutokana na
ukosefu wa fedha,lakini pia Kinana amewahidi wananchi kulitafutia
ufumbuzi wa haraka tatizo hilo na hatimaye mradi huo kukamilika na
kuwasiadia wananchi mbalimbali wa maeneo hayo.
Katibu
wa NEC-CCM wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (katikati) akihutubia
katika mkutano wa hadhara katika Kata ya Mahembe, Jimbo la Kigoma
Kaskazini.
Baadhi ya Wanakijiji cha Mahembe wakiwa kwenye mkutano huo wa hadhara
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akisoma orodha ya vijiji vitakavyopatiwa umeme
na maji katika wilaya ya Kigoma Vijijini. Kikiwemo Kijiji cha Mahembe
ambacho tayari kimepata umeme.
Mkutano
wa hadhara ukiendelea kwenye kijiji cha Mahembe,Kigoma vijiji ambapo
wananchi wengi walijitokeza kusikiliza yaliyokuwa yakisemwa kwenye
mkutano huo.
Vijana wa bodaboda wakiwa kwenye msafara wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana katika kijiji cha Mwandiga,Kigoma Vijijini
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipokelewa na wanachama mbalimbali wa
CCM,alipokuwa akiwasili kwenye ofisi ya makao makuu ya wilaya ya Kigoma
Vijijini,katika kata kijiji cha Mwandiga,Kigoma Vijijini .
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizunguma na baadhi ya Mabalozi mbalimbali wa
CCM (hawapo pichani),kwenye kikao chao cha ndani,kilichofanyika katika
ofisi ya makao makuu ya wilaya ya Kigoma Vijijini,katika kata kijiji cha
Mwandiga,Kigoma Vijijini .
Baadhi
ya Mabalozi mbalimbali wa CCM,wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Nduguu
Kinana alipozungumza nao kwenye kikao chao cha ndani,kilichofanyika
katika ofisi ya makao makuu ya wilaya ya Kigoma Vijijini,katika kata
kijiji cha Mwandiga,Kigoma Vijijini .
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwa emeongozana na Viongozi wengine wa
CCM,Mkoa na Wilaya katika kukagua mradi wa wajasiliamali wa
Kilimo,ndani ya kijiji cha Kidahwe Kigoma Vijijini mkoani Kigoma.
No comments:
Post a Comment