Na Mageth
Magosso,Kigoma
SINTOFAHAMU
ya wizi katika Ziwa Tanganyika Mkoa wa Kigoma imepelekea,leo Zaidi ya
lita 2,000 za mafuta ,injini saba za
mitumbwi zimeibwa sanjari na kutekwa kwa
mvuvi mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Bendela na majambazi wawili waliokuwa na silaha za moto.
Changamoto
kubwa inachangiwa na sekta ya uvuvi mkoani humo kutopewa kipaumbele kwa mujibu
wa vikao vya ujirani mwema baina ya nchi jirani hasa Congo DRC ambapo raia wake
hutumika kuhujumu uchumi wa wavuvi.
Sendwe
Ibrahimu ni mwenyekiti wa wavuvi Mkoa alisema Novemba 14 ,2014 saa 4.00 usiku
katika mwalo wa katonga uliopo manispaa ya kigoma ujiji na mwalo wa muyowozi
majambazi wawili wakiwa na silaha walifanikiwa kuiba injini saba,lita za mafuta
zaidi ya lita 2000 sanjari na kuteka mvuvi mmoja.
Alisema
baada ya kupewa taarifa ya tukio hilo usiku huo ndani ya dakika 15 aliwasiliana
na katibu tawala mkoa,mkuu wa idara ya majini na Novemba 15,mwaka huu majira ya saa 6.00
mchana wavuvi waliipata simu ya mkononi moja iliyosahaulika na majambazi hayo.
“tulipojaribu
kuitumia moja ya majina ya ile simu alipokea na walipohoji mahusiano na mwenye
simu alitoa lugha chafu,walielekea kusini mwa kijiji cha muyowozi askari
wangethubutu wangewakamata ,maisha ya wavuvi yapo rehani kwa sasa “ alibainisha Ibrahim.
Baadhi ya wavuvi walioibiwa mali zao ni pamoja na Hamza Juma,Ally Said,Geogre Thomas,Baruani
Mrisho,Mashaka Idd,Swabilu Mussa Bigili Sebastiani ambapo kwa nyakati tofauti wakiri kukutwa na mkasa huo huku wakibainisha kupata hasara ya vifaa mbalimbali vya uvuvi sanjari na kijana wao kutoweka anayedaiwa kuteka na wahalifu hao.
Akithibitisha
tukio hilo Kamanda wa Polisi Jafari Mohamed alisema ni kweli , kikosi cha askari kinawatafuta ziwani tangu
usiku wa 14/15 Novemba mwaka huu.
Hata hivyo baadhi ya wavuvi
wamepigwa na butwaa wakiomba serikali ingilie kati wizi wa mashine katika ziwa
hilo na kuwataka wabunge wa kigoma kaskazini na kusini wawajibike katika
hilo.
No comments:
Post a Comment