Mwili wa mtoto Mwamvua Mrisho(6)aliyeuawa kwa kunyongwa na mama yake mzazi Zuhura Sudi ambaye aliuwa watoto wake wawili na kuwachimbia mashimo na baadaye kuwafukia chumbani na Sebuleni |
Zuhura Sudi mara baada ya kuwanyonga watoto wake |
Mwili wa Mwamvua baada ya kufukuliwa na Askari Polisi |
Miili ya watoto wote wawili baada ya kufukuliwa. |
Katika hali isiyokuwa ya kawaida mwanamke mmoja mkazi wa
mtaa wa Utusi kata ya Chemchem Manispaa ya Tabora Zuhura Sudi(26) anadaiwa
kuwaua watoto wake wawili kwa kuwakaba
shingoni na baadae
kuwachimbia mashimo mawili
na kuwafukia.
Tukio hilo ambalo lilihuzunisha baadhi ya watu waliofurika
nyumbani kwa mwanamke huyo mtaa wa Utusi(Bakari) imedaiwa kuwa alilifanya wakati akiwa amebaki
nyumbani hapo alipokuwa akiishi yeye na babu yake ukiachilia mbali watoto hao
wawili ambao ni marehemu wakifahamika
kwa majina ya Mwamvua Mrisho(6) na Sudi mwenye umri wa miezi saba.
Taarifa iliyotolewa
kwa vyombo vya habari na kaimu kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP Juma Bwire imeeleza kuwa Zuhura akiwa nyumbani kwake na watoto
hao wawili aliwakaba shingo hadi kufa,kisha kuwafunga kwenye mifuko ya
sandarusi na kuwafukia katika mashimo
mawili aliyoyachimba sebuleni na chumbani.
Taarifa hiyo kutoka Jeshi la Polisi imebainisha kuwa
mtuhumiwa Zuhura atafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika huku
ikilaani vikali tukio hilo la kinyama lililofanywa na mwanamke huyo.
Kwa mujibu wa maelezo ya Mwenyekiti wa mtaa wa Utusi, Bibi
Aziza Mwenya,ushirikiano mkubwa baina
ya wananchi wa mtaa
huo ndio uliofanikisha kugundulika
kwa tukio hilo la
kinyama lililopoteza maisha
ya watoto hao
wasiokuwa na hatia.
Bibi Aziza alisema
baada ya kupokea taarifa kutoka
kwa Babu
wa mwanamke huyo
Zuhura anayefahamika kwa jina la
Shabani Ramadhani kuhusu kutoweka
kwa watoto hao wawili katika mazingira
ya kutatanisha,walilazimika
kufika nyumbani hapo
na kuanza kumhoji Zuhura
ambaye alikuwa akizuia watu
kuingia ndani kutokana na tukio hilo la kinyama alilolifanya.
Hata hivyo majirani kwa kushirikiana na Mwenyekiti wao wa
mtaa na baba wa mmoja wa watoto hao waliouawa
Bw.Mrisho Abdallah ambae alikuwa
mume wa Zuhura walimvamia na kumshika kwa nguvu
Mwanamke huyo ili waingie ndani
na kubaini kuwa kulikuwa na mashimo mawili aliyokuwa amewafukia watoto hao
ambao baadae walikuja kufukuliwa kwa msaada wa Jeshi la Polisi.
Katika mahojiano ya awali yaliyofanywa na mwandishi wetu na
muuaji huyo wakati akiwa chumbani mara baada ya kubainika kwa tukio hilo,Zuhura
alionekana kutokuwa na wasiwasi wowote
hatua ambayo baadhi ya watu walidai kuwa mwanamke huyo ana lengo la kupoteza
ushahidi kwa kuonesha ametokwa na akili
timamu.
Hata hivyo kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa majirani zake wa
karibu,mwaka 2013 Zuhura anadaiwa kumsababishia kifo mtoto wake mchanga wa kiume baada ya kumzidishia dozi ya malaria
wakati alipokuwa akiumwa.
No comments:
Post a Comment