Pages

KAPIPI TV

Thursday, November 20, 2014

KINANA ASHIRIKI KILIMO KATIKA SHAMBA LA WANANCHI KIJIJI CHA MKOTOKUYANA NACHINGWEA

1Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Nachingwea Mh. Mathias Chikawe wakati alipowasili katika kijiji cha Nkotokuyana jimbo la Nachingwea katika mwendelezo wa ziara yake ya mikoa ya Lindi na Mtwara itakayomchukua siku 16 akikagua utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 inayotekelezwa na srikali kwa pamoja na wananchi huku akihimiza uhai wa Chama cha Mapinduzi katika vijiji mbalimbali , Majimbo na wilaya Katika ziara hiyo Kinana anaongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi. (PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-NACHINGWEA-LINDI) 3 Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi akizungumza na Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mhe. Regina Chonjo mara baada ya msafara wa Katibu Mkuu kuwasili katika kijiji cha Mkotokuyana 4Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliiza Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mhe. Regina Chonjo mara baada ya kufika kwenye shamba la ufuta alilolikagua leo kijijini hapo, Kulia ni Mbunge wa jimbo la Nachingwea Mh. Mathias Chikawe na kushoto ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi 5Baadhi ya akina mama wanakikundi hichi wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM huku wakiwa wameshika majembe yao. 6Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kulia na Mbunge wa jimbo la Nachingwea wakikagua shamba la Mkotokuyana 7Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kilimo katika shamba hilo huku Mbunge wa jimbo la Nachingwea Mh. Mathias Chikawe akiwa amepanda akishuhudia kazi hiyo. 8Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiendelea na kazi 9Pamoja na vumbi kubwa kutimka wakati akifanya kazi hiyo Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana aliendelea na kazi. 10Kilimo kimepamba moto 16Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa ofisi ya serikali ya kijiji cha Naipanga Nachingwea. 15Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi katika kijiji cha Naipanga 14Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa jiko la shule ya Sekondari Nachingwea High School. 12Mbunge wa jimbo la Nachingwea Mh. Mathiasa Chikawe akishiriki katika kusafisha shamba la ufuta katika kijiji cha Mkotokuyana. 11Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kung'oa visiki katika shamba la wananchi la kijiji cha Mkotokuyana wilayani Nachingwea.

Wednesday, November 19, 2014

MAMIA WAJITOKEZA MAZISHI YA MWENDESHA BODABODA,WALAANI VIKALI MAUAJI HAYO-TABORA

Baadhi ya waendesha Bodaboda Tabora mjini wakishiriki Mazishi ya Mwenzao Deogratius Elmenglid  aliyeuawa kikatili katika tukio lililotokea hivi karibuni la Uporaji pikipiki eneo la Kata ya Malolo,Mazishi hayo yamefanyika Makaburi ya Ipuli Manispaa ya Tabora





"HIVI NI NANI ANAYEFANYA MAUAJI YA BODABODA TABORA?''

Mwili wa kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Deogratius Elmengled(18)aliyeuawa kwa kuchomwa visu maeneo mbalimbali ya mwili wake huko katika Kata ya Malolo jirani na Kanisa la RC Makokola eneo ambalo waendesha Bodaboda hupelekwa hapo na kuuawa kabla ya kuporwa Pikipiki zao,matukio ya aina hii yamekwishatokea mara kadhaa na kusababisha vifo vya watu watatu kwa nyakati tofauti.
Baaadhi ya watu wamekuwa wakijiuliza kuhusu mauaji ya waendesha Bodaboda hao lakini ni maswali yasiyokuwa na majibu ingawa kuna tetesi kwamba lipo kundi la watu wanne wanaoishi jirani la eneo hili linalofanyika mauaji ambao hufanya matukio hayo na kupora pikipiki.


"HAMU YANGU NI KUTAKA KUJUA KILICHOANDIKWA MAGAZETINI KILA SIKU"

Mmoja kati ya watoto wanaofanya biashara ya kuuza Sigara Tabora mjini akiangalia magazeti hali inayoonesha kuwa mtoto huyu ana hamu kubwa ya kupata habari kupitia kile kilichoandikwa kwenye magazeti.

UZUNDUZI NA UHAMASISHAJI WA MFUKO WA AFYA YA JAMII(CHF) WILAYANI kILINDI MKOANI TANGA

unnamedMeneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya afya Mkoa wa Tanga(NHIF)Ally Mwakababu kulia akimuelezea mikakati ya mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) Mkuu wa wilaya ya Kilindi,Suleimani Liwowa kulia kwake kabla ya kufanya uzinduzi wa Uhamasishaji wa wananchi kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii wilayani humo (CHF) zoezi ambalo linaendeshwa na Meneja huyo na maafisa kutokana makao makuu na mkoani Tanga kwa muda wa siku kumi. unnamed1 Mkuu wa wilaya ya Kilindi,Suleimani Liwowa akizungumza na viongozi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoa wa Tanga(NHIF) na watumishi wa Halmashauri hiyo Idara ya Afya ofisini kwake kabla ya kuanza uzinduzi wa uhamasishaji wananchi kujiunga na mfuko wa Afya ya Jamii(CHF). unnamed5Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilindi,Daudi Mayeji  akizungumza na viongozi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoa wa Tanga(NHIF) hawapo pichani waliomtembelea ofisini kwake kabla ya kuanza uzinduzi wa uhamasishaji wilayani humo kulia kwake ni Meneja wa Mfuko wa Bima ya Taifa Mkoa wa Tanga(NHIF) Ally Mwakababu kushoto ni Ofisa wa Mfuko huo kutoka makao makuu Isaya Shekifu. unnamed6Afisa Uanachama wa Mfuko wa Bima ya Taifa Mkoa wa Tanga (NHIF) Miraji Swalehe akiwaelimisha waendesha pikipiki kwenye kijiji cha Muheza Kata ya Masagalu wilayani Kilindi juu ya umuhimu wa kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) ili kuweza kupata matibabu muda wote. unnamed7Meneja wa Mfuko wa Bima ya Taifa Mkoa wa Tanga(NHIF) Ally Mwakababu akiwahimiza wananchi wa Kijiji cha Muheza Kata ya Masagalu wilayani Kilindi umuhimu wa kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) wakati wa uzinduzi wake uliofanywa na Mkuu wa wilaya ya Kilindi,Suleimani Liwowa. unnamed9Mwanachama wa Mfuko wa Afya ya Jamii
(CHF) tokea ulipoanzishwa wilayani humo akimuonyesha kadi zake Meneja
wa Mfuko wa Bima ya Afya Mkoa wa Tanga(NHIF) Ally Mwakababu. unnamed10Mkuu wa wilaya ya Kilindi Mkoani Tanga,Suleimani Liwowa akiwa kwenye picha ya pamoja na Meneja wa Mfuko wa Bima ya Afya Mkoa wa Tanga(NHIF)Ally Mwakababu  na maafisa wengine wa mfuko huo na madereva wa pikipiki “Bodaboda”mara baada ya kuwakabidhi kadi zao za uachama wa Kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF). unnamed12 DC Liwowa akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Muheza Kata ya Masagalu wilayani humo wakati akiwahamasisha kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) wakati wa uzinduzi wake.
Mwisho. unnamed13Afisa wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya
(NHIF)kutoka Makao Makuu ,Isaya Shekifu akiwahamisha wananchi wa Kijiji cha Muheza Kata ya Masagalu wilayani Kilindi mkoani Tanga juu ya umuhimu wa Kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF).

BIASHARA YA VITENGE KIGOMA YAVURUGWA NA VITENGE FEKI ZA WACHINA KIGOMA

Na Magreth Magosso,Kigoma

INADAIWA kuwa,Wachina wamechangia kufubaza Biashara ya vitenge Mkoa wa kigoma na kupelekea kushuka kwa makusanyo ya kodi za Forodha na hivyo Mamlaka ya Mapato Tawi la Kigoma kushindwa kufikia lengo  la kukusanya kiasi cha milioni 643,300,000 kwa kipindi cha Julai-Septemba 2014.

Akifafanua hilo  mbele ya  wandishi wa habari  jana katika ofisi ya mamlaka hiyo Kaimu Meneja wa tawi  Patrice Mushi  alisema serikali  idhibiti uingizaji holela wa bidhaa kutoka nje ya nchi  ambapo, makampuni ya kichina hutumia sera ya biashara huria hufoji bidhaa mbalimbali na hivyo kupunguza kasi ya walaji kutumia bandari ya  kigoma kuchukua vitenge kutoka nchi za magharibi .

“wachina wameua soko la vitenge ,makusanyo halisi  ya forordha ni milioni 1,062,806,736 bidhaa hii ndio chachu ,bidhaa ya mafuta si tija kwetu haitabiriki sasa vitenge vya  wax   feki za wachina wadau wanatumia bandari ya Dar-es-salaam  na wanauza  hapo serikali isimamie kanuni,tratibu tunakwama “alibainisha Mushi.

Pia alisema TRA kigoma imejiwekea mkakati wa kuimarisha ukusanyaji wa kodi kupitia mfumo wa kisasa(EFD),vitalu(Block management system) sanjari na kuendelea kuhamasisha wananchi wadai risiti wakati wanaponunua bidhaa madukani,ili kuzuia ukwepaji wa kulipa kodi kwa walengwa.

Aidha alisema wafanyabiashara wenye mtaji wa kuanzia milioni 14 wanahitajika kutumia mfumo wa kisasa wa( EFD) na kuahidi kufuatilia wasiotumia ipasavyo mashine hizo na adhabu kwa walaji wasiodai risiti za bidhaa walizonunua kwa mujibu wa sheria ya mwaka 2000 na kuzuia bidhaa haramu kwa walaji.

Hivyo makusanyo ya kodi kwa mwaka 2013/14 wamekusanya kodi za forodha kiasi cha  sh.bilioni 2.9 ambapo lengo ilikuwa wakusanye bilioni 3.2 sawa na 91% ya ufanisi,huku kodi za ndani wamefanikiwa kukusanya sh.bilioni 6.2 ambapo lengo likiuwa kiasi cha sh.7.179,400,000 sawa na 87%.

Kwa upande  wauza  vitenge soko la kigoma mjini na mwanga Ally Kisala na Tatu Amani kwa nyakati tofauti wakiri hali tete katika uzaji wa vitenge kutoka nchi ya DRC-kongo ,kutokana na bidhaa hiyo kushikwa na wachina ambao hutumia bandari ya  Dar-es-salaam kwa bei rahisi .

Awali walikuwa wakiuza vitenge pande tatu 500 kwa mwezi ,ambapo hivi sasa wanauza  pande tatu  20 kwa mwezi,hali inayowalazimu washindwe kuagiza kwa wingi bidhaa hiyo kutoka nchini Congo ,ambapo wax  kupitia kongo  huuzwa sh.27,000  cha Dar-es-salaam  sh.19,000.

Walisema ugumu wa maisha unachangia walaji wengi kuvamia vitenge kutoka  china ambavyo  vina bei rahisi ilihali havina viwango vya ubora  na kushauri walaji wathamini ubora wa bidhaa ili kuepukana na bidhaa rahisi ambavyo ni gharama kwa badae (uimara mdogo).

Tuesday, November 18, 2014

IGP MANGU AONGEZA ASKARI KITETO

E88A9486
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini,IGP Ernest Mangu akimsikiliza Diwani wa Kata ya Matui Wilayani Kiteto Bw.Athuman Kidawa wakati alipofanya ziara wilayani humo kufuatia kuwepo kwa migogoro ya ardhi baina ya wakulima na wafugaji iliyosababisha kutokea mapigano yaliyosababisha kutokea kwa  vifo.kushoto ni Afisa tarafa wa Matui Bw.Eliakimu Ndelekwa.(Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)E88A9514
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini,IGP Ernest Mangu akizungumza na wananchi  wa Kata ya Matui Wilayani Kiteto wakati alipofanya ziara wilayani humo kufuatia kuwepo kwa migogoro ya ardhi baina ya wakulima na wafugaji iliyosababisha kutokea mapigano yaliyosababisha kutokea kwa  vifo. (Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)E88A9421
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini,IGP Ernest Mangu akizungumza na Mtendaji wa Kijiji cha Chekanao, Kata ya Kiperesa , Wilayani Kiteto Bw.Omar Ndee (kulia) wakati alipofanya ziara wilayani humo kufuatia kuwepo kwa migogoro ya ardhi baina ya wakulima na wafugaji iliyosababisha kutokea mapigano yaliyosababisha kutokea kwa vifo.Katikati ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Deusdedit Nsimike pamoja na Mwenyekiti wa Kijiji hicho Bw.Japhet Chafu (Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)
 
Na Frank Geofray-Jeshi la Polisi, Kiteto.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Ernest Mangu ameahidi kuongeza idadi ya Askari katika kijiji cha Chekanao, kata ya Kiperesa wilayani Kiteto Mkoani Manyara kufuatia wananchi katika kijiji hicho kujitolea nyumba kwa ajili ya kuishi Askari kwa lengo la kuimarisha usalama katika maeneo yao kufuatia kuwepo kwa migogoro ya ardhi inayosababisha kutokea kwa mauaji.
 
IGP Mangu aliyasema hayo jana wakati alipokuwa katika ziara Wilayani Kiteto ya kujionea uharibifu uliojitokeza pamoja na kutafuta ufumbuzi wa migogoro hiyo iliyopelekea kutokea kwa vifo vya wakulima na wafugaji hivi karibuni katika wilaya hiyo ambapo watu kadhaa wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kutokana na vurugu hizo.
 
Alisema kufuatia kuwepo kwa umbali mrefu wa kituo cha Polisi na kijiji hicho atahakikisha askari wa kudumu wanakuwepo ili kushirikiana na wananchi katika kuwabaini wahalifu wanaofanya vurugu na kuendeleza migogoro hiyo ambapo wananchi nao waliahidi kujenga kituo cha Polisi.
 
Kwa upande wake Mtendaji wa Kijiji cha Chekanao Bw.Omar Ndee alisema wamekuwa wakipata shida kutokana na umbali mrefu wa kituo cha Polisi jambo ambalo limekuwa likifanya kuongezeka kwa vitendo vya uhalifu vinavyochangiwa na migogoro ya ardhi katika wilaya ya Kiteto.
 
Naye Mwenyekiti wa Kijiji hicho Japhet Chafu alilishukuru Jeshi la Polisi kwa kuimarisha usalama kijijini hapo tangu kutokea kwa mauji ya wakulima na wafungaji ambapo alibainisha kuwa bila kuwepo wao hali ingekuwa mbaya zaidi kutokana na kutokuwepo na muafaka baina ya wakulima na wafugaji.
 
“IGP hawa askari wako wasingekuwepo hapa usingekuta mtu lakini tunawashukuru sana hawa askari kwa kuwa hivi sasa hali ya usalama imerejea na hata shambani tumeanza kwenda” Alisema Bw.Chafu.
 
IGP Ernest Mangu alitumia ziara hiyo kuzungumza na Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya, Wakaguzi wa Tarafa pamoja na Askari Kata ili kutafuta ufumbuzi wa migogoro hiyo na kuimarisha hali ya ulinzi na usalama.

Monday, November 17, 2014

MAJAMBAZI YA CONGO YADAIWA KUIBA INJINI ZA MABOTI NA KUMTEKA MVUVI MMOJA -KIGOMA

 WAVUVI ZIWA TANGANYIKA
Na Mageth Magosso,Kigoma

SINTOFAHAMU ya wizi katika Ziwa Tanganyika Mkoa wa Kigoma imepelekea,leo  Zaidi  ya lita 2,000 za mafuta ,injini  saba za mitumbwi zimeibwa  sanjari na kutekwa kwa mvuvi mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Bendela  na majambazi  wawili waliokuwa na silaha za moto.

Changamoto kubwa inachangiwa na sekta ya uvuvi mkoani humo kutopewa kipaumbele kwa mujibu wa vikao vya ujirani mwema baina ya nchi jirani hasa Congo DRC ambapo raia wake hutumika kuhujumu uchumi wa wavuvi.

Sendwe Ibrahimu ni mwenyekiti wa wavuvi Mkoa alisema Novemba 14 ,2014 saa 4.00 usiku katika mwalo wa katonga uliopo manispaa ya kigoma ujiji na mwalo wa muyowozi majambazi wawili wakiwa na silaha walifanikiwa kuiba injini saba,lita za mafuta zaidi ya lita 2000 sanjari na kuteka mvuvi mmoja.

Alisema baada ya kupewa taarifa ya tukio hilo usiku huo ndani ya dakika 15 aliwasiliana na katibu tawala mkoa,mkuu wa idara ya majini na Novemba 15,mwaka huu majira  ya  saa 6.00 mchana wavuvi waliipata simu ya mkononi moja iliyosahaulika na majambazi hayo.

“tulipojaribu kuitumia moja ya majina ya ile simu alipokea na walipohoji mahusiano na mwenye simu alitoa lugha chafu,walielekea kusini mwa kijiji cha muyowozi askari wangethubutu wangewakamata ,maisha ya wavuvi yapo rehani kwa sasa “ alibainisha Ibrahim.

Baadhi ya wavuvi walioibiwa  mali zao ni pamoja na Hamza Juma,Ally Said,Geogre Thomas,Baruani Mrisho,Mashaka Idd,Swabilu Mussa Bigili Sebastiani  ambapo kwa nyakati tofauti wakiri kukutwa  na  mkasa  huo  huku  wakibainisha  kupata  hasara ya vifaa mbalimbali vya uvuvi sanjari na kijana wao kutoweka anayedaiwa kuteka na wahalifu  hao.

Akithibitisha  tukio  hilo Kamanda wa Polisi Jafari Mohamed  alisema ni kweli , kikosi cha askari kinawatafuta ziwani tangu usiku wa 14/15 Novemba mwaka huu.

Hata hivyo  baadhi ya wavuvi wamepigwa  na butwaa wakiomba serikali ingilie kati wizi wa mashine katika ziwa hilo na kuwataka wabunge wa kigoma kaskazini na kusini wawajibike katika hilo.

Saturday, November 15, 2014

TASWIRA YA ZIARA YA MWENYEKITI WA CHADEMA MH.FREEMAN MBOWE MIKOANI



Wananchi wa kijiji cha Igalula mkoani Kigoma, wakimsikiliza Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe wakati alipokuwa akiwahutubia katika mkutano wa hadhara wa Oparesheni Delete CCM juzi.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Kazuramimba mkoani Kigoma, katika mkutano wa hadhara wa Oparesheni Delete CCM juzi.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe akisalimiana na Bi. Mariamu Ramadhani (86), baada ya kuwasili katika kijiji cha Kapalamsenga mkoani Katavi, ambako alihutubia mkutano wa hadhara wa Oparesheni Delete CCM juzi.
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Zanzibar), Salumu Mwalimu akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Kazuramimba mkoani Kigoma, katika mkutano wa hadhara wa Oparesheni Delete CCM juzi.
Badhii ya waliokuwa viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa serikali ya kijiji cha Kapalamsenga katika jimbo la Mpanda Vijijini, wakimkabidhi kadi za CCM Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, walipoamua kujiunga na Chadema, baada ya mkutano wa Oparesheni Delete CCM, uliofanyika kijijini Hapo juzi.

"MASHINDANO YA UBORA WA BANGI KUFANYIKA UHOLANZI NA MAREKANI"

Huu si mzaha, bali ndiyo ukweli wenyewe. Mashindano hayo ya kushindanisha ubora wabangi yanayofanyika kila mwaka yakihusisha miji kadhaa ya Ulaya na Marekani ambapo yamejizolea umaarufu zaidi katika jiji la Amsterdam nchini Uholanzi yatafanyika hivi karibuni.

Mashindano hayo hukutanisha wadau wanaotumia uraibu huo ambapo wanapata fursa ya kujaribu bure aina mbailmbali za Bangi zilizoletwa na wakulima wanaolima bangi kutoka pande mbalimbali za dunia na kisha kuchagua iliyo bora kuliko zote.

Labda unaweza kushangaa zaidi kwamba mashindano hayo huwa yanafadhiliwa na gazeti moja maarufu linaloitwa HIGH TIMES na mashindano hayo yamekuwa yakifanyika kwa miaka takriban 27 sasa.

Mashindano hayo ambayo yamejizolea umaarufu yanajulikana kama The Cannabis Cup na kwa jiji la Amsterdam nchini Uholanzi yatafanyika kuanzia tarehe 23 mpaka 27 Novemba 2014 na kwa nchini Marekani yatafanyika tarehe tofauti tofauti kwa kila mji na yatahusisha miji yote huku yakipambwa na matamasha ya wanamuziki maarufu watakaoalikwa kutumbuiza.

Kwa wale wakulima wa uraibu huo watakaotaka kushiriki katika mashindano hayo wanaweza kujipatia tiketi za kushiriki kupitia mtandao wa Cannabiscup.com

Kwa maelezo Zaidi mnaweza kupitia mtandao huu:

http://remainintheknow.blogspot.co.uk/2014/11/high-times-cannabis-cup.html.

Friday, November 14, 2014

MANISPAA YA KIGOMA UJIJI YACHUNGUZA VINARA WA KUFOJI HATI ZA ARDHI HALMASHAURI

Na Magreth Magosso,Kigoma


INADAIWA kuwa,Manispaa ya Kigoma Ujiji,inanuka kwa migogoro ya ardhi ,hali iliyopelekea ofisi ya masjala kuchomwa  moto ,kwa nia ya kupoteza ushahidi wa nyaraka kadhaa zilizopo katika ofisi hiyo,dhidi ya wateja husika.


Mbali na hilo ilielezwa kuwa kuna timu ya watumishi wanaodaiwa  kufoji nyaraka ambapo mkurugenzi husika alipewa orodha ya vinara ,hivyo aliomba muda wa kulifanyia kazi suala zima la uchakachuaji wa faili za ardhi za wananchi .


 Baadhi ya madiwani walitaka maelezo ya kina juu ya athari zilizotokea kwenye ofisi hiyo,ingawa tayari manispaa wameshakarabati kabla ya kutoa ufafanuzi wa hilo na hatma ya wateja wenye madai mbalimbali ili kujua watasaidiajwe.


Akiuliza hoja hiyo katika kikao cha madiwani jana cha robo ya fedha Julai –Septemba 2014 /15  Diwani wa Ujiji Majengo  Shaban  Mkoko alisema wanashangazwa na ukimya wa  idara ya ardhi,ambapo  wananchi   wanahitaji  kujua  athari na namna ya kudhibiti haki kwa wahanga wa nyaraka zilizoungua .


“ najua “data base” imeungua lakini `soft copy ‘zitakuwepo ,idara na mwenyekiti wa kamati ya  mipango miji  semeni gharama za  mali  na nyaraka zilizoteketea kwa moto na uboreshaji wa jengo mmetumia kiasi  gani cha fedha ili umma ujue  hatua za nidhamu kwa walengwa zimefikia wapi? “ alihoji Mkoko.


Diwani wa kata ya Businde Makala Maulidi alisema changamoto ya migogoro ya ardhi imekithiri kwa watuimishi wa idara husika ,kitendo ambacho wanatoa hati feki kwa wananchi wasio na uelewa mpana wa mambo na kusisitiza sheria ya ardhi inatumika vibaya  kwa raia wasiojua mchakato wa kumiliki ardhi kiasili hadi hati.


Akijibia hayo Mwenyekiti wa kamati ya  mipango miji ,ujenzi na mazingira Adamu Musa alisema shida ni wananchi wenyewe wanachangia kupata hati feki na  manispaa itaendelea kuvunja nyumba zilizopo nje ya mipango miji kwa mujibu wa sheria husika na kusihi hati ni chachu ya kukopesheka na tasisi za kifedha.


Kaimu meya wa manispaa  Ruhomya Rashidi aliongeza kwa kusema kuwa,kuhusu hasara na gharama za ujenzi wa ofisi hiyo bado zipo katika mchakato wa kisheria na kudai polisi wanalifanyia kazi .


Akijibia hilo Kamanda wa Polisi mkoa wa hapa Jafari Mohamed alipohojiwa juu ya hilo alisema kweli mwezi mmoja ushapita ni hivi,“kiufupi manispaa haijataka kupata taarifa za thamani ya upotevu wa mali,milango ipo wazi kwa wateja  shida wao wenyewe labda wameridhika na uhalisia wa tukio”.


Katika kikao cha madiwani jana  ilipofika kwenye taarifa ya utumishi na utawala wandishi wa habari walitolewa nje ya ukumbi kwa madai ya kukosa sifa za ujumbe hatimaye  kikao kilihairishwa kimya kimya

kwa mujibu wa kablasha la mkutano husika wameazimia karani andikiwe barua ya uzembe kazini kwa kusababisha baadhi ya nyaraka kupotea,karani mpya wa masjara ateuliwe,vitasa vipya viwekwe na majina manne  ya watuhumiwa majina tunayo waitwe kwa ajili ya mahojiano zaidi..

WAZIRI WA AFYA NA USTAWI WA JAMII AFUNGUA KONGAMANO LA NHIF NA WAANDISHI WA HABARI MJINI DODOMA

1Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Mh. Dr. Seif Rashid akifungua Kongamano la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na wahariri pamoja na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali linalofanyika kwenye hoteli ya New Dodoma  mkoani Dodoma jana, Kongamano hilo la siku mbili linaendelea leo na linajadili mafanikio mbalimbali na changamoto zinazokabili mfuko huo katika mikoa mbalimbali na Halmashauri ambazo unatoa huduma zake. Kongamano hilo linamalizika leo(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-DODOMA) 2Naibu Katibu wa Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dr. Deo Mtasiwa  akizungumza katika kongamano hilo wakati akimkaribisha waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Seif Rashid ili kuzungumza na washiriki wa kongamano hilo. 3Kamimu Mkurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Khamis Mdee  akitoa maelezo kuhusu shughuli mbalimbali kwa mwaka mzima. 4Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa masoko na Utafiti NHIF,Raphael Mwamoto, Kaimu Mkurugenzi Tiba na Ushauri wa NHIF, Dk Mkwabi Fikirini na Mkurugenzi wa Mfuko wa Afya ya Jamii CHF Athman Rehani wakiwa katika mkutano huo. 5Hance John Mwankenja Afisa Mwandamizi , Matekelezo NHIF pamoja na maafisa wengine wa mfuko huo wakiwa katika kongamano hilo. 006Mkuu wa Wilaya ya Igunga Mh. Elibariki Kingu akitoa mada katika kongamano hilo. 6Mkurugenzi wa Mfuko wa Afya ya Jamii CHF Bw. Athman Rehani akitoa mada katika Kongamano hilo. 7Mkuu wa Wilaya ya Igunga na Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Fatma Said Ally wakiwa katika kongamano hilo. 9Baadhi ya wahariri na waandishi wa habari wakifuatilia mada mbalimbali katika kongamano hilo. 10Grace Kingalame wa TBC wa pili na wadau wengine wakiwa katika kongamano hilo. 11Hosea Cheyo wa TBC Mbeya kushoto na Tom Chilala wa Star TV wakifuatilia mada. 12Wanahabari mbalimbali wakifuatilia kongamano hilo. 13 14 15 Baadhi ya maofisa wa NHIF wakiandika mambo muhimu katika kongamano hilo.