Pages

KAPIPI TV

Wednesday, December 17, 2014

VIPAJI VINGI VINAPOTEA KWENYE MICHEZO BILA KUENDELEZWA

Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Tabora na mfadhili wamashindano ya Gulamali Cup Seif Hamis Gulamali kulia akiwa na katibu
mkuu Jumuiya ya UVCCM Taifa Sixtus Mapunda Kushoto.
mfadhili wa mashindano ya Gulamali Cup Seif Hamis
Gulamali akitoa nasaha zake kwenye mashindano hayo mara baada ya
hitimisho.(Picha zote na Hastin Liumba).


Na Hastin Liumba,Igunga
MCHEZO wa soka ni kati ya michezo inayopendwa zaidi duniani katika ya michezo yote ninayoifahamu ukiachia mchezo wa Mieleka ambao nao unafuatia kwa karibu kwa na wapenzi wengi.

Aidha licha ya kupendwa na watu mbalimbali kwa rika zote bado, soka linaoongoza kwa kuwa na faida kubwa zaidi kwa masuala ya kifedha na kimaisha.

Lakini pamoja na kupendwa mchezo huo tumekuwa tukishuhudia vipaji mbalimbali kwenye soka la vijana wadogo chini ya miaka 17 lakini haviendelezwi.

Vipaji hivyo vimekuwa vikionekana kwenye mashindano ya Copa Coca-Cola,umoja wa michezo kwa shule za sekondari Tanzania (UMISSETA) umoja wa michezo na Taaluma kwa shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA).

Hayo ni maneno ya mdau wa michezo na mwenyekiti wa (UVCCM) mkoa wa Tabora Seif Hamis Gulamali aliyosema wakati akifanya mahojiano na mwandishi wa makala hii mara baada ya mashindano ya ‘Gulamali Cup’ kumalizika wilayani Igunga.

Gulamali alisema alianzisha mashindano ya Gulamali Cup wilayani Igunga kwa lengo la kulinda vipaji vilivyopo ambavyo kimsingi vimekuwa vikipotea bila kuendelezwa.

Alisema bado tuna safari ndefu kufikia malengo ya kuwekeza kwenye soka letu la Tanzania kwani hakuna mipango ya kutunza vipaji vya vijana wetu vilivyo.

Alisema wenzetu waliofanikiwa wamewekeza kwenye soka la vijana wadogo lakini sisi tumekuwa tukishindwa kutunza vipaji vya vijana wetu hasa wale walio chini ya umri wa miaka 17.

Aidha anasema ipo haja tukaanzisha vituo maalumu vya vijana hususani soka ili vijana wanaoonyesha uwezo na vipaji waweze kuendelezwa.

Gulamali anasema hakuna ubishi kuwa soka ni ajira hivyo kama tunaamini hilo basi ipo haja ya kutengeneza njia ili kunusuru vipaji vya vijana wetu ambavyo hakuna ubishi vinapotea.

Kuanzisha mashindano ya Gulamali Cup.

Gulamali anabainisha kuwa alianzisha mahindano ya Gulamali Cup si tu kuwaweka vijana karibu kimahusiano bali kulinda vipaji ambavyo ni dhahiri vipo.

Anasema mashindano ya Gulamali Cup aliyaanzisha mwaka 2013 ambayo ilikuwa ni kwa mara ya kwanza yanafanyika wilayani Igunga.

Aidha anabainisha mwaka 2014 mashindano hayo ameyaendeleza kwa kufadhili kila kitu na kushirikisha ngazi za vijiji,kata na Tarafa.

Alisema mashindano ya Gulamali Cup yalianza kutimua vumbi mwezi Agosti 23,2014 kwa kushikisha timu nane toka kila kata ambapo wilaya ya Igunga kuna kata 26.

Aidha aliongeza kila timu kulikuwa na wachezaji 15 na kufanya idadi ya wachezaji walioshiriki mashindano ya Gulamali Cup kuwa ni wachezaji 390.

Timu zilizoshiriki mashindano hayo.

Mratibu wa mashindano ya Gulamali Cup Mathias Igese anasema tarafa ya Igunga ilitoa timu mbili zilizoingia fainali ambazo ni Bafana bafana Mbutu na Igunga Worriors.

Aidha katika fainali hiyo timu ya Igunga Worriors ilitwaa ubingwa wa mashindano ya Gulamali Cup kwa kuwalaza timu ya BafanaBafana iliyoshika nafasi ya Pili kwa jumla ya magoli 3-0 na mshindi wa Tatu ni timu ya Mto FC.

Zawadi za fainali.

Mratibu huyo anasema katika mashindano ya Gulamali Cup zawadi kwa bingwa wa fainali hiyo kwa timu ya Igunga Worriors alijinyakulia kikombe na sh 300,000,mshindi wa pili sh 200,000 na mshindi wa tatu sh 100,000.

Mashindano ngazi ya kata.

Mashindano haya ngazi ya kata Gulamali anasema mshindi wa kwanza kwa kila kata alipata zawadi ya seti moja na jezi yenye thamani ya sh 200,000 na mipira mwili yenye thamani ya sh 200,000.

Alisema washindi wa kila kata zawadi walizopata ni sh milioni 10,400,000 ukijumuisha zawadi za kila kata.

Sekondari za kata.

Gulamali anabainisha kuwa alitembelea kama ziara katika shule za sekondari za Kata na kutoa mipira mitatu kwa michezo ya mpira wa Pete,Volebo na mpira wa Miguu.

Alisema thamani ya mipira hiyo ni sh 400,000 ambapo jumla ya sekondari za zilizopo wilaya ya Igunga ni 33 na hivyo kufanya msaada huo kufikia sh milioni 13.2.

Mashindano ngazi ya Tarafa.

Anabinisha mashindano ya Gulamali Cup hayakuishia ngazi ya kata bali yaliendelea hadi ngazi ya Tarafa na kufanikiwa kutoa washindi wa ngazi hiyo na kuna Tarafa nne za tarafa ya Simbo,Manonga,Igurubi na Igunga.

Alisema kwa kila tarafa zawadi kwa washindi wa kwanza alipata Kikombe kikiwa na thamani ya sh 200,000,mshindi wa pili sh 200,000 na mshindi wa tatu sh 100,000.

Alisema ya zawadi hizo kwa kila kata ni sh 800,000 ambazo jumla ya gharama hiyo kwa Tafara nne ni sh milioni 3,200,000 na kufanya jumla ya gharama kuu ni sh milioni 26,800,000.

Aidha mfadhili huyo alitoa zawadi kwa marefa wanne waliochezesha mechi ya fainali sh 10,000 kila mmoja kwa kuchezesha mechi kwa kufuata sheria 17 za soka.

Aidha alisema amejipanga kupitia mashindano hayo amejipanga vyema kuendeleza mashindano hayo ili kulinda vipaji lakini pia mikakati iliyopo ni kuhakikisha kwenye mashindano yajayo ya Copa Coca-Cola bingwa atoke wilaya ya Igunga.

Nidhamu kwenye michuano hiyo.

Aidha alipongeza kwa dhati kwa timu zote zilizoshiriki ngazi zote kwa kuonyesha nidhamu ya hali ya juu.

“Napongeza kwa dhati kabisa kwani nidhamu mliyoonyesha kwenye mashindano haya kwani bila nidhamu kwenye mchezo wowote ule hayaendi”.alisema

Apongeza ushiriki wa timu.

Alisema amefarijika sana kuona ushiriki wa timu zote jinsi ulivyofanikiwa kwenye mashindano ya Gulamali Cup kwani imedhirisha ubora wake.

Alisema amejiridhirisha jinsi vijana alivyoafanikiwa kuwaweka karibu kwani michezo ni furaha,ajira na afya na kwamba kuanzisha mashindano hayo hayakuwa na itikadi za vyama yamejumuisha vijana wote.

Mgeni rasmi apongeza.

Katika mashindano hayo mgeni rasmi alikuwa ni katibu mkuu UVCCM taifa Sixtus Mapunda ambaye bila kusita alipongeza kwa dhati na kudai ni mfano wa kuigwa nchini.

Alisema katika fainali iliyohusisha timu Igunga Worriors na BafanaBafana Mbutu ameshudia vipaji vikubwa ambavyo kimsingi vinapaswa kuendelezwa.

Alisema na kuishauri shirikisho la soka kuweka utaratibu maalumu wa kutembelea wilayani kuangali vipaji vitakavyoibuliwa na kuviendeleza kwa maslahi ya taifa.

hastinliumba@gmail.com-0788390788.

No comments: