UONGOZI
wa chama cha Alliance for change and Transparency (ACT) mkoa wa Kigoma
umeahidi kuifikisha ofisi ya mkurugenzi wa wilaya ya Kigoma mahakamani endapo
hatua za maksudi hazita chukuliwa kunusuru
uchaguzi wa Kata ya Kagunga uliositishwa wakati wa uchaguzi.
Kauli hiyo imekuja baada ya Msimamizi msaidizi aliyejulikana kwa jina moja
la Mtisi kuiandikia barua chama cha ACT wametolewa katika uchaguzi huo kutokana
na makosa mbalimbali katika kujaza fomu husika.
Akifafanua hilo nje ya ofisi ya mkuu wa wilaya ya kigoma
Ramadhan Maneno alisema hujuma imepangwa baina ya chama tawala na ofisi ya
mkurugenzi kwa kushirikiana na mwanasheria wa halmashauri husika kwa mujibu wa
barua ya siri walioikamata ndani ya ofisi ya usimamizi wa uchaguzi.
Alisema awali baada ya kupata barua hiyo Novemba
28 mwaka huu uongozi wa chama hicho ulikata
rufaa ambapo kwa mujibu wa kamati ya rufaa ya wilaya ulitupilia mbali rufaa
hiyo kwa kuwa ilikuwa nje ya muda wa kupokea rufaa.
Rufaa haikusikilizwa na chama hicho
kilitolewa katika orodha ya vyama vitakavyopigiwa kura katika kijiji cha Zashe
Kata ya Kagunga wilaya ya Kigoma ambapo kitendo hicho kilizua hamaki kwa wananchi
na uchaguzi kuhairishwa kwa hila za watu
wachache.
Kwa nyakati tofauti wakielezea kwa uchache Mkurugenzi
wa wilaya Michael Mwandezi na Mwanasheria wake Idd Ndabhona walisema mchakato
wa upigaji kura una dosari nyingi na kushauri vyama vya upinzani wachukue hatua
za kisheria.
No comments:
Post a Comment