Pages

KAPIPI TV

Tuesday, January 27, 2015

LOCAL EU STATEMENT ON CLOSURE OF A NEWSPAPER IN TANZANIA

02EastAfrican

MWANAMKE ALIVYOUWA WATOTO WAKE WAWILI NA KUWACHIMBIA SHIMO NDANI YA NYUMBA YAKE

Mwili wa mtoto Mwamvua Mrisho(6)aliyeuawa kwa kunyongwa na mama yake mzazi Zuhura Sudi ambaye aliuwa watoto wake wawili na kuwachimbia mashimo na baadaye kuwafukia chumbani na Sebuleni
Askari Polisi wa Kituo kikubwa cha Polisi Tabora akiweka ulinzi mkali kwa Zuhura Sudi baada ya kuwauwa watoto wake wawili kwa kuwanyonga huko katika mtaa wa Utusi(Bakari)kata ya Chemchem manispaa ya Tabora.
Zuhura Sudi mara baada ya kuwanyonga watoto wake
Mwili wa mtoto Sudi(miezi saba)baada ya kufukuliwa ndani ya shimbo alilofukiwa na mama yake mzazi baada ya kuuawa kwa  kunyongwa,Sudi na Mwamvua walinyongwa na kuwekwa kwenye mifuko ya Sandarusi na kufukiwa kwenye mashimo yaliyochimbwa na mama yao mzazi Zuhura Sudi.
Mwili wa Mwamvua baada ya kufukuliwa na Askari Polisi
Miili ya watoto wote wawili baada ya kufukuliwa.

 Na Mwandishi wetu.

Katika hali isiyokuwa ya kawaida mwanamke mmoja mkazi wa mtaa wa Utusi kata ya Chemchem Manispaa ya Tabora Zuhura Sudi(26) anadaiwa kuwaua watoto wake wawili kwa kuwakaba  shingoni  na baadae kuwachimbia  mashimo  mawili  na kuwafukia.


Tukio hilo ambalo lilihuzunisha baadhi ya watu waliofurika nyumbani kwa mwanamke huyo mtaa wa Utusi(Bakari)   imedaiwa kuwa alilifanya wakati akiwa amebaki nyumbani hapo alipokuwa akiishi yeye na babu yake ukiachilia mbali watoto hao wawili ambao ni marehemu  wakifahamika kwa majina ya  Mwamvua  Mrisho(6) na Sudi mwenye umri wa miezi saba.


Taarifa iliyotolewa  kwa vyombo vya habari na kaimu kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora  ACP Juma Bwire imeeleza  kuwa Zuhura akiwa nyumbani kwake na watoto hao wawili aliwakaba shingo hadi kufa,kisha kuwafunga kwenye mifuko ya sandarusi  na kuwafukia katika mashimo mawili aliyoyachimba sebuleni na chumbani.


Taarifa hiyo kutoka Jeshi la Polisi imebainisha kuwa mtuhumiwa Zuhura atafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika huku ikilaani vikali tukio hilo la kinyama lililofanywa na mwanamke huyo.


Kwa mujibu wa maelezo ya Mwenyekiti wa mtaa wa Utusi, Bibi Aziza  Mwenya,ushirikiano mkubwa  baina  ya  wananchi  wa mtaa  huo  ndio uliofanikisha  kugundulika  kwa tukio  hilo  la  kinyama  lililopoteza  maisha  ya  watoto  hao  wasiokuwa  na  hatia.


Bibi  Aziza  alisema  baada  ya  kupokea taarifa  kutoka  kwa   Babu  wa  mwanamke  huyo  Zuhura  anayefahamika kwa jina la Shabani Ramadhani  kuhusu  kutoweka  kwa watoto  hao wawili katika  mazingira  ya kutatanisha,walilazimika  kufika  nyumbani  hapo  na kuanza  kumhoji  Zuhura  ambaye alikuwa akizuia watu  kuingia ndani kutokana na tukio hilo la kinyama alilolifanya.


Hata hivyo majirani kwa kushirikiana na Mwenyekiti wao wa mtaa na baba wa mmoja wa watoto hao waliouawa  Bw.Mrisho Abdallah  ambae alikuwa mume wa Zuhura walimvamia na kumshika kwa nguvu  Mwanamke huyo  ili waingie ndani na kubaini kuwa kulikuwa na mashimo mawili aliyokuwa amewafukia watoto hao ambao baadae walikuja kufukuliwa kwa msaada wa Jeshi la Polisi.


Katika mahojiano ya awali yaliyofanywa na mwandishi wetu na muuaji huyo wakati akiwa chumbani mara baada ya kubainika kwa tukio hilo,Zuhura alionekana kutokuwa na wasiwasi  wowote hatua ambayo baadhi ya watu walidai kuwa mwanamke huyo ana lengo la kupoteza ushahidi  kwa kuonesha ametokwa na akili timamu.


Hata hivyo kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa majirani zake wa karibu,mwaka 2013 Zuhura anadaiwa kumsababishia kifo mtoto wake mchanga  wa kiume baada ya kumzidishia dozi ya malaria wakati alipokuwa akiumwa.






Sunday, January 25, 2015

KAYMU TURNS TWO WITH A PROMISE OF EXPANSION TO FURTHER SHORES

kaymu logo copy



Kaymu Tanzania Country Manager, Erfaan Mojgani says “The significant growth of Kaymu over the past two years has been great motivation for us especially with our launch in Tanzania. The consumer demand for e-commerce has pushed Kaymu to grow and as 2015 goes on, we are looking to grow even further than we already have”




Friday, January 23, 2015

PATA FILAMU YA FOOLISH AGE KUPITIA MTANDAO

Katika maisha binadamu ana nyakati tatu, Wakati uliopita, wakati uliopo na wakati ujao. Wakati uliopita na ujao hana mamlaka nao bali wakati uliopo ndio hazina yake ya kujenga mustakabali wake ila kikwazo kikuu ni umri wake. Kuna umri anahitaji matunzo na ulinzi unaitwa utoto na kuna umri anahitaji heshima na matunzo  unaitwa uzee halafu kuna umri unaitwa mtu kamili ila kabla yake upo umri matata unaitwa FOOLISH AGE . Fuatilia hii kupitia mtandao .......

Kwa Kuangalia Filamu hii ya Kitanzania iitwayo Foolish Age au Knunua na iwe yako kupitia mtandao.

Ili kuweza kuangalia au kununua kupitia Mtandao unachotakiwa kufanya ni kutembelea tovuti hii



WANACHAMA WA FIBUCA TAWI LA ATTT WALALAMIKIA VITISHO TOKA KWA MWAJIRI WAO

Mkuu wa wilaya ya Tabora mjini Bw.Suleiman Kumchaya akizungumza  na baadhi ya wanachama FIBUCA tawi la kampuni ya ununuzi wa tumbaku nchini ATTT wakati wa semina fupi ya masuala ya uongozi iliyofanyika Tabora mjini.
Katibu wa FIBUCA mkoa wa Tabora Bw.Ramadhani Wakulichombe akisoma taarifa fupi ya maendeleo ya FIBUCA ambapo alieleza kuwa wanachama wa chama hicho wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali hususani za kutishwa na viongozi au waajiri katika maeneo yao ya kazi wakati wanapotetea haki za wafanyakazi ambao kimsingi ni wanachama wa FIBUCA.


 Na Juma Kapipi,Tabora.
CHAMA cha wafanyakazi wa asasi za fedha,viwanda,Benki,Uzalishaji wa nishati,Biashara na Kilimo FIBUCA tawi la Tabora kimelalamikia hatua za vitisho wanavyopatiwa wanachama wa chama hicho tawi la kampuni ya tumbaku ya ATTT kutoka kwa mwajiri wao na kusababisha baadhi ya wanachama kutaka kujitoa kwa kuhofia kupoteza ajira zao.

Akisoma taarifa fupi mbele ya kaimu mkuu wa mkoa wa Tabora Suleiman Kumchaya wakati wa semina ya viongozi wa tawi la  chama hicho  katika  kampuni  ya ATTT,Katibu wa FIBUCA mkoani hapa Ramadhani Wakulichombe alisema moja kati ya changamoto  kubwa  inayowakabili ni pamoja  na vitisho dhidi  ya  wanachama na viongozi wa tawi hilo.

Wakulichombe amebainisha  kuwa licha ya FIBUCA kuendelea kujitangaza  sehemu mbalimbali za waajiri na kufanikiwa kuingiza wanachama wengi ikiwemo wafanyakazi wa kampuni ya Association of Tanzania Tobacco Traders ATTT,lakini jambo la kushangaza ni kuona  uongozi wa kampuni ya ATTT ikihoji kwanini wafanyakazi hao wamejiunga na chama hicho jambo ambalo limekuwa likiwatishia na hata kufikia hatua ya kuanza kujitoa wakihofia kupoteza ajira.

Alisema hatua ya kampuni ya uongozi wa kampuni ya ATTT kutishia wanachama ni kinyume na sheria ya ajira na mahusiano kazini sehemu ndogo 'd' inayozungumzia uhuru wa kujumuika(Employees right to freedom of association)kifungu namba tisa(9) kwamba kila mwajiriwa anayo haki na kujiunga na chama cha wafanyakazi anachokiona kinamfaa.

Hata hivyo Katibu huyo wa FIBUCA ameiomba Serikali ya mkoa wa Tabora kuingilia kati na kulifanyia kazi suala hilo ambalo linawafanya wafanyakazi au wanachama wa chama hicho tawi la ATTT kutokuwa na uhuru wa kisheria katika maeneo yao ya kazi.

Akifungua semina hiyo kaimu mkuu wa mkoa wa Tabora Suleiman Kumchaya aliwataka vingozi wa FIBUCA kusimama imara wakati wanapotetea haki za wanachama wao pasipo kuvunja sheria.

Kumchaya alisema vitisho imekuwa ni jambo ambalo linalotumiwa sana na baadhi ya waajiri ikiwa ni moja ya hatua ya kuwanyonya wafanyakazi mahala pa kazi ili wao waweze kunufaika zaidi.

Aidha katika hatua nyingine baadhi ya wafanyakazi wa ATTT ambao hawakutaka kutaja majina yao wameeleza kuwa mwajiri wao amekuwa akilazimisha  wafanyakazi wake wajiunge  na chama cha Wafanyakazi wa Mashambani na Kilimo TPAWU ambacho wamedai kuwa kimekuwa kikilinda zaidi maslahi ya mwajiri kuliko mfanyakazi.

Walisema TPAWU ni chama ambacho kilikuwepo tangu awali kabla ya FIBUCA na hivyo wamedai kuwa kimeshindwa kutetea maslahi ya wafanyakazi ndio maana wakaamua kujiunga na FIBUCA ambacho mwajiri hakubaliani nacho na ndio sababu ya kuwepo kwa vitisho kwakuwa chama hicho kimekuwa kikiweka wazi na kutoa elimu ya haki za wafanyakazi na namna ya kuzidai.

Chama cha wafanyakazi FIBUCA ni chama huru kilichoanzishwa kwa mujibu wa sheria ya ajira na mahusiano kazini namba sita(6)ya mwaka 2004 na kupata usajiri wa kudumu mnamo tarehe 24 Julai 2009 kwa kupewa cheti namba 24 ambapo kilianzishwa na wafanyakazi wapatao 20 kutoka Benki ya NMB,NBC,NSSF na DAWASCO. 
     





UZINDUZI WA UPANDAJI MITI KIMKOA ULIOFANYIKA KIJIJI CHA NKINTO WILAYA YA MKALAMA -SINGIDA

SKYLIGHT BAND YAIBUA KIFAA KIPYA MITHILI YA KASUKU SI MWINGINE NI ASHURA KITENGE,NJOO LEO UMSHUHUDIE LIVE THAI VILLAGE

DSC_0014
Mratibu wa Skylight Band, Lubea akimkaribisha mdau wa bendi hiyo Miryam Kamaliza shot ya Tequila wakati wa show iliyobamba wakazi wa Dar Ijumaa iliyopita ndani ya kiota cha Thai Village, Masaki.
DSC_0017
Mratibu wa Skylight Band, Lubea akimimina kinywaji cha Tequila kwa Meneja wa Skylight Band, Aneth Kushaba AK47 Ijumaa iliyopita ndani ya kiota cha Thai Village.
DSC_0018
Meneja wa Skylight Band, Aneth Kushaba AK47 akipiga kilaji cha Tequila kupasha mwili joto kabla ya kupanda jukwaani, kinywaji hicho ni maalum kwa mashabiki wa bendi hiyo pindi wanapoingia kwenye kizingiti cha ukumbi huo wa Thai Village, Masaki jijini Dar.
DSC_0019
Msanii wa Skylight Band Joniko Music (katikati), akifungua dimba la burudani kwa mashabiki wa bendi hiyo huku akipewa sapoti na Aneth Kushaba AK 47 pamoja na Sam Mapenzi (kulia) wakati show zao za kila Ijumaa ndani ukumbi wa Thai Village Masaki, jijini Dar.
DSC_0115
Aaaah Komando Kipensi weeeeeee... si mwingine ni Le Manager her self Aneth Kushaba AK 47 mutoto ya Kisukuma akifanya yake jukwaani Ijumaa iliyopita ndani ya kiota cha Thai Village, Masaki jijini Dar......Tukutane baadae pale kati....Full MAU-KODAK kuwa huru kuomba picha na washikaji zako mdau wetu.
DSC_0034
Murembo mupya binti mwenye sauti ya kumtoa Nyoka pangoni, Ashura Kitenge akitoa burudani kwa mashabiki wa Skylight Band (hawapo pichani) ndani ya kiota cha Thai Village, Masaki jijini Dar es Salaam Ijumaa iliyopita huku akipewa sapoti na Rapa mkongwe Joniko Flower pamoja na Aneth Kushaba AK47.
DSC_0037
DSC_0126
Mashabiki wa Skylight Band wakijimwaga kwa raha zao.
DSC_0053
Meneja wa Skylight Band, Aneth Kushaba AK47 a.k.a #KomandoKipensi akiwa kwenye hisia kali wakati akitoa burudani kwa mashabiki wa bendi hiyo (hawapo pichani) Ijumaa iliyopita ndani ya kiota cha Thai Village, Masaki jijini Dar.
DSC_0056
Sam Mapenzi akiwapa raha mashabiki wa Skylight Band (hawapo pichani) huku akipewa sapoti ya back vocal na Rapa Joniko Flower pamoja na Sony Masamba.
DSC_0068
Daudi Tumba akifanya yake jukwaani kuhakikisha mashabiki wa Skylight Band wanapata ladha nzuri ya muziki wa Live ndani ya kiota cha Thai Village, Masaki jijini Dar Ijumaa iliyopita.
DSC_0072
Majembe ya Skylight Band yakijimwaga na sebene jukwaani kwenye show za bendi hiyo zinazofanyika kila Ijumaa ndani ya kiota cha Thai Village, Masaki jijini Dar.
DSC_0120
Mashabiki wa Skylight Band wakijiachia kwa raha zao ndani ya kiota cha Thai Village, Masaki jijini Dar.
DSC_0088
Vijana wa Skylight Band wakitimua vumbi jukwaani wakiongozwa na Sony Masamba.
DSC_0141
Twende kazi.... Sony Masamba akilisongesha na vijana wenzake.
DSC_0098
Rapa mkongwe kwenye muziki wa Live Joniko Flower (kushoto) akichana mistari huku wenzake wakitimua vumbi jukwaani.
DSC_0109
Sam Mapenzi asali ya warembo akiwa kenye hisia kali alipokuwa akiwapa haki yao mashabiki wa Skylight Band na nyimbo za kisasa zikiwemo Naija Flava, Reggae na zingine kibao....jamaa ni mkali asiyekubali ni mchawi...!
DSC_0131
Mashabiki wa Skylight Band wakijinafasi kwa raha zao.
DSC_0105
Rais wa #Wanamanyoya Sultan Gijegije (kulia) akipata ukodak na wanamanyoya Joshua Ndege (katikati) pamoja na mdau.
DSC_0082
Sura mpya ndani ya Skylight Band yenye sauti mithili ya ndege Kasuka si mwingine ni Ashura Kitenge akishow love na Joshua Ngoje back stage.
DSC_0083
Kisura mwingine wa Skylight Band anayefamika kwa jina la Baby (kulia) akipata ukodak na shosti yake back stage.
DSC_0106
Wadau nambari One wa Skylight Band wakishow love na Ukodak.
DSC_0149
Wanafahamika kwa jina moja #Wadananda a.k.a CUSTOMER CARE nao walipata Ukodak.
DSC_0154
#TeamWadananda wakishow love na mdau.
DSC_0159
Rapa wa Skylight Band Sony Masamba akishow love na wadau wa bendi hiyo baada ya kuhitimisha show ya Ijumaa iliyobamba ndani ya kiota cha Thai Village, Masaki jijini Dar. Tukutane baadae.

Thursday, January 22, 2015

FILAMU YA MDUNDIKO SASA YAPATIKANA KUPITIA MTANDAO


Katika maisha tunayoishi duniani sio vizuri kufanyiana mabaya, Kwani hujui kesho itakuaje. Malipo ni hapahapa Duniani . Fuatilia hii kupitia mtandao .......

Kwa Kuangalia Filamu hii ya Kitanzania iitwayo Fedheha au Knunua na iwe yako kupitia mtandao.

Ili kuweza kuangalia au kununua kupitia Mtandao unachotakiwa kufanya ni kutembelea tovuti hii



GOFU LA KIONGOZI WA WAJERUMANI LA MWAKA 1905