Pages

KAPIPI TV

Friday, December 19, 2014

UKAWA WAFANYA MANDAMANO -KIBONDO

Picha kutoka maktaba
Na Magreth Magosso,Kigoma
 
WANANCHI wapatao 2,600  kati  3,000 wanaoishi  katika vijiji vitatu vinavounda Kata ya Kumsenga iliyopo wilaya ya Kibondo Mkoa wa Kigoma,wameandama kwenda ofisi za Mtendaji wa kijiji kwa madai ya kutoutambua uongozi uliochaguliwa Desemba,14, Mwaka huu.

Sbabu ya kutoutambua uongozi uliochaguliwa ni ,kutokana na wagombea wa Umoja wa Katiba ya wananchi (UKAWA) Leonard Tamwuluki , Ledbord Loki  na mwingine kupitia chama cha NCCR-Mageuzi kuenguliwa siku ya uchaguzi kwa sababu ya kushindwa kujaza  kipenge cha kwanza katika fomu ya wagombea husika.

Akifafanua hilo Katibu wa Jimbo la Muhambwe Renatus Richard alisema kata ina vijiji vitatu ambavyo ni Kibuye,mkinama na kumsenga, awali wagombea walinyimwa fomu  kabisa ndipo Mwenyeviti  Chadema wa wilaya Kalaveri Ntigita  alimshinikiza mtaendaji na wakapewa fomu bila maelekezo ya ziada kwa wagombea  siku mbili kabla ya uzinduzi wa kampeni za kuwanadi  kwa umma.

“kila tukienda kwa mtendaji wa kijiji  Clement Charles tunakuta ofisi imefungwa na tukimpata ofisini anasema hakuna fomu,sasa bila shinikizo la Ukawa wilaya mgombea wetu Ladibord Loki  asingepata fomu,siku ya kupiga kura mtendaji anasema kipengele kwa kwanza katika fomu ni batili” alisema Richard.

Akiongoza mandamano hayo Mwenyekiti  Chadema  wilaya ya Kibondo  Nicolaus Kilunga alisema serikali imepora haki ya umma,kwa kitendo cha mtendaji kutumika kuhujumu uchaguzi ni kuwanyima haki wananchi kupata viongozi bora wa kusimamia miradi mbalimbali ya maendeleo.

Viongozi walioteuliwa kupitia Chama Cha CCM  si chaguo la wengi kwa kuwa amepitishwa bila kuwepo kwa chama cha upinzani chochote na kuahidi wahusika wa sakata la kuchafua uchaguzi huo watafikishwa  mahakamani kujibu tuhuma za udanganyifu wa chaguzi hiyo.
 
Kwa upande wa mgombea wa Chadema kata ya Kumsenga Ladibord Oscar akili kunyimwa fomu  mapema na baada ya shinikizo la uongozi wa juu alipata fomu siku chache kabla ya zoezi la kampeni za kunadiwa wagombea mbaya zaidi  mtendaji hakumwelekeza namna ya kujaza fomu na hatimaye alifutwa siku ya uchaguzi.

Baadhi ya wananchi wa hapo Jason Daud na Neema Jonathan walisema hawatashirikiana na uongozi wa serikali  katika kazi na miradi ya maendeleo isipokuwa shughuli za kijamii hasa mazishi tu.huku wakitaka uchaguzi urudiwe ili wachague chaguo lao.

Mwandishi wetu  alipohitaji kupata maoni ya upande wa chama cha Nccr-Mageuzi  ambao ndio waliosimamisha wagombea wao katika vijiji hivyo hawakuweza kupatikana katika simu zao za mkononi hazikuwa hewani halikadhalika kwa Katibu mwenezi wa ccm  Mkoa wa kigoma Masud Kalembe.

No comments: