Mkuu wa wilaya ya Mkalama mkoa wa Singida,Edward Ole Lenga,akipanda mti katika uzinduzi wa upandaji miti kimkoa uliofanyika katika kijiji cha Nkinto wilayani Mkalama |
Na Nathaniel Limu-Mkalama.
MKOA wa Singida umefanikiwa kupanda miti ya aina mbalimbali ipatayo 10,347, 870 sawa na asilimia 37 ya lengo la mkoa kupanda miti 27,500,000 kati ya mwaka 2010 na mwaka jana.
Hata
hivyo kwa mujibu wa wataalamu, asilimia 50 ya miti hiyo imekufa
kutokanana uhaba wa mvua, kuliwa na mchwa, uharibifu wa binadamu na
mifugo.
Hayo
yamesemwa juzi na mkuu wa mkoa wa Singida, Dr. Parseko Kone, wakati
akizungumza kwenye siku ya upandaji miti kimkoa ilifanyika katika kijiji
cha Nkito halmashauri ya wilaya ya Mkalama.
Alisema kutokana na mkoa kukabiliwa na tatizo la mvua haba, jitihada za kupanda miti huwa hazifikii malengo yanayokusudiwa.
“Hata
hivyo hilo halitukatishi tamaa. Napenda kutoa wito kwamba tupande miti
inayovumilia ukame, kutumia njia mbalimbali kwa vile pingili (cuttings)
za mininga mikuyu na jamii zingine zote zinazokubali hali ya hewa ya
mkoa wetu.
Aidha,mkuu
huyo wa mkao alitaja baadhi ya hatua mbalimbali zinazochukuliwa na
mkoa katika kupambana na hali ya kuenea kwa jangwa, ambazo ni kuanzisha
kampeni mbalimbali za upandaji miti ikiwemo kampeni ya msitu ni mali na
msitu ni mazingira.
“Pia
kampeni ya uhamasishaji wa kila kaya kupanda miti isiyopungua 10 na
taasisi zenye matumizi maalumu ya miti, tunaziagiza kuanzisha mashamba
yao ya miti,ili ziweze kujitosheleza kwa nishati hiyo”,alisema.
Katika
hatua nyingine Dr. Kone ametoa wito juu ya umuhimu wa wananchi
kuhakikisha wanahifadhi uoto wa asili uliopo kwa faida ya kizazi cha
sasa na kile kijacho.
“Kwa
kuwa miti mingi tunayopanda inakufa ni vyema watu binafsi na vijiji
watenge maeneo ya hifadhi za misitu ya uoto wa asili kwani hutoa kwa
haraka”,alisema.
Kwa
mujibu wa Dr. Kone, hadi sasa kuna vijiji 230 mkoa wa Singida vyenye
misitu ya asili ya ukubwa wa hekta zipatazo 520, 325.48.
Amesema misitu hiyo ya asili itumike kwa shughuli za ufugaji nyuki kibiashara, ili kumkomboa mwananchi kiuchumi.
No comments:
Post a Comment