Na Magreth Magosso,Kigoma
IMEFAHAMIKA kuwa,baadhi ya mitumbwi inayoibwa katika Ziwa
Tanganyika mkoani hapa imekuwa ikitumika kwenye kazi za doria katika mto Lukoga
mashariki ya nchi ya Congo-DRC.
Kauli hiyo imekuja baada ya baadhi ya mashine 2,mitumbwi 2
sanjari na karabai kumi za wavuvi kurudishwa kwa wahanga wa uvuvi kigoma ,kufuatia kamati ya wajumbe maalum kufuatilia mchakato wa kuzipata zana 18 ambazo
ziliibwa machi,3,2014 sambamba na kutekwa kwa mvuvi moja katika ziwa hilo.
Ally Mziya ni mmoja wa waliozipata zana hizo alisema wahalifu wanaoiba zana za uvuvi wanamahusiano
ya karibu na baadhi ya askari jeshi wa wilaya ya Kalemi ,hali inayochangia
kusuasua kwa zana 16 kurudishwa kigoma,kutokana na sheria ya nchi hiyo ,huku
akiomba serikali zote mbili zishirikiane
kwa dhati ili kuondoa changamoto hiyo.
Akijibu hilo Ubalozi mdogo wa DRC-Congo Ricky Molema alisema
kamati yao ya ulinzi wilaya ya kalemi imebaini kundi hilo la uhalifu wa ziwani na wapo katika mchakato wa kuwabana
waachane na kasumba hiyo, ili kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizo,huku
akidai si kweli wanatumia zana za wizi za kigoma katika kufanikisha doria zao.
Akikabidhi zana hizo kwa baadhi ya wavuvi Mkuu wa wilayani
kigoma Ramadhan Maneno alidai jumatatu atakuwa na mkutano na wadau wa uvuvi ili
kutambua raia wanaoishi kinyume na sheria ili warudishwe kwao kwa lengo la
kupunguza mtandao wa kihalifu unaoathiri uchumi wa wilaya ya kigoma na Uvinza.
Naye mgeni rasmi katika makabidhiano hayo,Mkuu wa MKoa huu
Lt.Mstaafu Issa Machibya alisema wavuvi
wawe sehemu ya polisi jamii ili kubaini viashiria vya uhalifu dhidi yao,hali
itakayokomesha unafiki miongoni mwao na kuwataka wakuu wa wilaya ya Uvinza na
Kigoma wabaini wahamiaji haramu ili kuwadhibiti na waishi kwa taratibu na sheria
za idara ya uhamiaji kwa lengo la kukomesha uhalifu mkoani hapo.
Ofisa upelelezi wa Mkoa Dismas Kisusi na Mwenyekiti wa wavuvi Ramadhan Kanyongo kwa nyakati tofauti walisema
vitendo vya uhalifu ziwani vilianza kushamiri katika ukanda wa mwambao wa ziwa Tanganyika
kuanzia mwaka 2011 hadi 2014 hali inayochangiwa na hali halisi ya mipaka ya
mkoa huo ,
Sanjari na bajeti finyu ya
ulinzi katika ziwa hilo,lakini leo(jana) Lt.Machibya amedai dolia zipo za
kudumu kwa siku 365 na kusisitiza wahalifu watakiona na kukiri zana zilizorudishwa ni chache kulingana na zilizochukuliwa.
No comments:
Post a Comment