INADAIWA kuwa,Manispaa ya Kigoma Ujiji,inanuka kwa migogoro
ya ardhi ,hali iliyopelekea ofisi ya masjala kuchomwa moto ,kwa nia ya kupoteza ushahidi wa nyaraka
kadhaa zilizopo katika ofisi hiyo,dhidi ya wateja husika.
Mbali na hilo ilielezwa kuwa kuna timu ya watumishi wanaodaiwa kufoji nyaraka
ambapo mkurugenzi husika alipewa orodha ya vinara ,hivyo aliomba muda wa
kulifanyia kazi suala zima la uchakachuaji wa faili za ardhi za wananchi .
Baadhi ya madiwani
walitaka maelezo ya kina juu ya athari zilizotokea kwenye ofisi hiyo,ingawa
tayari manispaa wameshakarabati kabla ya kutoa ufafanuzi wa hilo na hatma ya
wateja wenye madai mbalimbali ili kujua watasaidiajwe.
Akiuliza hoja hiyo katika kikao cha madiwani jana cha robo
ya fedha Julai –Septemba 2014 /15 Diwani
wa Ujiji Majengo Shaban Mkoko alisema wanashangazwa na ukimya wa idara ya ardhi,ambapo wananchi
wanahitaji kujua
athari na namna ya kudhibiti haki kwa wahanga wa nyaraka zilizoungua .
“ najua “data base” imeungua lakini `soft copy ‘zitakuwepo
,idara na mwenyekiti wa kamati ya
mipango miji semeni gharama za mali na
nyaraka zilizoteketea kwa moto na uboreshaji wa jengo mmetumia kiasi gani cha fedha ili umma ujue hatua za nidhamu kwa walengwa zimefikia wapi?
“ alihoji Mkoko.
Diwani wa kata ya Businde Makala Maulidi alisema changamoto
ya migogoro ya ardhi imekithiri kwa watuimishi wa idara husika ,kitendo ambacho
wanatoa hati feki kwa wananchi wasio na uelewa mpana wa mambo na kusisitiza
sheria ya ardhi inatumika vibaya kwa
raia wasiojua mchakato wa kumiliki ardhi kiasili hadi hati.
Akijibia hayo Mwenyekiti wa kamati ya mipango miji ,ujenzi na mazingira Adamu Musa alisema
shida ni wananchi wenyewe wanachangia kupata hati feki na manispaa itaendelea kuvunja nyumba zilizopo
nje ya mipango miji kwa mujibu wa sheria husika na kusihi hati ni chachu ya
kukopesheka na tasisi za kifedha.
Kaimu meya wa manispaa
Ruhomya Rashidi aliongeza kwa kusema kuwa,kuhusu hasara na gharama za
ujenzi wa ofisi hiyo bado zipo katika mchakato wa kisheria na kudai polisi
wanalifanyia kazi .
Akijibia hilo Kamanda wa Polisi mkoa wa hapa Jafari Mohamed
alipohojiwa juu ya hilo alisema kweli mwezi mmoja ushapita ni hivi,“kiufupi
manispaa haijataka kupata taarifa za thamani ya upotevu wa mali,milango ipo
wazi kwa wateja shida wao wenyewe labda wameridhika
na uhalisia wa tukio”.
Katika kikao cha madiwani jana ilipofika kwenye taarifa ya
utumishi na utawala wandishi wa habari walitolewa nje ya ukumbi kwa madai ya kukosa
sifa za ujumbe hatimaye kikao kilihairishwa
kimya kimya
kwa
mujibu wa kablasha la mkutano husika wameazimia karani andikiwe barua
ya uzembe kazini kwa kusababisha
baadhi ya nyaraka kupotea,karani mpya wa masjara ateuliwe,vitasa vipya
viwekwe na majina manne ya watuhumiwa majina tunayo waitwe kwa ajili ya
mahojiano zaidi..
No comments:
Post a Comment