Pages

KAPIPI TV

Friday, December 19, 2014

UKAWA WAFANYA MANDAMANO -KIBONDO

Picha kutoka maktaba
Na Magreth Magosso,Kigoma
 
WANANCHI wapatao 2,600  kati  3,000 wanaoishi  katika vijiji vitatu vinavounda Kata ya Kumsenga iliyopo wilaya ya Kibondo Mkoa wa Kigoma,wameandama kwenda ofisi za Mtendaji wa kijiji kwa madai ya kutoutambua uongozi uliochaguliwa Desemba,14, Mwaka huu.

Sbabu ya kutoutambua uongozi uliochaguliwa ni ,kutokana na wagombea wa Umoja wa Katiba ya wananchi (UKAWA) Leonard Tamwuluki , Ledbord Loki  na mwingine kupitia chama cha NCCR-Mageuzi kuenguliwa siku ya uchaguzi kwa sababu ya kushindwa kujaza  kipenge cha kwanza katika fomu ya wagombea husika.

Akifafanua hilo Katibu wa Jimbo la Muhambwe Renatus Richard alisema kata ina vijiji vitatu ambavyo ni Kibuye,mkinama na kumsenga, awali wagombea walinyimwa fomu  kabisa ndipo Mwenyeviti  Chadema wa wilaya Kalaveri Ntigita  alimshinikiza mtaendaji na wakapewa fomu bila maelekezo ya ziada kwa wagombea  siku mbili kabla ya uzinduzi wa kampeni za kuwanadi  kwa umma.

“kila tukienda kwa mtendaji wa kijiji  Clement Charles tunakuta ofisi imefungwa na tukimpata ofisini anasema hakuna fomu,sasa bila shinikizo la Ukawa wilaya mgombea wetu Ladibord Loki  asingepata fomu,siku ya kupiga kura mtendaji anasema kipengele kwa kwanza katika fomu ni batili” alisema Richard.

Akiongoza mandamano hayo Mwenyekiti  Chadema  wilaya ya Kibondo  Nicolaus Kilunga alisema serikali imepora haki ya umma,kwa kitendo cha mtendaji kutumika kuhujumu uchaguzi ni kuwanyima haki wananchi kupata viongozi bora wa kusimamia miradi mbalimbali ya maendeleo.

Viongozi walioteuliwa kupitia Chama Cha CCM  si chaguo la wengi kwa kuwa amepitishwa bila kuwepo kwa chama cha upinzani chochote na kuahidi wahusika wa sakata la kuchafua uchaguzi huo watafikishwa  mahakamani kujibu tuhuma za udanganyifu wa chaguzi hiyo.
 
Kwa upande wa mgombea wa Chadema kata ya Kumsenga Ladibord Oscar akili kunyimwa fomu  mapema na baada ya shinikizo la uongozi wa juu alipata fomu siku chache kabla ya zoezi la kampeni za kunadiwa wagombea mbaya zaidi  mtendaji hakumwelekeza namna ya kujaza fomu na hatimaye alifutwa siku ya uchaguzi.

Baadhi ya wananchi wa hapo Jason Daud na Neema Jonathan walisema hawatashirikiana na uongozi wa serikali  katika kazi na miradi ya maendeleo isipokuwa shughuli za kijamii hasa mazishi tu.huku wakitaka uchaguzi urudiwe ili wachague chaguo lao.

Mwandishi wetu  alipohitaji kupata maoni ya upande wa chama cha Nccr-Mageuzi  ambao ndio waliosimamisha wagombea wao katika vijiji hivyo hawakuweza kupatikana katika simu zao za mkononi hazikuwa hewani halikadhalika kwa Katibu mwenezi wa ccm  Mkoa wa kigoma Masud Kalembe.

Thursday, December 18, 2014

SERIKALI YAKUBALI AZIMIO ARUSHA KUHUSU HIFADHI YA JAMII

IMG_7245
Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum akitoa hotuba ya kufunga kongamano la Kimataifa la siku tatu kuhusu hifadhi ya Jamii lililoanza Disemba 15-17, 2014 jijini Arusha.(Picha zote na Eleuteri Mangi- Arusha).

Na Mwandishi wetu, Arusha
SERIKALI ya Tanzania imeridhia azimio la arusha kuhusi hifadhi ya jamii nchini Tanzania na kusema litatumika kama dira katika kunemeesha watanzania.

Azimio hilo ambalo limetoka baada ya mkutano wa siku tatu wa wadau mbalimbali wa hifadhi ya jamii kutoka bara la Afrika na mashirika ya kimataifa limeelezwa kuwa msingi mkubwa wa ajenda ya Tanzania kuhakikisha wananchi wake wanahaki sawa katika elimu, afya na mwendelezo wa kiuchumi.

Lengo likiwa ni kuhakikisha kwamba hifadhi ya jamii inasaidia kuwa na maendeleo endelevu kwa kuangalia maendeleo ya binadamu katika ujumla wake.

Mkutano huo wa siku 3 uliohusisha wataalamu 150 kutoka sekta mbalimbali nchini na barani Afrika wakiwemo watengeneza sera, watafiti na wataalamu wa masuala ya hifadhi.

Ukiwa umewezeshwa na serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na UNICEF, ILO, UNAIDS na taasisi ya utafiti wa sera za uchumi EPRI iliyopo Afrika Kusini (EPRI) , mkutano huo umeelezwa na waziri wa fedha Saada Mkuya Salumkwamba umeweka misingi imara ya kuwa na hifadhi ya jamii endelevu inayojibu mipango ya maendeleo ya taifa.
IMG_7158
Katibu Mkuu Wazara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile akisoma Azimio la Arusha linalohusu hifadhi ya Jamii, alisema kuwa historia imejirudia ambapo yapata miaka 47 (1967-2014) iliyopita Tanzania ilipitisha Azimio la Arusha lililolenga kupambana na maadui watatu ambao ni ujinga, maradhi na umaskini ambao Baba wa Taifa Mwl. Julius Kmbarage Nyerere aliwaita ni maadui wa taifa.

Kukiwa na wataalamu waliobobea katika mifumo ya hifadhi ya jamii kutoka Afghanistan, Bangladesh, Ethiopia, Ghana, Kenya, Lesotho, Malawi, Msumbiji, Afrika Kusini, Uganda, Zambia na Zimbabwe ulifanikiwa kutengeneza hoja zitakazotumika kufanya hifadhi ya jamii Tanzania kuwa endelevu.

Waziri Mkuya alishukuru kwa ushiriki wa mkutano na jinsi ulivyokuwa wazi na jinsi wataalamu walivyoweza kutengeneza azimio ambalo linaenda kuwa msingi katika utengenezaji wa sera na sheria kuhusu hifadhi za jamii nchini Tanzania na afrika kwa ujumla.

Mada kadhaa ziliwasilishwa katika mkutano huo ambazo zilizaa majadiliano yenye manufaa kuhusu mwelekeo wa hifadhi za jamii,utengenezaji wa mifumo ya kuweza kuendelea kuwepo kwa hifadhi ya jamii na umuhimu wa uratibu ndani ya serikali kuu, mitaa na mashirika yanayiotoa huduma za hifadhi ya jamii.
IMG_7135
Mwakilishi wa UNICEF Tanzania, Jama Gulaid (kushoto) na Naibu Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi, Mhe. Pereira Silima (Mb) wakisikiliza azimio la Arusha linalohusu hifadhi ya jamii wakati wa kufunga kongamano hilo.

Waziri huyo alisema kwamba wakati taifa linaelekea katika uchumi wa gesi utakaofanya kuwa na kipato cha kati ifikapo mwaka 2025 masuala ya hifadhi ya jamii yatakahakikisha haki katika kugawa keki ya taifa na kuhakikisha kwamba kila mwananchi anapata huduma za elimu, afya, na za kiuchumi kwa haki, kwa kuwa mifumo hiyo pia itatakiw akuchochea ajira na ujasirimali huku ilkilinda afya za wahusika.

Kwa upande wake Mwakilishi wa UNICEF nchini Dkt. Jama Gulaid akitoa neno la shukrani aliisifu Tanzania kwa kuanza mapema kusimamia masuala ya kinga ya jamii ikiwemo mifuko ya hifadhi ya jamii na misaada inayotolewa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kupitia mpango wake wa kunusuru kaya maskini zilizo katika mazingira hatarishi.

Aidha, Dkt. Gulaid aliipongeza Tanzania kwa kuwa na wimbo wa taifa unaozungumzia watu akiwataja kuwa ni wanawake, wanaume na watoto pamoja na bara la Afrika na watu wake licha ya kuwa na vivutio vizuri vya mlima Kilimanjaro, hifadhi ya Serengeti na visiwa vya karafuu.
IMG_7204
Mwakilishi wa UNICEF nchini Dkt. Jama Gulaid akitoa neno la shukrani wakati wa kufunga kongamano la Kimataifa la siku tatu kuhusu Hifadhi ya Jamii lililoanza Disemba 15-17, 2014 jijini Arusha na aliisifu na kuipongeza Tanzania kwa kuwa na wimbo wa taifa unaozungumzia watu akiwataja kuwa ni wanawake, wanaume na watoto pamoja na bara la Afrika na watu wake.
“Wimbo huu wa Tanzania tofauti na nyimbo za nchi nyingine ambazo wao wanazungumzia askari, watumwa, watawala wakiwemo Malkia na Wafalme”alisema Dkt. Gulaid.

Dkt. Gulaid aliwahakikishia wajumbe wa mkutano huo kuwa wote wapo salama na wapo kwenye mpango wa hifadhi ya jamii kwa kuwa wametambuliwa na kubarikiwa na wimbo wa taifa wa Tanzania ambapo wajumbe waliimba wimbo huo na kuhitimisha kongamano hilo.
DSC_1058
Washiriki wa Kongamano hilo wakiimba wimbo wa Taifa baada ya Mwakilishi wa UNICEF nchini Dkt. Jama Gulaid kutoa ombi kabla ya kumalizika kwa kongamano hilo.
IMG_7109
Naibu Waziri wa Fedha Adam Malima akisistiza jambo wakati wa kongamano la Kimataifa la siku tatu kuhusu Hifadhi ya Jamii lililoanza Disemba 15-17, 2014 jijini Arusha.
DSC_1061
Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum akitia saini Azimio la Arusha kwa niaba ya Serikali ya Tanzania wakati wa kongamano la Kimataifa la siku tatu kuhusu Hifadhi ya Jamii huku viongozi mbalimbali wa serikali na mashirika ya Umoja wa Mataifa wakishuhudia tukio hilo.
IMG_7267
IMG_7269
Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Serikali ya Tanzania na washiriki wa kongamano la Kimataifa la siku tatu kuhusu Hifadhi ya Jamii lililoanza Disemba 15-17, 2014 jijini Arusha akionesha nakala ya Azimio la Arusha alilosaini kwa niaba ya Serikali.
IMG_7271
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akimpongeza Wazri wa Fedha, Mh. Saada Mkuya Salum baada ya kusaini Azimio la Arusha kwa niaba ya Serikali ya Tanzania wakati wa kongamano la Kimataifa la siku tatu kuhusu Hifadhi ya Jamii (katikati) kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi, Mhe. Pereira Silima (Mb).
IMG_7272
Waziri wa Fedha, Mh. Saada Mkuya Salum (kushoto) akipeana mkono na Naibu Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi, Mhe. Pereira Silima (Mb) mara baada ya kusaini azimio hilo huku Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akishuhudia tukio hilo.
IMG_7102
Baadhi ya wajumbe wa kongamano la Kimataifa la siku tatu kuhusu Hifadhi ya Jamii lililoanza Disemba 15-17, 2014 jijini Arusha akifuatilia mada wakati wa kongamano hilo.
IMG_7173
IMG_7003
IMG_7043
Waziri wa Elimu na Mfunzo ya Ufundi Dkt. Shukuru Kawambwa (kushoto) akiteta jambo na Katibu Mkuu Wazara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile (kulia) mara baada ya kumalizika kongamano la Kimataifa la siku tatu kuhusu Hifadhi ya Jamii lililoanza Disemba 15-17, 2014 jijini Arusha.

MRATIBU MKAZI WA UMOJA WA MATAIFA AKUTANA NA RC ARUSHA

DSC_0175
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Arusha aliyeteuliwa hivi karibuni, Daud Felix Ntibenda alipomtembelea ofisini kwake kuzungumzia miradi mbalimbali inayofadhiliwa na mashirika ya Umoja wa Mataifa mkoani humo.
DSC_0170
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania Hoyce Temu (kushoto) akisaini kitabu cha wageni wakati Mkuu wa Mkoa na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa wkibadilishana mawazo kabla ya kuanza mazungumzo yao.
DSC_0178
Mkuu wa Mkoa wa Arusha aliyeteuliwa hivi karibuni, Daud Felix Ntibenda akizungumza na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (katikati) aliyeambatana na Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania Hoyce Temu.
DSC_0185
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez katika picha ya pamoja mara baada ya mazungumzo na uongozi wa mkoa wa Arusha ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Daud Felix Ntibenda (kulia) na kushoto ni Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha, Addo Mapunda.
DSC_0189
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez aliyeambatana na Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania Hoyce Temu (kushoto) katika picha ya pamoja na uongozi wa mkoa wa Arusha.
DSC_0198
Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha, Addo Mapunda akifafanua jambo kwa Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Daud Felix Ntibenda.

NAIBU MKURUGENZI MKUU WA UNESCO AWASILI JIJINI ARUSHA KUSHIRIKI MAHAFALI TAASISI YA MANDELA

UNESCO
Ofisa mwandamizi wa habari na mahusiano ya umma wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela, Bw. Karimu Meshack (kushoto) akijadiliana jambo ndani chumba cha mapumziko cha wageni mashuhuri na Mwakilishi mkazi shirika la UNESCO nchini Bi. Zulmira Rodrigues pamoja na Afisa mipango kitaifa, kitengo cha Sayansi UNESCO,Tanzania, Gabriela Lucas kabla ya kuwasili kwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Getachew Engida.
DSC_0516
Mwakilishi mkazi shirika la UNESCO nchini Bi. Zulmira Rodrigues akimlaki Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Getachew Engida wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kwa ajili kuhudhuria mahafali ya pili ya Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela jijini Arusha yanayofanyika kesho. Kulia ni Ofisa mwandamizi wa habari na mahusiano ya umma wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela, Bw. Karimu Meshack na wa pili Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya UNESCO, Dr. Moshi Kimizi.
DSC_0517
Mwakilishi mkazi shirika la UNESCO nchini Bi. Zulmira Rodrigues (katikati) akimlaki kwa furaha Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Getachew Engida (kushoto) aliyewasili jioni hii jijini Arusha na shirika la ndege la Ethiopia. Kulia ni Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya UNESCO, Dr. Moshi Kimizi.
DSC_0518
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Getachew Engida akisalimiana na Ofisa mwandamizi wa habari na mahusiano ya umma wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela, Bw. Karimu Meshack kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).
DSC_0524
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Getachew Engida akiwa na mwenyeji wake Mwakilishi mkazi shirika la UNESCO nchini Bi. Zulmira Rodrigues mara baada ya kuwasili wakielekea kwenye chumba cha mapumziko cha wageni mashuhuri.
DSC_0526

Wednesday, December 17, 2014

CHAMA CHA WAVUVI WATAKA WAFIDIWE-KIGOMA

Na Magreth Magosso,Kigoma

Chama cha wavuvi   Mkoa wa kigoma ,wameitaka wizara ya uvuvi na mifugo iweke bajeti ya  kuwafidia wahanga wa  janga  la kuibiwa zana za uvuvi katika ziwa Tanganyika kwa nia ya kuwapunguzia machungu ya madhira ya kuhujumiwa  na wahalifu katika shughuli za uvuvi  ziwani takribani  miaka 30.

Hayo yalijiri jana katika mkutano wa wazi uliofanyika katika mwalo wa Kibirizi  baina ya wavuvi  ,wamiliki wa mitumbwi  na uongozi wa  juu la Jeshi la Polisi  la hapa ,ukitaka  kuboresha mahusiano na ushirikiano wa dhati wa kukabiliana na changamoto ya kutekwa kwa wavuvi na uporwaji wa zana  ziwani  humo.

 Hamimu Wanyika  ni miongoni mwa wahanga walioathiriwa na changamoto hiyo alisema alianza shughuli za uvuvi mwaka 1984 na matukio ya uporajwi wa zana za wavuvi zilianza rasmi mwaka 1999 , na ameibiwa( injini) mashine 20 ambapo kwa  mwaka 2014  amebaki na mtumbwi mmoja usiokuwa na injini .

“hivi sasa nakodi injini moja 350 kwa siku 20 nina wake wanne,watoto 25 ,mmoja yupo chuo kikuu Dar-es-salaam ,wawili kidato cha Nne ,saba ni wanaume  wanabangaiza mitaani ,nimeshindwa kusomesha hawa wa kike ntawaoza tu nifanyeje,mwishoni mwa mwaka wizi huwa mkubwa mama acha tu” alisema mhanga huyo.

 Mwenyekiti wa ulinzi wa mazingira mwalo wa kibirizi ( BMU) Juma Hasani alisema kero hiyo ina miaka 30 na inapoteza ajira kwa vijana ,ambapo mtumbwi mmoja huajiri watu 12 na kushauri kamati za ulinzi na usalama wa Nchi zinazopakana na ziwa hilo, washirikiane na wawajibike kuzibiti wahalifu wakati tukio linatokea eneo husika.

Naye Katibu wa Umoja wa wavuvi kigoma(UWAKI) Mohamed Kasambwe alisema idara ya polisi ni chachu ya kuzorotesha adha hiyo,kutokana na wananchi wanaotoa miongozo ya kukomesha uhalifu huwazushia kesi za uongo kwa  kuwatupa mahabusu na wengine kudaiwa ni wahamiaji haramu.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa wavuvi Sendwe Ibrahimu alisema changamoto ya wizi ziwani imechangia  injini  800 za wavuvi  kuibiwa na kuitaka wizara husika itenge bajeti kwa ajili ya kuwafidia wahanga sanjari na halmashauri husika ichangie mafuta ya dharura kwa boti la doria ili kuzibiti majambazi katika tukio husika.

Ofisa Uvuvi Manispaa Harouni Chanda alisema awali manispaa ya kigoma ujiji ilikuwa ikikusanya zaidi ya milioni 50 kwa mwaka 2012/13 lakini kutokana na janga hilo wanakusanya chini ya milioni 20 kwa mwaka 2013/14  na kudai wametoa lita 1000  za mafuta kwa idara ya polisi kwa  lengo la kuongeza nguvu ya kupunguza uhaba huo.

Akijibia hayo Kamanda wa Polisi Jafari Mohamed alisema lengo la kukutana na wahanga ni kuweka mkakati wa kuokoa mali za wavuvi kwa wakati ,ambapo serikali haiwezi kuokoa janga kwa wakati kutokana na ukosefu wa fedha za kununua  mafuta  ya `speed boti ya doria kigoma ni shida.

Akubali kuunda kamati ya dharura miongoni mwa wavuvi kwa kushirikiana na Ofisa wa majini Nathaniel Lyambiko ,ambapo watakuwa na akiba ya mafuta na timu ya kikosi kazi ya kubaini wahalifu na namna ya kujipanga katika maeneo tete na kukabiliana na wahalifu husika.

Mkuu wa Mkoa wa kigoma Lt.Issa Machibya  hivi karibuni alitoa  agizo  lisemalo hivi`` kila halmashauri ihakikishe ifikapo 30,Novemba ichangie lita 1000 za mafuta  ili kuondoa adha ya usafiri wa kupambana na wahalifu wakati wa tukio “ .

 kipindi cha machi -Octoba  uporaji wa  zana za wavuvi umefanyika katika mwalo wa kibirizi na muyowozi ,ambapo Novemba 15,23 na 26  injini 15 zilishaporwa na kila injini huuzwa sh.milioni 7 sanjari na kupoteza ajira kwa vijana 180 ,hali inayotishia kuibuka kwa makundi ya kihalifu katika manispaa ya  kigoma Ujiji.

MIKATABA YA KIMATAIFA YAISAIDIA TANZANIA HIFADHI YA JAMII

DSC_0382
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dk Pindi Chana (kulia) akizungumza katika mkutano wa siku tatu wa kimataifa unaohusu hifadhi ya jamii unaotarajiwa kumalizika leo jijini Arusha. Katikati ni Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Mhe. Dkt. Kebwe Stephen Kebwe na kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima.(Picha na Zainul Mzige wa modewjiblog).

Na Mwandishi Wetu, Arusha
UTIAJI saini wa mikataba ya kimataifa, inayohusu hifadhi ya jamii kumeiwezesha Tanzania kuwa katika hatua nzuri ya kutekeleza ajenda yake ya kuhakikisha kwamba wananchi wake wanakuwa na haki sawa katika kujipatia maendeleo na ustawi.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dk Pindi Chana katika mkutano wa siku tatu wa kimataifa unaohusu hifadhi ya jamii mjini hapa.

Alisema mikataba mikubwa ya kimataifa ambayo Bunge la Tanzania limeridhia na iliyoleta mabadiliko makubwa katika sera na sheria nchini ni pamoja na Mkataba wa Kufuta Aina zote za Ubaguzi na Unyanyasaji kwa Wanawake (CEDAW) wa mwaka 1979, Mkataba wa Haki za Watoto (CRC) wa mwaka 1989 na Mkataba wa Afrika wa Haki za Watoto.
DSC_0394
Mkurugenzi mshiriki anayeshughulikia masuala ya program kutoka makao makuu ya UNICEF, Bi. Alexander Yuster, akiibua hoja kwenye mkutano mkubwa wa kimataifa wa hifadhi ya jamii ulioandaliwa na serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Fedha na wadau wengine kwa lengo la kubadilishana uzoefu juu ya nini cha kufanya kusaidia makundi maalumu katika jamii unaomalizika leo jijini Arusha. Kushoto ni Naibu Mkuu wa Kitengo cha Ushirikiano na Maendeleo kwenye Ubalozi wa Sweden nchini, Maria Van Berlekom.

Mikataba mingine ni Mpango wa Maendeleo wa Milenia (MDGs), Azimio la Umoja wa Mataifa Namba 1325 la mwaka 2000 na Azimio Namba 1820 la 2006, ambayo inazungumzia ushiriki na uwezeshaji wa wanawake katika kutanzua migogoro na ujenzi wa taifa.

Alisema kitendo cha kuridhia kwa mikataba na maazimio hayo, kinaonesha ni kwa namna gani serikali ina utashi wa utekelezaji wa maazimio hayo kwa lengo la kuhakikisha watoto na wanawake, wanalindwa dhidi ya vurugu za aina zozote na kuwanyima haki zao za msingi.

Dk.Chana alisema kwa kuzingatia ushiriki kuleta katika maendeleo ya nchi, Tanzania imetayarishwa Dira ya Maendeleo ya 2025 ikiwa na vipengele vyote vya haki vyenye lengo la kuongeza wigo wa ushiriki wa wanawake.

Aidha, ili kuhakikisha makundi maalumu yanalindwa, serikali pia imetengeneza Sera ya Maendeleo ya Watoto ya mwaka 2008, ambayo kwa sasa inapitiwa ili kuingiza mambo mengine yanayohusu haki za mtoto.
DSC_0350
Picha juu na chini baadhi ya washiriki wa mkutano mkubwa wa kimataifa wa hifadhi ya jamii wakiwemo watengeneza sera, watafiti na waendeshaji wa mifuko ya hifadhi kutoka mataifa ya Kenya, Uganda, Bangladesh, Mozambique, Lesotho, Malawi, Afrika Kusini, Ghana, Ethiopia, Zambia, Sudan Kusini na wenyeji Tanzania unaoendelea jijini Arusha.

Aidha, ikiwa imejikita kuondoa masuala ya kuondoa udhalilishaji wa kijinsia, serikali imefanya maamuzi mengi yenye manufaa pamoja na kushirikiana na wadau binafsi kuboresha maisha ya watanzania.

Alisema kwamba suala la wanawake na maendeleo, limeingizwa katika mkakati wa taifa wa kupunguza umaskini. Alisema mwaka jana serikali ilitengeneza programu ya taifa inayohusu wadau wengi ya miaka mitatu ya kuondokana na ukatili kwa watoto.

Mkutano huo unaozungumzia hifadhi, ulifunguliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Iddi ambaye alisema misingi imara imeshawekwa kusaidia hifadhi ya jamii kuelekea dira ya taifa ya kuwa na kipato cha kati ifikapo mwaka 2025.
DSC_0349

NHIF YAZUNGUMZIA TUZO TATU ZA UBUNIFU BARANI AFRIKA ZILIZOTOLEWA NA SHIRIKISHO LA KIMATAIFA LA TAASISI ZA HIFADHI YA JAMII(ISSA)KWA MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA

1Bima ya Afyaaa
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa NHIF Bw. Khamis Mdee wa pili kutoka kulia akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya mfuko huo wakati walipoonyesha tuzo ambazo mfuko huo ulitunukiwa nchini Morocco na Shirikisho la kimataifa la Taasisi za Hifadhi ya Jamii (ISSA) nchini Morocco hivi karibuni. kulia ni Mkurugenzi wa Uendeshaji (NHIF),Eugen Mikongoti, Kutoka kushoto Kaimu Mkurugenzi Tiba na Ushauri wa NHIF, Dk Mkwabi Fikirini na Mkurugenzi wa masoko na Utafiti NHIF,Raphael Mwamoto wakiwa katika mkutano huo uliozungumzia tuzo hizo.
Bima ya Afya
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa NHIF Bw. Khamis Mdee wa pili pamoja na wakurugenzi wa shirika hilo kulia Mkurugenzi wa Uendeshaji (NHIF),Eugen Mikongoti, Kutoka kushoto Kaimu Mkurugenzi Tiba na Ushauri wa NHIF, Dk Mkwabi Fikirini na Mkurugenzi wa masoko na Utafiti NHIF,Raphael Mwamoto wakionyesha tuzo zilizokabidhiwa kwa mfuko huo kutoka Shirikisho la kimataifa la Taasisi za Hifadhi ya Jamii (ISSA) nchini Morocco hivi karibuni
....................................................................................................................

Kwa miaka mingi sasa, Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya umekuwa mwanachama wa mashirikisho mbalimbali ya kimataifa ikiwemo Shirikisho la kimataifa la Taasisi za Hifadhi ya Jamii (ISSA), Shirikisho la Hifadhi ya Jamii la Nchi za Afrika Mashariki na Kati (ECASSA), na Shirikisho la kimataifa la Uchumi wa Afya (IHEA). 

Mashirikisho haya husaidia katika kubadilishana uzoefu katika maeneo mbalimbali, ushauri wa kitaalamu, viwango vya huduma, miongozo ya kiutendaji pamoja na kutumika kama jukwaa kwa wanachama kujenga na kuhamasisha mifumo endelevu katika hifadhi ya jamii. 

Taasisi hizi za kimataifa vilevile huhusika katika kutoa tuzo kwa Taasisi ambazo zinafanya vizuri katika ubunifu katika maeneo mbalimbali.

Shirikisho la kimataifa la Taasisi za Hifadhi ya Jamii (ISSA) limekuwa na utaratibu wa kushindanisha mifuko ya hifadhi ya jamii duniani kwenye maswala ya ubunifu katika maeneo mbalimbali ya kiutendaji yakiwemo; kuboresha huduma, utawala bora, matumizi ya teknolojia, ukusanyaji wa michango na matekelezo, uwekezaji, kufikisha huduma kwa wananchi waliyo sehemu ngumu kufikika, uhamasishaji wa Afya na uepushaji wa hatari makazini, pamoja na utekelezaji wa tathmini za uhai wa mifuko. Mashindano haya yalianza tangu mwaka 2008 na hufanyika kila baada ya miaka mitatu.

Tangu kuanzishwa kwa tuzo hizi, Mfuko umekuwa ukishinda tuzo katika maeneo mbalimbali. Mwaka 2008 Mfuko ulishinda tuzo moja ya ubunifu katika kuboresha huduma na mawasiliano kwa wanachama kupitia siku ya wadau (Clients Days).  

Mwaka 2011 Mfuko ulishinda tuzo nne katika masuala yafuatayo; Uboreshaji wa kitita cha mafao yanayotolewa na Mfuko; Usimamizi wa Mfuko wa Afya ya Jamii: katika kupanua wigo na jitihada za kufikia lengo la afya kwa Watanzania wote; Utoaji wa mikopo ya vifaa tiba na Uboreshaji wa majengo inayotolewa na Mfuko; Ugatuzi wa shughuli za Mfuko kwa kufungua ofisi za mikoa kuwasogezea huduma wananchi: Usimamizi bunifu kuongeza ufanisi katika utendaji.  

Kwa mara nyingine Mfuko umeshinda tuzo tatu za ubunifu katika sekta ya hifadhi ya Jamii Barani Afrika katika sherehe za kukabidhi tuzo hizo zilizofanyika tarehe 3 Disemba 2014 katika hoteli ya Sheraton mjini Casablanca, Morocco. Tuzo ambazo NHIF ilikabidhiwa ni katika eneo la utoaji wa huduma za matibabu za kibingwa maeneo magumu kufikika, kazi ambayo Mfuko umekuwa ukifanya kwa kushirikiana na wataalamu wa hospitali za rufaa nchini tangu mwaka 2012.

Tuzo nyingine ni katika eneo la TEHAMA katika utayarishaji pamoja na uwasilishaji wa madai ulioanzishwa kwa dhumuni la kupunguza malalamiko ya baadhi ya vituo vya Afya kuchelewa kulipwa madai yao. Kupitia mfumo huu, muda wa ulipaji wa madai hasa katika hospitali kubwa nchini umepungua kwa kiasi kikubwa sana. Mfumo huu ulianza tangu Januari 2012. Tuzo ya tatu ni juu ya huduma za matibabu kwa wanachama wastaafu ambayo imeanza tangu mwaka 2011.

 Fao la wastaafu linalenga kuwapa wananchi ambao walikuwa wanachama wa Mfuko na wenza wao uwezo wa kutibiwa kupitia Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya baada ya kustaafu ajira mpaka mwisho wa maisha
Mfuko utaendelea kufuata miongozo inayotolewa na mashirika ya kimataifa ili kutekeleza shughuli zake kiufanisi na kuhakikisha unatoa huduma bora kwa wanachama wake.  

Mfuko vilevile unadhamiria kuendelea kuboresha shughuli zake ili uweze kukidhi viwango vya kimataifa vinavyotolewa na Shirika la viwango la kimataifa (ISO) na hatimaye kuthibitishwa kwa kutimiza viwango hivyo katika kipindi kifupi kijacho.  

NHIF Mfuko pia unatarajia kwa kipindi kijacho kuweza kukidhi viwango vilivyowekwa na Shirikisho la kimataifa la Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (ISSA) na kupata ithibati ya kukidhi viwango vya kimataifa.

KAMANI AFUNGUA SEMINA KUHUSU MAKABILA YA ASILI

001
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi , Dk Titus Kamani akifungua semina ya siku mbili ya kimataifa inayozungumzia makabila ya asili, haki zao na namna ya kuboresha maisha na mifumo ya chakula . Semina hiyo inayofanyika Hoteli ya Kunduchi jijini Dar es Salaam inajiandaa kwa kongamano la dunia nzima kuhusiana na jamii za asili ambalo litafanyika Roma Italia, Februari 2015.(PICHA NA PHILEMON SOLOMON).
002
Mwakilishi Shirika la Kimataifa la maendeleo ya Kilimo, IFAD, Bw.Francisco Pichon akisisitiza jambo wakati wa kongamano hilo.
003
Washiriki wa semina hiyo kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika wakisikiliza kwa makini mada mbalimbali zilizotolewa kuhusu haki za makabila ya asili na namna ya kuboresha maisha yao na mifumo ya chakula .
004
005
006
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi , Dk Titus Kamani (Mb) akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau wa kongamano hilo.

VIPAJI VINGI VINAPOTEA KWENYE MICHEZO BILA KUENDELEZWA

Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Tabora na mfadhili wamashindano ya Gulamali Cup Seif Hamis Gulamali kulia akiwa na katibu
mkuu Jumuiya ya UVCCM Taifa Sixtus Mapunda Kushoto.
mfadhili wa mashindano ya Gulamali Cup Seif Hamis
Gulamali akitoa nasaha zake kwenye mashindano hayo mara baada ya
hitimisho.(Picha zote na Hastin Liumba).


Na Hastin Liumba,Igunga
MCHEZO wa soka ni kati ya michezo inayopendwa zaidi duniani katika ya michezo yote ninayoifahamu ukiachia mchezo wa Mieleka ambao nao unafuatia kwa karibu kwa na wapenzi wengi.

Aidha licha ya kupendwa na watu mbalimbali kwa rika zote bado, soka linaoongoza kwa kuwa na faida kubwa zaidi kwa masuala ya kifedha na kimaisha.

Lakini pamoja na kupendwa mchezo huo tumekuwa tukishuhudia vipaji mbalimbali kwenye soka la vijana wadogo chini ya miaka 17 lakini haviendelezwi.

Vipaji hivyo vimekuwa vikionekana kwenye mashindano ya Copa Coca-Cola,umoja wa michezo kwa shule za sekondari Tanzania (UMISSETA) umoja wa michezo na Taaluma kwa shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA).

Hayo ni maneno ya mdau wa michezo na mwenyekiti wa (UVCCM) mkoa wa Tabora Seif Hamis Gulamali aliyosema wakati akifanya mahojiano na mwandishi wa makala hii mara baada ya mashindano ya ‘Gulamali Cup’ kumalizika wilayani Igunga.

Gulamali alisema alianzisha mashindano ya Gulamali Cup wilayani Igunga kwa lengo la kulinda vipaji vilivyopo ambavyo kimsingi vimekuwa vikipotea bila kuendelezwa.

Alisema bado tuna safari ndefu kufikia malengo ya kuwekeza kwenye soka letu la Tanzania kwani hakuna mipango ya kutunza vipaji vya vijana wetu vilivyo.

Alisema wenzetu waliofanikiwa wamewekeza kwenye soka la vijana wadogo lakini sisi tumekuwa tukishindwa kutunza vipaji vya vijana wetu hasa wale walio chini ya umri wa miaka 17.

Aidha anasema ipo haja tukaanzisha vituo maalumu vya vijana hususani soka ili vijana wanaoonyesha uwezo na vipaji waweze kuendelezwa.

Gulamali anasema hakuna ubishi kuwa soka ni ajira hivyo kama tunaamini hilo basi ipo haja ya kutengeneza njia ili kunusuru vipaji vya vijana wetu ambavyo hakuna ubishi vinapotea.

Kuanzisha mashindano ya Gulamali Cup.

Gulamali anabainisha kuwa alianzisha mahindano ya Gulamali Cup si tu kuwaweka vijana karibu kimahusiano bali kulinda vipaji ambavyo ni dhahiri vipo.

Anasema mashindano ya Gulamali Cup aliyaanzisha mwaka 2013 ambayo ilikuwa ni kwa mara ya kwanza yanafanyika wilayani Igunga.

Aidha anabainisha mwaka 2014 mashindano hayo ameyaendeleza kwa kufadhili kila kitu na kushirikisha ngazi za vijiji,kata na Tarafa.

Alisema mashindano ya Gulamali Cup yalianza kutimua vumbi mwezi Agosti 23,2014 kwa kushikisha timu nane toka kila kata ambapo wilaya ya Igunga kuna kata 26.

Aidha aliongeza kila timu kulikuwa na wachezaji 15 na kufanya idadi ya wachezaji walioshiriki mashindano ya Gulamali Cup kuwa ni wachezaji 390.

Timu zilizoshiriki mashindano hayo.

Mratibu wa mashindano ya Gulamali Cup Mathias Igese anasema tarafa ya Igunga ilitoa timu mbili zilizoingia fainali ambazo ni Bafana bafana Mbutu na Igunga Worriors.

Aidha katika fainali hiyo timu ya Igunga Worriors ilitwaa ubingwa wa mashindano ya Gulamali Cup kwa kuwalaza timu ya BafanaBafana iliyoshika nafasi ya Pili kwa jumla ya magoli 3-0 na mshindi wa Tatu ni timu ya Mto FC.

Zawadi za fainali.

Mratibu huyo anasema katika mashindano ya Gulamali Cup zawadi kwa bingwa wa fainali hiyo kwa timu ya Igunga Worriors alijinyakulia kikombe na sh 300,000,mshindi wa pili sh 200,000 na mshindi wa tatu sh 100,000.

Mashindano ngazi ya kata.

Mashindano haya ngazi ya kata Gulamali anasema mshindi wa kwanza kwa kila kata alipata zawadi ya seti moja na jezi yenye thamani ya sh 200,000 na mipira mwili yenye thamani ya sh 200,000.

Alisema washindi wa kila kata zawadi walizopata ni sh milioni 10,400,000 ukijumuisha zawadi za kila kata.

Sekondari za kata.

Gulamali anabainisha kuwa alitembelea kama ziara katika shule za sekondari za Kata na kutoa mipira mitatu kwa michezo ya mpira wa Pete,Volebo na mpira wa Miguu.

Alisema thamani ya mipira hiyo ni sh 400,000 ambapo jumla ya sekondari za zilizopo wilaya ya Igunga ni 33 na hivyo kufanya msaada huo kufikia sh milioni 13.2.

Mashindano ngazi ya Tarafa.

Anabinisha mashindano ya Gulamali Cup hayakuishia ngazi ya kata bali yaliendelea hadi ngazi ya Tarafa na kufanikiwa kutoa washindi wa ngazi hiyo na kuna Tarafa nne za tarafa ya Simbo,Manonga,Igurubi na Igunga.

Alisema kwa kila tarafa zawadi kwa washindi wa kwanza alipata Kikombe kikiwa na thamani ya sh 200,000,mshindi wa pili sh 200,000 na mshindi wa tatu sh 100,000.

Alisema ya zawadi hizo kwa kila kata ni sh 800,000 ambazo jumla ya gharama hiyo kwa Tafara nne ni sh milioni 3,200,000 na kufanya jumla ya gharama kuu ni sh milioni 26,800,000.

Aidha mfadhili huyo alitoa zawadi kwa marefa wanne waliochezesha mechi ya fainali sh 10,000 kila mmoja kwa kuchezesha mechi kwa kufuata sheria 17 za soka.

Aidha alisema amejipanga kupitia mashindano hayo amejipanga vyema kuendeleza mashindano hayo ili kulinda vipaji lakini pia mikakati iliyopo ni kuhakikisha kwenye mashindano yajayo ya Copa Coca-Cola bingwa atoke wilaya ya Igunga.

Nidhamu kwenye michuano hiyo.

Aidha alipongeza kwa dhati kwa timu zote zilizoshiriki ngazi zote kwa kuonyesha nidhamu ya hali ya juu.

“Napongeza kwa dhati kabisa kwani nidhamu mliyoonyesha kwenye mashindano haya kwani bila nidhamu kwenye mchezo wowote ule hayaendi”.alisema

Apongeza ushiriki wa timu.

Alisema amefarijika sana kuona ushiriki wa timu zote jinsi ulivyofanikiwa kwenye mashindano ya Gulamali Cup kwani imedhirisha ubora wake.

Alisema amejiridhirisha jinsi vijana alivyoafanikiwa kuwaweka karibu kwani michezo ni furaha,ajira na afya na kwamba kuanzisha mashindano hayo hayakuwa na itikadi za vyama yamejumuisha vijana wote.

Mgeni rasmi apongeza.

Katika mashindano hayo mgeni rasmi alikuwa ni katibu mkuu UVCCM taifa Sixtus Mapunda ambaye bila kusita alipongeza kwa dhati na kudai ni mfano wa kuigwa nchini.

Alisema katika fainali iliyohusisha timu Igunga Worriors na BafanaBafana Mbutu ameshudia vipaji vikubwa ambavyo kimsingi vinapaswa kuendelezwa.

Alisema na kuishauri shirikisho la soka kuweka utaratibu maalumu wa kutembelea wilayani kuangali vipaji vitakavyoibuliwa na kuviendeleza kwa maslahi ya taifa.

hastinliumba@gmail.com-0788390788.

Tuesday, December 16, 2014

ACT KUMBURUZA MKURUGENZI MAHAKAMANI -KIGOMA

Na Magreth Magosso Kigoma.

UONGOZI  wa chama cha Alliance for change and Transparency (ACT) mkoa wa Kigoma umeahidi kuifikisha ofisi ya mkurugenzi wa wilaya ya Kigoma mahakamani endapo hatua za maksudi hazita chukuliwa kunusuru  uchaguzi wa Kata ya Kagunga uliositishwa wakati wa uchaguzi.

Kauli hiyo imekuja baada ya  Msimamizi msaidizi aliyejulikana kwa jina moja la Mtisi kuiandikia barua chama cha ACT wametolewa katika uchaguzi huo kutokana na makosa mbalimbali katika kujaza fomu husika.

Akifafanua  hilo nje ya ofisi ya mkuu wa wilaya ya kigoma Ramadhan Maneno alisema hujuma imepangwa baina ya chama tawala na ofisi ya mkurugenzi kwa kushirikiana na mwanasheria wa halmashauri husika kwa mujibu wa barua ya siri walioikamata ndani ya ofisi ya usimamizi wa uchaguzi.

Alisema awali baada ya kupata barua hiyo Novemba 28 mwaka huu uongozi wa chama hicho  ulikata rufaa ambapo kwa mujibu wa kamati ya rufaa ya wilaya ulitupilia mbali rufaa hiyo kwa kuwa ilikuwa nje ya muda wa kupokea rufaa.

Rufaa haikusikilizwa na chama hicho kilitolewa katika orodha ya vyama vitakavyopigiwa kura katika kijiji cha Zashe Kata ya Kagunga wilaya ya Kigoma ambapo kitendo hicho kilizua hamaki kwa wananchi na  uchaguzi kuhairishwa kwa hila za watu wachache.

Kwa nyakati tofauti wakielezea kwa uchache Mkurugenzi wa wilaya Michael Mwandezi na Mwanasheria wake Idd Ndabhona walisema mchakato wa upigaji kura una dosari nyingi na kushauri vyama vya upinzani wachukue hatua za kisheria.

BALOZI SEIF AFUNGUA MKUTANO WA HIFADHI NA KUELEZEA MAONO YA TAIFA

DSC_0005
Wageni mbalimbali wanaoshiriki mkutano mkubwa wa kimataifa wa hifadhi ya jamii ulioandaliwa na serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Fedha ulioanza leo katika kituo cha kimataifa cha mikutano cha Arusha (AICC) wakifanya usajili kabla ya kuanza kwa mkutano huo. (Picha zote na Zainul Mzige wa MOblog).

Na Mwandishi wetu
MAKAMU wa pili wa rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, amesema mpango wa serikali ya Tanzania wa hifadhi ya jamii ndio msingi wa sera ya kuondoa umaskini miongoni mwa watu wake ili kulifanya taifa kuwa la kipato cha kati ifikapo 2025.

Kauli hiyo imetolewa leo wakati akifungua mkutano mkubwa wa kimataifa wa hifadhi ya jamii ulioandaliwa na serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Fedha na wadau wengine kwa lengo la kubadilishana uzoefu juu ya nini cha kufanya kusaidia makundi maalumu katika jamii.

Katika Mkutano huo wa siku tatu unafanyika Katika kituo cha kimataifa cha mikutano cha Arusha (AICC) serikali imefanya maandalizi kwa kushirikiana na mashirika ya kimataifa kama UNICEF, ILO, UNAIDS na taasisi ya utafiti wa sera za kiuchumi yenye makao makuu nchini Afrika Kusini (EPRI).

Imeelezwa kuwa mkutamo huo umelenga kuchota maarifa mema kutoka Afrika Kusini ya namna ya kutengeneza sera za kuhudumia makundi maalumu ya wanawake, watoto, wazee, wasiojiweza na vijana ili kuboresha maisha yao, ikiwa ni sehemu ya mpango mkakati wa serikali wa kuinua kiwango cha maisha miongoni mwa wananchi wake.
DSC_0022
Mkurugenzi msaidizi Mkuu wa Shirika la Kazi duniani na Mkurugenzi wa kanda ya Afrika Aeneas C. Chuma (kulia) akiwasili kushiriki mkutano huo akiwa ameambatana na Afisa Habari wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) Tanzania, Bw. Magnus Minja (kulia) pamoja na Luis Frota kutoka ILO Afrika Kusini.

Balozi Seif Ali Iddi, alisema kwa kuzingatia nia ya serikali ya kuwa taifa lenye kipato cha kati mwaka 2025 serikali inaona haja ya kuangalia sera ili iweze kutoa haki kwa makundi yote kuelekea ustawi wa jamii ifikapo mwaka huo..

“Serikali imechukua hifadhi ya jamii kama mkakati wa kufikia dira ya ukuaji na maendeleo nchini. Kongamano hili limekusudia kuhakikisha kwamba muono unatengeneza hatua stahiki zinazotekelezeka kitaifa kukabiliana na changamoto za umaskini hivyo kuhakikisha ukuaji wa uchumi unakuwa endelevu na wenye maana kwa wananchi” alisema.

Alisema ili kufikia lengo hilo la uchumi endelevu, serikali inataka kuhakikisha wananchi wake wakiwemo wale maskini na wasiojiweza wanawezeshwa ili kutambua haki zao na kuifanya Tanzania kuwa taifa lenye nguvu na linalotoa haki sawa kwa wote.

Aidha kuwa taifa linaloangalia mahitaji ya watoto wake kama lishe, afya na elimu ili kuwasaidia kukua kwa furaha, kuwa wazalishaji na kukwepa mtego wa umaskini unazinga kizazi kwa kizazi.
DSC_0026
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania Hoyce Temu (kulia) akimwongoza Mkurugenzi msaidizi Mkuu wa Shirika la Kazi duniani na Mkurugenzi wa kanda ya Afrika Aeneas C. Chuma kuelekea kwenye chumba maalum cha wageni mashuhuri kabla ya kuanza kwa mkutano. Katikati ni Afisa Habari wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) Tanzania, Bw. Magnus Minja.

Balozi Iddi alisema kwamba amefurahi kuona kwamba ajenda za mkutano pia zimegusia kuzungumzia uimarishaji wa utendaji wa pamoja kati ya mipango ya hifadhi ya jamii kama TASAF, Mfuko wa afya ya jamii (CHF) na huduma za jamii zinazotolewa na wizara husika kama wizara ya elimu, afya, maji nakadhalika.

Hata hivyo aliwataka washiriki kuangalia ukusanyaji wa takwimu kuhusu masuala ya hifadhji ya jamii kwani kwa hali ilivyo sasa ukusanyaji huo si mzuri na unazuia maendeleo na uimarishaji wa huduma za jamii.

Alisema ipo haja ya kuboresha mazingira ya utawala ili kuwezesha kuimarisha hifadhi kwa wale waliokwishaipata, kubadili sheria ili kuwaingiza na wale ambao hawajapata huduma za hifadhi ya jamii.

Aliwataka washiriki kuangalia kwa makini changamoto zinazoikumba Afrika na Tanzania katika masuala ya hifadhi na kutolea majibu.
DSC_0030
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kulia) akisalimiana na Mkurugenzi msaidizi Mkuu wa Shirika la Kazi duniani (ILO) na Mkurugenzi wa kanda ya Afrika Aeneas C. Chuma.
Alizitaja baadhi ya changamoto hizo kuwa ni umaskini uliotapakaa ambao unasababisha watu kushindwa kupeleka michango katika hifadhi, misingi ya ukataji kodi ambayo huleta mushkeri kwa fedha za hifadhi, kuwepo kwa kundi kubwa lisilo katika sekta rasmi ya ajira na hivyo kupunguza idadi ya wachangaji katika prgramu zinazohitaji michango mfululizo na mabadiliko ya tabia nchi yanayotishia kuyumba kwa kilimo na ufugaji ambao ndio msingi wa mapato kwa wananchi wengi.

Alisema pia mabadiliko ya tabia nchi yanasababisha milipuko ya magonjwa mbalimbali kama Malaria na magonjwa mengine mapya kama Ebola na Dengue.

Changamoto nyingine ni kuwepo na gharama kubwa za utawala hasa katika siku za mwanzo za uanzishwaji wa mifuko ya hifadhi.

Mkutano huo wenye washiriki zaidi ya 150 una watu wa kariba mbalimbali wakiwemo watengeneza sera, watafiti na waendeshaji wa mifuko ya hifadhi kutoka mataifa ya Kenya, Uganda, Bangladesh, Mozambique, Lesotho, Malawi, Afrika Kusini, Ghana, Ethiopia, Zambia, Sudan Kusini na wenyeji Tanzania.
DSC_0033
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kushoto) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi msaidizi Mkuu wa Shirika la Kazi duniani na Mkurugenzi wa kanda ya Afrika Aeneas C. Chuma kabla ya kuwasili kwa mgeni rasmi Balozi Seif Ali Iddi.

Mkutano huo unatarajiwa kutoa mwelekeo wa namna ambavyo Tanzania inaweza kuanzisha mfumo wa hifadhi kwa ajili ya watu maskini na wale wenye mahitaji maalumu ili kuwawezesha kupata huduma za afya, elimu na kipato.

Naye Mkurugenzi msaidizi Mkuu wa Shirika la Kazi duniani na Mkurugenzi wa kanda ya Afrika Aeneas C. Chuma, amesema Umoja wa Mataifa umefurahishwa na kuwapo kwa kongamano hilo kwani suala la hifadhi ni msingi wa maendeleo katika uchumi wowote endelevu.

Alisema kuwapo kwa Hifadhi ya jamii inayoeleweka na yenye msingi imara husaidia wananchi kukabiliana na mabadiliko yoyote yale ya kiuchumi katika taifa lao.

Alisema shirika hilo katika miaka yote 95 ya uwapo wake inapigania hifadi ya jamii kama njia salama ambayo inahakikisha ukuaji wa jamii unaozingatia uwapo wa jamii inayozingatia ukuaji wa uchumi wenye haki kwa kila mmoja.
DSC_0065
Waziri wa Fedha, Mh. Saada Mkuya Salum (kushoto) akiwasili kwenye viwanja vya AICC jijini Arusha kushiriki mkutano mkubwa wa kimataifa wa hifadhi ya jamii ulioandaliwa na serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Fedha huku akiwa ameongozana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dr. Servacius Likwelile (katikati) pamoja na Mwakilishi wa UNICEF Tanzania, Jama Gulaid.

Pamoja na mafanikio ya dunia katika masuala ya afya na elimu, Mwakilishi huyo ameelezea changamoto kubwa inayokabili Tanzania ambayo ni vijana wengi kuingia katika soko la ajira ambalo ni finyu.

Mwakilishi huyo amesema kwamba kuanzia mwaka ujao hadi 2030 nchi za Afrika Kusini mwa jangwa la sahara wanatakiwa kutengeneza nafasi milioni 5 za kazi kila mwaka ili kuendana na ukuaji wa soko la wasaka ajira.

Alisema kutokana na ukweli huo hatua ya sasa ya Tanzania kutaka kuwa na msingi imara ya hifadhi ya jamii ni muhimu sana ili kukabiliana na mabadiliko yanayokuja katika afya, elimu na ajira.

Wakati huo huo Mratibu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mkurugenzi mkazi wa UNDP Alvaro Rodriguez amesema hifadhi ya jamii ni kitu muhimu kinachofanya watengeneza sera kukaa pamoja kuona namna nzuri ya kufanikisha masuala hayo.
DSC_0086
Waziri wa Fedha, Mh. Saada Mkuya Salum (katikati) akiwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mhe. Dkt. Shukuru Kawambwa (kushoto) pamoja na Naibu waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Mhe. Dkt. Pindi Chana wakielekea kumpokea mgeni rasmi Makamu wa pili wa rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Iddi.

Alisema matukio mbalimbali yanayoharibu ustawi wa jamii kama kuporomoka kwa uchumi duniani, mabadiliko kwenye tabianchi kumefanya kuwepo na haja ya kuhakikisha kwamba kuna misingi imara ya kutoa hifadhi kwa wananchi na kuboresha maisha yao.

Akizungumza katika mkutano huo kabla ya Makamu wa rais kuhutubia, Alvaro alisema kuna changamoto kubwa zinazokabili dunia.

Alipongeza serikali ya Tanzania kwa kuona haja ya kushirikiana na wadau wengine kuona namna bora ya kukabiliana na changamoto za maendeleo katika lengo la kuhakikisha kunauwezeshaji wenye lengo la kuwezesha ustawi wa jamii.

Alisema mada zitakazojadiliwa zitawezesha mwishoni mwa mkutano kuwapo na maazimio yenye kuwezesha kutengenezwa kwa mising bora ya hifadhi ya jamii ili kuwezesha maono ya maendeleo kufikiwa.

Mratibu huyo pia alielezea kuridhishwa kwake na mafanikio yanayopatikana nchini Tanzania kupitia TASAF ya kukabiliana na umaskini uliokithiri na kutoa nafasi ya maskini kuwa na uwezo wa kusonga mbele katika maendeleo ili kufikia maono ya taifa ya maendeleo endelevu yanayojali watu wote 2025 wakati taifa litakapokuwa la kipato cha kati.
DSC_0118
Mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa mkutano mkubwa wa kimataifa wa hifadhi ya jamii ulioandaliwa na serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Fedha, Makamu wa pili wa rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Iddi akisalimiana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dr. Servacius Likwelile mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya AICC jijini Arusha leo.
DSC_0120
Makamu wa pili wa rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Iddi , akisalimiana na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez alipowasili kwenye ufunguzi wa mkutano wa kimataifa wa hifadhi ya jamii.
DSC_0127
Mgeni rasmi Makamu wa pili wa rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Iddi akisalimiana na Mwakilishi wa Shirika la watoto duniani (UNICEF), Jama Gulaid.
DSC_0132
Mgeni rasmi Makamu wa pili wa rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Iddi (katikati) akiwa na Waziri wa Fedha, Mh. Saada Mkuya Salum pamoja na mwenyeji wao Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda wakielekea kwenye ukumbi wa mikutano.
DSC_0312
Picha juu na chini ni mgeni rasmi Makamu wa pili wa rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Iddi, akifungua mkutano mkubwa wa kimataifa wa hifadhi ya jamii ulioandaliwa na serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Fedha na wadau wengine kwa lengo la kubadilishana uzoefu juu ya nini cha kufanya kusaidia makundi maalumu katika jamii ulioanza leo jijini Arusha.
DSC_0328
Kwa picha zaidi ingia humu