Mti aina ya mbuyu uliopo kwenye yaliyokuwa makazi ya Wajerumani mwanzoni mwa miaka ya 1900 ambao ulitumika kunyongea watuhumiwa waliokuwa wakitiwa hatiani.Picha zote na Nathaniel Limu. |
Jengo
lililotumiwa na Wajerumani kama mapokezi kuanzia mwaka 1905 huko
katika kijiji cha Mkalama wilaya ya Mkalama.Jengo hilo baadae Waingereza
waligeuza matumizi na kuwa posta.
|
HALMASHAURI ya
wilaya
ya Mkalama Mkoa wa Singida, imeshauriwa kuzingatia uwezekano wa
kulikarabati na kulilinda jengo lililojengwa na Wajerumani mwaka 1905
lililopo
katika kijiji cha Mkalama, ili liwe makumbusho kwa kizazi cha sasa na
kile kijacho pia liwe kivutio kwa watalii wa ndani na nje ya
nchi.
Alisema aina ya ujenzi uliotumika kujenga jengo la makazi kiongozi
wa Wajerumani hao, likiwa pamoja na jengo ya mapokezi, mahakama
chumba cha kuhifadhia (mahabusu) wafungwa na lile la utawala, ni wa kipekee,
tofauti kabisa na ujenzi unaofanyika
hivi sasa.
Kidimanda alisema katika makazi hayo, pia upo mti aina ya mbuyu,
uliokuwa ukitumika kunyongea watuhumiwa wa makosa mbalimbali waliokuwa wanapewa adhabu ya kunyongwa hadi
kufa.
“Makazi haya ya Wajerumani ambayo baadaye walinyang’anywa na Waingereza,
yamejengwa juu ya mlima uliopo kwenye kijiji chetu. Kwa ujumla yanavutia mno. Kama
yatakarabatiwa na kulindwa, kwa vyo vyote yatakuwa chanzo kikubwa sana cha
mapato ya halmashauri yetu”,alisema Kidimanda.
Aidha,aliweza kutoa ushauri mwingine kwa kushauri kuwa halmashauri
inaweza kutafuta mwekezaji akajenga hoteli yenye ubora kwenye yaliyokuwa
makazi ya Wajerumani,itavutia watalii wa ndani kufika mahali hapo ili kuona majengo yaliyojengwa miaka 110
iliyopita.
Kwa mujibu wa Kidimanda , Wajerumani hao walikuwa
wanajishughulisha zaidi na kilimo na ilikuwa ni kosa kubwa kwa mtu ye yote
kwenda kinyume na matakwa yao.
Anasema baada ya kunyonga hadi kufa watu wengi kwenye mbuyu uliopo
kwenye makazi yao, na kubaini kuwa bado baadhi ya watu waliendelea na tabia ya
kutokutii maelekezo yao bila kuogopa adhabu hiyo, walianza kunyonga watu kwenye
mbuyu uliopo kwenye uwazi kijijini hapo, ili kila mtu aweze kushuhudia kwa
lengo la kuwaogofya.
No comments:
Post a Comment